Ninawasalimu rafiki zangu wote tulio ndani na nje ya Tanzania nimatumaini yangu kuwa tumeuanza mwaka 2013 kwa amani kabisa. Nami na team yangu nzima ya Utendaji Tunawatakia Happy New Year.
Mwaka 2013 umeanza kwa kasi sana juzi tu hapa tumesherekea mwaka Mpya Ghafla leo tarehe 8, nexr week nikiandika tayari katikati ya mwezi maisha yanasonga na siku zinasonga na mwaka utaisha tutaingia 2014.
Kati ya maneno ambayo watu wengi wanayo anaoanza kupanga mipango utasikia "mwakani nataka nianze kusoma" au "Mwakani nataka Nianze Kulima" mwingine ukumuuliza swali tu atakuambia Mwakani, utadhani mwakani huwa haifiki, Mwakani na Kesho vinapishana kidogo sana. Ukimwambia mtu tuonane lini anakuambia "kesho", au hela yangu unanilipa lini anajibu "kesho", ama ukienda maofisini kufatilia documents utasikia Njoo Kesho, Njoo Kesho ikianza hutaamini wengi huwa wanadhani Kesho iko mbali, Kesho haiko Mbali kama Mwakani ilivyo karibu.

Mwaka 2013 ndio huu umeshaingia kwa sasa yale uliyosema Mwakani sasa Mwaka ndo umeshaingia umejipangaje kutilimiliza uliyo yakusudia??kama bado una mawazo yale yale, fikra zile zile, mtazamo ule ule basi usitegemee tofauti na mwaka jana, nini kipya unacho unadhani kinaweza kukusababishia ukafanya jambo la tofauti??wengi wetu tumepanga mipango kwa ajili ya mwaka 2013 lakini ukitazama kwa kina mipango ya mwaka 2013 mingi inafanana na ile ile ya mwaka 2012 ni kama Ume Copy, Ume Edit na Ku Copy, kile ulichofanya mwaka jana ndio mwaka huu utafanya tena vile vile Jipya utakuwa umelipata wapi??Kwani umeona tofauti yoyote kwako kati ya tarehe 31 Dec, na tarehe 01 Jan, zote ziko vile vile kama Njaa iliuma kama jana, kama usingizi ulikushika kama jana, hakuna jipya linalotokea mwaka unapoanza mpya kiasi kwamba ukaamini kuna nguvu ya utendaji inakushukia kuanzia tarehe 01 January ambayo hiyo itakufanya wewe kuwa noma kuliko mwaka uliopita, mawazo uliyo nayo ni yale yale, mtazamo ni ule ule Jipya litatoka wapi??
Kuna mwandishi mmoja wa Vitabu aliwahi sema Huwezi Fanya zaidi ya Kile Unachokiwaza ama Kijua, kufanya jambo ambalo hujawahi kuwaza ana kutokulijua linaingia katika Category ya Miujiza, sababu Muujiza ni jambo ambalo hukuwahi kuwaza kuliweza ama kulipata na likakupata kwa njia ya ajabu, unless 2013 uamue kuishi kwa njia ya miujiza miujiza ndio utakuwa na matokeo mengi sana tofauti. Hata kama Umetabiriwa kwenye nyumba ya ibada kuwa mwaka 2013 wewe utakuwa unatisha funika sana haitakuwa kwako kama hautaamua kuwa na fikra mpya, Kama mawazo yako uliyonayo ndiyo yamekufikisha hapo Ulipo Kwanini Usibadilishe taarifa ulizo nazo ili uweze kufika mbalia, badilisha aina ya marafiki ulio nao, badilisha aina ya nguo ulizo nazo, badilisha aina ya taarifa ulizonazo katika ubongo, ikiwezekana badilisha hata sehemu ya kufanyia kazi, ikiwezekana develop tabia za kimaendeleo kwa afya ya akili yako. Huwezi kuwa na mawazo yale yale na fikra ile ile iliyokufikisha hapo ulipo kisha ukategemea mwaka 2013 ukafanya wonders.
Kama unayoyajua yamekufanya umefika hapo ulipo kuna mambo mawili lazima ujue yatakutokea ukiendelea kuwa na mawazo hayo hayo, kwanza lazima ujue utabaki kama ulivyo kama hautaamua kubadilika ama utapitwa na wakati sababu mawazo uliyokuwa unatumia mwaka 2012 ni mawazo ya mwaka 2011 kama ambavyo uko 2013 unatumia mawazo ya mwaka 2012. Yamkini mwaka 2013 uko kwenye season yako, kila mtu anakutafuta wewe, kama umaarufu umekujongea tayari, kama ni fedha zinazidi kukufuata jua jambo moja ukiwa na mawazo yale yale na fikra zile zile watu watasema hauna Jipya. Na kweli Jipya utakuwa umelipata wapi wakati unawaza wale wale unafanya yale yale kisha watu watakuchoka na kukukimbia.
Think Differently and Make A Difference.
Papaa Ze Blogger
Tel. 0713 494110
Twitter: Sasalijr
Facebook: Samuel Sasali
Email: samsasali@yahoo.com