Katika
kabila letu la Wanyasa, chakula cha asili cha kikabila ni ugali wa
muhogo pamoja na dagaa kutoka Ziwa Nyasa. Kwa mnyasa kupata chakula cha
namna hii basi unakuwa umemfikisha nyumbani kabisa kuliko kumpa chipsi
mayai au kitimoto na ndizi. Nilipokuwa kijijini wakai fulani niliona
jinsi mihogo inavyokaushwa, akina mama wa Kinyasa watajihimu asubuhi
kuimenya mihogo hiyo na kuiloweka kwa muda kisha kuwekwa juani ili iweze
kufaa baadae kwa kutwangwa kisha kupatikana unga wa muhogo wenye
kupikwa ugali hupatikana. Kuna familia zingine ukifika wakati wa jioni
huanua mihogo hiyo kwa kuiweka ndani kuhofia isiharibiwe na wanyama ama
hata kuibiwa pia maana ndo deal kwa familia zilizokuwa zinaaminika kwa
uchawi walikuwa wanaacha tu anayeiba yatamkuta ya kumkuta. Siku moja
nikamuuliza Marehemu Babu yangu "Kwanini Wengine wanatoa Mihogo kuingiza
ndani"?akaniambia kule kijijini kuna msemo wanautumia "mwanga wa
mbalamwezi haukaushi muhogo". Nilitamani kufahamu maana ya msemo huo
wenye kubeba maana kubwa sana nyuma yake.
Kuna
mambo ambayo kwenye maisha huwezi yabadili ni kama kutaka kulazimishia
mwanga wa mbalamwezi ukaushe mihogo, mihogo yake ni jua. Kuna watu wana
tabia ya kulazimishia kufanya mambo wasiyo na uwezo nayo. Yaani unataka
kufanya mambo ili watu wakukubali kuwa wewe mambo safi, unataka watu
wakuone na wewe uko juu una Samsang Galaxy wakati matumuzi yako ni
kupiga simu na kutuma SMS, unapiga picha event moja kesho una delete
picha hizo hizo kuweka event ya pili. Kwenye vikao vya harusi walizojaa
marafiki zako unatoa ahadi kubwa kubwa za harusi uonekane na wewe mambo
safi. Kuna mambo ya mbalamwezi kuna mambo lake jua ndo yanaenda.
Kwanini
unataka uishi zaidi ya vile ya ulivyo, kwanini unaishi maisha ya
kujitahidi??kwanini usiishi vile ulivyo kwani unapoteza nini unapokuwa
unaishi maisha yako ya kawaida. Hii tabia ya kutembelea kwa watu
kishaukakuta wenzio wana flat screens na wewe ukataka, ukakuta wana Sub
Woofers za Ukweli mwisho wa siku na wewe ukataka, Ukaenda kwa watu
ukakuta wana Kengere na wewe ukataka, ukakuta mtu ana BlackBerry na wewe
unajinyimaaaaaaaaaaaaaa eti na wewe uonekane upo kwenye Class kama
uwezo wako ni kutoa mwanga basi usitake kukausha mihogo kuna mambo
hayawezekani kwa sasa wala baadaae kwanini uyalazimishie?
Kizazi
chetu kimekuwa na changamoto sana eneo mojawapo lenye kuleta changamoto
ni kuoa na kuolewa. Unakuta saa nyingine kuna watu wanawafukuzia watu
mpaka wanakera, na siku hizi wanawake wenye uwezo wamekuwa ni sababu ya
kunyang'anya wanaume wa wanawake wasio kuwa na uwezo na wanaume wenye
tamaa wamejikuta wakidondokea kwenye mikono ya wanawake mabaradhuri.
Fedha ina ushawishi, fedha inatakatisha, fedha ni jawabu la mambo yote
sababu ya uwezo wa mwanamke kuweza kumudu kununua mambo yanayoweza
mfanya mwanaume aonekane nae katika jamii wamejikuta wakiacha mapenzi ya
kweli na kuingia kwenye tamaa, kuna rafiki yangu amehongwa gari, gari
kabisaaa lakini jamaa hana uhuru kabisa, kuna rafiki yangu amehongwa
chain ya 1.5 Milioni na Blackberry juu lakini anafungwa kupita mbwa wa
kizungu, inakufaidia nini kupata kila kitu na huku unapoteza mpaka uhuru
wako wa kucheka, unayemcheka fulani unaulizwa, unapomtazama mtu mara
mbili unaulizwa why?ni mara kumi kuwa na simu ya kitochi na kubaki na
mapenzi ya kweli. Kuna wanawake na wanaume wako tayari kufanya chochote
wanachoweza kutimiza tamaa zao za mwili, unaweza kupewa nyumba bure,
unaweza kupata gari bure, unaweza kupewa investment bure lakini huwezi
kupata amani ya kweli na uhuru wa kweli for free, kama unajua uwezo wako
kutoa mwanga usitake kukausha mihogo.
Heshima
ni kitu cha bure sana, lakini nani anataka kutunza heshima yake, rafiki
yangu aliwahi niambia "Papaa tangu nimeanza kutunza heshima haijawahi
nisaidia". Kwani unataka utunze heshima ili iukusaidie?kuwa na heshima
ni msaada mkubwa sana kwenye maisha, kujiheshimu, kuheshimiwa,
kushemiana ni jambo ambalo naona sasa linapoteza mkondo wake watu
wanakuambia its a matter of time itashuka leo kesho watu wanasahau, leo
unafanya jambo la kusikitisha jamii lakini kesho heshima inarudi mjini,
katika kila uovu kuna mtu wa kukutia moyo. Mwenye mbili havai moja, na
mwanga wa mbalamwezi hata siku moja hauwezi kausha mihogo, lina heshima
yako ili uheshimiwe.
Kufikiria
kutumia mwili wako kupata kazi, kufikiria kutumia mwili wako kupata
gari ama nyumba basi jiandae tena kutumia mwili wako kupanda cheo,
jiandae mwili wako kupata nafasi ya kwenda kusoma, jiandae kutumia mwili
wako ili usipunguzwe kazini, jiandae kutumia mwili wako kupata hela ya
mafuta, jiandae kutumia mwili wako kufanya service ya gari, jiandae
kufanya chochote kutumia mlango ulioufungua kwenye maisha yako, kama
unajua wewe ni mbalamwezi usitamani kazi za jua kila jambo lina makusudi
yake hapa duniani.
Kila
mtu atavuna alichopanda haijalishi unapanda hadharani ama gizani,
mchana jua humulika na usiku mbala mwezi hutoa mwanga. Mwanga wa
mbalamwezi haukaushi muhogo.
Think differently and make a difference
....//Papaa
0713 494110