Tunakila sababu ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Siku ya leo na uzima aliotupa mimi na wewe tunapoelekea kuhitimisha majira haya ya Pasaka na tukiwa tayari kwa ajili ya kusheherekea kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Mbali na yote tunakila Sababu pia sisi kama Watanzania kumshukuru Mungu kwa ajili ya Kupatika kwa Hati ya Muungano ambayo kwa Miaka 50 imekuwa ikisadikika kuwa haipo kumbe ipo Ikulu kwenye makabati kabati nalo ni jambo la kumshuuru Mungu ni matumaini yangu kuwa sasa majadiliano kuhusiana na Muungano kule Bungeni yatafikia muafaka lakini isije kuwa kuwa kupatikana kwa hati ya Muungano ni Kuziba shimo la Panya kwa kipande cha Kitumbua tukiamini Panya wa Kero za Muungano hata tusumbua tena tatizo la Panya ataanza kula kitumbua pole pole tukija kustuka kumbe tulitumia tiba ya muda kwa gonjwa sugu.
Kwa siku kama 4 wakazi wa Jiji la Dar-es-Salaam na vitongoji vyake wamekuwa wakiishi kwa mashaka sana kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, kuna watu wamepoteza makazi, kuna watu wamepoteza ndugu, kuna barabara zimeharibika, kuna nyumba zimejaza maji, kuna madaraja yamekatika, kuna madaraja yamepata nyufa hii yote ni kazi ya Mvua. Kuna watu walihamia maeneo ambayo hawakujua nyakati za Mvua huwa kunafananaje wengine wamejenga maeneo hayo na kuna wengine wamepangishwa maeneo hayo yanaweza kuwa ya makazi ama biashara mwisho wa siku wamekuja pata picha halisi kuyafahamu mambo yaliyofichika. Kila jambo linalotokea na kulitazama inategemea sana na angle uliyokaa na kulitazama jambo hilo. Mfano inawezekana kabisa kukosa Bunge la Katiba watu kuongea kuhusu hati ya Muungano yamkini mpaka leo isingepatikana, pengine kupitia mvua zilizonyesha wangeni walisafiri kwa siri matokeo yake kubomoka kwa madaraja kukasababisha wajisalimishe kwa wapenzi wao kila jambo linalotokea basi kuna somo la kujifunza ndio maana ninasema ni heri Mvua ikanyesha Ukajua wapi panavuja.
Mgonjwa anapokuwa anaumwa na ukawa na kazi ya kuuguza kuna mambo ya kujifunza kuna wanaokuja kumuona mgonjwa, kuna wanamuuguza mgonjwa, kuna wanaokuja kumuonea huruma mgonjwa na kuna wanaokwenda kupata habari tu za mgonjwa na mambo mengi kama hayo. Jambo hili ni hata kwa wanaopatwa na mafuriko sio kila mtu anayekwenda anaenda toa msaada.Watu wanapokuwa wakija hospitalini ni wengi sana sana na wengine kuwa nani ni nani pia walikuwa wamefahamiana hapo, marafiki waliokuwa hajaonana muda mrefu walikutana hapo. Kuna waliokuja wakacheka, kuna waliokuja wakarudi na maswali mengiiii, kuna walikuja wakatoka na majibu ya maswali yao mengiii, kuna waliokuja na kuliaaa lakini mwisho wa siku nikasema kupitia kuugua “Heri Mvua inyeshe tujue wapi panavuja”. Assume kama mgonjwa anayeumwa alikuwa na nyumba ya Siri mahali na alikuwa na mtoto pengine katika kulazwa kwake hospitali nyumba ndogo na mtoto nayo ikaja, watu ndo wakafunguka macho kweli kuumwa ni jambo baya lakini katika kuumwa kwake kuna jambo limefahamika.
Mgonjwa anapokuwa anaumwa na ukawa na kazi ya kuuguza kuna mambo ya kujifunza kuna wanaokuja kumuona mgonjwa, kuna wanamuuguza mgonjwa, kuna wanaokuja kumuonea huruma mgonjwa na kuna wanaokwenda kupata habari tu za mgonjwa na mambo mengi kama hayo. Jambo hili ni hata kwa wanaopatwa na mafuriko sio kila mtu anayekwenda anaenda toa msaada.Watu wanapokuwa wakija hospitalini ni wengi sana sana na wengine kuwa nani ni nani pia walikuwa wamefahamiana hapo, marafiki waliokuwa hajaonana muda mrefu walikutana hapo. Kuna waliokuja wakacheka, kuna waliokuja wakarudi na maswali mengiiii, kuna walikuja wakatoka na majibu ya maswali yao mengiii, kuna waliokuja na kuliaaa lakini mwisho wa siku nikasema kupitia kuugua “Heri Mvua inyeshe tujue wapi panavuja”. Assume kama mgonjwa anayeumwa alikuwa na nyumba ya Siri mahali na alikuwa na mtoto pengine katika kulazwa kwake hospitali nyumba ndogo na mtoto nayo ikaja, watu ndo wakafunguka macho kweli kuumwa ni jambo baya lakini katika kuumwa kwake kuna jambo limefahamika.
Kama hakuna mvua nyumba za mabondeni na zenyewe zina raha yake full hewa, wale wa wanaokaa Jangwani huku Dar-es-Salaam wakati wa majira ya Kiangazi wana maisha mazuri kama wengine. Kwa wakazi wa maeneo korofi kama Sinza usiombe mvua ikanyesha ukajua maji yanavyojaa na kuziba barabara, kwa maeneo ya Kariakoo wakati wa mvua ndipo ambapo watu hufungulia chamber za maji taka. Ukitaka kuhamia kwenye nyumba mpya hamia wakati wa mvua ndipo utajua kuwa nyumba uliyohamia inavuja ama la. Kuna wakati ni heri mvua ikanyesha ukajua wapi pana vuja ili uweze kurekebisha.
Mvua inaponyesha na kugundua wapi panavuja kuna mambo matatu ya kufanya, kwanza kama tatizo lenyewe ni dogo unaweza kuziba kwa kumuita fundi ama ukaaamua kutengeneza mwenyewe sababu issue sio kubwa sana, jambo la pili ukigundua sehemu inavuja unataka kujua nini nimepelekea kuvuja kwa nyumba hapo sasa kunahitaji ukarabati wenye kugharimu kubomoa sehemu Fulani Fulani ili kuweza kuweka sawa pale panapovuja so hapo kuna gharama za fixing. Lakini njia ya tatu ni kuhama kabisa eneo hilo, kama kwa wakazi wa Jangwani ili kuepuka usumbufu wakati wa mvua ni kuhama maeneo yanayovuja sana na kuhamia maeneo salama.
Kuna watu ambao kwenye mahusiano yao ama ndoa zao kuna matatizo yanayohitaji tu marekebisho machache ili kuzuia tatizo lililopo, kuna watu wao wanahitaji aje fundi kabisa ndio wale unaowaona wanakwenda kwa washauri ama wazazi ama wasimamizi wa harusi zao nia na makusudi ni kusaidia kuzuia ndoa ama mahusiano kuharibika na kuna wale sasa ambao wao unaona wanaamua kabisa kuvunja ndoa zao na wengine kuachana nao kwa sababu gani uimara wa nyumba unapimwa wakati wa dhoruba.
Kuna watu ambao kwenye mahusiano yao ama ndoa zao kuna matatizo yanayohitaji tu marekebisho machache ili kuzuia tatizo lililopo, kuna watu wao wanahitaji aje fundi kabisa ndio wale unaowaona wanakwenda kwa washauri ama wazazi ama wasimamizi wa harusi zao nia na makusudi ni kusaidia kuzuia ndoa ama mahusiano kuharibika na kuna wale sasa ambao wao unaona wanaamua kabisa kuvunja ndoa zao na wengine kuachana nao kwa sababu gani uimara wa nyumba unapimwa wakati wa dhoruba.
Kwenye maisha kuna watu na taasisi zao inawezekana tukawa tunasema afadhari hili limetokea tumeujua ukweli, kuna mambo huwa yanatokea kama ajali, “coincidence” kwenye maisha kweli jambo linaweza kuwa ni baya lakini kupitia jambo hilo kuna ukweli mwingine uliokuwa umejificha huwa unajulikana. Unaweza kuta mtu ana watoto wa Siri amezaa na mtu mwingine kwenye Familia yake ya ndoa hawajui, siku akifa ndo wale watoto wanajulikana wakija mlilia mama ama baba yao. Unaweza kuta mdada kumbe alipataga mtoto zamani akaenda mficha kwa “bibi yake” huko kijijini na huku mjini mdada akaendelea na maisha yake, siku ikitokea Yule mtoto kule kijijini akaumwa ama akafa basi kuna jambo lingine huwalinatokea kwa kujulikana ni kama “Coincidence” Fulani ndo maana unasikia mtu “heri nimeujua ukweli”.
Katika mambo mengi sana yanayotokea kwenye maisha yetu kuna upande wa hasara na kuna upande wa kujifunza kile ambacho kinatokea. Pamoja na ubaya wa jambo kuna heri ya jambo hilo ndio maana katika msiba kuna Kufa Kufaana, lakini kuna mambo ambayo yanapelekea jambo lingine kufahamika kwa sababu ya tatizo lililotokea. Mvua ikinyesha tunajua wapi panavuja kama isingenyesha yamkini tusingefahamu lolote. Hujawai ona mwanaume kila siku simu yake iko mkononi siku hiyo ikatokea pengine ugonjwa ama kusahau simu nyumbani ndipo mkewe akaamua kuichukua simu hiyo na kukagua Hamad, anakutana na vitu vya ajabu, pengine ndipo anapogundua mume wake ni Shoga ama anauza madawa ya kulevya yapo mambo mengi sana yanayoonekana kama ni tatizo lakini kuna somo la kujifunza.
Kwenye maisha ya biashara unaweza kuta kila siku unapata hasara, kwa kupata hasara unaweza kujua hasara inatokana na nini. Hasara inakupa sababu ya kuboresha biashara yako. Heri ukapata hasara ukajua safari ya pili nini kilipelekea hasara mara ya kwanza. Ukijua wapi panavuja itakupa fursa ya kujiimarisha upya.
Kwenye mahusiano kuna watu wengi sana wanachukuaga maamuzi yasiyo sahihi kwa kugundua mtu wake kumbe anatabia Fulani. Wengi hutafuta suluhu ya kuhama badala ya kuangalia kama sehemu yenye tatizo inaweza rekebishika, ama inahitaji kubomolewa kwa maana ya kutoa maelekezo na njia mbadala badala ya kukimbilia kumuacha mtu. Assume mtu unayempenda kwa dhati ukagundua kumbe ana mtoto wan je ya ndoa, then wewe uka opt kuondoka na kumuacha utakuwa umejenga ama umebomoa? au unamuacha mtu sababu anatafuna vibaya ama akilala anakoroma na wewe hupendi wa kukoroma, heri umejua anakoroma ili uweze msaidia. Kuna wanawake hawapendi wanaume waongea kwa hasira, au wenye hasira wanatamani wanaume ambao ni reasonable hawawezi fanya kituko mbele za watu yaani hawawezi waabisha, kama watu hao hawajaoana mshukuru Mungu kuwa Heri Mvua imenyesha ukajua wapi panavuja, Kama Mtu wako sio mwaminifu na umegundua cha msingi usianze mtukana jiulize tu hii mvua inayoingia ndani imepitia wapi ili uzibe?. Unaweza ukawa kwenye mahusiano tu hata kwenye ndoa hujaingia siku ikatokea umemuudhi mpenzi wako ukashangaa anazira eti anasusa ana kasirika mpaka anavunja simu badala ya kumuacha na kumkimbia mshukuru Mungu kosa ulilolifanya limepelekea umejua tabia ya mpenzi wako, heri mvua ikanyesha ukajua wapi panavuja.
Jifunze kuelewa mambo kwa mlengo chanya, usiutazame sana mkono unaokuonesha mwezi ulipo ila tazama mwezi unaooneshwa. Hakuna kitu kinatesa duniani kama mtu akufanyie kitu ambacho hujui kwanini anakufanyia ama umefanyiwa, hakuna kitu kibaya kama ufukuzwe kazi halafu hujui kwanini umefukuzwa kazi, hakuna kitu kibaya kama hujui kwanini unapata hasara kwenye biashara, hakuna kitu kibaya kama Mchungaji washirika wake kuhama kanisa huku yeye hajui kwanini Washirika wanahama, vivyo hivyo kwenye mapenzi hakuna kitu kinachotesa kama ukampenda mtu sana then from nowhere akawa hakupendi tena unabaki kujiuliza maswali usiku mzima bila majibu, kuna watu wanakonda sababu ya kuwaza “why this happening to me”? kuna rafiki yangu alipelekwa kulazwa kabisa hospitali, kuna watu wanaombewa utadhani wanaumwa kumbe mapenzi yanatesa, mapenzi yana nguvu kuliko mauti.
Maisha ni changamoto jambo lolote unaloligundua kupitia “Coincidence” mshukuru Mungu badala ya kuanza kuanza kuchukua maamuzi sio, pengine kupitia kufukuzwa kazi ndo umegundua rafiki yako yuko tayari kujiua ili asiishi bila ajira, BiBlia inasema “All thing(s) works for good”. Kama kupitia kitu Fulani au issue Fulani ndo umegundua kitu kingine basi mshukuru Mungu kwa kilichotokea sababu kimekuwezesha kujua kitu kingine. Kumtuhumu muhusika hata kosa utetezi kwa sababu moja ama nyingine. Heri Mvua ikanyesha ukajua wapi Panavuja ili uchukue hatua za marekebisho ama kuhama.
Tuko pamoja.
Papaa
0713 494110