CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

Papaa On Tuesday......Shida Haina Mjuzi Wala Mwenyewe......Think Positive



Ikiwa imebaki siku moja iwe tarehe 14 Novermber kusheherekea siku yangu ya Kuzaliwa na kuhitimisha Mwaka wangu wa mwisho kabisa kuwa Single ili niweze kuingia katika Next Level ya Uandishi wa Papaa On Tuesday, sababu ninajua kila level ya maisha ina mtazamo wake wa kiufahamu katika kutazama mambo mbalimbali yanavyoendelea mtu anayefanya biashara kama angekuwa anaandika Papaa On Tuesday uandishi wake ungekuwa unatofautiana sana na yule anayefanya kazi za Ofisi, Mchungaji angekuwa anatofautiana sana Daktari vivyo hivyo Single na Mtu mwenye familia piga ua kuna namna tunatofautiana tunavyo experience maisha. I am so excited ninapoitazama Season 2 ya Uandishi wa Papaa On Tuesday.

Maisha tunayoishi na miaka tuliyonayo kila mtu analo neno la kusema kabisa kuwa kuna hatua amepiga na kuna mahali ametoka kwenda mahala pengine. Kupitia mashauri ya wazazi ana wazee na watu wazima na elimu tunayoisoma shuleni na mafundisho ya dini tunayosikia kila tunapokwenda katika nyumba za ibada yanatuelekeza namna ya kukabiliana na Changamoto mbalimbali katika maisha. Na katika maelekezo ama mafunzo haya yamkini huwa tunajiaminisha kuwa tumeelewa kabisa kile ambacho tunatakiwa kukifanya katika maisha. Kama kuna jambo halijawahi kukupata ni rahisi sana kukosoa na kuwacheka ama kumcheka yule linayemshinda ukijiaminisha kuwa either ni lege lege ama anajidekeza wazungu wakasema "experience is a good teacher" kwenye makala zangu za Papaa On Tuesday mwenzi june kuwa Usitukane Wakunga wakati Uzazi Ungalipo gonga hapa kama haukuwa umesoma...http://samsasali.blogspot.com/2012/06/papaa-on-tuesdayusitukane-wakunga.html. Jambo linapokuwa limekupata basi unajikuta masomo yale yote uliyojifunza kukabiliana na jambo ama shida yanapokuwa yanapotea na practically unaanza kukabiliana na hiyo Changamoto.
Shida haina mjuzi wala haina mwenyewe kuna nyakati tumekuwa tukijiuliza WHY ME??WHY ME Always??na kudhani shida ni zetu peke yetu na dunia nzima hawana shida kama sisi, na wakati mwingine tumeona kama kipimo cha shida za wengine ni kidogo kama sio chepesi kuliko tulichopimiwa sisi zinapotukabili na kuona wengine wana ujuzi nazo na wanaweza kuzikabili kuliko sisi tunavyoweza kuzikabili, nyakati zingine tumedhani maumbile yetu yamesababisha tupate shida tulizo nazo, wengine wanadhani wangekuwa na maumbile kama akina fulani leo hii wangekuwa wako mbali, wengine wanalaumu rangi walizonazo na kuona Mungu alikosea, wengine wanalaumu ukoo walio zaliwa wengine wanalaumu elimu walizozipata na kuzikosa na kudhani kama wangekuwa kama fulani basi shida zao zingetatulika kirahisi sana sana. Kuna siku Niliwahi andika laiti kama Mioyo ingekuwa ya Vioo gonga hapa usome...http://samsasali.blogspot.com/2011/07/papaa-on-tuesdaylaiti-kama-mioyo.html kuwa wengine wamenyamaza unadhani wao ni wajuzi wa shida walizonazo na wao hawana shida kuliko wewe. Shida haina mwenyewe wla shida haina Mjuzi.
Kuna nyakati zingine tumepata shida tuka waeleza watu badala ya kutusaidia ndio wakatukatisha tamaa kabisa, kuna nyakati tuliwaeleza watu shida zetu zikageuka kuwa matangazo kwenye jamii changamoto inayotukabili kizazi chetu nani yuko tayari kukabiliana na shida??hiki kizazi ambacho swali likiwa gumu mtu anaandika google, Kizazi ambacho level ya Uvumilivu na Kustahimili kinazidi kushuka, Kizazi ambacho watu wako tayari kuuwa wapate fedha, Kizazi ambacho mtu yuko tayari kufanya harusi ya mamilioni keshokutwa akamuacha Mkewe, Kizazi ambacho mtu anakaa na relationship miaka 8 kisha anamuacha mtu kwa sababu amepata mwenye fedha, Kizazi ambacho kwa sababu ya Njaa watu wamekuwa tayari kuuza miili yao kwa ushoga na uchangudoa ili kukabiliana na njaa, Kizazi ambacho Wanafunzi wanataka kuishi sawa na Wafanyabiashara kizazi kinachopenda 'Soft Touch and Appear". Nani yuko tayari Kukaa  kwenye ndoa ambayo hawana mtoto kwa miaka kadhaa, nani yuko tayari asisaliti imani yake ili mradi apitie jambo fulani.
Kila mtu ana shida na changamoto zake shida haina mjuzi wala mwenyewe unaweza ukawa na Kila kItu kwenye maisha ukawa na fedha ukawa na gari ukawa na mavazi mazuri na mke ama mume mzuri lakini hakuna amani ndani ya ndoa, unaweza kuwa na mshahara mzuri na nyumba nzuri lakini hauna inner satisfaction, inawezekana ukawa unafanya biashara unapata fedha kila siku lakini una ugonjwa unaokutesa, unaweza kuwa na elimu nzuri sana na akili njema sana ajabu hupati Usingizi na unakunywa mpaka madawa na sindano, yawezekana una umbile zuri sana na raha sana lakini ukiwa period mpaka hauoni thamani ya kuishi unatamani kufa, pengine una kila kitu unachodhani unapaswa kuwa nacho lakini unajiuliza kwanini wanaume wanakukimbia, asikuambie mtu shida haina mjuzi wala haina mwenyewe. Kuna mambo kadha wa kadha ambayo kwa watu wasiotujua kwa vile tumeamua kuyaficha tunaonekana tuko pouwa sana lakini kama leo ingekuwa kila mtu shida yake inaonekana Live Live kama CCTV ndipo ungejua kuwa shida haina mwenyewe wala haina mjuzi maana wewe unaloliweza mwingine linamshinda lile linalokushinda yeye analiweza unatamani mbadilishane lakini sasa sio fungu lake wala lako la kugawa shida hizo.
Unafanya nini unapotokea unashida???Unaomba Mungu, Unalaumu waliopelekea shida??Unalaumu Background yako??Unalaumu mwenzi wako na kujiona wewe ni bora kuliko mwenzako, Unamlaumu Mwajiri wako??Think Positive. Jijengee tabia ya Kukabiliana na Changamoto zinazokukabili wewe mwenyewe Kikamilifu chukua wajibu wa Kutafuta Ufumbuzi wewe mwenyewe pasipo kulaumu wengine, jione wewe pia ni sehemu ya tatizo na unapaswa kutafuta ufumbuzi kwa namna moja ama nyingine. Kuna Ujinga mmoja nimeuona kwenye maisha ya Usuluhishi tangu nilipopata neema ya kusuluhisha baadhi ya migogoro ya watu. Nakumbuka kulikuwa na ndoa moja ina misukosuko sana, mkaka ambaye ni mume kupitia Papaa On Tuesday ninazoziandika aliamini kabisa moyoni mwake kuwa akiongea na mimi suluhu itapatikana, simfahamu wala hanifahamu ila alijenga imani, nilipoongea nae akaniaelezaaaaa nikasikiliza nikaona kweli ni tatizo nikaomba nionane na mke wake nae nilipokutana nae akanielezaaaaa mwisho nikabaini shida iko wapi tukatengeneza appointment ya wote wawili, nikamwomba sana Mungu anipe mpenyo wa suluhu katika jambo hilo la wanandoa. Siku tuliyokutana kila mtu alielezaaaaaaaaa yaani kila mtua alifunguka ki hasa kisha tukauliza OK tumeshasikia What Next???Kila Mtu akaona kosa lake wakaombana msamaha yakaisha Ujinga niliokuja ubaini ni kwamba Mambo ambayo mngekaaa wenyewe nyumbani na kuongea na kufunguka eti mnahitaji awepo mtu Neutral ambaye yeye infact atakayoyaongea ninyi wenyewe ndo watekelezaji wa jambo hilo ambalo. Huwa ninajiuliza hivi Mshauri wa mambo nae yakimsibu ya Kumsibu anaendaga wapi??Ok labda niseme mimi yakinisibu huwa ninaenda wapi, na huko ninakoendaga nae yakimsibu ya Kumsibu anaendaga wapi???Shida haina mwenyewe.

Niliwahi kusema Ukizimia siku ya Taabu Nguvu zako ni Chache... http://samsasali.blogspot.com/2010/07/papaa-on-tuesdayukizimia-siku-ya-tabu.html.

Ze Blogger
0713494110