CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

Papaa On Tuesday.....Kuelimika ni Kubadilika, Ujinga ni Kuamua

Zikiwa zimebaki siku 16 kabla ya Event Ya Friends On Friday Funga Mwaka yenye Jina la Extravaganza kufanyika pale Makumbusho, ninayo haja ya Kumshukuru Mungu kwa ajili ya Ulinzi wake, kipindi hiki cha Msimu wa Campus Night na shughuli zingine za Kijamii na Kitumishi nimekuwa nikitembea angani na barabarani lakini Mungu amekuwa Mlinzi Kwangu. Sina budi ya kusema asante kwa Mungu kwa Uzima na Afya na uwezo wa Kuwakilisha Papaa On Tuesday Kila inapofika siku ya Leo.

Tarehe 17 January, 2012 niliandika Papaa On Tuesday yenye heading Lile Ninalotaka Kulifanya Silifanyi, Nisilotaka Kulifanya Ndilo Ninalolifanya gonga hapa kama Hukusoma....http://samsasali.blogspot.com/2012/01/papaa-on-tuesdaylile-ninalotaka.html.
Mwaka wakati unaanza nilitoa tahadhari ya kuwa pamoja ya kuwa na Mikakati tuwe waangalifu maana yale tunayoyapanga mengi hatutayafanya. Jichunguze mambo mangapi ulipanga mwaka huu umeyafanya ukiacha yale yaliyoibuka tu na kukwamisha mipango yako ya mwaka huu. Zimebaki siku arobaini na moja (41) mwaka huu kumalizika jiulize swali kuna ulilofanya la kujivunia??




Ninakumbuka Miaka hiyo ya zamani wakati nasoma Makongo High School alikuwepo Mwalimu anaitwa "Kombaha" mwalimu huyu alikuwa na msemo aliokuwa anapenda sana kuusema tukiwa darasani hasa mwanafunzi anapokosea/misbehave alikuwa anasema "Mambo Huanzia Nyumbani". Siku moja nilimuuliza Mwalimu tukiwa Nje ya darasa maana hasa ya Msemo wake huo akanijibu "Ukimuona Mtu ameonesha tabia fulani mbaya basi jua alikuwa nayo tangu zamani sema ailikuwa haijapata nafasi, mabadiliko yoyote ambayo mtu anataka kuyafanya katika maisha lazima aanze na yeye mwenyewe, aanze na familia yake ndipo wengine watafuata" siku mwelewa mwalimu yule kutokana na Ufahamu wangu ulivyokuwa nyakati zile. Mabadiliko ya kweli huanza na mtu mwenyewe ndipo wengine watafuata. Pastor Carlos aliwahi sema "Huwezi waambia Watu Yesu anabadilisha Wakati wewe Mwenyewe hujabadilika". Kizazi chetu kina changamoto kubwa sana ya ku-deal na tatizo badala ya Ku-deal na chanzo cha tatizo hasa yale matatizo yanayotuhusu sisi wenyewe.





Sisi ni Kizazi kinachojua tatizo ni nini, na suluhisho ni nini, lakini hatutaki kufuata suluhisho linalotupasa kufanya halafu tunataka mabadiliko yawe chanya kana kwamba tumetumia njia inayotupasa kuifuata. Kizazi hiki kina jua kabisa Ukifanya jambo fulani matokeo yake ni fulani, lakini tunataka kutumia njia ile ile mbaya halafu tupate matokeo mazuri. Sisi ni kizazi kinachojua kabisa Ukifanya ngono zembe matokeo yake ni magonjwa ya Kuambukiza ama Mimba, lakini ajabu watu wanafanya ngono zembe halafu wanategemea kabisa magonjwa yasiwepo na wala mimba zisiwepo ndio maana vikitokea unakuta mtu anachanganyikiwa yaani ukimuuliza huyu mtu alikuwa hajui matokeo??atakuambia anajua sasa ajabu alitaka kutumia njia mbaya kumpa matokeo mazuri. Sisi ni Kizazi kinachojua kabisa usipoweka akiba ya fedha kwenye maisha yako utakuwa hauna maendeleo pamoja na kujua hayo yote sisi ndio watu tunaoongoza kwa kutumia fedha vibaya, sio wanafunzi, sio vijana sio watu wazima, kuna watu wanapata fedha kila iitwapo leo lakini hakuna cha maana anachofanya kwenye maisha ukimuuliza fedha zako unazifanyiaga nini cha maana utakuta hakuna cha maana anachofanya na fedha hizo.





Kuna mambo kadha wa kadha ambayo tunajua tusipoyafanya tutapata mabadiliko mazuri lakini mwisho wasiku tunaishia kufanya hayo hayo. Watu wanaofanya diet wanajua kabisa wakila Kitimoto na vyakula Vya Mafuta watazidi kunenepa, ajabu hiyo hiyo Diet aliyojipangia inamshinda. Wenye Vitambi wanawake kwa Wanaume na wale wanene wanajua kabisa ukifanya nini kwa Ukamilifu Kitambi kinapungua within a short time lakini ajabu hatufanyi, Wanafunzi wanajua kabisa Ukijiandaa tangu shule ama chuo kinafunguliwa hautakomaa kusoma siku za Mitihani lakini ajabu siku zingine zote mtu anatazama Movie mitihani ikiianza tu unamuona mtu ndo anaanza kusoma. Sisi ndio Kizazi ambacho mtu anajua anatakiwa kulipa Kodi ya nyumba mwenzi December, lakini miezi yote anakula hela zake ikifika kipindi cha Kodi ya Nyumba ndo anaanza Kukopa ili kulipa Kodi ya Nyumba, Sisi ndio Kizazi ambacho Kinamchagua Mgombea ambaye anatoa rushwa ili akatusaidie kumaliza tatizo la rushwa, sisi ndio Kizazi ambacho chombo kinachohusika kuchunguza Watoa Rushwa na Wala Rushwa kinapokea Rushwa ili kuwakinga wala rushwa, sisi ndio Kizazi ambacho Washauri Wa Mambo ya Ndoa za wengine Zikitaka Kustawi zinatakiwa ziwe vipi wakati za Kwao zinawashinda Kuziboresha, sisi ndo Kizazi ambacho Watu Unao Waamini ndio Wanaokusaliti, sisi ndio Kizazi ambacho timu zetu Simba na Yanga tunajua Tatizo ni Viongozi lakini Tunamfukuza Kocha. Sisi ni Kizazi Kinachojua madhara ya Sigala lakini tukaamua kuvuta.




Ni rahisi kuwasaidia wengine kuliko kijisaidia mwenyewe, ni rahisi kuwafokea wengine wanapokosea lakini tukasahau na sisi tunakosea, ni rahisi kuwanyoshea wengine vidole kwa mambo wanayokosea na kusahau sisi pia tunakosea. Matatizo mengi ya Msingi hatuko serious kuyatatua hata kama tunajua hiki tunachokifanya ni cha muda tu, siku za nyuma niliwahi andika Usizibe Shimo La Panya Kwa Kipande Cha Mkate..http://samsasali.blogspot.com/2011/10/papaa-on-tuesdayunaziba-tundu-la-panya.html. Wengi wa wanaoenda kuomba ushauri sehemu fulani mara nyingi sana huomba ushauri pasipo kueleza kiini hasa ila kasehemu tu ka kiini, unajikuta tatizo unalo deal nalo silo hasa linalopelekea tatizo kuwepo tabia hii imepenya kwenye Jamii yetu la kuto ku deal na tatizo la Msingi, tangu zamani tulipokuwa wadogo wazazi walitumia fimbo kutukataza mambo waliyokuwa hawayapendi kilichotokea walitujaza hofu ya kufanya mbele zao wengine fimbo ziliwasaidia wengine ziliwasaidia namna ya kubadilisha mbinu mbadala ili wasichapwe. Kufundishika ni Kubadilika huwezi kusema umeelewa wakati hujabadilika.




Mtu mwenye kuonesha kuwa amelielewa tatizo na ufumbuzi wake basi ni yule anayeamua kubadilika kueleka  kwenye maendeleo. Haitakusaidia kujua suluhu ya jambo kisha usifanye kwa faida yako na Jamii yako niliwahi andika kwenye Papaa On  Tuesday kuwa "Thawabu Ya Mtendaji, Haifanani na Msemaji" gonga hapa...http://samsasali.blogspot.com/2011/01/papaa-on-tuesdaythawabu-ya-mtendaji-wa.html. Mambo huanzia nyumbani, mabadiliko ni Mchakato, lakini ni mchakato wenye nidhamu pia. hakuna jambo baya kwenye maisha kama "Kuchukuliwa" ukisikia watu wanasema "tunakuchukulia sana" ujue wameshakuchoka sema ndo hivyo hawana namna. Inawezekana wamejitahidi kukusaidia wameona hausaidiki waka opt kukuchukulia kama mzigo ambao Mungu amewapa kwenye maisha. Kwenye ndo usipende kuchukuliwa ni ishara mbaya sana kwenye kizazi chetu, kwenye Jamii usiwe mtu wa kuchukuliwa. Kama unajua jambo fulani ukilikomalia utapata matokeo mazuri kwanini usilikomalie. Discipline ya kwenye maisha ni kitu cha msingi sana otherwise tutajua rushwa ni adui wa haki na sisi tutaendelea kutoa na kupokea, sisi tutajua kabisa ukifanya jambo A utakuwa na madhara ya afya lakini watu watasema "nimeshindwa kujizuia". Kujifunza ni Kubadilika Ujinga ni Kuamua. Mambo Huanzia Nyumbani.
Think Differently Make A Difference.
Papaa
0713 494110.