Nina
Kila Sababu Ya Kumshukuru Mungu aliyetupa nafasi hii ya leo Kwa ajili
ya kuweza kulitimiza tena Kusudi la kuumbwa kwetu na kuwepo duniani.
Papaa
On Tuesday ya leo ni Tafakari ya rafiki yangu wa Siku Nyingi Mussa
Billegeya ambaye ni Mbunge Mtarajiwa wa Jimbo moja miaka michache ijayo
katika Kanda Ya Ziwa. Tafarakari hii aliitoa katika forum ya Marafiki
Huru.
Kuna
Msemo wa Kibiblia usemao kila jambo lina wakati wake, Naamini huu msemo
huwa uko sahihi kabisa. Lakini kifalsafa, Wanadamu huwa tunafarijiana
kwamba Ukiwa Hai Bado, It's Never Too Late!
Hivi Majuzi rafiki yangu Mussa akiwa Ofisini pale MANCON na Mkurugenzi Prosper Mwakitalima, wakiwa wanazungumza mambo mbali mbali ya maisha ikafika time ya kuongelea suala moja linahusiana na Kuoa. Prosper aligusia huo msemo, na kueleza kwamba hata kuoa huwa kuna wakati wake, na mtu asipooa wakati wake wa kuoa unapofika, inaweza ikamsumbua kuja kuoa baadaye - hata kama atakuwa anataka!
Juu ya Msemo huo ninajenga Papaa On Tuesday ya leo!
Ni kweli kabisa kwamba kila jambo lina wakati wake, NA KILA WAKATI KATIKA MAISHA UNA JAMBO LAKE! Tangu utoto hadi uzee. Ni muhimu sana kuelewa jambo la kila Wakati (na sio tu wakati wa kila jambo)!
Kuna namna nyingi sana za kutambua wakati wa jambo unapofika, na mara nyingi, watu wengi, huwa tunakuwa na bahati ya kufahamu kwamba wakati wa jambo fulani maishani mwangu umewadia, au basi, huwa tunaweza kufahamu kwamba Jambo la Wakati Huu ni hili! Kwa bahati mbaya sana, watu wengi huwa tunaona kama vile linalowezekana leo hata kesho litawezekana - KOSA!
Wakati wa jambo unapowadia, huambatana na mambo mengi ikiwa ni pamoja na Nguvu ya Kulitekeleza, Hamu ya Kulitekeleza, Msukumo wa Kulitekeleza, Akili ya Kulitekeleza, Mafunuo ya Kulitekeleza, Faida za Kulitekeleza, Watu wa Kukusaidia kulitekeleza, Kibali cha Kulitekeleza... n.k n.k. Hali hii hujitokeza kwa jambo lolote katika maisha pale wakati wake unapofika - liwe ni wazo la kusoma, biashara, huduma, kuoa/kuolewa n.k.
Ni Sawa sawa na Mwanamke Mjamzito unapofika wakati wa kujifungua haijalishi alikuwa anaenda salon, ama anaenda Kanisani Wakati Wa Kujifungua ukifika kuanzia akili na kila kiungo kinataarifa kuwa wakati wa ku-deliver umefika hata angekuwa anapenda chips mayai saa hizo hazina tena nafasi sababu wakati wa jambo kutokea umefika katika maisha.
Kwa Nini Watu Huzikosa Hizo Nyakati/Fursa?
Kama nilivoeleza hapo juu, watu wengi huwa wanapoona wakati huo umefika, huanguka katika mtego wa kudhani ni kawaida kwa huo wakati kufika, hivyo huo wakati hautaondoka mpaka WAO watakapofanya jambo husika.! Watu wengi huwa hawaelewi kwamba wakati wa kila jambo hupita ili kupisha wakati wa Jambo jingine! Linalowezekana leo, sio sahihi kudhani kwamba litawezekana HATA KESHO, Kesho inaweza kuwa ni wakati wa Jambo lingine! Kwa watu wengi, pale wakati unapofika, huwa hawapendi kufanya haraka kulifanya jambo husika kwa sababu, wengi, huwa wanapenda kwanza KUU-ENJOY huo wakati ambao wanakuwa wanayaona mafanikio yao waziwazi vichwani na ndotoni mwao, hivyo hawaoni sababu ya kufanya haraka KUFANYA KWELI....
Ngoja-ngoja yao huendelea mpaka wakati wa jambo unapopita, huku wao wakiamini kwamba wakati huo hautaondoka KWA SABABU HAWAJAFANYA - KOSA!!!! Wakati huwa haumsubiri Mtu, Mtu anapaswa kwenda na Nyakati!
Ni kitu cha hatari kudhani kwamba kwa sababu leo unajisikia nguvu, msukumo, hamasa na una fursa ya kufanya jambo, ukadhani kwamba hali hiyo itaendelea siku zote - la, Hasha! "Kesho" unaweza ukaamka na ukashangaa ile nguvu, msukumo na hamasa uliyokuwa nayo jana imepotea ndani mwako, zaidi tu kwamba umebakia na kumbukumbu ya picha nzuri ya vile ambavyo hali ingekuwa iwapo ungelikuwa umechukua hatua na kufanya jamvo husika!
Nini Huwa Kinatokea Pale "Wakati Wako" wa Kufanya Jambo Unapokupita!
Kwa kawaida, mtu anapopitwa na wakati wake wa kufanya jambo hubaki na picha nzuri na "ladha" ya lile jambo ambayo aliipata wakati lilipomjia au wakati wake ulipokuwa umefika. Mtu hubaki akijifariji - nitafanya tu, nitafanya tu, kwa maana tayari nilishapata picha na mpango wa namna ya kufanya!!! Ndio maana kuna tahadhari kubwa sana ya Wadada ama Wakaka ambao wakati wa Kuoa ama kuolewa Ulipofika wakadhani bado wanamuda basi ule msukumo nao ukaisha ndio maana unaweza kuta mtu anabaki kusema tu enzi zangu ilikuwa a,b,c enzi zetu a,b,c ndio maana unakuta mtu ana kazi nzuri, ana mshahara mzuri ana maisha mazuri unashangaa kwanini huyu mtu hatafuti mwenza, kumbe ule msukumo wa kufanya ulishapita. Huwezi kuwa kijana siku zote wazazi wetu wengi wamebaki na story tu enzi zetu bana, enzi zetu bana basi na huo wakati nasi utatukuta ambapo watoto wetu watashangaa kwanini hatukununua viwanja kwa ajili ya miaka 10 ama 20 ijayo, watasema baba au mama ulikuwa wapi wakati wenzako wananunua??kila siku tunasema tutafanya kesho ama mwezi ujao mwisho wa siku hatufanyi. Lakini anapokuja kutaka kujaribu, hushangaa jinsi ambavyo jambo lile lile ambalo juzi alikuwa analiona rahisi sana, leo linaweza kuwa gumu mno, zito mno, lenye kukatisha tamaa na kuanza hata kushawishika kwamba yawezekana yale matokeo mazuri na faida aliyokuwa anaidhania juzi labda haikuwa sahihi au haikuwa kweli! Mtu huanza kujifariji "Labda zilikuwa ndoto tu za mchana" au kama sungura "Sizitaki Mbichi hizi" wakati akiwa anakata tamaa na hata kuamua kuliacha lile jambo kabisa!
Kama ni Biashara, mtu hushangaa vile inavyoweza kuwa ngumu, wakati mwingine akijihisi kwamba hana mawazo mazuri au uwezo wa kuifanya, japo ni majuzi tu alikuwa anaiona kwamba ndiyo inaweza "kumtoa" kimaisha! Kama ni Kuoa/Kuolewa, mtu huweza kushangaa ghafla akaanza kuona kama vile Hakuna Mtu Anayefaa Kumuoa, kama Vile yeye hajakakaa kikuoa-oa vile (au ki-kuolewa-olewa vile); Anazidi kuona kama vile Hakuna watu wenye Sifa za Kuwaoa au wa Kumuoa yeye n.k. Kumbe???/ Kwenye Biblia tunasoma habari ya Mtu mwenye Kupooza ambaye alikaa kwenye birika miaka na miaka na Kila Mara Malaika alikuwa anakuja kutibua maji ndani ya kisima hicho anayekuwa wa kwanza kuingia yeye anakuwa mzima. Swali la Kujiuliza huyu kilema aliyekaa zaidi ya miaka 30 pale pembeni ya birika kweli kabisa alikuwa serious kupona??au alikuwa ana enjoy kuwepo pale, sababu hata Yesu alipomuuliza Wataka kuwa mzima akaanza story nyingi kuwa hakuna wa kumsogeza hakuna wa Kumsaidia. Mara nyingi sana tumekuwa tukilaumu wengine ndio wametusababishia hali tuliyonayo kumbe wakati ulipokuwa umefika hatukuwa tayari kwenda na wakati huo. Kwenye Kiingereza wanasema Golden Chance Never Come Twice. Nilisema wiki iliyopita miaka 10-15 ijayo utakuwa ukijilaumu kwa mambo ambayo ulitakiwa uyafanye leo ukadhani bado una muda. Uzee hauna taarifa, utu uzima hauna hodi ikilala ukiamka utu uzima huu hapa. Wazazi wanakaa na watoto wao kila siku ghafla wanashangaa watoto wamesha balehe ama vunja ungo still wao hata kiwanja hawajanunua. Wiki iliyopita niliandika "Kama wengine Wanaweza Kwanini Wewe Usiweze" kuna watu ambao session hii kwa maana ya majira haya wanajisikia kabisa kufanya jambo fulani la kimaendeleo lakini wamejawa na woga wa kuamua. Hata siku moja Woga hawezi kukupa maendeleo kwenye maisha. Mara 2 kwenye maisha yangu baada ya kumaliza shahada yangu ya Kwanza nilijiunga na Masomo ya Masters ajabu nikakosa amani kabisa ya ndani ya kusoma nika Postpone mwaka ukaja Mwaka uliofuata Siku soma tena baada ya kuingia class siku ya kwanza. Kila mwanadamu ana "inner voice". Sema kwa kuto kujua utasikia tunasema, Unajua nilisikia kakiktu ndani ama machale yalinicheza, ndio maana asilimia kubwa ya watu waliowahi kutapeliwa ukiwauliza mpaka unatapeliwa ulikuwa hujui??atakuambia kuna kitu nilihisi nikapuuzia. Kuwa makini sana na nyakati tulizonazo maana kila Jambo Lina Majira yake na Kila Majira yana Mambo yake.
MALAIKA AKITIBUA MAJI, USIENDELEE KUJIULIZA NINI CHA KUFANYA, ZAMA UPONE, IKIKUPITA MWAKA HUU, UNAWEZA KUSUBIRI HATA MIAKA 40...!!!
Think Differently and Make a difference.
Papaa
0713 494110
samuel_sasali@yahoo.com
Facebook. Samuel Sasali
Tweeter: Samsasali
Sype: Sasalijr.