CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

***NILIYOJIFUNZA KUHUSU USAFIRI WA NDEGE NA MAISHA YETU***


Mambo kadhaa niliyotafakari na kujifunza katika kusafiri kwangu hata kama sio sana(Maana najua wapo wapimaji),hususani usafiri wa anga nimeona kabisa mchakato mzima unafanana kabisaaaa na Maisha yetu ya kila siku!!
i. Kwanza mtu unakuwa na destiny,yaani mahali unakwenda na hapo unaamua muda na namna ya kwenda huko uendako na yamkini hata saa au siku ya kwenda!
*Hii ni sawa kabisa na maisha maana mtu huwa na ndoto au mipango fulani au destiny kisha unaamua mwenyewe ni lini uanze safari kuelekea ndoto yako!

ii. Hili ni basi kwa maana ya "basi"kama mabasi mengine Ila sema hili linapita angani(Airbus), kwahivyo unakuwa na tiketi kisha boarding pass na unapanda na kukaa kama basi la kawaida tu!
*Katika maisha kuna mambo mbalimbali mengine sio tofauti na wengine Ila tu hufanyika tofauti na wengine!

iii.Ukiwa ndani ya ndege kwa kuwa sio sebuleni kwako yako maelezo na maelekezo muhimu za kuzingatia ili safari yako Iwe murua...mfano urefu wa safari,umbali toka usawa wa bahari na usalama ndani ya ndege...ni muhimu kuzingatia ingawa wengi hupuuzia wakidhani wao ni wenyeji sana!
*Katika maisha ni muhimu sana kuzingatia maelekezo, mafunzo na hekima kabla ya kuanza safari kwenda kwa ndoto yako,hata kama una kipaji ni muhimu sana kujifunza namna ya kufanya na kipaji chako ili wewe na wote wanaofaidika na kipaji hicho wafurahi.... So ni muhimu kuwa na washauri,waelekezaji na mentors kwa Kizungu!!

iv.Ndege ikitaka kuondoka,huanza kwanza kuondoka ilipopaki na kwenda kuanzia mwanzo kabisa wa barabara ya kukimbilia (running track) na na hapo huanza kukimbia kwa nguvu lakini hupita usawa uleule ambao ilikuwepo kisha kuondoka....
*Kama ambavyo ndege huenda kuanzia mbali na kisha kupitia pale pale kabla ya kuondoka basi hata katika maisha ni vivyo hivyo...kabla ya kuanza ndoto zako ni kama huwa unaenda kujianza mahali kisha unapita pale pale kwa watu wako au katika mazingira yako na kusema sasa ndio naenda eeh!! Na huku chini watu wanasema Oooh jamani yuleeee!!
(Zaidi ya hapo Nataka kusisitiza kuwa hata uweje hauendi kuishi mbinguni jamii yako ni hiyo so wewe ni jamii tu)

v.Ndege hukimbia sana kwa barabara ya kukimbilia kabla ya kupaa na wewe Ukiwa ndani utasikia mtetemeko zaidi hapo na mara ikianza tu kuiacha ardhi ni kama vile husikii saaana na angani huwezi Ona spidi yake maana ni kama imesimama tu!!...Iko maana kubwa sana ndege kukimbia chini kabla ya kuruka!!
*Ukianza safari kwenda kwa ndoto yako usikurupuke, unahitaji kujipasha na kujihakiki kuwa sasa uko tayari kwa matumizi ya wafaidikaji na ndoto au maono au vipaji vyako!!
(Usijaribu kukimbiakimbia haraka haraka eti upae haraka basi una hatari ya kurudi chini kwa kuanguka au kuanza upya... Unaweza ukaexperience misukosuko lakini ndio sawa lazima mtetemeko kwanza before ung'ae!

vi. Na Ukiwa chini unaweza ukadhani kuwa huku juu ndio kuna Network kubwa ya mitandao ya simu kwasababu huwa tunapanda miti zamani kuitafuta lakini ukweli ni kuwa huku juu hakuna network kabisa labda kama kwa simu maalum!! Kwahiyo ni muhimu kutumia network ya huko chini vema na sio kutaraji ya huko juu utachemka!!
*Ni rahisi sana kuona utaruka muda sio mrefu na hivyo kuanza kudharau watu au kupuuzia network zako za kitambo eti kisa utakutana au unatazamia kukutana na watu wengine wakubwa huko juu...Nakwambia kabisa usije ukaharibu uhusiano wako na Mtangazaji au Mwalimu aliyekufundisha mpaka ukafika hapo eti kisa unafahamiana na mwenye Chombo cha habari au mwenye shule...utafeli haraka sana

vii.Jambo la saba la mwisho kwa tafakari ya leo ni kuwa ukiwa chini huwa unaona mawingu na unajua yako mbali sana na mara ukiwa ndani ya ndege unayakuta mawingu moshi, hapo unaweza ukajisemea aah kumbe mawingu yako hapa tu,lakini ukweli ni kuwa mawingu yale ya Blue (sky) yako mbali sana sana na hata ndege haiwezi sogelea hatA.... Sasa ni muhimu kujua tofauti ya Clouds na Sky ili usije ukaoverexpect kisha ukapata frustration!
*Ni rahisi sana kuelezea possibility ukiwa hujaanza safari kuelekea huko,yawezekana ni rahisi kusema kuhusu jinsi ilivyo rahisi kufanya biashara fulani na ukachambua faida hapo au jinsi ya kufahamika au jinsi yeyote ya kwenda utazamiapo... Na labda tu ndio umejaribu kidogo tu na ukapata appreciation au umaarufu au kafaida kidogo tu basi unadhani safari imeisha.... Kuwa makini aisee Oooh!!

Nimetumia muda wangu wa angani vema kuandika hii mpaka natua naamini kuna Mtu itamsaidia somewhere, kama sio wewe basi ndugu waweza endelea tu na mambo yako na Amani iwepo!!

....Labda kuna wakati nitasema ya huko angani na kutua but I don't promise, hiyo ilinijia tu basi nikaona si vema nikapuuzia!!

NAAMINI WALE WOTE WENYE AKILI TIMAMU NA WENYE NDOTO ZAO ITAWAFAA HII NA WALE WANENAJI AU WASHAURI MWAWEZA TUMIA HII KUKAZIA MSEMAYO HUKO!!

Ubarikiwe sana na uwe na wakati Mzuri!!!

(c)King Chavvah, 2014
#LearnToLearnLearning!!! 

Papaa On Tuesday.....Heri Mvua Ikanyesha Ukajua Wapi Panavuja!!


Tunakila sababu ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Siku ya leo na uzima aliotupa mimi na wewe tunapoelekea kuhitimisha majira haya ya Pasaka na tukiwa tayari kwa ajili ya kusheherekea kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo.


Mbali na yote tunakila Sababu pia sisi kama Watanzania kumshukuru Mungu kwa ajili ya Kupatika kwa Hati ya Muungano ambayo kwa Miaka 50 imekuwa ikisadikika kuwa haipo kumbe ipo Ikulu kwenye makabati kabati nalo ni jambo la kumshuuru Mungu ni matumaini yangu kuwa sasa majadiliano kuhusiana na Muungano kule Bungeni yatafikia muafaka lakini isije kuwa kuwa kupatikana kwa hati ya Muungano ni Kuziba shimo la Panya kwa kipande cha Kitumbua tukiamini Panya wa Kero za Muungano hata tusumbua tena tatizo la Panya ataanza kula kitumbua pole pole tukija kustuka kumbe tulitumia tiba ya muda kwa gonjwa sugu.
Kwa siku kama 4 wakazi wa Jiji la Dar-es-Salaam na vitongoji vyake wamekuwa wakiishi kwa mashaka sana kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, kuna watu wamepoteza makazi, kuna watu wamepoteza ndugu, kuna barabara zimeharibika, kuna nyumba zimejaza maji, kuna madaraja yamekatika, kuna madaraja yamepata nyufa hii yote ni kazi ya Mvua. Kuna watu walihamia maeneo ambayo hawakujua nyakati za Mvua huwa kunafananaje wengine wamejenga maeneo hayo na kuna wengine wamepangishwa maeneo hayo yanaweza kuwa ya makazi ama biashara mwisho wa siku wamekuja pata picha halisi kuyafahamu mambo yaliyofichika. Kila jambo linalotokea na kulitazama inategemea sana na angle uliyokaa na kulitazama jambo hilo. Mfano inawezekana kabisa kukosa Bunge la Katiba watu kuongea kuhusu hati ya Muungano yamkini mpaka leo isingepatikana, pengine kupitia mvua zilizonyesha wangeni walisafiri kwa siri matokeo yake kubomoka kwa madaraja kukasababisha wajisalimishe kwa wapenzi wao kila jambo linalotokea basi kuna somo la kujifunza ndio maana ninasema ni heri Mvua ikanyesha Ukajua wapi panavuja.

Mgonjwa anapokuwa anaumwa na ukawa na kazi ya kuuguza kuna mambo ya kujifunza kuna wanaokuja kumuona mgonjwa, kuna wanamuuguza mgonjwa, kuna wanaokuja kumuonea huruma mgonjwa na kuna wanaokwenda kupata habari tu za mgonjwa na mambo mengi kama hayo. Jambo hili ni hata kwa wanaopatwa na mafuriko sio kila mtu anayekwenda anaenda toa msaada.Watu wanapokuwa wakija hospitalini ni wengi sana sana na wengine kuwa nani ni nani pia walikuwa wamefahamiana hapo, marafiki waliokuwa hajaonana muda mrefu walikutana hapo. Kuna waliokuja wakacheka, kuna waliokuja wakarudi na maswali mengiiii, kuna walikuja wakatoka na majibu ya maswali yao mengiii, kuna waliokuja na kuliaaa lakini mwisho wa siku nikasema kupitia kuugua  “Heri Mvua inyeshe tujue wapi panavuja”. Assume kama mgonjwa anayeumwa alikuwa na nyumba ya Siri mahali na alikuwa na mtoto pengine katika kulazwa kwake hospitali nyumba ndogo na mtoto nayo ikaja, watu ndo wakafunguka macho kweli kuumwa ni jambo baya lakini katika kuumwa kwake kuna jambo limefahamika.
Kama hakuna mvua nyumba za mabondeni na zenyewe zina raha yake full hewa, wale wa wanaokaa Jangwani huku Dar-es-Salaam wakati wa majira ya Kiangazi wana maisha mazuri kama wengine. Kwa wakazi wa maeneo korofi kama Sinza usiombe mvua ikanyesha ukajua maji yanavyojaa na kuziba barabara, kwa maeneo ya Kariakoo wakati wa mvua ndipo ambapo watu hufungulia chamber za maji taka. Ukitaka kuhamia kwenye nyumba mpya hamia wakati wa mvua ndipo utajua kuwa nyumba uliyohamia inavuja ama la. Kuna wakati ni heri mvua ikanyesha ukajua wapi pana vuja ili uweze kurekebisha.

Mvua inaponyesha na kugundua wapi panavuja kuna mambo matatu ya kufanya, kwanza kama tatizo lenyewe ni dogo unaweza kuziba kwa kumuita fundi ama ukaaamua kutengeneza mwenyewe sababu issue sio kubwa sana, jambo la pili ukigundua sehemu inavuja unataka kujua nini nimepelekea kuvuja kwa nyumba hapo sasa kunahitaji ukarabati wenye kugharimu kubomoa sehemu Fulani Fulani ili kuweza kuweka sawa pale panapovuja so hapo kuna gharama za fixing. Lakini njia ya tatu ni kuhama kabisa eneo hilo, kama kwa wakazi wa Jangwani ili kuepuka usumbufu wakati wa mvua ni kuhama maeneo yanayovuja sana na kuhamia maeneo salama.

Kuna watu ambao kwenye mahusiano yao ama ndoa zao kuna matatizo yanayohitaji tu marekebisho machache ili kuzuia tatizo lililopo, kuna watu wao wanahitaji aje fundi kabisa ndio wale unaowaona wanakwenda kwa washauri ama wazazi ama wasimamizi wa harusi zao nia na makusudi ni kusaidia kuzuia ndoa ama mahusiano kuharibika na kuna wale sasa ambao wao unaona wanaamua kabisa kuvunja ndoa zao na wengine kuachana nao kwa sababu gani uimara wa nyumba unapimwa wakati wa dhoruba.

Kwenye maisha kuna watu na taasisi zao inawezekana tukawa tunasema afadhari hili limetokea tumeujua ukweli, kuna mambo huwa yanatokea kama ajali, “coincidence” kwenye maisha kweli jambo linaweza kuwa ni baya lakini kupitia jambo hilo kuna ukweli mwingine uliokuwa umejificha huwa unajulikana. Unaweza kuta mtu ana watoto wa Siri amezaa na mtu mwingine kwenye Familia yake ya ndoa hawajui, siku akifa ndo wale watoto wanajulikana wakija mlilia mama ama baba yao. Unaweza kuta mdada kumbe alipataga mtoto zamani akaenda mficha kwa “bibi yake” huko kijijini na huku mjini mdada akaendelea na maisha yake, siku ikitokea Yule mtoto kule kijijini akaumwa ama akafa basi kuna jambo lingine huwalinatokea kwa kujulikana ni kama “Coincidence” Fulani ndo maana unasikia mtu “heri nimeujua ukweli”.
Katika mambo mengi sana yanayotokea kwenye maisha yetu kuna upande wa hasara na kuna upande wa kujifunza kile ambacho kinatokea. Pamoja na ubaya wa jambo kuna heri ya jambo hilo ndio maana katika msiba kuna Kufa Kufaana, lakini kuna mambo ambayo yanapelekea jambo lingine kufahamika kwa sababu ya tatizo lililotokea. Mvua ikinyesha tunajua wapi panavuja kama isingenyesha yamkini tusingefahamu lolote. Hujawai ona mwanaume kila siku simu yake iko mkononi siku hiyo ikatokea pengine ugonjwa ama kusahau simu nyumbani ndipo mkewe akaamua kuichukua simu hiyo na kukagua Hamad, anakutana na vitu vya ajabu, pengine ndipo anapogundua mume wake ni Shoga ama anauza madawa ya kulevya yapo mambo mengi sana yanayoonekana kama ni tatizo lakini kuna somo la kujifunza.
Kwenye maisha ya biashara unaweza kuta kila siku unapata hasara, kwa kupata hasara unaweza kujua hasara inatokana na nini. Hasara inakupa sababu ya kuboresha biashara yako. Heri ukapata hasara ukajua safari ya pili nini kilipelekea hasara mara ya kwanza. Ukijua wapi panavuja itakupa fursa ya kujiimarisha upya.

Kwenye mahusiano kuna watu wengi sana wanachukuaga maamuzi yasiyo sahihi kwa kugundua mtu wake kumbe anatabia Fulani. Wengi hutafuta suluhu ya kuhama badala ya kuangalia kama sehemu yenye tatizo inaweza rekebishika, ama inahitaji kubomolewa kwa maana ya kutoa maelekezo na njia mbadala badala ya kukimbilia kumuacha mtu. Assume mtu unayempenda kwa dhati ukagundua kumbe ana mtoto wan je ya ndoa, then wewe uka opt kuondoka na kumuacha utakuwa umejenga ama umebomoa? au unamuacha mtu sababu anatafuna vibaya ama akilala anakoroma na wewe hupendi wa kukoroma, heri umejua anakoroma ili uweze msaidia. Kuna wanawake hawapendi wanaume waongea kwa hasira, au wenye hasira wanatamani wanaume ambao ni reasonable hawawezi fanya kituko mbele za watu yaani hawawezi waabisha, kama watu hao hawajaoana mshukuru Mungu kuwa Heri Mvua imenyesha ukajua wapi panavuja, Kama Mtu wako sio mwaminifu na umegundua cha msingi usianze mtukana jiulize tu hii mvua inayoingia ndani imepitia wapi ili uzibe?. Unaweza ukawa kwenye mahusiano tu hata kwenye ndoa hujaingia siku ikatokea umemuudhi mpenzi wako ukashangaa anazira eti anasusa ana kasirika mpaka anavunja simu badala ya kumuacha na kumkimbia mshukuru Mungu kosa ulilolifanya limepelekea umejua tabia ya mpenzi wako, heri mvua ikanyesha ukajua wapi panavuja.

Jifunze kuelewa mambo kwa mlengo chanya, usiutazame sana mkono unaokuonesha mwezi ulipo ila tazama mwezi unaooneshwa. Hakuna kitu kinatesa duniani kama mtu akufanyie kitu ambacho hujui kwanini anakufanyia ama umefanyiwa, hakuna kitu kibaya kama ufukuzwe kazi halafu hujui kwanini umefukuzwa kazi, hakuna kitu kibaya kama hujui kwanini unapata hasara kwenye biashara, hakuna kitu kibaya kama Mchungaji washirika wake kuhama kanisa huku yeye hajui kwanini Washirika wanahama, vivyo hivyo kwenye mapenzi hakuna kitu kinachotesa kama ukampenda mtu sana then from nowhere akawa hakupendi tena unabaki kujiuliza maswali usiku mzima bila majibu, kuna watu wanakonda sababu ya kuwaza “why this happening to me”? kuna rafiki yangu alipelekwa kulazwa kabisa hospitali, kuna watu wanaombewa utadhani wanaumwa kumbe mapenzi yanatesa, mapenzi yana nguvu kuliko mauti.

Maisha ni changamoto jambo lolote unaloligundua kupitia “Coincidence” mshukuru Mungu badala ya kuanza kuanza kuchukua maamuzi sio, pengine kupitia kufukuzwa kazi ndo umegundua rafiki yako yuko tayari kujiua ili asiishi bila ajira,  BiBlia inasema “All thing(s) works for good”. Kama kupitia kitu Fulani au issue Fulani ndo umegundua kitu kingine basi mshukuru Mungu kwa kilichotokea sababu kimekuwezesha kujua kitu kingine. Kumtuhumu muhusika hata kosa utetezi kwa sababu moja ama nyingine. Heri Mvua ikanyesha ukajua wapi Panavuja ili uchukue hatua za marekebisho ama kuhama.

Tuko pamoja.

Papaa
0713 494110

*TAFSIRI NZURI YA MAFANIKIO*


Habari zenu!!
Maishani mwetu zipo hulka nyingi sana na nyingine huzaa tabia nzuri au hatari,kila mmoja anatamani kufanikiwa sana na kuwa na kila kitu akitakacho....lakini jambo moja ambalo nimekuwa nalitafakari maishani mwangu ni hili,naishi ili iweje na mwisho wa maisha yangu utakuwaje? Nini kitasemwa au kuandikwa kuhusu mimi,naam nitasema nini mbele ya kiti cha enzi?
Na haya ndio mambo niliyojifunza na ninatamani kushare na wenzangu, Mafanikio sio magari na majumba,ila hayo ni matunda ya mafanikio,ukifanikiwa kuwa hivyo vyote ni vema sana lakini bado hicho siyo kipimio cha mafanikio....ni kama vile ukiamua kupika wali au ubwabwa,kwa hicho chakula kutoa harufu haizuiliki,ila hujapika ili upate harufu,basi na mafanikio hupimwa kwa ndoto au malengo uliojiwekea kufikiwa,na hata iweje hatuwezi kupimwa kwa kujifananisha na wengine kama tumefanikiwa au lah maana kila mmoja ana ndoto zake,kila mmoja ana makusudi yake na kila mmoja ana yake yakuyatimiliza!!
Usije ukaumia sana maishani kwa kujikakamua kupita kiasi,wala usije ukawagombanisha watu ili upate sifa kwa mmoja wao,wala usijitahidi kuwaonyesha watu vile usivyo!!
Usijisikie vibaya classmate wako akinunua gari ama kujenga kabla yako,au usikasirike mwimbaji mwenzio akitoa albamu nne hali wewe una moja,ama akialikwa hata nje ya nchi na wewe hujakwenda popote!
Maisha ni kama mtihani,sasa usijaribu kuangalizia majibu maana kila mmoja ana karatasi yake ya maswali!
Iko neema kumsaidia kila mmoja kufikia ndoto zake,kama akiwa consistent!
Kwanini nimesema hayo, nimeona katika maisha haya tunajitahidi mno kushindana,kusemana na kuhukumiana pasipo sababu,hivi mtu mwenye ndoto ya kutengeneza roketi na yule mwenye ndoto ya kujenga nyumba inayotembea,kama wakikamilisha ndoto zao watakuwa sawa??
Muhubiri amesema kuna mambo ameyaona chini ya jua nayo ni ubatili mtupu,akasema sio wenye akili ndio hufanikiwa ama wenye mbio sana ndio hupata medani,maana kuna wakati wale waouvu kabisa ndio hupata nafasi hivyo baki kwa njia ya hatma yako,usijitahidi kushindana na yeyote wala kutupa mawe kwa wengine!!
N.B; Sifurahii sana magomvi,ila najua yamkini yasiepukike,sasa kama ukipishana na mtu kwa namna yeyote ile usikimbilie kusema na kutangaza kila mahali ama kuandika kila mahali,tena wengine huenda mbali zaidi na kuingia kwa mitandao ya kijamii na kufungua akaunti mpya kwa majina mengine,yamkini kijana akajifanya binti na kuanza kutupa mawe kwa mwenzake,huo nao ni ubatili,maana kwa kufanya hivyo unakuwa umejifungia minyororo mwenyewe,jifunze kutafuta suluhu na kukaa kimya,ukiwa mwepesi wa kuongea sana kuhusu wengine kwa ubaya,saa utakayopatana naye tena mtu huyo hautakuwa na amani kila uonapo yote uliyomfanyia,na kwa kukosa amani moyoni ni kukosa mafanikio!!!


*Ni vema sasa ukafanya mambo yale ambayo yanakupa amani na utulivu maishani mwako,wombee wenzako wafanikiwe katika ndoto zao,usijisifu wala kusema wengine ni kitu gani ila wewe,maisha ni hatua na mafanikio ni mzunguko!!
Natamani tupendane kweli na kusaidiana na kushauriana katika kila hali,maana maisha haya si ya kudumu!!
Yamkini Mungu amekupa fedha ili uwasaidie wengine, lakini kinyume chake imekuwa fimbo kwa masikini,angalia sana yamkini pia hapo kwako zinapita tu-Muhubiri 2:26!


**Basi mafanikio ya kweli ni kuweza kuishi ndoto zako au aina ya maisha upendayo,kuwa na amani na watu wote na kumpendeza Mungu,kuwasaidia wenye uhitaji na kuwatia moyo wakuzungukao na na kuishi kwa staha pasipo kuwakwaza wengine,unaweza fanya yote haya hata kama unafedha kidogo sana,ilimradi moyo wako una amani na maisha unayoishi,basi fanya bidii ili uzidi kustawi katika yale uyatamaniyo kesho,amen**
MUNGU AWABARIKI SANA WANAOFANYA KAZI ZAO NA KUJITAHIDI KUWASAIDIA WENGINE KWA MAOMBI,USHAURI NA HATA KWA MALI,NINA HAKIKA THAWABU YENU IPO!!


Na King Chavala
0713883797

Andika C1 Kwenda 15678 KUMPIGIA KURA AMANI PAUL,FANYA HIVYO SASA!!!


Kwa mara ya kwanza Blogger  na .CEO..Amani Paul amefanikiwa kuingia kwenye fainal za "Tanzania Annual Young Professional Awards"katika kipengele cha "CAPTAIN OF THE INDUSTRY" ambapo vigezo vilivyoangaliwa ni pamoja na

Excellent in taking initiatives Done at least 1 project Provide purpose of project, provide project outcomes to the organisation and community kwa maelezo zaidi gonga hapa mdau wangu http://taypa.co.tz/?get=category
Bwana Amani Paul amefika hatua hii kutokana na kuanzisha tamasha la kila mwaka la utamaduni(Haydom Cultural Festival) lenye lengo siyo kukuza utali wa Utamaduni nchini bali pia kufungua fursa kwa wananchi hasa waliopo vijijini kufaidika kiuchumi na kijamii pia.
Akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akiwa ameshika gazeti la Ohayoda.
 
 Pia,kutokana na jitihada za kuanzisha gazeti la Ohayoda (ambalo sasa litaitwa Mwanajamii)gazeti la kwanza kabisa katika mkoa wa Manyara na linaloandika habari za kijamii hususani za vijijini.

Kutokana na hayo yote Amani Paul anaomba kura yako ili aweze kushinda tuzo hiyo kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno C1 kwenda 15678.Washiriki wamegawanywa katika vipengele 3 na kila kipengele kina washiriki 3.C1 ndiyo namba yake ya ushiriki.
Mshindi atatangazwa  mwishoni mwa mwezi Februari 2014...Kwa habari zaidi soma  gazeti la The Guardian hapa http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?I=63975

TAKEN FROM UNCLE JIMMY TEMU!!

JE UMEPATA NAKALA YA FILAMU YA KIKRISTO YA KITANZANIA YA SIKU ZA MWISHO-666???

 HAYA YALIKUWA NI MAANDALIZI YA UZINDUZI WA FILAMU HIYO ILIYOANDIKWA NA MCHUNGAJI KADUMA NA KUCHEZWA NA WAIGIZAJI MBALIMBALI AKIWEMO SAMUEL SASALI!
 KUTOKA KUSHOTO NI BOMBY JOHNSON,KING CHAVAAH,MCHUNGAJI KADUMA,AMANI KAPAMA PAMOJA SAMUEL SASALI!!
YAMKINI SIKU HIYO MTAKUWA STUDIO KAMA HIVI KUPIGA PICHA MARA MNATWALIAWA NA MPIGA PICHA ANAPAKI PEKE YAKE AU VICE VESA INAWEZA KUWA KWELI!!

BASI JIPATIE NAKALA YAKO SASA ILI USAIDIE KUIPELEKA INJILI KWA WENGINE WENGI ZAIDI BAADA YA KUJIFUNZA KILICHOPO NDANI NA KUWASHIRIKISHA WENGINE!!!

HAPPY NEW YEAR 2014!!

HONGERENI KWA SHEREHE NZURI YA NOELI YA 25/12/2013 NA HIVYO TUNAWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2014!!!

KWA NIABA YA TIMU NZIMA TUNAKUTAKIA MEMA, USIACHE KUTEMBELEA BLOG YAKO...TUMERUDI UPYA KIVINGINE!!

HAPA NDIO NYUMBANI KWA MAWAZO YENYE AKILI YANAYOTEKELEZEKA!!!

KING CHAVALA
President-Chavala Ideas platform!!