CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

Papaa On Tuesday.....Kuelimika ni Kubadilika, Ujinga ni Kuamua

Zikiwa zimebaki siku 16 kabla ya Event Ya Friends On Friday Funga Mwaka yenye Jina la Extravaganza kufanyika pale Makumbusho, ninayo haja ya Kumshukuru Mungu kwa ajili ya Ulinzi wake, kipindi hiki cha Msimu wa Campus Night na shughuli zingine za Kijamii na Kitumishi nimekuwa nikitembea angani na barabarani lakini Mungu amekuwa Mlinzi Kwangu. Sina budi ya kusema asante kwa Mungu kwa Uzima na Afya na uwezo wa Kuwakilisha Papaa On Tuesday Kila inapofika siku ya Leo.

Tarehe 17 January, 2012 niliandika Papaa On Tuesday yenye heading Lile Ninalotaka Kulifanya Silifanyi, Nisilotaka Kulifanya Ndilo Ninalolifanya gonga hapa kama Hukusoma....http://samsasali.blogspot.com/2012/01/papaa-on-tuesdaylile-ninalotaka.html.
Mwaka wakati unaanza nilitoa tahadhari ya kuwa pamoja ya kuwa na Mikakati tuwe waangalifu maana yale tunayoyapanga mengi hatutayafanya. Jichunguze mambo mangapi ulipanga mwaka huu umeyafanya ukiacha yale yaliyoibuka tu na kukwamisha mipango yako ya mwaka huu. Zimebaki siku arobaini na moja (41) mwaka huu kumalizika jiulize swali kuna ulilofanya la kujivunia??
Ninakumbuka Miaka hiyo ya zamani wakati nasoma Makongo High School alikuwepo Mwalimu anaitwa "Kombaha" mwalimu huyu alikuwa na msemo aliokuwa anapenda sana kuusema tukiwa darasani hasa mwanafunzi anapokosea/misbehave alikuwa anasema "Mambo Huanzia Nyumbani". Siku moja nilimuuliza Mwalimu tukiwa Nje ya darasa maana hasa ya Msemo wake huo akanijibu "Ukimuona Mtu ameonesha tabia fulani mbaya basi jua alikuwa nayo tangu zamani sema ailikuwa haijapata nafasi, mabadiliko yoyote ambayo mtu anataka kuyafanya katika maisha lazima aanze na yeye mwenyewe, aanze na familia yake ndipo wengine watafuata" siku mwelewa mwalimu yule kutokana na Ufahamu wangu ulivyokuwa nyakati zile. Mabadiliko ya kweli huanza na mtu mwenyewe ndipo wengine watafuata. Pastor Carlos aliwahi sema "Huwezi waambia Watu Yesu anabadilisha Wakati wewe Mwenyewe hujabadilika". Kizazi chetu kina changamoto kubwa sana ya ku-deal na tatizo badala ya Ku-deal na chanzo cha tatizo hasa yale matatizo yanayotuhusu sisi wenyewe.

Sisi ni Kizazi kinachojua tatizo ni nini, na suluhisho ni nini, lakini hatutaki kufuata suluhisho linalotupasa kufanya halafu tunataka mabadiliko yawe chanya kana kwamba tumetumia njia inayotupasa kuifuata. Kizazi hiki kina jua kabisa Ukifanya jambo fulani matokeo yake ni fulani, lakini tunataka kutumia njia ile ile mbaya halafu tupate matokeo mazuri. Sisi ni kizazi kinachojua kabisa Ukifanya ngono zembe matokeo yake ni magonjwa ya Kuambukiza ama Mimba, lakini ajabu watu wanafanya ngono zembe halafu wanategemea kabisa magonjwa yasiwepo na wala mimba zisiwepo ndio maana vikitokea unakuta mtu anachanganyikiwa yaani ukimuuliza huyu mtu alikuwa hajui matokeo??atakuambia anajua sasa ajabu alitaka kutumia njia mbaya kumpa matokeo mazuri. Sisi ni Kizazi kinachojua kabisa usipoweka akiba ya fedha kwenye maisha yako utakuwa hauna maendeleo pamoja na kujua hayo yote sisi ndio watu tunaoongoza kwa kutumia fedha vibaya, sio wanafunzi, sio vijana sio watu wazima, kuna watu wanapata fedha kila iitwapo leo lakini hakuna cha maana anachofanya kwenye maisha ukimuuliza fedha zako unazifanyiaga nini cha maana utakuta hakuna cha maana anachofanya na fedha hizo.

Kuna mambo kadha wa kadha ambayo tunajua tusipoyafanya tutapata mabadiliko mazuri lakini mwisho wasiku tunaishia kufanya hayo hayo. Watu wanaofanya diet wanajua kabisa wakila Kitimoto na vyakula Vya Mafuta watazidi kunenepa, ajabu hiyo hiyo Diet aliyojipangia inamshinda. Wenye Vitambi wanawake kwa Wanaume na wale wanene wanajua kabisa ukifanya nini kwa Ukamilifu Kitambi kinapungua within a short time lakini ajabu hatufanyi, Wanafunzi wanajua kabisa Ukijiandaa tangu shule ama chuo kinafunguliwa hautakomaa kusoma siku za Mitihani lakini ajabu siku zingine zote mtu anatazama Movie mitihani ikiianza tu unamuona mtu ndo anaanza kusoma. Sisi ndio Kizazi ambacho mtu anajua anatakiwa kulipa Kodi ya nyumba mwenzi December, lakini miezi yote anakula hela zake ikifika kipindi cha Kodi ya Nyumba ndo anaanza Kukopa ili kulipa Kodi ya Nyumba, Sisi ndio Kizazi ambacho Kinamchagua Mgombea ambaye anatoa rushwa ili akatusaidie kumaliza tatizo la rushwa, sisi ndio Kizazi ambacho chombo kinachohusika kuchunguza Watoa Rushwa na Wala Rushwa kinapokea Rushwa ili kuwakinga wala rushwa, sisi ndio Kizazi ambacho Washauri Wa Mambo ya Ndoa za wengine Zikitaka Kustawi zinatakiwa ziwe vipi wakati za Kwao zinawashinda Kuziboresha, sisi ndo Kizazi ambacho Watu Unao Waamini ndio Wanaokusaliti, sisi ndio Kizazi ambacho timu zetu Simba na Yanga tunajua Tatizo ni Viongozi lakini Tunamfukuza Kocha. Sisi ni Kizazi Kinachojua madhara ya Sigala lakini tukaamua kuvuta.
Ni rahisi kuwasaidia wengine kuliko kijisaidia mwenyewe, ni rahisi kuwafokea wengine wanapokosea lakini tukasahau na sisi tunakosea, ni rahisi kuwanyoshea wengine vidole kwa mambo wanayokosea na kusahau sisi pia tunakosea. Matatizo mengi ya Msingi hatuko serious kuyatatua hata kama tunajua hiki tunachokifanya ni cha muda tu, siku za nyuma niliwahi andika Usizibe Shimo La Panya Kwa Kipande Cha Mkate..http://samsasali.blogspot.com/2011/10/papaa-on-tuesdayunaziba-tundu-la-panya.html. Wengi wa wanaoenda kuomba ushauri sehemu fulani mara nyingi sana huomba ushauri pasipo kueleza kiini hasa ila kasehemu tu ka kiini, unajikuta tatizo unalo deal nalo silo hasa linalopelekea tatizo kuwepo tabia hii imepenya kwenye Jamii yetu la kuto ku deal na tatizo la Msingi, tangu zamani tulipokuwa wadogo wazazi walitumia fimbo kutukataza mambo waliyokuwa hawayapendi kilichotokea walitujaza hofu ya kufanya mbele zao wengine fimbo ziliwasaidia wengine ziliwasaidia namna ya kubadilisha mbinu mbadala ili wasichapwe. Kufundishika ni Kubadilika huwezi kusema umeelewa wakati hujabadilika.
Mtu mwenye kuonesha kuwa amelielewa tatizo na ufumbuzi wake basi ni yule anayeamua kubadilika kueleka  kwenye maendeleo. Haitakusaidia kujua suluhu ya jambo kisha usifanye kwa faida yako na Jamii yako niliwahi andika kwenye Papaa On  Tuesday kuwa "Thawabu Ya Mtendaji, Haifanani na Msemaji" gonga hapa...http://samsasali.blogspot.com/2011/01/papaa-on-tuesdaythawabu-ya-mtendaji-wa.html. Mambo huanzia nyumbani, mabadiliko ni Mchakato, lakini ni mchakato wenye nidhamu pia. hakuna jambo baya kwenye maisha kama "Kuchukuliwa" ukisikia watu wanasema "tunakuchukulia sana" ujue wameshakuchoka sema ndo hivyo hawana namna. Inawezekana wamejitahidi kukusaidia wameona hausaidiki waka opt kukuchukulia kama mzigo ambao Mungu amewapa kwenye maisha. Kwenye ndo usipende kuchukuliwa ni ishara mbaya sana kwenye kizazi chetu, kwenye Jamii usiwe mtu wa kuchukuliwa. Kama unajua jambo fulani ukilikomalia utapata matokeo mazuri kwanini usilikomalie. Discipline ya kwenye maisha ni kitu cha msingi sana otherwise tutajua rushwa ni adui wa haki na sisi tutaendelea kutoa na kupokea, sisi tutajua kabisa ukifanya jambo A utakuwa na madhara ya afya lakini watu watasema "nimeshindwa kujizuia". Kujifunza ni Kubadilika Ujinga ni Kuamua. Mambo Huanzia Nyumbani.
Think Differently Make A Difference.
Papaa
0713 494110.

"News of VICTORY international Magazine" issue no.4 IS COOOMING OUT SOON!!!

THIS IS A NEW CHRISTIAN MAGAZINE, THAT IS BEEN RELEASED IN INTERVAL OF TWO TO THREE MONTHS AND HERE IS COVER OF THE NEXT ISSUE!!!
YOU CAN OPT TO LEARN DIFFERENT ARTICLES FROM DIFFERENT MINISTERS OF GOD AS WELL AS ADVERTISE WITH IT!!
THE MAGAZINE IS AVAILABLE IN ALMOST ALL CITIES OF TANZANIA!!!

FOR MORE INFO, PLEASE CALL +255 655 271 144

JE UNGEPENDA KUSHIRIKI ONGEA NA JANET TV TALK SHOW?? WAKATI NDIO HUU UNAKARIBISHWA SANA!!!!

ONGEA NA JANET SHOW NDANI CHAVALA IDEAS PLATFORM
HABARI NJEMA KWA WAPENZI WA CLOUDS TV, DSTV NA ONGEA NA JANET SHOW!!
KWA YEYOTE ANAYEPENDA KUSHIRIKI MOJA KWA MOJA KATIKA RECORDING YA VIPINDI HIVYO MUALIKO UKO WAZI KWA KILA MTANZANIA MWENYE AKILI TIMAMU BILA KUJALI RANGI, DINI WALA KABILA!!!
IKIWA UNAWEZA KUONGEA,KUCHEKA,KUPIGA MAKOFI,KUULIZA MASWALI NA KUCHANGIA MAADA ITAKAYOKUWA MEZANI SAA HIYO BASI WEWE NI MTU WA MUHIMU SANA!!
USILAZE DAMU AMUA KUSHIRIKI SASA, RECORDING ITAFANYIKA JUMATATU, JUMANNE NA JUMATANO PALE LION HOTEL, SINZA KIJIWENI,BARABARA YA TANDALE KUANZIA SAA NNE ASUBUHI MPAKA KUMI JIONI!!
(KILA SIKU ZITAREKODIWA SHOW NNE...MBILI KATI YA SAA NNE MPAKA SABA NA BAADA YA LUNCH MBILI ZINGINE)
HAKUNA KIINGILIO KAMA UKITAKA KUSHIRIKI, MUHIMU NI KUTHIBITISHA MAPEMA KUWA UTAHUDHURIA LINI NA UTHIBITISHO HUO MWISHO NI JPILI SITA USIKU!!!
WEWE TUMA TU UJUMBE WENYE JINA LAKO KUWENDA NAMBARI UZIONAZO HAPO JUU!!

ANGALIZO;
MAADA ZITATUMWA KWA WALE TU WATAKAOTHIBITISHWA KUSHIRIKI NA KUMBUKA WAANDAAJI WANASHIKIRIA HAKI YA KUMZUIA MTU YEYOTE KUSHIRIKI IKIWA ATAZINGATIA MISINGI NA KANUNI ZA KIPINDI!!!

KAMA MPAKA HAPA HUJAELEWA BASI ULIZA SASA KUPITIA
0713 883797

MC/COMEDIAN CHAVALA ASHERESHA BOTTLE PARTY(WELCOME FRESHERS) YA KILIMANJARO KWA MAFANIKIO MAKUBWA SANA!!!

HABARI ZENU!!
MC CHAVALA
KING CHAVALA
MWISHONI MWA WIKI ILIYOISHA, NAMAANISHA NOV 9, NILIBAHATIKA KUWEPO MKOANI KILIMANJARO KATIKA MKESHA MAALUM WA KUWAKARIBISHA FIRST YEARS NA WENGINE WANAORUDI KUENDELEA NA MASOMO YAO, LAKINI PIA MKESHA HUO ULIKUWA NA MALENGO KUTANGAZA RASMI MAANDALIZI YA CAMPUS NIGHT YA KILIMANJARO INAYOTARAJIWA KUWA KATIKATI YA JANUARY!!
BOTTLE PARTY HII ILIANDALIWA NA KUDHAMINIWA NA KANISA LINALOJISHUGHURISHA SANA NA VIJANA KATIKA MANISPAA YA MOSHI NALO SI LINGINE BALI NI "MANA TERBANACLE BIBLE CHURCH(MTBC) LILILOKO MAENEO YA KWA ALPHONCE UNAPOELEKEA KB.
COMEDIAN CHAVALA leading The Song "Tukue"
KATIKA PARTY HII VYUO MBALIMBALI VYA MOSHI MJINI VILIWAKILISHWA NA WANAFUNZI PAMOJA NA WALIMU WAO NA PIA VIJANA WASOMI TOKA MITAANI PIA WALIKUWEPO.
President Chavala motivating
KULIKUWA NA IBAADA YA KUSIFU NA KUABUDU YA NGUVU IKIONGOZWA NA MTBC PRAISE TEAM NA KWAYA ZA MUCCOBS NA KCMC PAMOJA NA WAIMBAJI BINAFSI KUTOKA VYUONI,


PIA KULIKUWA DRAMA, STAND UP COMEDY(BY KING CHAVALA);DANCE NA SPECIAL RELATIONSHIP AND LOVE AFFAIRS INTERVIEW, AMBAYO ILIONGOGWA NA MC CHAVALA NA COUPLE MBILI, MOJA YA MCHUNGAJI MR&MRS DICKSON MTALITINYA NA MR&MRS MSOKWA!!!
MC CHAVALA WITH MR&MRS D. MTALITINYA DURING THE LIVE INTERVIEW
MBALI NA HAYO YOTE KULIKUWA NA NYAMA CHOMA,CHIPS,VYAPATI,CHAI,KAHAWA, SODA NA VINGINE VINGI VIFAAVYO KWA PARTY!!!
HAKIKA ULIKUWA WAKATI MZURI SANA!!
NILIFURAHI SANA KUPATA FURSA HII NA ZAIDI HESHIMA NA KIBALI CHA KIPEE KWA MKOA WA KILIMANJARO!
MC CHAVALA WITH CHRISTIAN FASHION MODELS
JUMAMOSI NILIBAHATIKA KUPATA LUNCH UHURU HOTEL,HII NI HOTELI YA KISASA YA KKKT, IKO MAENEO YA SHUNT TOWN NA JIONI NIKAWA ZOMBA HOTEL, KWA LENGO LA KUWAPONGEZA VIJANA WALIOHITIMU KCMC NA MMOJAWAO ALIKUWA NI DENNIS KAPINGA.
NEEMA SHOO & KING CHAVALA
NILIBAHATIKA KUWA INTERVIEW NA KILIMANJARO FM JUMAPILI ASUBUHI NA BAADAE NIKAELEA ARUSHA KWA MAJUKUMU MENGINE YA KIKAZI,KITUME NA KIMAPUMZIKO!!!MC CHAVALA DOING MODELLING
AHSANTENI SANA MARAFIKI NA WOTE KWA MAOMBI YENU, SAFARI BADO INAENDELEA!!!

HAPPY BIRTHDAY SAMUEL SASALI a.k.a Papaa Ze Blogger!!!

 CHAVALA IDEAS PLATFORM NA WAFANYAKAZI WAKE WOTE WANAYO FURAHA YA PEKEE KWA AJILI YA RAFIKI, KAKA NA MSHAURI PAPAA, KWA KUSHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA LEO!!!
TUNAJISIKIA VIZURI SANA NA TUNAKUTAKIA MAISHA MAREFU YENYE FANAKA NA BARAKA ILI UZIDI KUATHIRI ULUIMWENGU WAKO KATIKA MTAZAMO CHANYA!!!
TUNATAMBUA PIA MCHANGO WAKO KATIKA JAMII KUPITIA VIPAJI VYAKO MBALIMBALI...TUMEFARIJIKA KUWA UMEANZA KUANDIKA KATIKA KATIKA BLOG HII KILA JUMANNE(PAPAA ON TUESDAY)

“The people who get on in this world are the people who get up and look for the circumstances they want, and, if they can't find them, make them. ”


 “Life at its noblest leaves mere happiness far behind; and indeed cannnot endure it.... Happiness is not the object of life: life has no object: it is an end in itself; and courage consists in the readiness to sacrifice happiness for an intenser quality of life.”


 “Life is no brief candle to me. It is a sort of splendid torch which I am permitted to hold for the moment, and I want to make it burn as brightly as possible before handing it on to future generations.”


“If you have an apple and I have an apple and we exchange apples then you and I will still each have one apple. But if you have an idea and I have an idea and we exchange these ideas, then each of us will have two ideas.”
George Bernard Shaw (1856-1950);
Playwright, Nobel Prize Winner


MUCH LOVE BROTHER!!!

Fredy Chavala
President-Chavala Ideas Platform 
Dsm

Papaa On Tuesday......Shida Haina Mjuzi Wala Mwenyewe......Think PositiveIkiwa imebaki siku moja iwe tarehe 14 Novermber kusheherekea siku yangu ya Kuzaliwa na kuhitimisha Mwaka wangu wa mwisho kabisa kuwa Single ili niweze kuingia katika Next Level ya Uandishi wa Papaa On Tuesday, sababu ninajua kila level ya maisha ina mtazamo wake wa kiufahamu katika kutazama mambo mbalimbali yanavyoendelea mtu anayefanya biashara kama angekuwa anaandika Papaa On Tuesday uandishi wake ungekuwa unatofautiana sana na yule anayefanya kazi za Ofisi, Mchungaji angekuwa anatofautiana sana Daktari vivyo hivyo Single na Mtu mwenye familia piga ua kuna namna tunatofautiana tunavyo experience maisha. I am so excited ninapoitazama Season 2 ya Uandishi wa Papaa On Tuesday.

Maisha tunayoishi na miaka tuliyonayo kila mtu analo neno la kusema kabisa kuwa kuna hatua amepiga na kuna mahali ametoka kwenda mahala pengine. Kupitia mashauri ya wazazi ana wazee na watu wazima na elimu tunayoisoma shuleni na mafundisho ya dini tunayosikia kila tunapokwenda katika nyumba za ibada yanatuelekeza namna ya kukabiliana na Changamoto mbalimbali katika maisha. Na katika maelekezo ama mafunzo haya yamkini huwa tunajiaminisha kuwa tumeelewa kabisa kile ambacho tunatakiwa kukifanya katika maisha. Kama kuna jambo halijawahi kukupata ni rahisi sana kukosoa na kuwacheka ama kumcheka yule linayemshinda ukijiaminisha kuwa either ni lege lege ama anajidekeza wazungu wakasema "experience is a good teacher" kwenye makala zangu za Papaa On Tuesday mwenzi june kuwa Usitukane Wakunga wakati Uzazi Ungalipo gonga hapa kama haukuwa umesoma...http://samsasali.blogspot.com/2012/06/papaa-on-tuesdayusitukane-wakunga.html. Jambo linapokuwa limekupata basi unajikuta masomo yale yote uliyojifunza kukabiliana na jambo ama shida yanapokuwa yanapotea na practically unaanza kukabiliana na hiyo Changamoto.
Shida haina mjuzi wala haina mwenyewe kuna nyakati tumekuwa tukijiuliza WHY ME??WHY ME Always??na kudhani shida ni zetu peke yetu na dunia nzima hawana shida kama sisi, na wakati mwingine tumeona kama kipimo cha shida za wengine ni kidogo kama sio chepesi kuliko tulichopimiwa sisi zinapotukabili na kuona wengine wana ujuzi nazo na wanaweza kuzikabili kuliko sisi tunavyoweza kuzikabili, nyakati zingine tumedhani maumbile yetu yamesababisha tupate shida tulizo nazo, wengine wanadhani wangekuwa na maumbile kama akina fulani leo hii wangekuwa wako mbali, wengine wanalaumu rangi walizonazo na kuona Mungu alikosea, wengine wanalaumu ukoo walio zaliwa wengine wanalaumu elimu walizozipata na kuzikosa na kudhani kama wangekuwa kama fulani basi shida zao zingetatulika kirahisi sana sana. Kuna siku Niliwahi andika laiti kama Mioyo ingekuwa ya Vioo gonga hapa usome...http://samsasali.blogspot.com/2011/07/papaa-on-tuesdaylaiti-kama-mioyo.html kuwa wengine wamenyamaza unadhani wao ni wajuzi wa shida walizonazo na wao hawana shida kuliko wewe. Shida haina mwenyewe wla shida haina Mjuzi.
Kuna nyakati zingine tumepata shida tuka waeleza watu badala ya kutusaidia ndio wakatukatisha tamaa kabisa, kuna nyakati tuliwaeleza watu shida zetu zikageuka kuwa matangazo kwenye jamii changamoto inayotukabili kizazi chetu nani yuko tayari kukabiliana na shida??hiki kizazi ambacho swali likiwa gumu mtu anaandika google, Kizazi ambacho level ya Uvumilivu na Kustahimili kinazidi kushuka, Kizazi ambacho watu wako tayari kuuwa wapate fedha, Kizazi ambacho mtu yuko tayari kufanya harusi ya mamilioni keshokutwa akamuacha Mkewe, Kizazi ambacho mtu anakaa na relationship miaka 8 kisha anamuacha mtu kwa sababu amepata mwenye fedha, Kizazi ambacho kwa sababu ya Njaa watu wamekuwa tayari kuuza miili yao kwa ushoga na uchangudoa ili kukabiliana na njaa, Kizazi ambacho Wanafunzi wanataka kuishi sawa na Wafanyabiashara kizazi kinachopenda 'Soft Touch and Appear". Nani yuko tayari Kukaa  kwenye ndoa ambayo hawana mtoto kwa miaka kadhaa, nani yuko tayari asisaliti imani yake ili mradi apitie jambo fulani.
Kila mtu ana shida na changamoto zake shida haina mjuzi wala mwenyewe unaweza ukawa na Kila kItu kwenye maisha ukawa na fedha ukawa na gari ukawa na mavazi mazuri na mke ama mume mzuri lakini hakuna amani ndani ya ndoa, unaweza kuwa na mshahara mzuri na nyumba nzuri lakini hauna inner satisfaction, inawezekana ukawa unafanya biashara unapata fedha kila siku lakini una ugonjwa unaokutesa, unaweza kuwa na elimu nzuri sana na akili njema sana ajabu hupati Usingizi na unakunywa mpaka madawa na sindano, yawezekana una umbile zuri sana na raha sana lakini ukiwa period mpaka hauoni thamani ya kuishi unatamani kufa, pengine una kila kitu unachodhani unapaswa kuwa nacho lakini unajiuliza kwanini wanaume wanakukimbia, asikuambie mtu shida haina mjuzi wala haina mwenyewe. Kuna mambo kadha wa kadha ambayo kwa watu wasiotujua kwa vile tumeamua kuyaficha tunaonekana tuko pouwa sana lakini kama leo ingekuwa kila mtu shida yake inaonekana Live Live kama CCTV ndipo ungejua kuwa shida haina mwenyewe wala haina mjuzi maana wewe unaloliweza mwingine linamshinda lile linalokushinda yeye analiweza unatamani mbadilishane lakini sasa sio fungu lake wala lako la kugawa shida hizo.
Unafanya nini unapotokea unashida???Unaomba Mungu, Unalaumu waliopelekea shida??Unalaumu Background yako??Unalaumu mwenzi wako na kujiona wewe ni bora kuliko mwenzako, Unamlaumu Mwajiri wako??Think Positive. Jijengee tabia ya Kukabiliana na Changamoto zinazokukabili wewe mwenyewe Kikamilifu chukua wajibu wa Kutafuta Ufumbuzi wewe mwenyewe pasipo kulaumu wengine, jione wewe pia ni sehemu ya tatizo na unapaswa kutafuta ufumbuzi kwa namna moja ama nyingine. Kuna Ujinga mmoja nimeuona kwenye maisha ya Usuluhishi tangu nilipopata neema ya kusuluhisha baadhi ya migogoro ya watu. Nakumbuka kulikuwa na ndoa moja ina misukosuko sana, mkaka ambaye ni mume kupitia Papaa On Tuesday ninazoziandika aliamini kabisa moyoni mwake kuwa akiongea na mimi suluhu itapatikana, simfahamu wala hanifahamu ila alijenga imani, nilipoongea nae akaniaelezaaaaa nikasikiliza nikaona kweli ni tatizo nikaomba nionane na mke wake nae nilipokutana nae akanielezaaaaa mwisho nikabaini shida iko wapi tukatengeneza appointment ya wote wawili, nikamwomba sana Mungu anipe mpenyo wa suluhu katika jambo hilo la wanandoa. Siku tuliyokutana kila mtu alielezaaaaaaaaa yaani kila mtua alifunguka ki hasa kisha tukauliza OK tumeshasikia What Next???Kila Mtu akaona kosa lake wakaombana msamaha yakaisha Ujinga niliokuja ubaini ni kwamba Mambo ambayo mngekaaa wenyewe nyumbani na kuongea na kufunguka eti mnahitaji awepo mtu Neutral ambaye yeye infact atakayoyaongea ninyi wenyewe ndo watekelezaji wa jambo hilo ambalo. Huwa ninajiuliza hivi Mshauri wa mambo nae yakimsibu ya Kumsibu anaendaga wapi??Ok labda niseme mimi yakinisibu huwa ninaenda wapi, na huko ninakoendaga nae yakimsibu ya Kumsibu anaendaga wapi???Shida haina mwenyewe.

Niliwahi kusema Ukizimia siku ya Taabu Nguvu zako ni Chache... http://samsasali.blogspot.com/2010/07/papaa-on-tuesdayukizimia-siku-ya-tabu.html.

Ze Blogger
0713494110

....JUST VOLUNTEER TO LEARN TO VOLUNTEER!!!!


VOLUNTEERING IS NOT "A EASY/LOWLY PAYING EMPLOYMENT' BUT MORE THAN A PLATFORM TO REACH YOUR HIGHER DREAMS!!!!

I do hope that this idea will meet you rightly!!
i have meet very many people with wrong perception over this issue of volunteerism, many are treating it as low wage temporal job...that is why they either don't get those chances or when they got them, they under underperform!!
VOLUNTEERING is a willing will and act of the heart, just to pay-off a certain duration of your time to save others' objectives while gaining from it indirectly!!

This task and all sacrifices that are associated with is supposed to be under the burden of A VOLUNTEER!!
Volunteering gives candidate a room to access the following benefits, which s/he couldn't dared before;
ONE....A volunteer get an opportunity to learn how written theories and materials that s/he has been studying at school work in real life!!(In other words...A practical based field work)

 TWO...A volunteer get the chance to build self confidence either before men or before himself or herself in achieving his/her dreams

THREE....A volunteer get chance to access the network, for there is great difference between Home staying job seeker and Volunteering job seekers

FOUR.....A volunteer learn to live humbly and investiture, this gives chance to save with the whole heart and concentrate on job and not payments!!

FIVE.....Volunteering is the only major platform of giving back, at least a direct way to pay back gratitude to society!!

ALWAYS REMEMBER THAT A COMPANY CAN'T JUST HIRE SOMEONE THEY DON'T KNOW REGARDLESS OF HIS/HER QUALIFICATION COMPARED TO SOMEONE WHO HAS BEEN TRUSTFUL VOLUNTEERING AT THAT PARTICULAR COMPANY!!

Nowadays things have changed, very many students are in collages and universities and so so so many others are coming, but the question is where will all those people be placed?? So the only way to survive and to penetrate to the bright future, i argue to pawn yourself in volunteering somewhere for sometime before you stand alone for your destiny....weather you want to be employed or you want to employ yourself ,still you need to volunteer and learn how things are operating!!!

........if you are just starting a collage now then start saving now so that during those days of volunteering, you will be free from unnecessary stresses and if you have already started your field work, then be very keen and very trustful for may be that is the place where you might get the chance to volunteer and may be to be employed totally!!

A CHALLANGE
Many people can;t volunteer because they placed money forward and they don't know that any good thing need investment and other lack patriotism spirit, so they feel pity to save their fellows and or they tend to ignore these minor and casual jobs....and many companies refuses to take many students for field works or volunteering because many of them are lazy, untrustworthy and they are vision-less!!

WHAT I BELIEVE IS THAT....HARD WORKING, TRUST, VISION AND INTEGRITY COUNT A LOT TO SOMEONE'S DIGNITY AND VOLUNTEERING IMPLY HUMILITY OF A PERSON, I HAVE BEEN VOLUNTEERING FOR YEARS IN DIFFERENT PROJECTS, ORGANIZATION AND EVENTS AND NOW YOU CAN SEE ME HERE I AM...STILL STANDING!!!
....JUST TRY TO VOLUNTEER SOMEWHERE!!! IF YOU FEAR THE COSTS/EXPENSES THEN FIND A PLACE NEAR BY YOUR HOME PLACE!!

VOLUNTEERING MIGHT SEEM TO BE A VERY CRAZY IDEA THIS TIME, ESPECIALLY WHEN YOU GAIN ZERO, BUT I WANT TO ASSURE YOU THAT ONCE YOU GET TO LEARN THE JOB THEN YOU CAN EASILY DO YOURS FOR YOUR OWN SAKE!!!

N.B; if you wish to know more and may be you want to be connected to such opportunities then make sure we communicate!!
>>Getting an opportunity of volunteering somewhere needs extra efforts and preparation so be ready when you want to volunteer for real!!

THANK YOU FOR READING AND UNDERSTANDING THIS IDEA WELL AND I BELIEVE YOU WILL WORK OUT ON IT!!!

CHAVALA IDEAS PLATFORM
President
+255 713 883797

.....eti ni kweli kuwa AJALI IMEMWONGEZEA PROSPER MWAKITALIMA UMAARUFU????

imepita muda kidogo bila kuonana na my PS na ndio maana uliona kimya, lakini nakumbuka mara ya mwisho tumeonana tulikuwa na hili la kuzungumza......

JE MATATIZO AU CHANGAMOTO VINAWEZA KUMPATIA MTU UMAARUFU AU NAFASI KUMBWA YA KUFANIKIWA?
Na swali hili lilikuja baada ya mtu mmoja kunituma salamu kwa my PS lakini yeye akasema hata hamfahamu, sasa hapo ndio tukaanza kuchambua na kugundua kuwa hata katika mambo mabaya kuna mazuri ndani yake!!!
My PS alipata ajali mbaya sana na kila mtu alibaki kushangaa na hata sasa bado wanaendelea kushangaa kuwa katika ajali mbaya kama ile mtu anawezaje kuwa mzima??
na mbaya zaidi na hata wafanyakazi na madaktari bigwa walipigwa na butwaa kuona ni jinsi gani watu walivyokuwa wengi kumuona my PS akiwa hospitali, hali sio msanii au mwanasiasa au chochote chenye kujustify umati ule wa watiu!!!
na hata baada ya pale sasa, wengi wanamfahamu na hata kama hawajawahi kuonana, basi humwita "Mwakitalima wa ajali ya gari" na hali wakiita hivyo mshikaji anaendelea kupokea kazi na maisha ndio yanaeleweka!!!

Nikaongezea jambo moja kuwa usiwe na mtazamo finyu, kiasi cha kuki-critisize kila kitu, sababu tu hukipendi...unajua imewahi kutokea msiba fulani wa Jambazi sugu mwenye genge na hapo msibani kila mtu alikuwa akiongea lake na jambo la kushangaza, wakati wengi wakisumlia ukatili wake, huyu mmoja alikuwa akisimulia jinsi YULE JAMAA ALIVYOKUAGA SMART!!!
Unajua nini unaweza kujifunza unyenyekevu au kujali kutoka kwa mshirikina au kahaba!!!


NATAMANI UBADILIKE NA UBADILISHE MTAZAMO, NA KILA WAKATI JITAHIDI KUONA POSITIVITY YA EVERY IDEA THAT PASSES YOUR WAY!!

Ahsante sana my PS
King Chavala
+255 713 883797

Papaa On Tuesday...If You Want To Go Fast, Go Alone, If You Want To Go Far Go Together.

Zangu Salamu ziwafikie Wanafunzi wote wa SAUT pale Nyakato Kwa Upendo wao Mwingi waliouonesha Kwangu kwa siku nilizokuwa hapo Chuoni Kwao. Kwa heshima ya Kipekee nimshukuru Adolf Nzwalla pamoja na wafanyakazi wa HCC Alive FM 91.9 Kwa masafa ya Mkoani Mwanza. Mlinifanya nikajisikia bado niko Dar, Mungu sio Filikunjombe Mwezi wa December, 2012 ratiba yetu iko kama Kawaida.

Ninamshukuru Mungu Kwa kuniwezesha leo Kuandika Papaa On Tuesday ya 44 kwenye mwaka huu nikiwa nimebakiza POT 8 kutimiza 52 Kufunga Mwaka 2012. Mungu ni Mwema sana kwa kila iitwapo leo.
Kaika Clip niliyoitupia hapo Juu utamsikia President Barroso akieleza Msemo wa Papaa On Tuesday Ya leo ambayo kwa mara ya kwanza Mwaka Jana mwezi kama huu November, niliandika POT yenye kichwa cha habari kama hiki cha leo. Gonga hapa kwa kumbukumbu isiyooza..http://samsasali.blogspot.com/2011/05/papaa-on-tuesdayif-you-want-go-fast-go.html.
Kati ya Mambo ambayo Watanzania na Waafrika tunapenda hasa ni Kukutana ama Vikao, hata kama kuna Option ya Technolojia lakini still watu wanapenda kukutana. Na Mnapokutana kuna kuwa mijadala mirefu ambayo mwisho wa siku unaweza mkakuta mnaarisha maamuzi mliyotaka kuafikiana sababu kumekuwa na lundo la mawazo.mnajikuta kwenye kikao mnaambiana 'Kila Mtu akatafakari Kisha alete Majibu". Badala ya Kukaa Kikao Kimoja mnajikuta mnakaa Vikao Vitatu. Ingawa kwenye wengi hapaharibiki neno lakini Wapishi wengi Huaribu Mchuzi.
Kuna baadhi ya mambo kwenye maisha ukitaka kufanya na watu wengi na kushirikisha watu wengi utajikuta uko pale pale badala ya kusonga mbele hasa mambo ya maendeleo. Kuna baadhi ya mambo basi amua mwenyewe amua kiume amua kujilipua utasonga. Miluzi mingi humpoteza Mbwa lazima ifike hatua uweze kuamua mambo ili uweze kwenda haraka. Sio Kila Mtu anaweza kuwa na mzigo na kile ulichonacho ndani ya moyo wako. Unaweza kuta wewe ndiye unayeingia gharama ya Muda, fedha na pengine hata maumivu ya nafsi sababu kuna mtu anataka kuamua hatma ya jambo fulani. Kuna nyakati kwenye maisha tumeruhusu kunyanyaswa kwa Mkataba wa Kujiona kuwa fulani anatakaiwa aamue kwa niaba yako. Unaweza kuta umemshirikisha mtu ama watu jambo fulani ambalo watu hao jambo hilo hawajalipa Uzito wewe uliolipa jambo hilo. Matokeo yake imepita wiki, miezi umeshindwa kuendelea mbele sababu tu unahitaji kufanya kwa pamoja. Kwa wale ambao tumewahi kuishi maisha ya "Gheto" ambako mnachanga Kununua Luku ama kama Mna share Luku na Mpangaji mwenzio na zamu yake ya kununua Luku imefika ghafla anakuambia hana hela siku hiyo swali la kujiuliza utasubiri zamu iende sawa ukae gizani ama uamue kununua Luku sababu una issue zako za msingi zinahitaji umeme. Jiulize kuna mambo mangapi tumehairisha kufanya sababu 'Wajumbe" wamekataa kupitisha hiyo idea wakati wewe still unaona kuna Mpenyo katika hilo wazo. Wakati mwingine ni vema watu wakaku-Join mbele ya safari baada ya kuamua kufanya wewe mwenyewe.
Ni kweli tunawahitaji watu katika maisha yetu, Ni kweli umoja ni Nguvu na ukweli ni kwamba watu wanatusaidia kwenda mbali zaidi, wanatusaidia kutuongezea mawazo, wanatusaidia kututia moyo tunapoamua kwa pamoja, Mkiwa wengi mnagawana hata maomivu ya kushindwa kwa jambo, Mkiwa wengi mnagawana hata hasara ya jambo na kwa sababu hiyo inakufanya ufanye sawa sawa na kundi linavyoamua na sio wewe unavyoamua katika maisha. Ukitaka kwenda mbali zaidi kwenye maisha nenda na watu ila kama unataka kwenda na speed ya kimaendeleo basi amua kufanya mwenyewe. Kuna kazi, mahusiano na hata biashara tumewahi poteza sababu ya opinion za watu. Wiki 2 zilizopita niliandika POT kuhusu Kusikiliza Sauti ya Ndani. Lazima uwaze nini unafanya na kwafaida ya nani na Kwanini unafanya. 
Asilimia kubwa ya watu waliofanikiwa katika maisha ni watu walioamua kufanya pasipo kusubiri kila kitu kimekaa shwari, ukishaanza kuuliza uliza kwa watu jambo la kuamua leo itakuchukua wiki nzima kwa jambo ambalo una uwezo wa kuamua kwa haraka. Mbaya zaidi unakuta kwa sababu ya ushauri wa watu unachelewa kufanya maamuzi uliyotakiwa kufanya leo. Sikatai kupata maamuzi ya watu ni kweli utafika mbali sana, lakini ukitaka kufanya haraka basi unahitajika kujitwisha mslaba wako kila iitwapo leo.If You want to go Fast Go Alone, If You Want To Go Far Go Together.