John Shabani:Mwalimu na Mwimbaji wa
Injili aliyepitia magumu ya maisha.
John Shabani
|
JOHN Shabani si jina geni masikioni mwa watu hasa wapenzi wa
muziki wa injili na wanafunzi wa muziki huo.
John mzaliwa wa kijiji cha Kirando katika kitongoji cha
Nyankima, kata ya sunuka, Wilaya ya Kigoma Vijijini, anatokea katika ukoo wa
waumini wazuri wa dini ya kiislam.
Muimbaji huyo ambaye umaarufu wake uliwika baada ya kushiriki
tamasha la pasaka ambalo anasem akuwa liliinua uimbaji wake na anatamani kama
atapewa nafasi ya kushiriki tena kwa miaka ijao ikiwemo mwaka huu.
Anasema kuwa historia yake baada ya kumaliza elimu ya msingi
katika shule ya msingi kirando, alijiunga na elimu ya sekondari, lakini
kutokana na itikadi za kidini, alijikuta akiwa katika wakati mgumu wa kupigwa
vita na wazazi, kwasababu ya uamuzi wake wa kujiunga na Dini ya kikristo hali
iliyomsababishia muimbaji huyo kuishi miaka mingi akiwa mbali na wazazi wake.
Mwaka 1992, John akiwa kijana mdogo, alipata ufadhili wa kwenda
nchini Kongo ambako huko alijifunza muziki na kusoma Chuo cha Biblia na ndipo kipaji
chake cha kutunga nyimbo na kuimba kilijitokeza kwa kasi.
Muimbaji huyo anasema kuwa hakutaka kuona mtu yeyote akiwa
katika hali ya kukata tamaa, maana alifahamu madhara yake kwasababu hiyo,
alianzisha vikundi mbalimbali vya vijana akiwa na lengo la kuwaelimisha ili
kujikwamua katika hali ya kukata tamaa na kutokujihusisha na vitendo viovu kama
vile madawa ya kulevya, Ukahaba na anasa za kila aina mambo ambayo aliyapiga
vita.
Shabani anasema kuwa ameishi miaka mingi kama yatima, lakini
hali hiyo imemsaidia kujifunza mengi na kuwa na tabia njema, kumheshimu na
kumthamini kila mtu, hali hiyo ilimfanya kupata kibali machoni pa wengi.
Anasema kuwa amekuwa msaada kwa vijana wengi ndani na nje ya
nchi na kuwakwamua waliokuwa wamekata tamaa na kujihusisha na vitendo viovu.Pia
kutokana na ujuzi wa muziki alioupata na kipaji alichonacho cha kutunga,
kuandika nyimbo na kuimba, anasema kuwa amekuwa msaada kwa waimbaji mbalimbali
binafsi na vikundi , hasa nyimbo za Injili.
Mwaka 2001 John alifunga pingu za maisha na Debora Shabani na
mwaka 2002 walifanikiwa kupata mtoto wa kike aitwae Joyce, akiwa na maana ya
kuyasahau maisha ya huzuni na shida na kujitabiria maisha ya furaha.
Mwaka 2004, John aliajiriwa katika kampuni ya Msama promotions
ya jijini Dare es salaam, kampuni inayojihusisha na kuinua vipaji na pia
kuwainua vijana na watu wa rika na jinsia zote waliokata tamaa ya maisha na
hasa wale walioko vijiweni wakijihusisha na madawa ya kulevya, ukahabaa
Albamu yake ya kwanza Marufuku kukata tama anasema kuwa imewasaidia
wengi waliokata tamaa na kuwapa matumaini mapya albamu hiyo na nyingine
alioirekodi mwaka 2009 zilizoitwa huu ni wakati wangu na Moyo wangu.
John ametembelea nchi mbalimbali, akijifunza maisha ya watu
ikiwemo kugundua kwamba karibu asilimia kubwa ya wanadamu, awe maskini, tajiri,
msomi au asiye na elimu, wenye vyeo au waajiriwa, watoto kwa wakubwa, wanaume
kwa wanawake, awe mzungu au mweusi n.k, wote kwa njia moja au nyingine
wamepitia katika hali ya kukata tamaa au kukatishwa tamaa na jambo fulani, mtu,
watu, hali au mazingira fulani.
Ndipo mwaka 2006, alipata maono na msukumo mkubwa wa kuandika
Kitabu ambacho kitakuwa msaada kwa njia moja au nyingine kwa kila
atakayekipata. Kitabu hicho kinaitwa Marufuku kukata tama. Kitabu hicho pamoja
na kile kiitwacho “Mafanikio yatokanayo na kusifu na kumwabudu Mungu”
vinategemea kukamilika baada ya miezi miwili.
Mwaka 208 sitausahau ilikuwa
ni siku ya huzuni na majonzi, siku ya kilio na kuomboleza. ni siku alipofariki
mke wake mpendwa na mwimbaji maarufu wa muziki wa Injili, Debora Shabani,
mwimbaji aliyegusa mioyo ya watu wengi ndani na nje ya nchi, niliumia sana
lakini sikukata tamaa”anasema.
Shabani alitunukiwa tuzo ya heshima pamoja na cheti kwa kutambua
mchango wake kwa ajili ya kuinua vipaji na pia kuchangia kuinua muziki wa
Injili Afrika mashariki na kati. Pamoja na hayo amekua akianzisha vikundi
mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu Tuzo anayosema kuwa ilitolewa na kampuni ya
Christian promoters Ltd, Pia ni miongoni mwa waanzilishi na kiongozi wa Chama
cha muziki wa injili Tanzania (Chamuita).
Mwaka 2011, John alipata heshima kubwa kama mwalimu, kuongoza
kundi la waimbaji (Tanzania gospel all stars) kuimba wimbo maalum wa miaka 50
ya uhuru wa Tanzania.
Anasema kuwa pamoja na mzigo mkubwa aliokuwa nao kwa kidogo
anachopata,amehakikisha kuwa anaisaidia jamii, hasa watu wenye ulemavu, wajane
na yatima Vijana waishio katika mazingira magumu, pamoja na wakimbizi. Tayari
ameanza mikakati ya kusajili Taasisi Hope Foundation kwa ajili ya maono hayo.
Pamoja na malengo mbalimbali aliyonbayo Shabani, lakini pia ni
kuwa na kituo cha watoto na vijana, lengo ni kuandaa kizazi chenye maadili
mema, kuibua, kutambua na kuinua vipaji vya watoto na vijana, mbinu na mikakati
ya kuwakwamua watoto
Pia anasema kuwa mpango huo unalenga kutafuta ufadhili kwa ajili
ya kuaendeleza vijana kielimu pamoja na kuwawezesha pale inapobidi, kuandaa
matamasha ya watoto na vijana, kuunganisha watoto na vijana wengine duniani,
kuwapa kipaumbele watoto na vijana wenye elemavu, kuwa na kiwanja kwa ajili ya
michezo mbalimbali ya watoto na vijan.
Kwa sasa anajishughulisha na kufundisha bendi,vikundi na
waimbaji binafsi na kusema kuwa lengo ni Kufundisha kuimba au kunyoosha,Jinsi
ya kuitumia sauti kuitunza na kuitawala, Historia ya muziki na maadhi ya muziki, Sifa
na mbinu za kuwa mwimbaji bora, Matumizi ya kipaza sauti,Kuwatungia nyimbo au
kurekebisha nyimbo zilizotungwa tayari, Kutoa ushauri kwa wanaotatarajia
kuingia studio, mbinu za kuitangaza albamu au nyimbo zikubalike na Kutengeneza
muziki wenye viwango.