CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

Papaa On Tuesday...Usipoziba Ufa Utaweza Kujenga Ukuta??


Ikiwa hang over ya Pasaka ikiendelea kwa baadhi ya watu wengine leo wameingia ofisini huku wamekunja nyuso zao walitamani leo iwe Jumanne Ya Pasaka ili wasiende maofisini lakini hata wangeweka mwezi wa Pasaka ajabu siku ya kwenda ungekunja tu uso wako.

Robo ya kwanza ya Mwaka imeisha tumeingia robo ya pili bado unamatumaini ama ndo unaona tarehe zinasogea sogea na unabaki hujielewi elewi??jipange aisee mwaka utaisha na mambo yatakuwa yale yale. Wahenga walisema usipoziba ufa utajenga Ukuta. Ni maneno ya hekima ambayo mababu zetu walituachia ajabu katika kizazi chetu watu wengi hawaijui hii wao wanajua tu methali za Kizungu, misemo ya mababu wazungu wakiamini ndio yenye maana zaidi.

Maisha ni muunganiko wa mambo mengi sana ambayo yanakujenga wewe kama wewe na yananijenga mimi kama mimi. Kuna mambo ambayo pole pole unayejenga ama unayafanya leo unadhani unaweza kuyamudu tu hata madhara yake hapo baadae. Unasahau kuwa tabia hiyo inatengeneza Ufa ambao baadae itakulazimu kutengeneza Ukuta. Gharama ya Ukuta haifanani kabisa na gharama ya kuziba ufa.

Yamkini wengine wamekuwa wakienda kanisani ama misikitini pale wanapojisikia kufanya hivyo kwao zile sio nyumba za Ibada ni nyumba za Msimu, leo mtu anakuja kesho anakuwa amechoka. Hakuna haja ya Kujiita wewe ni Mkristo wewe Ni Muislam safi wakati nyumba ya Ibada kwako ni kama Kituo cha Sensa mara moja kwa mwaka ama miaka mitano. Unaenda Kanisani ili Ukifa wajue wewe ni muumini wa Kanisa hilo??unaenda unapoenda ili upate mume ama mke??umewahi kujiuliza leo nafsi yako nani unayemtegemea katika kila unachofanya??unaamini una connections??unajiamini sababu ya mumeo ama mkeo ama kazi uliyonayo??Ukampuuzia Mungu kwa hayo unayoyafanya ukadhani wewe ndio nambari one sababu unapiga hela kila siku, nikukumbushe tena, amelaaniwa kila Mwanadamu anayemtegemea mwanadamu na kumfanya kuwa kinga yake, hivi umewahi waza huyo unayemtegemea mpaka unawadharau wengine siku akifa utakuwa mgeni wa nani??unadhani cheo ulicho nacho na nafasi uliyonayo ndio imekuwa tiketi ya kuwa fuska na kunyanyasa wengine??Chozi la Munyonge Malipo Kwa Mungu baba FM Academia huwa wanasema. Biblia iko wazi apandacho mtu ndicho atakachovuna. Ni heri ukajirudi leo maana gharama ya kujenga ufa uliouweka kwenye maisha na watu wanakuzunguka unaweza jengeka kuliko siku umepoteza kazi, ama umelazwa hospitalini hoi, au unayemtegemea kuwa ndo boss wako siku Mungu akaamua tu kukufundisha adabu wewe na watu wenye tabia kama yako, si unajua kila kifo cha Mbongo kuna kitu cha kujifunza??siku ya kufa haina taarifa uliza waliodondokewa na Ukuta pale town Posta Dar watakuambia.
Kuna tabia ambazo pole pole zinaendelea kwenye maisha yetu ambazo tunadhani madhara yake ni madogo hapo baadae na tunashindwa kujiuzia kwa sasa na tunasahau kuwa gharama ya kujenga ufa ni ndogo. Mara kadhaa nimekaa na watu ambao wanadai wameokoka na katikati ya mazungumzo wakatoa na matusi, mwanzoni nilijua utu wa kale bado unawasumbua wengine nikawasaidia na wengine sikuweza pata hiyo fursa. Lakini mwisho wa siku nikajiuliza huyu jamaa na hii tabia siku akiwa madhabahuni ghafla likamponyoka tusi akiwa ameshika Microphone itakuwaje??majuto ni mjukuu, na usipoziba ufa kuna siku itakugharimu kujenga ukuta. Kuna wengine kwa siri sana wamekuwa wakitoka nje ya ndoa zao, wengine imekuwa sio siri tena na wengi wameingia kwenye mateso ya ndoa wakiwa bado vijana sana. Nilipofanya utafiti wangu usio rasmi nikagundua wengi wao sio kwamba walikuwa hawahisi kabisa sio kwamba walikuwa hawajui kabisa ila hawakujua tatizo litakuja kuwa kubwa kiasi hicho by the way walijua wenza wao wataacha. We haijawahi kukutokea kwenye maisha mtu anakuomba msamaha mpaka analia kwa kosa alilofanya halafu baada ya siku chache anafanya tena kosa lile lile na anajuta vile vile mwisho wa siku anakuambia hawezi kuacha utafanyaje??siku muulize alianzaje anzaje??alianya pole pole ufa umebomoa tabia  njema sasa kazi ni kujenga Ukuta. Kuna watu wanatabia za Kujichua kwa ajili ya kujitimiza kimapenzi, unajua madhara yake hapo baadae ya Kimwili na Kisaikolojia??ndio maana kizazi chetu kimekuwa na changamoto kubwa sana ya Kutimiziana na Kutoshelezeana Katika tendo la ndoa, wanawake wengi sana wana suffer katika ndoa zao sababu ni wachache ambao wanafurahia tendo, wanaume wengi wako busy, wanaume wengi hawana uwezo wa kutimizia hitaji la wake zao, ukitazama hili kwa kina utaona lilianza kama ka ufa lakini wengine limeshabomoa ndoa nyingi sana.
Maumivu huanza pole pole kwenye maisha yetu na majuto ni mjukuu, wengi wanajuta kwenye maisha yao si kwa sababu ya yale waliyoyafanya hapo nyuma ila wengi wanajiuliza sababu ya kufanya, hujawaji kutana na mtu anajiuliza kwanini niliamua kufanya jambo fulani, why I decided to get marriage na huyu jamaa, najiuliza kwanini niliamua a....b...c, au wengine wanajiuliza Kwanini fulani kajiua, Kwanini fulani kajinyonga. Watu wengi huwa hawaangalii sana wanachokifaanya ila wanaangalia sababu ya kufanya kile unachotaka kukifanya. Kuna vijana wengi wanataka tu kuoa kwa sasa ama kuolewa umewahi jiuliza sababu ya wewe kutaka kuoa kwa sasa ama kuolewa??Sababu yako ya ndani kabisa ambayo ulikuwa nayo pengine umri umesonga, ama ulikuwa na maumivu ya nafsi ama ulikuwa umempenda mtu kwa sababu ya makalio yake na miguu yake basi jua jambo moja usishangae kwa kile kitakachotokea pale ambapo mambo yatakuwa yanajitokeza sababu maamuzi yale base katika tamaa na sio upendo utavuna sawa sawa na unavyopanda. Unajua level ya Kukinai mambo kwa wanaume wengi iko juu sana kuliko wanawake, unaweza kuta mwanaume anatazama taarifa ya habari baada ya dakika chache kesha badilisha stesheni, unaweza kuta mwanaume kabla ya Kukupata alikuwa simu, ma sms, ma appointment kibao baada ya kukupata mambo yooote ni kama sio yeye aliyekuwa anafanya hayo hapo kabla, kwenye yale makanisa yenye utaratibu wa kupiga magoti wakati wa Kusali angalia nani huwa wananyanyuka mapema kabla ya wenzao. Wengi wamekuwa wakidhani wanaume wana mapepo sio kweli kuna ufa umejengwa kwenye maisha ya watu wengi sana ambapo hata ukiwauliza hao wanaume wenyewe hawajui. Kwa sisi tuliojua na kuamua kubadilika tunazidi kujiimarisha katika hili maana Biblia yangu inasema Utaifahamu kweli na Hiyo Kweli itakuweka huru. Kama itakufaa daka kama haitakufaa potezea maana ufa kila mtu anaoujenga kwenye maisha yeye mwenyewe ndiye mwenye kazi ya kuujenga ukuta hapo baadae, ninachojiuliza ni kitu kimoja kama mtu aliona gharama kuziba ufa je ataweza kujenga Ukuta??

Ze Blogger
0713 494110
Facebook: Samuel Sasali
Twetter: Sam Sasali\
Skype: SasaliJr