CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

Papaa On Tuesday....Mtu Aonavyo Nafsini Mwake Ndivyo Alivyo


Ninakila Sababu ya Kumshukuru Mungu kula Inapoitwa leo kwa ajili ya Upendo wake kwangu kwenye maisha yangu, ninamshukuru Sababu nina ishi vile atakavyo na sio kama watu wengi watakavyo maana kwenye Kiswahili tunajifunza methali inayosema "Miluzi Mingi Inampoteza Mbwa" we unadhani uwongo??we ishi kama watu wanavyotaka nakuambia utapotea sana. Jua kwanini Upo na Unapaswa Kufanya Nini kwenye maisha utafurahia maisha yako.

Kwenye maisha nimekutana na watu wengine walitakiwa kuwa Wanajeshi wamekuwa Viongozi wa dini, nimekutana na watu walitakiwa kuwa Waalimu Kwa sababu mbali mbali wamekuwa Askari wa Barabarani, kuna watu walitakiwa kuwa Askari Magereza wamekuwa wake za Wachungaji kwani we unadhani bongo maisha yana formula??wengi tunafanya kazi ili tupate hela, kuna wacheza movie wengi sana wako maofisini, kuna waandishi wa habari wengi sana wanauza mitumba, kuna wabunifu wengi sana mambo wako sehemu kwa ajili ya
kuganga njaa, kwani we hujijui unapaswa kwa nani??wengine wameajiriwa katika kazi ambazo kwa kweli hawafurahii wanaenda maofisini huku wamekunja nyuso siku wanayocheka ni siku ya Mshahara tu lakini ndani ya mioyo yao wanajua kabisa hawana furaha wanachofanya kwa sasa.

Wewe Unajiona ni nani ndani yako??Kwanini hujaanza kufanya unavyojiona??maana katika kuona tunatofautiana kuna wengine wanajiona wao ni kama mapanzi na kuna wengine wanajiona wao ni kama Simba. Katika maisha ukishinda nafsi yako ujue hakuna cha kukuzuia katika maisha. Wengi tumeshindwa kuwa vile tunavyojiona ndani, vile unavyojiona ndani inaweza kukufanya Ukafurahia ama Ukanyong'onyea maana mtu aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo. Kuna watu wanapokuwa wanawaza mambo mbalimbali wao wanajiona kabisa hawawezi, anatazama changamoto mbalimbali akijumlisha akitoa anajiona kabisa amefeli zoezi hata kabla hajalifanya, we hujawahi kukutana na mtu anasema "mimi nilijua tu kuwa nitashindwa", mara nyingi sana tunakuwa na picha ya ndani pengine tunashinda ama tunashindwa katika mambo fulani.

Unavyojiona nafsini mwako ndivyo ulivyo, kuna mambo ukitazama unaona kabisa unaweza kufanya na ukafanya vizuri, kuna watu wanajua yaani wakiamua kabisa wakiamua ile kutoka ndani ya mioyo wanaweza fanya mambo mazuri sana, kuna watu wanajua kabisa yaaani wakiamua ile ki kweli kweliiiii wanaweza kuimba sana, kuna watu wakiamua ile kikweliii Kweliii Wanaweza Kufanya maajabu, utasikia mtu anasema "Mi Nikiamua Mimi, Mtashangaa" ajabu sana huyu mtu unashangaa haamui. Huyu Mtu kuna picha anaiona ndani yake ambayo mtu mwingine haioni vile ilivyo, tatizo sasa hofu, shaka, wasi wasi swali linakuja "What If mambo yasiwe vile ninavyodhani", nafsi inaona picha kubwa ya kuweza ila akili inaanza ushuhuda.

Hofu na mashaka na wasi wasi na kuto kujiamini kumesababisha watu wengi sana katika maisha wasiamue ile kikweliii Kweliii, huwezi kuishinda hofu as longer you have an Option, huwezi kuamua Kikwelii Kweliii sababu unajia mbadala, Ukimuona Mtu ameamua Kikwelii Kweliii Ujue amekataa Kutosheka na Afadhari. Ukitosheka na Afadhari kwenye maisha hauwezi kuthubutu, utakuwa unajiona kabisa wewe ni Simba lakini Unamatendo ya Mbuzi, Ikitazama Simba wengine unajiona kabisa mbona mimi ni Simba??lakini ikifika saa ya kuunguruma kama Simba unalia Meeee Meee Kama Mbuzi. Ukijitazama nafsini mwako unajua Kabisa Uwezo wa Kufanya zaidi ya hapo unapofanya sasa unao lakini hujawahi jiuliza kwa nini haufanyi kwa kiwango kile kile??we unadhani uko huvyo ulivyo sababu huwezi??huitaji mtu wa pili kukuthibitishia kuwa unaweza unajua kuwa unaweza na nafsi yako inakushihudia kuwa unaweza issue sasa kuishinda hofu.

Yaani mtu ana hofu kubwa ya kuogopa hofu ambayo haipo, utamsikia mtu anasema mara niamue kikwelii kweliii Ibumeeee, itokee negative sijui itakuaje?tuna mawazo mengi sana yanayoshindana na nafsi zetu, nafsi inasema Unaweza akili inasema hujaona wenzio wamechemsha, nafsi inasema unaweza kufanya zaidi, akili inasema utajichosha bure, Ukiweza Ishinda nafsi yako na akili yako jua hakuna wa kukuzuia, ugomvi wa nafsi na akili hauwezi kuisha kwenye maisha maana mwili unajipendelea sababu uko njee nafsi inataka kujilipua uende kule unakopaswa kwenda ndio maana Biblia ikaandika "roho/nafsi i radhi lakini mwili ni dhaifu" achana kabisa na mtu wa nje anasababu milioni 5 za kutokufanya kitu kimoja ambacho nafsi na roho yako viko tayari kufanya.

Unajiona wewe ni nani na kwanini hujaanza fanya kile ambacho wewe unajiona unapaswa kuwa, ukitazama vizuri utagundua kwanza haujauamua kuwa vile unavyotaka kuwa na pili una hofu ya kule unakotaka kuwa unahisi mambo yanaweza kuwa sio mambo ukabaki kujuta, umeona heri ubake hapo hapo ulipo kwenye maisha kuliko uende usikokujua, mwaka huu hautaakuwa tofauti sana na mwaka jana, waliofanya mapya ni wale walioamua kufanya mambo mapya, risk takers watu wanaothubutu ndio ambao hupiga hatua katika maisha yao. Mtu aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo.