Kuna utapeli fulani
unaendelea Tanzania na inaelekea wanaoufanya wamefanikiwa sana na wanaendelea
kufanikiwa kwani ni wa muda mrefu sasa. Nadhani matapeli hawa wanatumia ujinga
wetu maana sisi sio watu wakutafuta sana usahihi wa mambo kabla ya kusema au
kutoa maamuzi, pamoja na ujinga wetu wa kutaka kufanikiwa kwa haraka kwa njia
yeyote ile hata kama hatujafanya kazi na bila kutumia akili. Utapeli huu sio
mwingine bali ni ule wa wale watu wanaompigia mtu simu wakijifanya wanakujua
kabisa na wanaweza hata kukupa some backgrounds zako za kazi, ajira au elimu na
meninge hadi ukashawishika kuwa unayeongea naye ni mtu unayemfahamu/munayefahamiana
na hivyo kutokua na hofu na uhalisia wa anachokuambia. Baada ya hapo wanaanza
kukushawishi juu ya kuwasaidia kupata madawa ya kuhifadhi nafaka kwa madai kuwa
mawakala wao ambo wamekua wakizipata toka kwao wameanza kuleta uswahili hivyo
kwa vile unayeongea naye ndio anahusika na suppy, basi ameona ni vema akutumie
wewe “mpendwa anayekujua” ili angalau upate hiyo commission kubwa ambayo huwapa
ho mawakala na mugawane kidogo. Mara nyingi wanasema wanafanya kazi na shirika
la chakula duniani (FAO) au shirika la wakimbizi duniani (UNHCR) na wako
Kigoma.