.....WARAKA TOKA HONEYMOON!!
Nikiwa
bado niko honeymoon naomba leo nizungumze na wewe kuutambua Moyo wa
Mwanamke.Ni wazi kua moyo wa mwanamke ni wa utofauti sana kuliko sisi
tunavyomtazama napenda kuchukua nafasi hii kukufahamisha au
kukutambulisha mwanamke aliyebeba kusudi lako,hatima yako,mwanamke
aliyesababisha Mungu ashike damu kwa mara ya kwanza maana kuna sababu
kubwa sana ya Mungu kumtoa mwanamke katika ubavu wa mwanaume kuna sababu
kubwa sana ya Mungu kuruhusu damu kumwagika,Mungu sio katiri na wala
hakufanya jambo la kinyama na wala hakutaka kumuumiza Adamu ila alikuwa
na kusudi na malengo maalumu sana na jambo zuri sana kwa Adamu ndio
maana alifanya yeye mwenyewe kazi hiyo ya upasuaji,maeneo mengine yote
Mungu aliamuru watu wachinje wanyama na damu ifanye kazifulani na hata
kwa Yesu aliruhusu apigwe na kuchomwa mkuki ili damu ifanye kazi lakini
kwa Adamu aliingia mwenyewe hakuitaji mikono ya mtu ndio maana maandiko
yanasema mke mwenye busara hutoka kwa Bwana'
Hapa inatubidi kuliangalia kiundani sana
kusudi la Mungu kumtoa mwanamke kwa mwanaume kwa kuusoma moyo wa
mwanamke aliyebeba kusudi lako.Kwa nini mimi Samuel Sasali nili mpenda
mke wangu kipenzi Milembe John Madaa,hakuna anayependa bila sababu na
hakuna anayependwa bila sababu zinzomfanya,mtu kupenda au kutopenda hata
Mungu alikuwa sababu za kuupenda ulimwengu hata kumtoa mwana wa pekeee
ulimwenguni.Kupenda sio dhambi na kutopenda sio dhambi upendo ni sehemu
ya maisha na ni Mungu ambaye ameweka kwa mwanadamu hivyo.LOVE imetoka kwa mungu sio mtu ameamua kupenda jua kuwa love ni sehemu ya maisha hata wanyama wanapenda na wana wivu wao kwa wao lakini love ya mwanadamu ni kubwa na inanguvu kuliko wanyama sababu nilizo nazo kwanini ninapenda na kwanini natakiwa kumpenda?
(a)Kwa sababu naitaji kufalijiwa (nafsi)
(b)Kwa sababu naitaji kukamilishwa (mwanz 2:18)
(c)Kwa sababu Upendo ni Asili
(d)Kwa sababu ni mpango wa Mungu
(e)Kwa sababu nahitaji kupendwa
Love haijengwi kwa mali,pesa,watoto,uzuri,elimu,wadhifa wako,Uaskofu,Uchungaji,Utume,Udaktari.Upendo unajengwa kwa maneno matamu (palatable word) (sweet word) maneno yenye uwezo wa kukamata hisia ya mtu na kumfanya achilie maisha yake kwako yanatakiwa maneno yenye nguvu ya ushawishi na hata sex haijengi ndoa bali sex ni (thanksgiving) ni sadaka ya shukurani baada ya mambo muhimu kufanyika watu wengi wamedanganyika kuwa sex ndio upendo kitu ambacho sicho na ni afundisho potofu,vitu vinavyotengeneza upendo ni vidogo sana na vinadharauliwa sana kama busu,kukumbatia,mawasiliano na muda wa kutosha na mwenzi wako.
Upendo unafanya mtu kujua kusudi la kuumbwa fulani kwa ajili ya mtu fulani,mwanadamu amegawanyika katika sehemu kuu tatu 1)Nafsi 2)Roho 3)Mwili kumbuka moyo unahitaji kufarijiwa,unahitaji kupendwa na unahitaji kuheshimiwa.
Papaa