CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

Papaa On Tuesday…..Unao Uwezo Wa Kuchagua Cha Kufanya Lakini Huna Uchaguzi na Matokeo Ya Kile Ulichokichagua Kukifanya.

Tukiwa bado katika Maombolezo ya Kupoteza ndugu zetu katika Mkoa wa Arusha kwa sababu zinazosadikika ni za kisiasa nachukua fursa hii kuwapa pole ndugu zetu wote ambao wamefariki lakini pia na wote waliojeruhiwa hasa hasa Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha rafiki yangu na mtumishi katika Shamba la Bwana Bw. Amani Golugwa pole sana na “majanga” ya Kisiasa. Nimeamini kweli tunao uchaguzi wa nini cha kufanya lakini hatuna uchaguzi wa kuzia matokeo ya kile tulichokichagua kinapotokea. Ukichagua Siasa basi matokeo ya Siasa ujue huna maamuzi nayo.

Wengi tuko leo hivi tulivyo kama matokeo ya kile ambacho tulikichagua katika maisha, na wakati huo tuliona sie ndio wenye mana kuliko wengine wote wakati wa kuchagua lakini hatukujua kuwa kile tulichokichagua hatuna uwezo wa kuhimili matokeo yake ya kwenye maisha. Wengi wetu wakati tunahimizwa kwenda shule tuliendekeza ubishoo na usharubalo, tulikuwa na uwezo wa kuamua either kusoma ama kuendekeza ujinga wa makuzi wakati huo kwa kufuata mkumbo wa mambo yaliyokuwa yakiendelea. Pengine kila ukikaa unajicheka kwa kile ambacho ulikichagua wakati huo na ukasahau methali ya Majuto ni Mjukuu waliponena wahenga, tulijiona sisi ndio tunaojua kuliko wale waliokuwa wakituasa na kutuhusia. Leo tumekuwa na akili tunatamani zile zama tulizokuwa tunakula chips na kuvaa raba za gharama na kuendekeza ubishoo zirudi tena ili tufanye kweli, lakini wapi kila jambo na majira yake. Wengine tunasoma Elimu za Watu wazima sit u tulikuwa na tatizo la ada kipindi hicho la hasha ila tulipokuwa nacho tulitumia na kilipoisha tukajijutia kwenye maisha.

Kuna mdada mmoja rafiki yangu anaishi kwenye mateso makubwa ya ndoa yake na amebaki kujutia maamuzo aliyoyachagua kuyafanya kisa na mkasa anasema hakujua, kama angelijua angechagua kuendelea na maisha yake kwanza ndipo achague kuolewa akiwa na akili timamu. Majanga mengi sana ambayo tunapitia kwenye ndoa na mahusiano ni kutokana na maamuzi yetu ya kukurupuka, maamuzi yetu ya kujiaminisha kuwa tuko sahihi kuliko wengine matokeo yake tunabakia kufa na tai shingoni. Kwani uwongo??ukikaa mwenyewe hujiambia kuwa laiti kama ungelijua usongechagua kuolewa ama kuoa Fulani kisa na mkasa matokeo ya kile ulichokichagua kwenye maisha. Kuna wengine walitaka kuolewa so kilichotokea wakabeba mimba wakidhani maisha yale ya honey baby and sweetheart yataendelea, kongwa walilojitishwa na nira walizojifunga wamebaki kulilia moyoni, mkiwaona barabarani na kwenye facebook utadhani ni ndoa ya mfano kumbe si lolote si chochote kila mtu analala chumba chake nyumbani hakuna furaha ambayo inadhaniwa ipo wakiwa nje ya mlango wa nyumba yao wakikaa wenyewe wanatamani sana kurejesha maisha siku ambazo walikuwa wanacheka na kwenda kula bata na kuitana majina ya mahaba, leo yamebaki kuitana “wewe”, “Nanii”, “Stella”, “Sultani” dry dry dryyyyyyyyyy. Lady Jay d anasema anatamani kuwa kama zamani lakini ndo zama zimeisha tena maisha yamebaki kuishi kwenye matokeo yake.


Kuna Ofisi Fulani nilifanya kazi zamani kuna jamaa alicha kazi baada ya kupata kazi sehemu nyingine kwa ahadi ya project mpya alipohama kwetu akaenda kwingine ambako huko project ikakosa hela akabaki mtaani akajuta sana kwa uamuzi wake wa kuacha kazi alikuwa na muda wa kuchagua kuacha kazi ama kuanza upya sehemu nyingine matokeo ya maamuzi yetu mengi hayamo ndani ya matakwa yetu. Unaweza kuacha kazi sehemu moja ili ufanye kazi kwingine ukashangaa ulikokwenda ndo unapunguzwa wewe ama unahama nyumba moja kwenda nyingine kumbe unakokwenda ndo kuna zoezi la upanuzi wa barabara unabaki kusema ng’ombe wa masikini hazai. Wengine wamepata watoto mapema si kwa sababu walikuwa wanapenda kuzaa bali bali kilichotokea “ajali” ikasababisha waanze kuitwa “mama” ama “baba” wakati wa kudungunyuana walikuwa wanasikia raha ila ilipofika ujauzito wengine wakasema wakatoe ama wakatoa ujue ulikuwa na uchaguzi wakati wa kuamua lakini ukasahau unawajibika na matokeo ya kile ulichokiamua kwenye maisha yako.


Kuwajibika na matokeo ya yale tunayoyaamua ni wachache wetu wako tayari unapotaka kufanya maamuzi kwenye maisha jua kabisa wewe unawajibika na matokeo ya maamuzi unayochukua kwenye maisha. Kila ambacho unakichagua kukifanya jua kina matokeo na uwe tayari kupokea matokeo ya kile ulichokichagua kukifanya kwenye maisha.

0713 494110