CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

Papaa on Tuesday(PAPAA ON HONEYMOON)....Wewe ni sehemu ya maisha yangu (You're the part of ma life)

.....WARAKA TOKA HONEYMOON!!


Nikiwa bado niko honeymoon naomba leo nizungumze na wewe kuutambua Moyo wa Mwanamke.Ni wazi kua moyo wa mwanamke ni wa utofauti sana kuliko sisi tunavyomtazama napenda kuchukua nafasi hii kukufahamisha au kukutambulisha mwanamke aliyebeba kusudi lako,hatima yako,mwanamke aliyesababisha Mungu ashike damu kwa mara ya kwanza maana kuna sababu kubwa sana ya Mungu kumtoa mwanamke katika ubavu wa mwanaume kuna sababu kubwa sana ya Mungu kuruhusu damu kumwagika,Mungu sio katiri na wala hakufanya jambo la kinyama na wala hakutaka kumuumiza Adamu ila alikuwa na kusudi na malengo maalumu sana na jambo zuri sana kwa Adamu ndio maana alifanya yeye mwenyewe kazi hiyo ya upasuaji,maeneo mengine yote Mungu aliamuru watu wachinje wanyama na damu ifanye kazifulani na hata kwa Yesu aliruhusu apigwe na kuchomwa mkuki ili damu ifanye kazi lakini kwa Adamu aliingia mwenyewe hakuitaji mikono ya mtu ndio maana maandiko yanasema mke mwenye busara hutoka kwa Bwana'
 Hapa inatubidi kuliangalia kiundani sana kusudi la Mungu kumtoa mwanamke kwa mwanaume kwa kuusoma moyo wa mwanamke aliyebeba kusudi lako.Kwa nini mimi Samuel Sasali nili mpenda mke wangu kipenzi Milembe John Madaa,hakuna anayependa bila sababu na hakuna anayependwa bila sababu zinzomfanya,mtu kupenda au kutopenda hata Mungu alikuwa sababu za kuupenda ulimwengu hata kumtoa mwana wa pekeee ulimwenguni.Kupenda sio dhambi na kutopenda sio dhambi upendo ni sehemu ya maisha na ni Mungu ambaye ameweka kwa mwanadamu hivyo.
 LOVE imetoka kwa mungu sio mtu ameamua kupenda jua kuwa love ni sehemu ya maisha hata wanyama wanapenda na wana wivu wao kwa wao lakini love ya mwanadamu ni kubwa na inanguvu kuliko wanyama sababu nilizo nazo kwanini ninapenda na kwanini natakiwa kumpenda?
(a)Kwa sababu naitaji kufalijiwa (nafsi)
(b)Kwa sababu naitaji kukamilishwa (mwanz 2:18)
(c)Kwa sababu Upendo ni Asili
(d)Kwa sababu ni mpango wa Mungu
(e)Kwa sababu nahitaji kupendwa

 Love haijengwi kwa mali,pesa,watoto,uzuri,elimu,wadhifa wako,Uaskofu,Uchungaji,Utume,Udaktari.Upendo unajengwa kwa maneno matamu (palatable word) (sweet word) maneno yenye uwezo wa kukamata hisia ya mtu na kumfanya achilie maisha yake kwako yanatakiwa maneno yenye nguvu ya ushawishi na hata sex haijengi ndoa bali sex ni (thanksgiving) ni sadaka ya shukurani baada ya mambo muhimu kufanyika watu wengi wamedanganyika kuwa sex ndio upendo kitu ambacho sicho na ni afundisho potofu,vitu vinavyotengeneza upendo ni vidogo sana na vinadharauliwa sana kama busu,kukumbatia,mawasiliano na muda wa kutosha na mwenzi wako.
 Upendo unafanya mtu kujua kusudi la kuumbwa fulani kwa ajili ya mtu fulani,mwanadamu amegawanyika katika sehemu kuu tatu 1)Nafsi 2)Roho 3)Mwili kumbuka moyo unahitaji kufarijiwa,unahitaji kupendwa na unahitaji kuheshimiwa.

Papaa

SASA SAMUEL SASALI AMEKAMILISHWA NA MILEMBE MADAHA NA TANGU LEO ATAITWA MR.!!!

HONGERENI SANA SAMUEL SASALI NA MILEMBE MADAHA KWA KUFIKIA HATUA HIYO YA KUWA MUME NA MKE......"SAMILEMBE"

CERTIFIED MR SAMUEL AND MRS MILEMBE SASALI
SASA HAWA NI MUME NA MKE RASMI NA HIVYO NDIO VYETI VYAO VYA NDOA!!
NA HIYO HATUA HAPO JUU ILIFIKA BAADA TU YA KIAPO CHA KILA MMOJA KWA MWENZAKE PAMOJA NA PETE YA AHADI YA NDOA NA KUTUNZA KIAPO HICHO
 VAA PETE HII,IWE ISHARA YA AGANO LANGU KWAKO.....
 VAA PETE HII.....
GROOM'S MEN PAMOJA NA SAMUEL SASALI

MAIDS KUMPAMBA MILEMBE
KULIKUWEPO GROOM'S MEN NA MAIDS 30 KUIPAMBA HARUSI HII YA PAPAA SEBENE!
WALIINGIA KWA FURAHA SANA NA KILA MMOJA ALIFURAHIA UCHANGAMFU WAO

MR SAMUEL AKIONGEA NA KUMSIFIA MKEWE
MRS MILEMBE MADAHA WA SAMUEL AKIONGEA
TUKAPATA KUSIKIA SAUTI ZAO,WAKASEMA NA HATIMAYE WAKAPUMZIKA KIDOGO KABLA YA KUANZA ZOEZI LA KEKI!
MR & MRS SAMUEL AND MILEMBE SASALI
HATIMAYE WALIKATA KEKI NA KULA NA

KIPEKEE WALITOA ZAWADI YA KEKI KWA WATU WAO KADHAA MUHIMU SANA, AMBAO WAMEKUWA MSAADA KWA KILA MMOJA WAO NA KWA MAHUSIANO YAO.....BAADHI YA WALIOPEWA ZAWADI YA KEKI NI PAMOJA NA WAZAZI WA PANDE ZOTE MBILI,
 MILEMBE ALIPELEKA UKWENI...
NA HUKU PIA VIVYO HIVYO!

KAMATI YA MAANDALIZI,MARAFIKI HURU,AFLEWO TEAM,DK PARVINA,PROSPER MWAKITALIMA,APOSTLE ONESMO NDEGI, LINDA TEMBA NA DK.HURUMA NKONE, MCHUNGAJI ALIYEFUNGISHA NDOA HIYO!!
KEKI KWA MCHUNGAJI NA MKE WAKE

KEKI KWA PROSPER MWAKITALIMA

KEKI KWA DK PARVINA
HATIMAYE WATU WALIKUJA KUMPONGEZA KWA KUCHEZA NA KUMRUSHA JUU SANA...
NA BAADA YA HAPO MENGI YALIENDELEA,KAMA VILE KUONA SHORT DOCUMENTARY NA HATIMAYE CHAKULA,NA HAPO WALITUMBUIZA THE VOICE,SAMWEL YONAH, AMANI KAPAMA, BOMBY JOHNSON PAMOJA NA KING CHAVALA-MC NA KIBAO MAALUM KABISA KWA MAHARUSI "SAMILEMBE"
KING CHAVALA-MC
WATU WALIKUWA WAKITOA ZAWADI MLANGONI,LAKINI KUNA BAADHI YA WATU AU MAKUNDI MAALUM YALILAZIMIKA KUPELEKA MBELE ZAWADI ZAO.
KAMATI YA MAANDALIZI ILIENDA MBELE KWA KUCHEZA KAMA HIVI
CHRISTIAN BLOGGERS NAO HAWAKUBAKI NYUMA KATIKA KUMPONGEZA MWENZAO!
"SAMILEMBE"

HATIMAYE BAADA YA YOTE WALIPIGA PICHA NA KUONDOKA KUELEKEA HUKO AMBAKO HAKUNA AJUAYE NA WAO HUJUA TU WAKISHARUDI!!

SHUKRANI NYINGI SANA KWA KAMATI YA MAANDALIZI  NA KILA ALIYEHUSIKA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE KUFANIKISHA JAMBO HILI,AHSANTE SANA MWENYEKITI NOEL TENGA KWA KUKUBALI KUTUMIKA KUBEBA JUKUMU HILI!

KWA NIABA YA TIMU NZIMA CHA YA CHAVALA MEDIA, TUNAWATAKIA KILA LAKHERI NA MAISHA MAREFU SANA YENYE FURAHA NA AMANI NA UPENDO WA KWELI WATU HAWA MUHIMU SANA KWETU,AMEN!!

IMEANDIKWA NA 
King Chavala MC
+255 713 883 797