Tunakila
sababu ya Kumshukuru Mungu kwa ajili ya siku hii ya leo ya Jumanne ya
kwanza kwenye nusu ya pili ya Mwaka 2013, mwaka umeisha ingia nusu wenye
kumaliza vyuo wameshamaliza, wenye kuendelea wanaendelea wenye kusoma
wanakazana, wenye mipango ya biashara wanakazana, wenye kuanzisha
familia nao wamo wapo pia ambao mpaka sasa hawajajisoma wapo wapo tu
yamkini wala hawajui kama na Obama alikuwepo nchini kwetu.
Miaka
michache iliyopita niliwahi kuwa na Supervisor Mchina ambaye tulikuwa
na kawaida ya kukutana Dept yetu na ku-plan mambo ya wiki na pia kupitia
report za utendaji kazi. Ninakumbuka siku moja tukiwa kwenye kikao
alichora duara mbili moja ikiwa kubwa na nyingine ndogo ikiwa ndani ya
ile kubwa. Namkumbuka Mr. Charles Guo aliniambia duara la nje linaitwa
"Uwezo Halisi" na duara la ndani linaitwa "Uwezo wa Sasa". Tofauti ya
Kile unachokifanya sasa na Kile unachoweza Kukifanya sasa kipo kwenye
kitu kinaitwa "Kuamua". Nakumbuka alitumia mfano huo wakati tunaongea
issue za Performance Management alisema Watu wengi sana wanafanya mambo
mengi sio katika Uwezo wao halisi, Uwezo walionao kutenda ni Mkubwa
zaidi kuliko kile wanacho kifanya na kinachotofautisha kile
wanachokifanya sasa na Kile ambacho wanaweza kukifanya kinajengwa na
tofali kubwa lenye kuitwa "KUAMUA KUFANYA". Kuamua kufanywa kunaletwa na
Kichochezi (motivation) ama Catalyst ama sababu ya mtu kufanya ndio
maana kwenye makampuni kuna incentives mbalimbali ili kuchochea uwezo wa
wafanyakazi kwenda extra mile.
Wiki
hii katika Ujio wa Rais wa Marekani nimekumbuka sana mfano huu wa
Supervisor wangu kuwa mambo mengi sana ambayo tunayafanya sasa kumbe
tunaweza kufanya zaidi ya pale tunapofanya ambapo ndipo kwenye uwezo
wetu halisi iwapo tu TUTAAMUA kufanya kikamilifu. Wiki hii nimeshuhudia
jiji la Dar-es-Salaam likiwa safi na likiwa halina foleni zisizo na
sababu, barabara za katikati ya Jiji zinapigwa deki usiku na Mchana,
Jiji limekuwa safi na Salama likarudisha maana halisi ya Jina tulipopewa
na Sultan kutoka Oman kuwa ni "Haven Of Peace" ni "Bandari Ya Salama".
Nimeona Watu wakilindwa usiku na Mchana kila kitu kimekaa kama
kinavyopaswa, wamachinga wameondolewa kwa nguvu kupisha Obama apite,
Barabara ya Ubungo pale kwenye Mataa ilikuwa na Makorogeshi ya Kutosha
pametengenezwa usiku na Mchana taa zinawaka vizuri kumbe uwezo wa
kufanya tunao sana iwapo tu tutaamua kufanya sisi kama Watanzania pasipo
ujio wa Obama.
Kinachofanywa
na Serikali ya Tanzania ni Reflection ya Maisha halisi ya Watanzania
kama sio Waafrika kwa Ujumla. Nakumbuka Wakati ninasoma mpaka Chuo Kikuu
ile wiki ya Kuelekea kwenye Mitihani ndipo unaona watu sasa ndo
wanashika vitabu kisawasawa kumbe unajiuliza swali kwanini mtu anakesha
namna hii kumbe alikuwa hajaamua kusoma, kama angeanza semester wakati
inaanza yamkini maisha yake ya kusoma yangekuwa yako mbali uwezo na upeo
wake ungekuwa wa kutisha lakini ajabu ng'ombe analishwa siku ya mnada.
Sisi ni watu ambao kwenye nyumba zetu kuna vyombo ambavyo havitumiki
mpaka waje wageni, hata kama mtakuwa hamna wageni miaka 800 lakini kuna
glass ziko kwenye kabati, kuna sahani ziko kwenye kabati ambazo wenyeji
hawazitumii mpaka aje mgeni utashangaa mgeni akija nyumbani ndipo siku
hiyo mtakunywa na soda, ndipo siku hiyo mtatumia sahani nzuri, ndipo
siku hiyo mtapelekwa kuoga mchana, ndipo siku hiyo utaona mpaka goti la
mkeo ama mama akiwakaribisha wageni kwenda kuchukua chakula ajabu ni
kwamba Mgeni ama wageni wakisha ondoka tunarudi katika maisha yetu yale
yale ya sahani za plastiki na soda za sikukuu kumbe kuna siku tukiamua
kama familia tunaweza kula kama kuna wageni na hakuna madhara.
Ninakumbuka
enzi hizo ninasoma shule ya Msingi ilikuwa siku kama kuna wakaguzi
wanakuja ama mgeni fulani kututembelea siku hiyo bustani zote ndipo
zitatifuliwa, zitamwagiwa na kupendeza, kwaya ya shule itafanya mazoezi
ya nyimbo za kumpamba mgeni rasmi mpaka atajiramba kwa sifa, tabia hii
ipo kwenye nyumba zetu za Ibada na Makanisa penye ugeni tutafanya zaidi
ya kawaida hata sare tutashona, tabia hii ipo kwenye maofisi yetu, tabia
hii ipo kwenye familia zetu, zipo kwenye mahusiano ya boyfriend na
girlfriend na wachumba uwezo wa kufanya zaidi ya kile unachofanya sasa
na kuzorotesha ndoa yako upo kwenye KUAMUA. Kwneye maisha yetu ya
kawaida pia kuna watu ambao hawavai vizuri mpaka wawe na ugeni
hawasafishi vyumba vyao mpaka siku akisikia anatembelewa, hawabadilishi
mashuka na mapazia mpaka uwepo ugeni haya mambo ndiyo ambayo yapo kwenye
Jamii yetu tofauti ya kile tunachokifanya sasa na Uwezo wetu wa kufanya
upo kwenye Kuamua.
Kila
mtu anaujua uwezo wake wa kufanya zaidi ya kile anachokifanya sasa
lakini tatizo hujaamua kufanya, yamkini unaimba, yamkini ni mwandishi,
yakini unasoma, yamkini ni Mwajiriwa ama Mwajiri kile unachokifanya kwa
sasa kama ukiamua kikweliii ukaweka miguu yote ndani ya hicho
ukifanyacho basi ungekuwa mbali kupita maelezo. Inawezekana unachukulia
pouwa kile unachokifanya kwa sababu hujaamua kwenda extra mile, assume
leo ukaamua ubadilike ubadilishe aina ya huduma unayofanya, ukaamua leo
upate feedback ya kile unachokifanya uone watu watakuambia nini yamkini
unafanya kitu ambacho kinakuharibia biashara yako, yamkini unaweza ukawa
unafanya jambo chini ya kiwango ambacho wateja wanategemea
ukijichunguza kiukweliii unaweza kufanya zaidi ya hicho unachofanya. Leo
hii ukiamua ufanye kwa uhalisia wako uwezo wako wa juu kabisa kufanya
unadhani utakuwa wapi, leo hii nikaamua kusaka news kwa uwezo wangu
kikweliii ninaweza kuwa na gazeti la Gospel Today, leo hii ukaamua
kuboresha ndoa yako kwa uhalisia wake utafurahia ndoa yako, ukiamua leo
kuongea na Wateja unaowafikia kwa biashara ama huduma yako unadhani
wataongea namna gani yamkini kuna kazi umewahi fanya ukaharibu na yule
uliyemfanyia amekuwa wakala wa kusambaza uharibifu wa kile ulichofanya
kwenye kazi yake, yote yawezekana kwenye maisha UKIAMUA.
Tofauti
ya waliofanikiwa na kwenye maisha na wale wasiofanikiwa ipo kwenye
KUAMUA. Wengi wetu tumebaki kuwa wachambuzi na wakosoaji na sio watu
wenye kuamua, wengi huwa wanasisimka wakisoma Papaa On Tuesday lakini
kasheshe iko kwenye Kutendea kazi. Yesu akasema anaheri yule anayesikia
na Kutenda. Upo hivyo ulivyo kwa sababu ya aina ya maisha uliyoyaamua na
siku ukiamua kufanya utashangaa kwanini ulichelewa kufanya maamuzi
sababu kubwa Unaweza kufanya lakini yamkini hujaamua kufanya ingawa
unajua ndani ya Moyo wako UKIAMUA kikwelii kufanya unaweza kufanya na
kubadilika. Yamkini umekuwa ukitamani kubadilika tabia fulani kwenye
maisha yako lakini umekuwa ukiindekeza ili uendelee kuwa nayo huku
ukitambua fika tabia hiyo ndiyo imekuwa kikuharibia kila siku kwenye
maisha lakini hujaamua tu kubadilika ukiamua inawezekana.
Hatma
ya Maisha yako yanategemeana sana na MAAMUZI unayoyafanya kwenye
maisha, ukiamua kubadilika utaona mabadiliko ukipotezea mabadiliko
utajipoteza mwenyewe, ukitazama duara lako kubwa la uwezo ulio nao
halifanani kabisa na kile ambacho unakifanya na unajua UKIAMUA
inawezekana tatizo halipo kwenye kile unachokifanya tatizo lipo kwenye
Maamuzi yako ya kuamua kufanya kwa utashi wa ndani kabisa.
Kuna
bloggers wengi sana bado hawajaamua kufanya, kuna wafanyabiashara
wakubwa sana wenye mafanikio wanaogopa kufanya, kuna presenters wazuri
sana lakini hawajaamua kufanya kile walichoumbiwa kufanya sababu ya
wasiwasi wa ndani,sababu ya maneno ya watu, yamkini sababu ya kiimani,
ama una mashaka watu watakuonaje watakuchukuliaje utaendelea kubaki kama
ulivyo sababu tu hujaamua kuwa vile unavyotaka kuwa kwa kuangalia tu
mazingira ya nje, adui nambari one wa mafanikio yako ni nafsi yako
mwenyewe. Ukimtafuta mtu yeyote aliyefanikiwa kwenye maisha atakuambia
"aliamua".
Tofauti
ya Wewe na wale uonaoona wamefanikiwa ipo kwenye Kuamua, ukiamua kulala
njaa siku 7 ili kutimiza ndoto yako itakuwa, ukiamua leo kuacha tabia
za kijinga kwenye maisha yako utapiga hatua, ukiamua kutulia utaoa ama
utaolewa, ukiamua kukuwa kiufahamu ndipo utakapofanikiwa kumbuka kuamua
ndiko kutakutofautisha na wasio amua.
Amua Sasa.
Ze Blogger
0713 494110