CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

Papaa On Tuesday...Hata Ukizima Mshumaa Wa Mwenzio Haufanyi Wako Uwake Zaidi

Ninakila Sababu Ya Kumshukuru Mungu kwa ajili ya siku ya Leo kwa Kuweza Kutupa tena Uzima katika Maisha haya tuliyo nayo. Kuna Kila sababu ya Kumshukuru Mungu,kuna rafiki yangu Zulfa alitoka kwenda Matembezi ya Weekend amepata ajali wamekata Mguu sasa ni Kilema. Hata kama hakuna aliyekufa ama kuwa kilema kuna Kila sababu ya Kumshukuru Mungu kwamba tunaishi.

Mwanamuziki Elton John akiwa na Bernie Taupin Mwaka 1973 waliuandika wimbo "Candle In The Wind" ukiwa maalum kwa ajili ya heshima ya Marehemu Marilyn Monroe. Maisha 


yetu ya kila siku kwenye dunia hii ni kama Mshumaa, Ka nafasi ulikonako hapo ofisini 
kwako ni kama ka mshumaa, sehemu ya biashara uliyopo ni kama ka mshumaa, maisha yetu

 ya kila siku ni kama Mshumaa ambapo mishumaa hii inatufanya kuwa nuru, Mishumaa hii 

inatufanya kufahamika na kukubalika kutokana na mwanga tunaoutoa, njia tunayoionesha

yenye kuleta mafanikio.

Ingawa Kila mtu ana mshumaa wake kuna wengine wamekuwa na jitihada mwamwi 

(Mwanzo Mwisho) kuhakikisha mishumaa ya wengine inazima ili ibaki peke yao kutoa 

mwangaza na kuonekana wao ni bora kuliko wengine. Kumulika kwako wewe na kutoa

mwangaza na kung'aa kwenye maisha kuna wanyima usingizi wengine, kuna wakosesha raha

 wengine, ukiuliza hasa kama kuna sababu ya msingi wala hakuna sababu ila tu yeye 

hafurahii mafanikio wengine wanayopata hata kama nae ana mafanikio lakini unakuta

 anahitaji zaidi. Maisha yenyewe haya yetu ya kila siku Unafukuzana na hela ya Unga, 

Ukipata hela ya unga unagundua Chumvi imeisha, unakimbiza hela ya chumvi ukipata 

umegundua pampass zimeisha kila siku ni mbio mwamwi lakini ajabu from no where kuna

 mtu hapendi mafanikio yako.


Kwa kadri ambavyo tumekuwa tukiwaponda wengine kwa kile wanachokifanya basi vivyo


 hivyo na sisi tumekuwa tupondwa mahala pengine kwa kile tunachokifanya. Kuna watu 

hawapendi mafanikio yako live live ama kuna wale wa Silent Killers ukipata tatizo ama 

baya likikufika wanakutana wanagongeana mikono wanasema "Tulijua hafiki mbali" wewe 

ni Mkristo au Muislam wa wapi unayefurahia kushindwa kwa Mwanadamu Mwenzio. Wewe 

umekuwa Mtu wa Kushangilia kwa matatizo ama kukwama kwa wengine??maisha ni 

Mzunguko zamu yako itafika tu.




Kwenye maisha nimekutana na Watu ambao bila sababu wananichukia, inawezekana hata 


wewe umekutana na watu ambao wanachukia mafanikio yako bila sababu. Akipatikana mtu

 akamuuliza pengine hata pasipo kufahamu akamuuliza "Inaonekena Stella biashara

 zinamuendea pouwa sana ndo maana ameweza nunua gari", basi huyu anayekuchikia bila

 sababu utadhani ndo ana majibu yako yote atasema "aaah wapi unadhani hela yake,

 kahongwa lile gari, umalaya tu hakuna kitu anafanya mjini.." huyu mtu anaongea sana

 negatives kuhusu wengine. Kila anachoulizwa cha kwako yeye anaponda mbaya anaongea 

negatives mwanzo mwisho, kama ni kazi ofisini anakuongelea vibaya mpaka wengine 

wanashangaa, anatamani kuzima mshumaa wako ili wake ubaki unawaka raha yake wewe

 ufukuzwe kazi abaki yeye ndo aonekane bora,ukiwa na tabia hiyo kwisha habari yako.


Kuna watu wanachukia mafanikio ya wenzao bila hata sababu, furaha yao wao ni kuona


 wenzao wana huzuni siku zote, ukikutana nao wanakupa pole mpaka machozi yanawatoka

 kumbe mioyo yao ina kung'ong'a, anachukia kila hatua ya maendeleo yako. Kwanini kuzima

 Mshumaa wa mwenzio ili uonekane wako ndo unawaka??maisha hayako hivyo, unaweza

 ukamfanyi mtu leo ubaya ili uonekane wewe ndo boss, unataka uonekane wewe ndo Alfa

 and Omega, jua kitu Kimoja wewe sio Mungu wa Kumpangia Mtu maisha yake inawezekana

 hujui kuwa unatumika kumuandaa hiyo unayomfanyia huyo mtu kuwa na future nzuri. 

Kumpiga teke Chura ni Kumsaidia Kuruka. Kama tunajisikia raha kuumiza mioyo ya watu ili

sisi tuonekane bora kuliko wengine. Kuna Wakristo kabisa lakini ni wanafiki wakubwa 

kutwa kucha kutamani wenzao wakwame ili wao waonekane bora zaidi.


Kwenye maisha tunayoishi nasema tena kumpiga teke chura ni kumsaidia kuruka kuna 

wengine wala hawajui kuwa wanatumika kuwaimarisha wengine kwa maneno yao, leo

 ukinisema pembeni kwa watu inakusaidia nini, kama kuna mtu unajua hafanyi vizuri kuhusu

 kitu fulani kwanini usimwambie??Kuna watu wao ni Ma-Master of everything kama redio

 moja maarufu hapa nchini wao wanajua kila kitu kwenye vipindi vyao. Tunatamani

 wengine wachemshe ili unachokifanya wewe kionekane kuwa bora. Huu sio Ukristo wala

 sio Uislam hata ma Ma-Budha hawafanyi hivyo ni Upagani wa hali ya Juu. Inakusaidia nini

 kumsema mtu kuzima mshumaa wa mtu wakati unajua Mshumaa wako hautafika mbali.

 Usilewe Sifa kwa sifa unazozipata leo, leo watu wanakushangilia sababu una hela ama una

 kipawa kila sifa iko kwako, kuna siku vitaisha kuna siku atakuja bora kuliko wewe kama 

wenzako walivyoachwa ndivyo ambavyp utaachwa, niliwahi kuandika Usitukane Wakunga

 wakati Uzazi Ungalipo. Usijione bora kwa Mshahara unaoupata kwa kazi ya sasa maisha ni

 kupokezana ndugu yangu. Mungu sio Filikunjombe mwenzako itafika zamu yake. Wewe 

wadharau watu sababu wewe unajiona bora kuliko wao, roho mbaya haojawai kupanda bei

 tangu imeanza kutumika zaidi ya kushuka bei, tafuta wenye roho mbaya kama wewe 

ambao kwenye maisha wamekuwa wakitamani wengine wasitokelezee wabaki wao kama

 miungu watu kama waliwahi kufika mbali, ukizima mishumaa ya wengine jua tu na wako

 utazimwa tena ghafla mno saa usiyodhani, maana kabla ya wewe alikuwepo mwengine

kama wewe.



Ipo haja ya sisi kama Vijana, Watanzania na Wakristo Kusaidiana, kuna watu wana mawazo

 ya ajabu sana wanaonaga eti ukimpa "deal" fulani eti atatoka, unaogopa kumtoa mtu??

unataka utoke peke yako basi wewe sio Mungu ukigoma kutoa watu utashangaa wanakupita

 wewe bado umesimama pale pale. Biblia inasema wazi ni heri Kutoa kuliko Kupokea,

 haijakataza kupokea ila heri ipo kwenye kutoa, Unavyotaka watu Wakufanyie kwenye

 Maisha Wafanyie wewe wengine, kama unataka Kutolewa kwenye maisha ukatoka, basi

 kwanza anza kusaidia wengine kutoka leo. FM Academia wana Chorus inasema "Aliyekupa

 wewe ndiye kawanyima wao, dunia mafungu saba" kuwa makini.


Think differently and Make a Difference, kumbuka Muosha huoshwa, Kila aliye mwalimu leo

 aliwahi kuwa Mwanafunzi.



Papaa Ze Blogger.

0713 494110.