CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

....MPAKA IDEA HII ITAKAPOELEWEKA....


HARAKATI ZA KUKUZA VIPAJI HALISI HUSUSANI

VICHEKESHO VYA KIKRISTO ZINAENDELEA KUZAA

MATUNDA PAMOJA NA CHANGAMOTO ZILIZOPO!!!!

Salaam!

Ni muda sasa umepita tangu harakati za kutambulisha Christian comedy Tanzania zianze,matunda na matokeo mazuri yanaonekana japo bado hakijafikia kile kiwango ambacho kinapendeza mbele ya macho ya dunia. Ingawa bado ninaamini kuwa mwisho mwa mwaka huu 2012 tutakuwa tumepiga hatua ya maana.

Nimeweza kufikia mikoa mingi ya Tanzania japo kufanya kidogo utambulisho na kuangalia mazingira ya vipaji vya huko,mpaka leo ninaandika hapa imebaki mikoa minne tu ya Tanzania Bara,ambayo ni Ruvuma,Rukwa,Mara na Kagera na Pemba kwa Zanzibar ambapo bado sijafika, lakini naamini kabla Ya June 2013 nitakuwa nimefika kila sehemu ya Tanzania na kurudia tena kwingine!
Shauku yangu ni kuona watu hususani vijana wanaishi maisha yao mazuri,wakila matunda ya vipaji vyao,lakini pia jamii ikielimika na kuburudika kwa vipaji hivyo na si kukereka tu!

Kanisa linalo jukumu kubwa sana kuhakikisha vipaji na vipawa vinavyoibuliwa na kukuzwa kanisani haviendi kupata umaarufu duniani kwa mwavuli wa ulimwengu bali vibaki kuwa utukufu kwa Mungu kila vinapoonekana na kutambuliwa.....sio sifa kwa kanisa kumsikia msanii wa ulimwengu akisema mimi nilianzia kanisani kuimba kwaya au Sunday skuli,sasa unajiuliza kilichomkimbiza ni nini? Kwanini ameacha kuimba kwaya? Majibu yake yatakuwa rahisi tu.....HUKU NDIO KUNALIPA!!!!

Katika harakati zangu nimegundua mambo ambayo ni muhimu kusema wazi wazi kabisa, kanisa lina shida,tena shida kubwa na shida yenyewe inatokana na mambo kama haya;

a.    Vijana wengi hawajitambui wala kujielewa,sasa usipojielewa vema hauwezi kuwa na utulivu mzuri,utakuwa unatangatanga huku na kule ili mradi tu ubahatishe njia ya kutokea na ndio unajikuta watumishi wa Mungu wanahaha mpaka wanavamia pesa chafu!

b.    Viongozi wengi wa makanisa hawana dira na visomeo vya alama za nyakati,wengi wako na mitindo ya kizamani na hawawezi kukubali haraka,kulea wala kukuza vipaji vya vijana wa kisasa...na ukweli ni kwamba vijana wa leo wana namna yao ya kuwakilisha vipaji vyao.

c.    Kanisa halipendi kuwatia moyo kwa kulipia sawasawa thamani ya vipaji hivyo ili viendelee kukua kanisani, wengi huwabana vijana na kuwapa majukumu mengi,hata wakaacha mambo yao mengine lakini mwisho wa siku wanaambiwa ni huduma na hivyo wanaambulia hamna kitu....hivi uliwahi kuona wapi watu wanalipia kodi za nyumba zao na kula huduma?

d.  Wakristo wengi hawana uzalendo na vipaji vya nyumbani kwao,yaani vipaji vya makanisani; wengi wanapenda kazi za duniani zaidi na hata kama ni za dini basi ni zile za kutoka nje. Na wakristo ndio  wanaongoza kwa kudurufu au kuburn kazi za wasanii, hivi kama sisi wenyewe tusipowaunga mkono kwa kununua kazi halisi, ni nani atakayefanya hivyo?

e.    Na jambo lingine ni wale wasanii wenye majina makubwa kutowapa support ya kutosha wale wasanii wanaochipukia, wasanii wakubwa wamekuwa wakiwatisha makanisa machanga kwa kudai malipo makubwa kila wanapoitwa au kualikwa na wengine wamekuwa wakisemwa kwa tabia mbaya wanayoionyesha mbele ya jamii kama vile kiburi,majivuno,majigambo na uasherati/uzinzi.

NI MPAKA MATATIZO HAYA YATAKAPOPATIWA UFUMBUZI WA KUDUMU NDIPO FURAHA YA VIPAJI HALISI KANISANI INAKAPOKUZWA MARADUFU NA HII INAANZA NA KILA ALIYE MKRISTO...YAANI INAANZA NA WEWE!!!

Lakini bado nina imani kubwa kuwa tukiweka nguvu zetu za kutosha huko mambo yatakuwa mazuri tu! Kanisa lazima liiongoze nchi kwa kila kitu yaani kijamii,kisiasa,kiserikali,kiuchumi na kiroho.

Harakati bado zinaendelea na hazitakoma mpaka hapo nitakapoona Vipaji halisi vya Kikristo,hususani Ucheshi wa Kikristo unatambulika vilivyo.

Ninamshukuru Mungu sana kwani harakati hizi zimeibua vipaji vya maana na bado vingi vinakuja zaidi....yaani ninapoona kazi za Richard Chidundo; Gerald Mrema; Emmanuel Mathias Manu(MC pilipili); 1st Q dancers na wengine wengi hata wale ambao walikuwa kwenye secular na sasa wako huku kama vile Masanja Mkandamizaji,basi nafarijika sana na kutiwa moyo kuwa saa inakuja ambayo kila mkoa utajivunia vijana wenye vipaji katika maeneo yao huko.

Rai yangu ni moja tu....kila aliyeamua kumtumikia mungu kwa kipaji chake,basi na afanye hivyo kwa kumaanisha na kwa lengo la kuujenga ufalme wa Mungu na si vinginevyo....ubaya wala uchafu wowote usitajwe juu yako na ushirikiano na wenzako uzidi zaidi na zaidi,juu ya yote ujitahidi kujifunza kila siku ili ubunifu wako usipungue wala kuzoeleka.

Mungu wangu na awabariki,pamoja sana katika harakati hizi!!!

King Chavala
The great MC and Founder of Christian Standard and Stand Up Comedy in Tanzania