CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

Breakthrough Conference Kuanza Rasmi Leo...Kawe Makuti



Lile Kongamano Kubwa lenye jina la "Kongamano La Mpenyo" linatarajiwa kuanza rasmi leo katika Kanisa la Kawe Makuti chini Ya Apostle Onesmo Ndegi...

Akiongea na Chomoza Pamoja na blog Hii, Apostle Ndegi amesema Kongamano hilo litahudumiwa na watumishi Wa Mungu Kutoka Ndani na Nje Ya Tanzania. Kongamano hilo linatarjiwa kuanza rasmi tarehe 25 Mpaka Jumapili nani ya Kanisa la Hilo.

Campus Night 2013 Ndani Ya Mikoa Minne



Ile Event Kubwa ya Kujumisha Wanafunzi wa Tanzania almaarufu kama Campus Night mwaka 2013 itafanyika kwenye Mikoa Minne chini ya Coordination ya Kanisa la VCCT na Makanisa Shirikishi katika Mikoa husika.

Mchungaji Dr. Huruma Nkone aliongea na Blog Hii pamoja na Kipindi chako Nambari One Chomoza Ya Clouds Tv kuhusiana na Maandali ya Campus Night 2013 itakayofanyika Dar, Kilimanjaro, Arusha na Mbeya

KULA MATUNDA SIO LAZIMA USHAURIWE NA DAKTARI!!!

Habari zenu!
Watu wengi sana hawana tabia ya kula matunda ipasavyo! wengine huona kama ni chombezo mezani,wengine ni ziada na wengine ni mpaka daktari aseme!

KULA MATUNDA KUNA FAIDA NYINGI SANA,HIZI NI BAADHI YA HIZO CHACHE;
a.Matunda mengi ni dawa, maana yana virutubisho asilia
b. Matunda yana Vitamini nyingi sana na madini, na matunda mengi yana Vitamin C
c. Matunda hususani yale yenye nyuzi nyuzi (rouphages) husaidia mmeng'enyo na uyeyushaji wa chakula mwilini.
d. Matunda huongeza damu mwilini na kusafisha pia mfano ndizi huongeza vitamini K ,ambayo inasaidia sana kwa WALE WENYE MATATIZO YA KUTOKA DAMU PUANI.
e. Matunda yenyewe ni mlo wa kutosha kabisa na kwa mujibu wa wataalamu mtu anaweza kuishi kwa matunda tu na bado akawa na afya njema kuliko mtu anayekula vyakula vingine!
Punguza kula mafuta mengi na sukari kwa mbadala wa matunda!

Kuna matunda mengine watu wanaona ni kama viungo tu lakini nataka nikwambie matunda na mbogamboga kama vile NYANYA,KAROTI,LIMAO ni matunda safi sana na viungo kama TANGAWIZI,VITUNGUU SAUMU NA VITUNGUU MAJI unaweza kula kwa kutafuna maana husafisha mwili na damu sana!

UNAPOKULA MATUNDA UNAKULA VITU ASILI,DAWA ASILI,MADINI NA VITAMINI ASILI,MAJI NA SUKARI YA ASILI....Hivyo kama huna utaratibu wa kula matunda basi anza sasa!!!

Huna haja ya kunywa chai asubuhi kila siku,wakati mwingine anza na matunda tu na hata unapolala usijichindilie na chakula kingi kizito,unaupa mwili kazi ngumu na kisha unalala, hivyo utashangaa unamka mchovu na kitambi kinatoka bila mpangilio!!

ANZA SASA KULA MATUNDA KWA AFYA YAKO!!!!

Niulize nikushauri
0713883797

Papaa On Tuesday...Usione Ukadhani

Ikiwa ni siku ya pili tangu nilipoutangazia umma rasmi kuwa sasa nimeamua kuvunja Ukimya na Kumtangaza Mchumba wangu ninayetarajia kufunga nae ndoa nimekwisha anza ku-experience maisha mengine tofauti ya yale ya kabla ya Jumapili. Ni Kwa neema ya Mungu leo nimefika hapa.

Leo nimejisikia vema tukatazama kile ambacho Diwani ya Mloka tulikisomaga kinaitwa Usione Ukadhani. Watu wengi sana wakiona jambo ama wakimuona mtu wanadhani kwenye Kiingereza wao wanasema "dont judge a book by its cover" ingawa kuna mdhanio mwengine ni wakweli mwingine vema ukasikia ama ukapitia ilikuweza kuwa na majibu sahihi. Mara nyingi sana jamii imekuwa na wepesi wa kufikia hitimisho ya kile ambacho wao wanakidhani ni sahihi kumbe sio. Mara kadhaa kwenye maisha yangu kuna watu waliwahi  nidharau kuwa siwezi kufanya kitu kutokana na muonekano wangu kumbe sio kabisa usione ukadhani.

Kutokana na mfumo wa maisha ya Watanzania na Waafrika kwa ujumla mambo mengi sana tunajifunza ukubwani tukiwa wadogo ni familia chache sana zinatoa mwanya wa mtoto kuji express feelings zake na ndoto zake na tangu utotoni tulifundishwa kuwa mambo mengi ni mabaya pasipo kuambia ubaya wake na tulifundishwa kukosea jambo lolote ni vibaya zaidi ndio maana kuna watu wakifeli mitihani wanaamua kujiua sababu kwenye maisha yake ameambiwa kufeli ama kushindwa jambo ni kitu kibaya. Ukiwa mtoto ukiongea ongea sebuleni na kupiga piga meza ukawa unaimba nyimbo za kitoto utaambiwa kelelee, nyamazaaa basi unakuta unapoteza confidence na saikolojia yako inaambiwa hutakiwi kufanya jambo hili mbele ya wazazi. Ukiwa mtoto ukasema "mama mie mchumba wangu mtoto wa Mzee Charle" usiku huo huo utachapwa fimbo kuwa umeanza kuharibika matokeo yake saikolojia ya ufahamu inaambiwa kuwa kupenda mtu ni vibaya na kwa kuwa umri wa kutoka nyumbani kwa wazazi kwetu sisi ni pale unapoweza kujitegemea unajikuta mambo mengi sana unajifunza sio mbele ya wazazi ama watu waliokulea ndio maana kuna mambo mengi sana wazazi wetu hawajui kama tunajua kwa ufahamu wao wazazi wanadhani watoto wao hawajui kumbe watoto ndio wamegeuka waalimu.
Nakumbuka zamani enzi zetu wakati tunakuwa kabla video hatujaja kuangalia sebuleni baba na mama wanakuwa wanaingalia kwanza kama kuna sehemu sio nzuri basi alikuwa anakaa na remote control ikifika lile eneo anazima anapeleka mbele kidogo kisha tunaendelea. Kwa sisi watoto watundu tangu zamani tulikuwa tunamaswali hivi pale anapopeleka mbele kuna nini?basi wengine walienda extra mile tukavizia wakati baba na mama hawapo tukawasha tukaangalia mwanzo mwisho ila baba na mama wakirudi wanajua hatujui kuna nini. Tofauti na Kizazi cha sasa ambacho wao hutazama kanza kupitia mitandao kisha kama watatazama na familia watoto ndo wanawaambia wazazi sasa "baba hapo forward kidogo sio pazuri" sasa najiuliza mtoto ndo anamwambia baba aforward kwa manufaa ya nani baba ama yeye mtoto??Usione Ukadhani watu kizazi hiki hawajuio kwa taarifa yako watu huwa wanaambiana.

Usione leo mtu hana chochote ukadhani ataendelea kuwa kama alivyo, watu huwa wanabadilika kwenye maisha priorities nyingi sana za wanaume huwa zinabadilika pia kutokana na umri aliokuwa nao, majukumu aliyokuwa nayo na Marital Status yake pia. Kabla ya kuwa na mpango wa kuoa kwenye maisha atakuwa anawaza kula bata atakuwa anawaza kukutana na Jack, Rose, Mwamntumu, kwenda movie, kwenda mlimani City, akishaanza kuwa na mahusiano majukumu yanabadilika harusi ikikaribia kama mimi utakuwa unawaza Shella la Bibi harusi, Kiatu Cha Bibi harusi, Suti ya Bwa. Harusi Ukumbi, Mc pole pole akili inaanza kuwaza majukumu. Ukishapata familia sasa na mtoto utaanza kuwaza Pumpus za mtoto, mara bima ya afya ya Mtoto, ada ya shule, Mke nae avae,afanya kazi, mtaanza kufikiri Miradi ya kifamilia,mtawaza kujenga usione leo mtu yupo yupo ukadhani ataendelea kubaki alivyo. Akili hukuwa kwa kuzoeshwa ingawa inawezekana sio wote lakini Kibongo bongo tunakuwa kwa kukosea sana ukubwani hata namna ya kuishi na mume na mke tangu utotoni akili imejizoeza kujificha ficha hata kama ni halali.
Jambo usililolijua ni kama usiku wa giza unaweza ukaona leo mtu amekuwa na mafanikio ukadhani yalikuja kirahisi rahisi kwenye maisha. Kuna watu ukisikiliza hatua zao za maisha unajiona kabisa wewe unadeka unataka mafanikio wakati hata kushinda njaa mchana tu huwezi kuna watu mpaka leo wametoboa kwenye maisha wanahistoria ambazo ukizisikiliza kuna nyakati waliomba usiku usiingie sababu hawana sehemu za kulala walitamani kama kuna mahali wanaweza uza njaa basi wangeuza kwa bei yoyote ili wasiwenazo milele kuna watu walishinda njaa si kwa sababu walitamani kufunga la hasha hakuna chakula usione ukadhani kila kitu kinakuja bure. Tamaa mbaya ya mafanikio ya haraka haraka ndio inayopeleka mtoto wa masikini akiwa form four anawaza kuwa na blackberry yuko tayari kufanyiwa chochote apate blackberry used. Usione Mtu ukadhani kila mtu anaendesha gari leo amenunua kihalali wengine wamenunua ka kudhalilisha maisha yao ili waonekane. Usione leo watu wameajiriwa kwenye makampuni makubwa ukajua wameshinda interview za kazi walishinda interview za ngono ndio wakapataKama kuna kitu Watanzania kinatutesa ni Ulimbukeni. Usine Ukadhani.

Usione wanandoa wanaongoza kuingia kwenye ukumbi wa harusi wako pamoja wamevaa vizuri ukadhani hilo tabasamu ndilo walilokuwa nalo wakiwa nyumbani. Ungepata fursa ya kujua undani wao ndipo ambavyo ungefuta dhana yako ya kuolewa ili na wewe tu uwe na mume sababu uliosoma nao wameolewa, uliocheza nao wanawatoto, ungefuta dhana ya kuoa sababu mke wako ana umbile la namba 8, mke wako aonekane ana makalio, ama mweupe au mweusi kwani unaolea jamii ama unaoa kwa utashi wako mwenyewe wengi waliokimbilia ndoa kwa sababu za kijamii wamejikuta wamekwama na kama ingekuwa dini yetu ya Kikristo inaruhusu talaka wengi wangechukua talaka pamoja na kuto kuruhusu watu wanatoka wamechokaaaa. Rafiki yangu mmoja alinichekesha akasema kuna wengine wamefika stage wanaombea basi hata wafe ili wapumue maana hawa wanandoa wakiwa mbele za watu full matabasamu full kushikana mikono lakini wakiingia tu kwenye gari kurudi nyumbani maisha ya Chui na Paka yanarudi kuna wanawake leo wanatamani  wangeolewa na wanaume masikini wachume pamoja kuliko waliowachagua wanaume wenye uwezo wamejikuta wanaambulia majuto kuliko furaha usine ukadhani.

Usione watu wanavaa tai na sketi nzuri wanafanyakazi kwenye maofisi ukadhani wanafuraha na kazi zao, shida ndio zinasababisha waendelee kwenda ofisini wengine hawana hata mishahara wana mikopo kupita Serikali ya Tanzania, kuna watu wanaenda maofisini hawana hata mikataba ya ajira zao yaani hawana hatma ya kesho yao itakuaje kiajira, we usione watu wanavyojiupara na kula chips kuku ukadhani mambo yao safi, simu zao nzuri hazina vocha, mabegi yamejaa vipodozi vinavyokaribia kwisha, nguo wamekopa pale kwa mdada anayepitisha ofisini kwao kwa muonekano wa njee utadhani wanaraha kuliko wewe, ukitaka kujua uhondo wa ngoma uingie ucheze usione ukadhani ndugu yangu.

Maisha kila siku ni kujipanga unaweza ukadharaulika leo ukajipanga ukashangaa wale aliokuwa wanakucheka ndio baadae wanakupongeza watu huwa wanakawaida ya kudharau watu usitegemee kupendwa kabla ya kudharauliwa kwanza. Mtu mmoja anayekutia moyo wakati wa shida ni muhimu zaidi kuliko jeshi linalokushangilia baada ya ushindi. Usione ukadhani wewe jipange ili kuweza kusonga mbele. 

Think Differently and Make A difference.

Usione Ukadhani.

Samuel Sasali
0713 494110
Facebook: Samuel Sasali
Skype: SasaliJr

Samuel N. Sasali HAS THOUGHT DIFFERENTLY and HE HAS SHOWN A DIFFERENCE!!!!

Hello friends,fans and readers!!
I do believe that we are all doing well and we are fine!
Well then i am humbly inviting you very specially to CHAVALA MEDIA Blog
When the Sasali was vowing to MILEMBE

Zoomed edition
.....HE WAS CARRIED JUST LIKE A PIECE OF SOMETHING!!!!

Today i have a very testimonial post/news about a SAMUEL SASALI a.k.a Papaa /The Blogger/ The MC na may be you know him as TV Presenter,Motivational Speaker and May be Event Organizer but all in all he is the same guy, He is the thinker, ambitious and very unique friend of friends, allow me to declare my interest,Yes He is my Twin!


In most of his writings and presentations he has this say "THINK DIFFERENTLY TO MAKE A DIFFERENCE"...I real admire this say and i understand it more than what it says....Yes! among many things he has said and done this one was proved his uniquness!!
 ....Here Milembe was also vowing to Sasali....
 Samuel Sasali used that opportunity to give special offering to God, and he did that for two reasons and that are getting a beautiful girl and having another job as TV presenter...this also imply that the guy thought differently and surely the mass was very differnt!!!
Senior Pastor of VCCT, Rev.Dk Huruma Nkone with couples

Being a first born of a Long time pastor Rev.Nathanael Sasali and a brother of Pastor Mathew Sasali who got married 8 years ago with three children now, being MC of very many events and being involved in a number of relationship THEN last sunday we have all witnessed a DIFFERENT THOUGHT that is not relating to any of anybody and it has never seen anywhere else......YES THE BROTHER HAS FINALLY ENGAGED A BEAUTIFUL LADY,Doctor by proffessional and polite by nature; MILEMBE JOHN MADAHA.

Sometime back Papaa ever told me that....WHEN A POPULAR DATES....It is a challange! and from experience he said he will write a book soon after getting marriage and i have real realized that it is not as simple as someone can imagine....i am in the same trailer and i always pray that i don't mess on this matter.
....I WILL BE WAITING FOR THE BOOK FROM SASALI NOW!!!
 Special Lunch at Kawe beach together with friends!!

The way Papaa has configured and potrayed himself in his community, the way he has contributed his efforts and finances to others' visions and the level of his committment to his friends  and how he has touched people's hearts....it is what many friends and other people has experienced on sunday!!

Very many people came from different angles of the city and for sure the church was packed, great celebration, massive cameras of private and public mass medias and prolonged busy scheduled continuous party
Samuel intruducing Milembe at home party

The Event took place At VICTORY CHRISTIAN CENTRE TABERNACLE (VCCT) soon after the Sunday Mass.
 and THERE after  friends came together at Kawe beach for Lunch and because Samuel is the man of the people,then he just ate his lunch and went for live interview at DPC where there was an event "YOUTH TALENTS EXPLOSION CONCERT" and then he went to moderate another FUNDRISING Oriented Concert by Hananasifu Orphanage Centre Children who were also launching their DVD,at Victorious Church around Mabibo External then afterward there was a special dinner party at his father's house at Tegeta.

Hope now you can understand when i say this guy is unique is always thinking differently....can you imagine his younger brother married 8yrs back but still he had cataut to assist him dearly, The day of his engagement he has very many events to attend and made it!

I ARGUE ALL READERS AND FRIENDS TO SUPPORT THIS BROTHER VERY CLOSELY AND LOVELY AS HOW HE HAS PROVEN WORTHY INTO YOUR ISSUES...THE JOURNEY HAS JUST BEGAN AND THERE ARE LOT OF ISSUES TO DO FOR HIM....HE IS FAMOUS AND HE DESERVE THE BEST FOR WHAT HE HAS CONTRIBUTED INTO THE SOCIETY SO FAR.

Finally i would wish to encourage you all to support the work, the ministry and talents of my twin in any way you can but willingly...you can choose to be his friend in SOCIAL MEDIA, you can choose to Watch his Tv program "CHOMOZA" via Clouds TV at every sunday on 1800hrs, all read his educative posts in social media profiles or in blogs such as 
http://samsasali.blogspot.com http://chavalamedia.blogspot.com
And may be attending "FRIENDS ON FRIDAY"(FoF).

I HAVE WRITTEN ALL THIS TO YOU VERY CLEARLY AND CONFIDENTLY AS I AM VERY CLOSE TO HIM AND I EVEN MODERATED THE DINNER PARTY IN TAGETA, THE WEDDING IS ANTICIPATED TO BE ON 26TH OCTOBER 2013....All other detailed informations to be communicated to you via different medias including this one!!!


>>>BUT YOU CAN CHOOSE TO PLEDGE/SEND YOUR CONTRIBUTION NOW TO 0713494110
IN ORDER TO RESERVE YOUR SEAT or TO SHOW YOUR LOVE!!!
Samuel & Milembe
......THIS IS HOW THE DAY WAS CONCLUDED AT TEGETA!!!!

Thank you all and i wish him all the best in every single step untill marriage and ever
 BY
+255 713 883 797
King Chavala-MC

#....NI MARUFUKU!!!#(03).....Kuvaa nguo zenye maandishi ya AJABU AJABU!!!

#....NI MARUFUKU!!!#
Ni marufuku kwa mtu yeyote mwenye akili timamu,mstaarabu na mwenye future na anayejiheshimu kuvaa fulana/nguo au niseme T-shirts ambazo zina maneno asiyofahamu maana yake au hata kama ana fahamu maneno yasiyo faa....yaani wewe unanua tu bora ni Tshrt,zingine zina matusi aitha kujitusi mvaaji,au wengine wanaosoma au hata kuaibisha jamii yako.....Nimekutana na mtu amevaa tshrt imeandikwa..."I am proud of My Virgin Grandma" na mtu yuko happy tu dah! inawezekanaje Bibi yako mama yake na mama yako awe bikra hata sasa kama sio matusi hayo? 

MAMA YAKO ALIZALIWAJE NA BADO BIBI YAKO AKABAKI BIKRA KAMA SIO USHIRIKINA HUO????

 Unajua maana ya haya maandishi kwa tshrt hii?
Au mtu unavaa tu?

Kwanini basi usiulize kwanza kabla au mara tu unaponunua?\

Na watu wengine wala hawatakwambia utashangaa wanakucheka tu,kila ukivaa na wewe unaweza kudhani wanakufurahia kumbe kejeli!

JE UNAJUA KAMA NGUO KAMA HIZI ZIMEBEBA MAANA NA KUPIGIA DEBE MASHOGA NA WASAGAJI?

Nimeona nyingi sana lakini masikini wengine huwa hawajui maana yake hivyo wanavaa tu, na sehemu nyingine wazazi wengine huwanunulia watoto wao dah! haiwezekani mtu mzima akavaa Tshrt inayomtambulisha kama "kahaba mpole" mbona zipo nguo kibao zenye maneno mazuri tena ya lugha yetu ya kiswahili kwanini kuvaa kitu unachokielewa....najua unanielewa na yamkini umewahikuona na wewe mtu akiwa amevaa kituko....kama unakumbuka basi tupia mfano wa uliyowahi kuiona na useme ...HATA HII MARUFUKU KABISA!!!
ANGALIZO:Kwa wale wanaopenda kuvaa hivyo hivyo makusudi kabisa basi yamkini wana maana zao ambazo wangependa watu wajue bila wao kuongea kwa mdomo....hao ni issue nyingine,lakini wewe sio mmoja wa WASIOJITAMBUA NA KUJIKUBALI SAWASAWA NA UUMBAJI WAO,basi nimesema marufuku kabisa!!!

>>>Hii ni kwa ajili ya watu wenye akili timamu tu wanaojitambua na kujiheshimu tu.....vigezo na masharti kuzingatiwa!!

@Kwa hisani kubwa ya Chavala Ideas Platform <chavalamedia.blogspot.com>

NAMNA MBALIMBALI YA KUPIKA WALI!!!

Habari zenu!
Najua watu wengi sana wanapenda wali kuliko chakula kingine chochote na hata wale wasioa na kuolewa basi pishi lao kubwa ni Tambi na Ubwabwa na wale wa mikoani(nje ya Dar hupendelea kupika ugali)
Yamkini wewe unajua kupika wali na Rice cooker basi!
Lakini mchele una aina nyingi sana za kuupika kama vile wali wa maua,wali uliokaangwa na mbogamboga na kutaja aina chache;
Naam hivi ndivyo asemavyo
Chef Issa Kapande
KWA WALE NDUGU ZANGU MLIOKO UGHAIBUNI MCHELE ASILIMIA 90% HAUNA LADHA NA HARUFU NZURI KAMA TULIOUZOEA NYUMBANI CHUKUA UJANJA HUU ILI UFANYE WALI WAKO UWE WA KUNUKIA NA LADHA SAFI KABISA



Karoti iliyokwaruzwa vizuri, nyanya na vitunguu vilivyokatwa katika umbo dogo dogo rahisi kwa kuiva


Mchanganyiko wa karoti, kitunguu na nyanya katika kikaango chenye mafuta na moto mkali pika kwa dakika 5 tu usiache ziive sana kisha changanya wali wako ambao umeshaiva.



Huu ni wali ulioiva na ukachanyanywa na mchanyiko wako wa caroti, utapata harufu nzuri na ladha nzuri sana kwa kupata harufu na ladha nzuri zaidi unaweza ongezea pilipili hoho au girigilani ( Corriender leaves).


Mahitaji
720gram caroti iliyokwaruzwa

480gram Basmati rice ( mchele wa pishori) iliyopikwa

2 vitunguu vikubwa vikate katika size ndogo

1 Nyanya moja kubwa ikate katika size ndogo

1 fungu la majani ya girigilani

2 kijiko kikubwa cha chakula karanga zilizokaangwa kwajili ya kupambia

3 kijiko kidogo cha chai cha mafuta ya kula

Chumvi weka kulingana na ladha na mahitaji yako

Jinsi ya kuandaa:

Pasha moto sufuria lako au kikaango weka mafuta kisha weka vitunguu kaanga kiasi tu visiungue au kua na rangi ya kahawia vilainike tu inatosha.

kisha weka nyanya zikaange mpaka zichanganyike kabisa zitengeneze rojo rojo
Kisha weka caroti zilizokwaruzwa katika mchanganyiko wako kaanga na zichanganyike vizuri

Kisha weka wali wako wa basmati ulioiva katika mchanganyiko wako wa karoti changanya vizuri kisha mimina majani ya girigilani na changanya pole pole mwisho kabisa weka karanga zako ambazo zimekaangwa vizuri kama unatumia.

Mapishi haya unaweza tumia mchele wa aina yeyote ile sio lazima mchele wa basmati 
Source; http://activechef.blogspot.com

Papaa On Tuesday…..Unao Uwezo Wa Kuchagua Cha Kufanya Lakini Huna Uchaguzi na Matokeo Ya Kile Ulichokichagua Kukifanya.

Tukiwa bado katika Maombolezo ya Kupoteza ndugu zetu katika Mkoa wa Arusha kwa sababu zinazosadikika ni za kisiasa nachukua fursa hii kuwapa pole ndugu zetu wote ambao wamefariki lakini pia na wote waliojeruhiwa hasa hasa Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha rafiki yangu na mtumishi katika Shamba la Bwana Bw. Amani Golugwa pole sana na “majanga” ya Kisiasa. Nimeamini kweli tunao uchaguzi wa nini cha kufanya lakini hatuna uchaguzi wa kuzia matokeo ya kile tulichokichagua kinapotokea. Ukichagua Siasa basi matokeo ya Siasa ujue huna maamuzi nayo.

Wengi tuko leo hivi tulivyo kama matokeo ya kile ambacho tulikichagua katika maisha, na wakati huo tuliona sie ndio wenye mana kuliko wengine wote wakati wa kuchagua lakini hatukujua kuwa kile tulichokichagua hatuna uwezo wa kuhimili matokeo yake ya kwenye maisha. Wengi wetu wakati tunahimizwa kwenda shule tuliendekeza ubishoo na usharubalo, tulikuwa na uwezo wa kuamua either kusoma ama kuendekeza ujinga wa makuzi wakati huo kwa kufuata mkumbo wa mambo yaliyokuwa yakiendelea. Pengine kila ukikaa unajicheka kwa kile ambacho ulikichagua wakati huo na ukasahau methali ya Majuto ni Mjukuu waliponena wahenga, tulijiona sisi ndio tunaojua kuliko wale waliokuwa wakituasa na kutuhusia. Leo tumekuwa na akili tunatamani zile zama tulizokuwa tunakula chips na kuvaa raba za gharama na kuendekeza ubishoo zirudi tena ili tufanye kweli, lakini wapi kila jambo na majira yake. Wengine tunasoma Elimu za Watu wazima sit u tulikuwa na tatizo la ada kipindi hicho la hasha ila tulipokuwa nacho tulitumia na kilipoisha tukajijutia kwenye maisha.

Kuna mdada mmoja rafiki yangu anaishi kwenye mateso makubwa ya ndoa yake na amebaki kujutia maamuzo aliyoyachagua kuyafanya kisa na mkasa anasema hakujua, kama angelijua angechagua kuendelea na maisha yake kwanza ndipo achague kuolewa akiwa na akili timamu. Majanga mengi sana ambayo tunapitia kwenye ndoa na mahusiano ni kutokana na maamuzi yetu ya kukurupuka, maamuzi yetu ya kujiaminisha kuwa tuko sahihi kuliko wengine matokeo yake tunabakia kufa na tai shingoni. Kwani uwongo??ukikaa mwenyewe hujiambia kuwa laiti kama ungelijua usongechagua kuolewa ama kuoa Fulani kisa na mkasa matokeo ya kile ulichokichagua kwenye maisha. Kuna wengine walitaka kuolewa so kilichotokea wakabeba mimba wakidhani maisha yale ya honey baby and sweetheart yataendelea, kongwa walilojitishwa na nira walizojifunga wamebaki kulilia moyoni, mkiwaona barabarani na kwenye facebook utadhani ni ndoa ya mfano kumbe si lolote si chochote kila mtu analala chumba chake nyumbani hakuna furaha ambayo inadhaniwa ipo wakiwa nje ya mlango wa nyumba yao wakikaa wenyewe wanatamani sana kurejesha maisha siku ambazo walikuwa wanacheka na kwenda kula bata na kuitana majina ya mahaba, leo yamebaki kuitana “wewe”, “Nanii”, “Stella”, “Sultani” dry dry dryyyyyyyyyy. Lady Jay d anasema anatamani kuwa kama zamani lakini ndo zama zimeisha tena maisha yamebaki kuishi kwenye matokeo yake.


Kuna Ofisi Fulani nilifanya kazi zamani kuna jamaa alicha kazi baada ya kupata kazi sehemu nyingine kwa ahadi ya project mpya alipohama kwetu akaenda kwingine ambako huko project ikakosa hela akabaki mtaani akajuta sana kwa uamuzi wake wa kuacha kazi alikuwa na muda wa kuchagua kuacha kazi ama kuanza upya sehemu nyingine matokeo ya maamuzi yetu mengi hayamo ndani ya matakwa yetu. Unaweza kuacha kazi sehemu moja ili ufanye kazi kwingine ukashangaa ulikokwenda ndo unapunguzwa wewe ama unahama nyumba moja kwenda nyingine kumbe unakokwenda ndo kuna zoezi la upanuzi wa barabara unabaki kusema ng’ombe wa masikini hazai. Wengine wamepata watoto mapema si kwa sababu walikuwa wanapenda kuzaa bali bali kilichotokea “ajali” ikasababisha waanze kuitwa “mama” ama “baba” wakati wa kudungunyuana walikuwa wanasikia raha ila ilipofika ujauzito wengine wakasema wakatoe ama wakatoa ujue ulikuwa na uchaguzi wakati wa kuamua lakini ukasahau unawajibika na matokeo ya kile ulichokiamua kwenye maisha yako.


Kuwajibika na matokeo ya yale tunayoyaamua ni wachache wetu wako tayari unapotaka kufanya maamuzi kwenye maisha jua kabisa wewe unawajibika na matokeo ya maamuzi unayochukua kwenye maisha. Kila ambacho unakichagua kukifanya jua kina matokeo na uwe tayari kupokea matokeo ya kile ulichokichagua kukifanya kwenye maisha.

0713 494110

HATIMAYE SAMUEL SASALI a.k.a PAPAA ATAKUWA AKITANGAZA UCHUMBA RASMI TAR 23/06/2013 PALE VCCT!!

Hello marafiki na wasomaji wote wa Blog hii!!
Leo ninawaletea habari njema  zilizoambatana na mwaliko  maalum kwa watu wote wenye mapenzi mema na Samuel Sasali, The Blogger, MC,Mzee wa Ideas mengi ambaye mara zote husema Mungu alimnyima urefu akamjalia Mdomo (kuongea sana) na kukosa aibu pia!!!
Baada ya sarakasi za kutosha za kutafuta mwenzi wa kumfaa hatimae pacha wangu amegota na kumpata mlimbwende wa pekee aliyewashinda wanawake zaidi ya Bilioni 4 duniani na kuwa wa pekee...Usukani mdogo unaoendesha Merikebu kubwa!!!
 Ndio ni binti huyu Dk Milembe John Madaha ambaye ameteka moyo wa kaka Mkubwa na kwa huyu Papaa amegeuka rapper,mwana mashairi na mtiifu sana!!
Kama una kumbukumbu nzuri, blog hii imewahi kum-ZOOM kijana huyu kama mmoja ya vijana wanaopaswa kuigwa na vijana wengine,fuata link umfahamu vema;

.http://chavalamedia.blogspot.com/2012/08/salaam-leo-katika-kipengele-hiki.html

Basi habari njema ndio hii, jumapili hii wewe na wenzako wote ambao ni marafiki wa kweli Samuel Sasali au ni msomaji  wake wa Papaa On Tuesday au ni Mwanachama wa Marafiki Huru au ni mpenzi wa Friends On Friday au umewahi kufundishwa na yeye popote pale,shuleni, chuoni au kanisani au hata kama amewahi kusherehesha shughuli yako yeyote ile..basi sasa ni saa ya kumuunga mkono kwa kumaanisha!!

Ni jumapili hii ya tar 23/06/2013 kuanzia saa nne asubuhi pale Mbezi Beach A katika kanisa la VICTORY CHRISTIAN CENTRE TABERNACLE (VCCT),Unaweza ukapanda gari mpaka mwenge na kupanda usafiri wa kanisa unaondoka hapo tatu na nusu ama ukachukua bajaji mpaka huko kanisa la hema,au ukapanda gari mpaka kawe mwisho na kupanda bajaji pia mpaka kanisani au ukashuka Mbezi Tanki bovu na kuchukua bajaji au bodaboda mpaka kanisani...lakini kama unakuja na private car njoo na barabara ya Mwai Kibaki(zamani old bagamoyo road) kisha baada tu ya daraja utaona kibao kushoto kwako kama ukitokea mwenge then fuata njia hiyo kwa hakika huwezi kupotea!!

Ni marufuku kuja mikono mitupu na ni marufuku kuja peke yako,namaanisha jaribu kubeba zawadi ya pongezi na usiache kuwajulisha wengine wanaomfahamu Papaa!!

Haitakuwa siku ya kawaida kwa hakika maana Papaa ni baadhi ya vijana nguli ambae tayari alikuwa kwenye kundi la ma-senior bachelors na sasa rasmi anaanza kuaga aga kundi hilo....na hata harusi yake itakuwa mwishoni wa October, kama hakutakuwa na badiliko lolote basi itakuwa 26TH OCTOBER.. hivyo mwenye macho na asome na kuelewa!!!

Mimi binafsi kwa niaba yangu mwenyewe na kwa niaba ya Blog hii na wafanyakazi wote wa Chavala Ideas Platform ninatamka baraka nyingi kwa rafiki yangu mkubwa na pacha wangu Samuel pamoja na Shemeji yangu,his wife to be ....Mungu awaonekanie katika kila hatua ya michakato hii mpaka hapo watakapooana!!!
Na kwa hakika tuko bega kwa bega,naam tuko tayari kutoa mchango wowote ule wa hali na mali utakaohitajika ili kufanikisha shughuli hii,KWA HAKIKA NINAMKUBALI SANA PAPAA KWA JINSI ALIVYO NA ALIVYO MCHAKARIKAJI,HE IS AMONG MY BEST FRIEND IN TOWN!!!
Kwa wale msiomfahamu zaidi basi msiache kutembelea Blog yake kila siku
"samsasali.blogspot.com"

NA MWALIKO HUU NIMEUTOA KWA HIARI YANGU KWA NIABA YAKE,HIVYO KAMA UKIKWAMA AU UKIWA NA SWALI LOLOTE NAMNA YA KUFIKA HAPO KANISANI BASI USISITE KUWASILIANA NASI,NASI TUTAKUSAIDIA KUFIKA!!

+255 713 883 797
King Chavala-MC

#.....NI MARUFUKU!!!#(02)....Kwa Mwanaume Kufungua au Kupekua Mkoba wa Kike!!!


HABARI ZENU!!!!
Ni marufuku kwa kijana yeyote yule wa kiume au mwanaume kufungua au kupekua pochi au mkoba wa kike kwasababu yeyote ile hata kama ni rasmi,kama sio chini ya usimamizi na ruhusa maalum sana ya mwenye mkoba au pochi hiyo!!



Ni tabia mbaya sana kupekua pekua either kutafuta pesa kwenye pochi ya dada yako au mama yako au kutafuta ushaidi wowote ule kwa pochi ya mpenzi au mkeo....Je unajua pochi au mkoba wa kike unabebaga vitu gani? Je unafikiri pochi ya kike ni kapu la sokoni au? Vipi kama vilivyomo humo vikikupandisha presha ama kukupofusha,nani atakusaidia? na utajiteteaje?...Vipi kama ukivunja vya kuvunjika au kumwaga vya kumwagika? Vipi kama ukikuta picha ya ndugu yako either mjomba au mzazi utafanyaje?
Kama vile ambavyo sio rahisi wewe kumruhusu binti kupekua wallet yako vivyohivyo na wewe heshimu yao...nimewahi kuona baadhi ya vijana na wanaume wakinyang'anya na kupekua kwa lazima mikoba ya wadada au pochi za wamama na kisha kuwatupia chini,nilikuwa safarini na niliumia sana....na siku moja nilikutana na rafiki yangu mmoja na nikataka kumpokea mkoba na akakataa kabisa na kunieleza mengi na hapo ndio nikakumbuka maonyo ya mama kuwa ni marufuku kubeba mkoba wa kike isipokuwa kwa kibali maalum tena mkoba wa mtu maalum kama vile mkeo au mpenzi rasmi!!
Yamkini unafanyaga haya lakini hujui kama ni tabia mbaya,na wakati mwingine huwa unadhani ndio kujali,basi nikwambie wazi kabisa....Ni marufuku,tena marufuku tena marufuku kabisaaaaa!!
ukome ukomae kabisa...na hii ni kwa faida yako kijana,carrying someone's handberg might be an attitude of a gentleman but "pekuling" and "tafutaing" is a habit of Wamataifa...sasa nimesema marufuku,kama unabisha unaweza kuendelea tu!
Hii ni marufuku maalumu kwa watu wenye akili timamu tu!!

@Kwa Hisani kuwa ya Chavala Ideas Platform <chavalamedia.blogspot.com> (c)2013

Chavala Ideas Platform presents "TANZANIA GOSPEL SINGERS' BREAKFAST"....3rd Episode!!

HII NI FURSA MAALUM KWA WAIMBAJI WOTE WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA, MNAKARIBISHWA KWA CHAI YA ASUBUHI JMOS YA TAR 15/06/2013 PALE VCC-VICTORIA KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI...NJOO UMSIKILIZE MWALIMU NA MWANAMUZIKI SAMUEL YOHA AKIONGEA KWA KINA KUHUSU MUZIKI...HAKUNA KIINGILIO!!
KWA MAELEZO ZAIDI 0713 883 797
AU TEMBELEA http://gospelstandardbase.blogspot.com