Friends On Friday Twende Kazi
Friends On Friday Event Number Moko ya Vijana wa madhehebu yote ilifanyika Ijumaa ya Wiki Iliyopita na safari Hii Friends On Friday Inakujua tarehe 6 Sept, 2013 ikiwa na Jina "FOF Maridadi"
Blogger Ambwene Mwamwaja Afafanua Gospel Kitaa Blog Inavyokusanya Habari
Mtangazaji wa WAPO Radio na Mmiliki wa Blog Ya Gospel Kitaa, amefunguka na kueleza kuwa ana network Kubwa ya watu wanaompa habari karibu nchi nzima na Kuweza kuziratibu akiwa Nchini Uingereza. Blogger huyo maarufu Ambwene Michael Mwamwaja alieleza kuwa mbali na kupata taarifa hizo pia huzifanyia uthibitisho wa habari kabla hajazituma katika Blog.
Blogger huyo maarufu ambaye kwa sasa anaishi Nchini Uingereza yuko nchini kwa mapumziko mafupi ambapo alieleza kwa kina namna ambavyos aliweza iwakilisha Tanzania katika Tuzo za Africa Gospel Music Awards ambapo Mwanamuziki wa Injili Kutoka Tanzania Christina Shusho aliwakilisha Vema nchi ya Tanzania.
Mwamwaja ni Mmiliki wa blog ya www.gospelkitaa.blogspot.com aliyasema hayo alipokuwa akihojiwa na Kipindi nambari one cha Gospel Tanzania "Chomoza".
KUNA VITA NDIO, LAKINI PIA KUNA SHEREHE JESHINI....HONGERA LUTENI FRANK MNDEME!!!
Kwa namna ya kipekee, natamani uone ni jinsi gani Shughuli ya Kuoa inavyoheshimiwa hata na Jeshi....wanaamini mwanajeshi pia anahitaji msaidizi na mwenza, na ndio maana ukianza mafunzo ya jeshi,ama kujiunga na jeshi na kuwa mwanajeshi....unatakiwa kulitumikia jeshi ukiwa single kwa miaka 6 (Sijui kama katazo hili lina nguvu hata sasa) na ndio unaruhusiwa kuoa kiheshima!!
Luteni Frank Mndeme na mkewe |
Unaweza kuona jinsi heshima ilivyo... |
Yaani hii ni Official Hongera! |
HUU NI MFANO WA HARUSI ZA KIJESHI, NIMEPATA PICHA CHACHE ZA NAMNA ILIVYOKUWA WAKATI LUTENI FRANK MNDEME ALIPOOA SIKU CHACHE ZILIZOPITA!!
Huyu ni mdogo wa Mathew Mndeme, mmoja wa waandishi wa Blog hii....Simple Man with always a story to tell!
CHAVALA IDEAS PLATFORM Inawatakia kila lakheri na fanaka ya maisha mema wanandoa hawa...furaha ya ndoa na upendo wa kweli udumu na kukua kila leo,Amen!
Hotline; +255 713 883 797
Papaa On Tuesday.....Kwanini Hatujifunzi Kutokana na Makosa?
Unakuta makosa ya matumizi mabaya ya Mshahara wako yanajirudia kila mwezi hakuna siku ambayo mshahara ukakutana, mshahara wa mwezi huu haujawahi kusalimiana na mashahara wa mwezi ujao wanapishana siku wiki nzima, makosa hayo yamekupelekea kwenye madeni ya kila mwezi unajikuta wewe ukishika mshahara huna chako umewashikia wengine hela zao unabaki kujisikia vibaya kujisikia vibaya hakukusaidii mwezi ujao usirudie makosa, kujifunza katika tatizo na kuamua kubadilika ndiko kutakusababisha kubadilika kutoka katika hali uliyonayo.
Kuna watu wamewahi jichukia nafsi zao na tabia zao, na kuna wengine waliwahi jiapiza kuwa hawata rudia tena lakini ndo utadhani wamejiapiza kufanya zaidi ya alivyokuwa anafanya mwanzo. Kujifunza ni mfumo wa kila siku lakini kujifunza kutokana na Makosa hata Serikali yetu imekuwa ni tatizo. Makosa yale yale yanayotokea kwenye Serikali na kupelekea upotevu wa fedha nyingi za Serikali, ndio huo huo pia utatokea mwakani na mwakakeshokutwa pia. Makosa yale yale yanayoitesa CCM ndiyo makosa hay ohayo yatatesa NCCR-Mageuzi ndo hay ohayo yataitesa CHADEMA na ndo hay ohayo yataitesa TLP. Sababu zile zile za kufeli kwa wadogo zetu kwenye shule za Sekondari mwaka huu ndo hizo hizo pia zitasababisha mwakani watu wafeli. Makosa yale yale tuliyofanya kwenye Uchaguzi wa mwaka 2010 ndo yale yale 2015 kwani kuna jipya??
Changamoto kubwa sana ambayo inainyemelea Tanzania yetu ni watu kupenda kuambiwa, yaani akiwa anaumwa yeye mwenyewe hawezi kujitesa kunywa maji, ila Daktari akimwambia asipokunywa maji atakufa basi atakunywa maji mpaka atawaboa, wengi wanaenda Gym siku hizi si kwa sababu wanapenda mazoezi aaah wanaenda “kujikinga na magonjwa” wakisha pungua unene wanarudia yale yale. Kama hauna “mood” ya mazoezi yatakushinda utafanya siku mbili tatu unaacha why?hatujifunzi kupitia makosa yetu.
Kila mtu anapaswa kujifunza kutokana na makosa, usiogope kukosea sababu ni sehemu ya kujifunza ukiogopa kukosea hautakuja kuweza ila ukikosea unajua kwanini ulikosea na nini au wapi urekebishe. Kabla ya kujua kuendesha baiskeli wengi walidondoka, kabla ya kuweza kuendesha gari wengi waligonga kwenye Reverse ila walipogonga ndivyo walivyozidi kujifunza. Kujifunza ni gharama,gharama ya kujifunza ni ndogo ukilinganisha na gharama ya kurudia kosa lile lile, kuna mambo ambayo pengine yana gharimu maisha yako kwa sasa kwa sababu tu kukosea kuchagua kitu Fulani, pengine gari ulilonunua linakugharimu sababu tu ya kukosea kuchagua, wengine wenzi wao wa maisha, wengine ni taaluma zao kila mtu ana “makovu yasiyokuwa na hisia” ambayo yanatesa watu wengi.
Zahma ambayo mtu ameipata kutafuta nyumba ya kupanga na kujikusanyia kodi ya nyumba ndo makosa hay ohayo yatatokea katika kutafuta nyumba na kukusanya kodi, kwanini?sababu hatuna utamaduni wa kujifunza kutokana na makosa. Makosa yale yale waliyofanya wazazi wetu katika umri wao wa kufanya maamuzi mazito ndiyo hayo hayo pia yatatokea na kwetu na kwenye vizazi vyetu. Usipojijengea utamaduni wa kujifunza hakuna wa kukufunza kwa kizazi chetu. Kwani wewe unafunzwa na nani makosa yale ambayo wewe uliyafanya ukaharibikiwa mapema si ajabu watoto wako pia yakawatokea kwa mwamvuli wa "uzungu" watoto wako katika umri wako ule wa kujua mema na mabaya watadondokea katika shimo lile lile. Tarehe ya mtoto kuzaliwa iko mbele kuliko anniversary ya Harusi yenu.
Kuna watu huwa wanasema usijifunze kwa walioshindwa maana na wewe utashindwa, kuna mtu aliwahi sema if you have never done any mistake,you have never tried something new. Kwanini uogope kujifunza kwa walioshindwa, kujifunza kwao kwenye mapungufu yao inasababisha mwerevu kujua njia gani aspite, kujifunza kwa waliofanikiwa peke yake ni mfumo ambao tumetengenezewa ili kutujengea ujasiri wa kuogopa. ndio maana kwenye interviews hata za ndoa utakuta wanaitwa watu ambao wamefanikiwa wanaonesha namna ambavyo wamefanikiwa mbona hatujawahi waita watu ambao wamechemsha tukawahoji kwanini walichemsha?kisa na mkasa eti hatuna jipya la kujifunza kwa walioshindwa ni kweli hatuna la kujifunza, katika kushindwa kwako mambo mengi ni kweli huwezi mfunza mtu?labda kama hatujajua makosa yetu ni yepi ndio maana hatuwezi wafunza wengine kile tulichokosea. Wote tunapenda story ya Petro aliyemkana Yesu mara tatu kisha akatengeneza, lakini hakuna mtu anayejifunza kwa Yuda aliyemkana Yesu kisha akajitundika kitanzi.
…//Papaa
0713 494110
Subscribe to:
Posts (Atom)