Niwape pole Watanzania Kwa Msiba Uliotupata kwa ajili ya Padri aliyepigwa risasi kule Visiwani Zanzibar. Wiki Iliyopita niliandika Papaa On Tuesday nikasema Kama hatuwezi Kuziba Ufa Tutaweza Kujenga Ukuta??leo tunashindwa kuwadhibiti watu wachache wanaofanya fujo kutowesha hii amani je kweli kabisa wakifanya fujo nchi nzima hawa ndugu zetu tutaweza kweli wazuia?
Nakumbuka mwaka 2010 tulishuhudia tukio la Ki-historia kuhusu ndugu zetu wa Chile ambao walikaa ardhini kwa muda mrefu lakini hatimaye walifanikiwa kutoka. Katika story ya Chile nimependa story ya Jamaa aliyekuwa ameziba shimo la panya kwa kipande cha mkate na matokeo yake akaharibu. Katika wale waliokuwa ardhini kuna jamaa alikuwa na mke wake na kumbe jamaa pia alikuwa na nyumba ndogo ambayo alikuwa anaihudumia muda mrefu kwa siri. Siku ya kutoka kwenye shimo wanawake wote wawili wakawa wanamijihamu ya kumuona na kuwa nae teh teh yaani unaokoka na mauti tu unafikia kesi. Kuna siku tu ukweli utajulikana kwenye maisha yetu, tutajua chanzo cha vurugu hizi kweli ni uchinjaji ama kuna mengine, tutajua tu kuwa unamwibia mwajiri wako, tutajua tu wewe sio mwaminifu kwenye ndoa yako watu watajua tu wewe sivyo hivyo unavyoonekana.
Kwenye maisha yangu nimejifunza kufanya kazi na watu wengi sana hasa vijana na wanafunzi wakati mwingine watu wazima kabisa. Kuna wakati watu wazima Mitume na Manabii, Wakurugenzi na Wafanyabiashara tumewahi kukaa na kuongea mambo mbalimbali ya kimaendeleo kwa ajili ya huduma