CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

NAMNA MBALIMBALI YA KUPIKA WALI!!!

Habari zenu!
Najua watu wengi sana wanapenda wali kuliko chakula kingine chochote na hata wale wasioa na kuolewa basi pishi lao kubwa ni Tambi na Ubwabwa na wale wa mikoani(nje ya Dar hupendelea kupika ugali)
Yamkini wewe unajua kupika wali na Rice cooker basi!
Lakini mchele una aina nyingi sana za kuupika kama vile wali wa maua,wali uliokaangwa na mbogamboga na kutaja aina chache;
Naam hivi ndivyo asemavyo
Chef Issa Kapande
KWA WALE NDUGU ZANGU MLIOKO UGHAIBUNI MCHELE ASILIMIA 90% HAUNA LADHA NA HARUFU NZURI KAMA TULIOUZOEA NYUMBANI CHUKUA UJANJA HUU ILI UFANYE WALI WAKO UWE WA KUNUKIA NA LADHA SAFI KABISA



Karoti iliyokwaruzwa vizuri, nyanya na vitunguu vilivyokatwa katika umbo dogo dogo rahisi kwa kuiva


Mchanganyiko wa karoti, kitunguu na nyanya katika kikaango chenye mafuta na moto mkali pika kwa dakika 5 tu usiache ziive sana kisha changanya wali wako ambao umeshaiva.



Huu ni wali ulioiva na ukachanyanywa na mchanyiko wako wa caroti, utapata harufu nzuri na ladha nzuri sana kwa kupata harufu na ladha nzuri zaidi unaweza ongezea pilipili hoho au girigilani ( Corriender leaves).


Mahitaji
720gram caroti iliyokwaruzwa

480gram Basmati rice ( mchele wa pishori) iliyopikwa

2 vitunguu vikubwa vikate katika size ndogo

1 Nyanya moja kubwa ikate katika size ndogo

1 fungu la majani ya girigilani

2 kijiko kikubwa cha chakula karanga zilizokaangwa kwajili ya kupambia

3 kijiko kidogo cha chai cha mafuta ya kula

Chumvi weka kulingana na ladha na mahitaji yako

Jinsi ya kuandaa:

Pasha moto sufuria lako au kikaango weka mafuta kisha weka vitunguu kaanga kiasi tu visiungue au kua na rangi ya kahawia vilainike tu inatosha.

kisha weka nyanya zikaange mpaka zichanganyike kabisa zitengeneze rojo rojo
Kisha weka caroti zilizokwaruzwa katika mchanganyiko wako kaanga na zichanganyike vizuri

Kisha weka wali wako wa basmati ulioiva katika mchanganyiko wako wa karoti changanya vizuri kisha mimina majani ya girigilani na changanya pole pole mwisho kabisa weka karanga zako ambazo zimekaangwa vizuri kama unatumia.

Mapishi haya unaweza tumia mchele wa aina yeyote ile sio lazima mchele wa basmati 
Source; http://activechef.blogspot.com