CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

Papaa On Tuesday…..Unao Uwezo Wa Kuchagua Cha Kufanya Lakini Huna Uchaguzi na Matokeo Ya Kile Ulichokichagua Kukifanya.

Tukiwa bado katika Maombolezo ya Kupoteza ndugu zetu katika Mkoa wa Arusha kwa sababu zinazosadikika ni za kisiasa nachukua fursa hii kuwapa pole ndugu zetu wote ambao wamefariki lakini pia na wote waliojeruhiwa hasa hasa Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha rafiki yangu na mtumishi katika Shamba la Bwana Bw. Amani Golugwa pole sana na “majanga” ya Kisiasa. Nimeamini kweli tunao uchaguzi wa nini cha kufanya lakini hatuna uchaguzi wa kuzia matokeo ya kile tulichokichagua kinapotokea. Ukichagua Siasa basi matokeo ya Siasa ujue huna maamuzi nayo.

Wengi tuko leo hivi tulivyo kama matokeo ya kile ambacho tulikichagua katika maisha, na wakati huo tuliona sie ndio wenye mana kuliko wengine wote wakati wa kuchagua lakini hatukujua kuwa kile tulichokichagua hatuna uwezo wa kuhimili matokeo yake ya kwenye maisha. Wengi wetu wakati tunahimizwa kwenda shule tuliendekeza ubishoo na usharubalo, tulikuwa na uwezo wa kuamua either kusoma ama kuendekeza ujinga wa makuzi wakati huo kwa kufuata mkumbo wa mambo yaliyokuwa yakiendelea. Pengine kila ukikaa unajicheka kwa kile ambacho ulikichagua wakati huo na ukasahau methali ya Majuto ni Mjukuu waliponena wahenga, tulijiona sisi ndio tunaojua kuliko wale waliokuwa wakituasa na kutuhusia. Leo tumekuwa na akili tunatamani zile zama tulizokuwa tunakula chips na kuvaa raba za gharama na kuendekeza ubishoo zirudi tena ili tufanye kweli, lakini wapi kila jambo na majira yake. Wengine tunasoma Elimu za Watu wazima sit u tulikuwa na tatizo la ada kipindi hicho la hasha ila tulipokuwa nacho tulitumia na kilipoisha tukajijutia kwenye maisha.

Kuna mdada mmoja rafiki yangu anaishi kwenye mateso makubwa ya ndoa yake na amebaki kujutia maamuzo aliyoyachagua kuyafanya kisa na mkasa anasema hakujua, kama angelijua angechagua kuendelea na maisha yake kwanza ndipo achague kuolewa akiwa na akili timamu. Majanga mengi sana ambayo tunapitia kwenye ndoa na mahusiano ni kutokana na maamuzi yetu ya kukurupuka, maamuzi yetu ya kujiaminisha kuwa tuko sahihi kuliko wengine matokeo yake tunabakia kufa na tai shingoni. Kwani uwongo??ukikaa mwenyewe hujiambia kuwa laiti kama ungelijua usongechagua kuolewa ama kuoa Fulani kisa na mkasa matokeo ya kile ulichokichagua kwenye maisha. Kuna wengine walitaka kuolewa so kilichotokea wakabeba mimba wakidhani maisha yale ya honey baby and sweetheart yataendelea, kongwa walilojitishwa na nira walizojifunga wamebaki kulilia moyoni, mkiwaona barabarani na kwenye facebook utadhani ni ndoa ya mfano kumbe si lolote si chochote kila mtu analala chumba chake nyumbani hakuna furaha ambayo inadhaniwa ipo wakiwa nje ya mlango wa nyumba yao wakikaa wenyewe wanatamani sana kurejesha maisha siku ambazo walikuwa wanacheka na kwenda kula bata na kuitana majina ya mahaba, leo yamebaki kuitana “wewe”, “Nanii”, “Stella”, “Sultani” dry dry dryyyyyyyyyy. Lady Jay d anasema anatamani kuwa kama zamani lakini ndo zama zimeisha tena maisha yamebaki kuishi kwenye matokeo yake.


Kuna Ofisi Fulani nilifanya kazi zamani kuna jamaa alicha kazi baada ya kupata kazi sehemu nyingine kwa ahadi ya project mpya alipohama kwetu akaenda kwingine ambako huko project ikakosa hela akabaki mtaani akajuta sana kwa uamuzi wake wa kuacha kazi alikuwa na muda wa kuchagua kuacha kazi ama kuanza upya sehemu nyingine matokeo ya maamuzi yetu mengi hayamo ndani ya matakwa yetu. Unaweza kuacha kazi sehemu moja ili ufanye kazi kwingine ukashangaa ulikokwenda ndo unapunguzwa wewe ama unahama nyumba moja kwenda nyingine kumbe unakokwenda ndo kuna zoezi la upanuzi wa barabara unabaki kusema ng’ombe wa masikini hazai. Wengine wamepata watoto mapema si kwa sababu walikuwa wanapenda kuzaa bali bali kilichotokea “ajali” ikasababisha waanze kuitwa “mama” ama “baba” wakati wa kudungunyuana walikuwa wanasikia raha ila ilipofika ujauzito wengine wakasema wakatoe ama wakatoa ujue ulikuwa na uchaguzi wakati wa kuamua lakini ukasahau unawajibika na matokeo ya kile ulichokiamua kwenye maisha yako.


Kuwajibika na matokeo ya yale tunayoyaamua ni wachache wetu wako tayari unapotaka kufanya maamuzi kwenye maisha jua kabisa wewe unawajibika na matokeo ya maamuzi unayochukua kwenye maisha. Kila ambacho unakichagua kukifanya jua kina matokeo na uwe tayari kupokea matokeo ya kile ulichokichagua kukifanya kwenye maisha.

0713 494110

HATIMAYE SAMUEL SASALI a.k.a PAPAA ATAKUWA AKITANGAZA UCHUMBA RASMI TAR 23/06/2013 PALE VCCT!!

Hello marafiki na wasomaji wote wa Blog hii!!
Leo ninawaletea habari njema  zilizoambatana na mwaliko  maalum kwa watu wote wenye mapenzi mema na Samuel Sasali, The Blogger, MC,Mzee wa Ideas mengi ambaye mara zote husema Mungu alimnyima urefu akamjalia Mdomo (kuongea sana) na kukosa aibu pia!!!
Baada ya sarakasi za kutosha za kutafuta mwenzi wa kumfaa hatimae pacha wangu amegota na kumpata mlimbwende wa pekee aliyewashinda wanawake zaidi ya Bilioni 4 duniani na kuwa wa pekee...Usukani mdogo unaoendesha Merikebu kubwa!!!
 Ndio ni binti huyu Dk Milembe John Madaha ambaye ameteka moyo wa kaka Mkubwa na kwa huyu Papaa amegeuka rapper,mwana mashairi na mtiifu sana!!
Kama una kumbukumbu nzuri, blog hii imewahi kum-ZOOM kijana huyu kama mmoja ya vijana wanaopaswa kuigwa na vijana wengine,fuata link umfahamu vema;

.http://chavalamedia.blogspot.com/2012/08/salaam-leo-katika-kipengele-hiki.html

Basi habari njema ndio hii, jumapili hii wewe na wenzako wote ambao ni marafiki wa kweli Samuel Sasali au ni msomaji  wake wa Papaa On Tuesday au ni Mwanachama wa Marafiki Huru au ni mpenzi wa Friends On Friday au umewahi kufundishwa na yeye popote pale,shuleni, chuoni au kanisani au hata kama amewahi kusherehesha shughuli yako yeyote ile..basi sasa ni saa ya kumuunga mkono kwa kumaanisha!!

Ni jumapili hii ya tar 23/06/2013 kuanzia saa nne asubuhi pale Mbezi Beach A katika kanisa la VICTORY CHRISTIAN CENTRE TABERNACLE (VCCT),Unaweza ukapanda gari mpaka mwenge na kupanda usafiri wa kanisa unaondoka hapo tatu na nusu ama ukachukua bajaji mpaka huko kanisa la hema,au ukapanda gari mpaka kawe mwisho na kupanda bajaji pia mpaka kanisani au ukashuka Mbezi Tanki bovu na kuchukua bajaji au bodaboda mpaka kanisani...lakini kama unakuja na private car njoo na barabara ya Mwai Kibaki(zamani old bagamoyo road) kisha baada tu ya daraja utaona kibao kushoto kwako kama ukitokea mwenge then fuata njia hiyo kwa hakika huwezi kupotea!!

Ni marufuku kuja mikono mitupu na ni marufuku kuja peke yako,namaanisha jaribu kubeba zawadi ya pongezi na usiache kuwajulisha wengine wanaomfahamu Papaa!!

Haitakuwa siku ya kawaida kwa hakika maana Papaa ni baadhi ya vijana nguli ambae tayari alikuwa kwenye kundi la ma-senior bachelors na sasa rasmi anaanza kuaga aga kundi hilo....na hata harusi yake itakuwa mwishoni wa October, kama hakutakuwa na badiliko lolote basi itakuwa 26TH OCTOBER.. hivyo mwenye macho na asome na kuelewa!!!

Mimi binafsi kwa niaba yangu mwenyewe na kwa niaba ya Blog hii na wafanyakazi wote wa Chavala Ideas Platform ninatamka baraka nyingi kwa rafiki yangu mkubwa na pacha wangu Samuel pamoja na Shemeji yangu,his wife to be ....Mungu awaonekanie katika kila hatua ya michakato hii mpaka hapo watakapooana!!!
Na kwa hakika tuko bega kwa bega,naam tuko tayari kutoa mchango wowote ule wa hali na mali utakaohitajika ili kufanikisha shughuli hii,KWA HAKIKA NINAMKUBALI SANA PAPAA KWA JINSI ALIVYO NA ALIVYO MCHAKARIKAJI,HE IS AMONG MY BEST FRIEND IN TOWN!!!
Kwa wale msiomfahamu zaidi basi msiache kutembelea Blog yake kila siku
"samsasali.blogspot.com"

NA MWALIKO HUU NIMEUTOA KWA HIARI YANGU KWA NIABA YAKE,HIVYO KAMA UKIKWAMA AU UKIWA NA SWALI LOLOTE NAMNA YA KUFIKA HAPO KANISANI BASI USISITE KUWASILIANA NASI,NASI TUTAKUSAIDIA KUFIKA!!

+255 713 883 797
King Chavala-MC

#.....NI MARUFUKU!!!#(02)....Kwa Mwanaume Kufungua au Kupekua Mkoba wa Kike!!!


HABARI ZENU!!!!
Ni marufuku kwa kijana yeyote yule wa kiume au mwanaume kufungua au kupekua pochi au mkoba wa kike kwasababu yeyote ile hata kama ni rasmi,kama sio chini ya usimamizi na ruhusa maalum sana ya mwenye mkoba au pochi hiyo!!Ni tabia mbaya sana kupekua pekua either kutafuta pesa kwenye pochi ya dada yako au mama yako au kutafuta ushaidi wowote ule kwa pochi ya mpenzi au mkeo....Je unajua pochi au mkoba wa kike unabebaga vitu gani? Je unafikiri pochi ya kike ni kapu la sokoni au? Vipi kama vilivyomo humo vikikupandisha presha ama kukupofusha,nani atakusaidia? na utajiteteaje?...Vipi kama ukivunja vya kuvunjika au kumwaga vya kumwagika? Vipi kama ukikuta picha ya ndugu yako either mjomba au mzazi utafanyaje?
Kama vile ambavyo sio rahisi wewe kumruhusu binti kupekua wallet yako vivyohivyo na wewe heshimu yao...nimewahi kuona baadhi ya vijana na wanaume wakinyang'anya na kupekua kwa lazima mikoba ya wadada au pochi za wamama na kisha kuwatupia chini,nilikuwa safarini na niliumia sana....na siku moja nilikutana na rafiki yangu mmoja na nikataka kumpokea mkoba na akakataa kabisa na kunieleza mengi na hapo ndio nikakumbuka maonyo ya mama kuwa ni marufuku kubeba mkoba wa kike isipokuwa kwa kibali maalum tena mkoba wa mtu maalum kama vile mkeo au mpenzi rasmi!!
Yamkini unafanyaga haya lakini hujui kama ni tabia mbaya,na wakati mwingine huwa unadhani ndio kujali,basi nikwambie wazi kabisa....Ni marufuku,tena marufuku tena marufuku kabisaaaaa!!
ukome ukomae kabisa...na hii ni kwa faida yako kijana,carrying someone's handberg might be an attitude of a gentleman but "pekuling" and "tafutaing" is a habit of Wamataifa...sasa nimesema marufuku,kama unabisha unaweza kuendelea tu!
Hii ni marufuku maalumu kwa watu wenye akili timamu tu!!

@Kwa Hisani kuwa ya Chavala Ideas Platform <chavalamedia.blogspot.com> (c)2013