#.....NI MARUFUKU KABISAAAA#
Ni marufuku
kabisaa kufanya mambo au marekebisho au matengenezo usiyoruhusiwa juu ya
kitu au jambo la kuazima bila ruhusa ya mwenyewe!
Kwa kawaida kitu cha kuazima hakina uhuru wa kutosha,kwani umepewa kwa kipimo....waswahili wanasema...."Nguo ya kuazima haisitiri Matako"
Kuna mambo mengi tunajiamulia wenyewe juu ya vitu vya kuazima na kwa kweli huwa inakuwa sio sawa,kwa mfano;
a)Mtu anakuazima simu yako aongee na mtu mara moja maana yake imeisha
airtime ambayo nayo alikopa na hapo mlipo hamna access ya
kununua....sasa unakuta mtu baada ya kupiga kwanza anaanza *102#....hivi
hicho ndio umeomba au? na haishii hapo unakuta ameongea na simu zaidi
ya hata alivyoomba yaani unakuta mtu kajiachia kama yake vile na bado
credit ikiisha na kwako eti anakopa na anapiga tena mpaka na hiyo
inaisha na hapo hajakwambia kitu...sasa wewe unashangaa ukitaka kupiga
yule mrembo anakwambia....hauna salio la kutosha kupiga simu...basi
unanunua vocha faster....unashangaa message.....Ahsante kwa kulipa
deni.....na bado unadaiwa ......ahhhh dah sasa ndio nini hivi?
Hapo
ulipokuwa umemuachia basi kapiga picha,kafungua na picha zako na mpaka
bundle yako ya internet imeisha eti kisa anadownload miziki...Sasa wenye
tabia hiyo nawaambia Marufuku,acheni kuwakwaza wenzenu,mimi tabia ya
hata tu kuazimana simu wala sioni kama ina mashiko sana kipindi hiki
ambako simu ziko tele na mawasiliano ni rahisi kwa
yeyote!!!.....Umewezaje kununua simu na unashundwa kununua vocha??
b)Mtu anakuazima gari na unampa kwa roho safi tu,halafu anakwaruzana
huko na kikimbiza gari gereji mchwara huko wanaanza kukuharibia gari
hali angekwambia wewe una fundi wako unayemwamini,sasa anafanya hayo
yote na hasemi,wewe ukija kushtuka siku moja unakuta some spears kwenye
gari hazipo....ama mtu anakwenda huko halafu anakutana na stickers basi
ananunua na kubandika kwa gari yako....hivi umeazima gari yangu
ukanipambie au utumie na kuirudisha,tena mbaya zaidi eti mtu anakuwekea
masticker ya kipepo kabisa na yeye anafurahia...sijui Majani,Kappa au
Monster Power...jamani Ni Marufuku kabisaaa,ukiazima kitu kirudishe
hivyo hivyo na usijifanye wewe ndio mwenyejiiiiiiiii
c)Mtu
amekuja kwako kukutembelea may be anakaa wiki moja au siku kadhaa,kwa
kuwa ni mgeni hapa ni nyumbani pa kuazima...sasa unakuta mtu anaanza
kupanga na kupangalua mara kochi hili ageuzie kule,pambo hili aweke kule
yaani wewe ukitoka kwa mishe mishe unakuta everything has
changed,jamani hapa kwako? hata kama umetamani kunisaidia kwanini
usiniulize? unajua kuna saa mnavuruga mahusiano ya watu hivi hivi,yaani
mwenyewe mlimbwende amepanga na kupamba na umekubali for sake of love
halafu huyu mfukunyuku anakuja na kuharibu kisha anaondoka,unafikiri
akija huyo mlimbwende siku moja unamwambiaje kama sio dharau hiyo!!!!
Ipo mifano mingi sana,lakini nimesema marufuku tena marufuku kabisa!!
HESHIMU MIPAKA YA CHOCHOTE UNACHOPEWA,SIO UNAKARIBISHWA SEBULENI WEWE UNAENDA MPAKA CHUMBANI AAAAH!!
......Sema neno na wewe kama tumeelewana!!!
N.B;Hii ni kwa faida ya mahusiano na urafiki wa ko na watu,na hii
inawahusu watu wenye akili timamu tu na wanaojielewa na kujitambua!!
@Kwa hisani kubwa ya Chavala Ideas Platform <http://chavalamedia.blogspot.com/>
(c)2013