Kuna utapeli fulani
unaendelea Tanzania na inaelekea wanaoufanya wamefanikiwa sana na wanaendelea
kufanikiwa kwani ni wa muda mrefu sasa. Nadhani matapeli hawa wanatumia ujinga
wetu maana sisi sio watu wakutafuta sana usahihi wa mambo kabla ya kusema au
kutoa maamuzi, pamoja na ujinga wetu wa kutaka kufanikiwa kwa haraka kwa njia
yeyote ile hata kama hatujafanya kazi na bila kutumia akili. Utapeli huu sio
mwingine bali ni ule wa wale watu wanaompigia mtu simu wakijifanya wanakujua
kabisa na wanaweza hata kukupa some backgrounds zako za kazi, ajira au elimu na
meninge hadi ukashawishika kuwa unayeongea naye ni mtu unayemfahamu/munayefahamiana
na hivyo kutokua na hofu na uhalisia wa anachokuambia. Baada ya hapo wanaanza
kukushawishi juu ya kuwasaidia kupata madawa ya kuhifadhi nafaka kwa madai kuwa
mawakala wao ambo wamekua wakizipata toka kwao wameanza kuleta uswahili hivyo
kwa vile unayeongea naye ndio anahusika na suppy, basi ameona ni vema akutumie
wewe “mpendwa anayekujua” ili angalau upate hiyo commission kubwa ambayo huwapa
ho mawakala na mugawane kidogo. Mara nyingi wanasema wanafanya kazi na shirika
la chakula duniani (FAO) au shirika la wakimbizi duniani (UNHCR) na wako
Kigoma.
Zaidi ya mwaka mmoja
sasa nikiwa ofisini walinipigia na aliyekua anaongea name alianza kwa
kujitambulisha kama graduate wa kitivo cha uhandishi cha chuo Kikuu Mlimani na
kwamba tulisoma wote mwaka mmoja wakati nikisoma degree ya kwanza lakini huenda
simkumbuki kwa sababu nilikua kiongozi wa fellowship na siwezi kuwa nakumbuka
wote niliokua nawaongoza. Yeye alikua fellowship. Alikua akiongea kwa kicheko na “bwana yesu”
asifiwe nyingi ili kunionesha ni kwa kiasi gani namfahamu na tunafahamiana. Kwa
bahati mbaya wakati ananipigia nilishasikia kwa umbali juu ya utapeli huo ambao
kwa kipindi hicho ndio ulikua umeanza tu na kushika kasi huku watu wengi wakiwa
wamepoteza mamilioni. Hivyo alipoanza kuongea ujinga wake wa kunipa commission
and all that, nilimwambia tu kuwa sina muda wa kujihusisha na biashara aliyokua
“anataka kunisaidia ili nipate pesa za bure”, kwa haraka na bila jasho. Alikua
disappointed sana kwa jibu langu hasa kutokana na muda mrefu alioutumia
kunishawishi nikubali “msaada aliokua ananipa kama mpendwa mwenzake”.
Leo asubuhi majira ya
saa nne nilipokea simu kwenye line yangu ya tigo na number iliyonigia ni 0717-093260. Mtu aliyenipigia alikua
anaongea kwa uchangamfu mkubwa na kwa furaha huku akitaja majina yangu yote na
kuniuliza iwapo kwa sasa niko DSM au nimesafiri. Aliniambia kuwa kafurahi
kusikia kuwa niko DSM kwani ndipo zilipo ofisi zao na kwamba alitaka
kuniunganisha zao ili nikachukue mzigo ambao utakua na cha juu kizuri sana.
Nilipoona anaendelea nilimuomba ajitambulishe...akaniambia anaitwa Lameck na
kuwa alishafanya kazi Planet International hapa chuo kikuu. Alipotamka hivyo
nikaanza kupata ukakasi kwani hapajawahi kuwa ofisi ya kampuni hiyo hapa Mlimani.
Nikamuuliza yuko wapi kwa sasa na kwa msisitizo akanijibu kuwa kwa sasa yuko
Serengeti National Park. Nikamuuliza iwapo anafanya kazi na TANAPA..akasema
hapana bali yuko na shirika moja la Kijerumani
linalojishughulisha na wanyamapori...na akijua kuwa niko Chuo Kikuu
alitafuta style nzuri ya “kuniingiza alipokusudia” ...maana
alianza kunieleza kuwa shirika lao linafanya “tafiti za wanyama pori katika
mbuga yetu ya Taifa kubwa sana”. Bado nikiwa najaribu kuunganisha “idadi
ya nukta kadhaa” akaniona mjinga sana na kuanza kunielezea jinsi
wanyawa walioko Serengeti wanavyo migrate kila mwaka kwenda Kenya.....na kuwa
wanahama wengi kama elfu mbili hivi...(nikapata nukta nyingine)..then
nikaingilia na kumsaidia kuwa hawavuki kwa maelefu bali ni zaidi ya milioni moja wanahama
na kurudi kila mwaka. Pomaja na utafiti kazi nyingine wanayofanya ni pamoja na
kutoa chanjo kwa wanyama hawa maana wanaporudi wanakua wamerudi na magonjwa toka Kenya.
Hapa ndipo alipopotea
njia zaidi kwani kati ya jambo ninalolijua kwa mapana kidogo ni hii movement ya
wild beasts, zebra na wengine walioko Serengeti . Nikamuonesha kushangaa kuwa
wanawezaje kuwapa chanjo wanyama wengi
namna hii (na kumuonesha najua chanjo ni nini nikajifanya mhaya kidogo na kutamka
vaccination)...akaanza kujichanganya kuwa wao wana njia tatu za kutoa
chanjo maana ni kweli kuwa wanyama ni wengi...kwanza wanatengeneza
majosho/mabwawa/madimbwi ambayo wanaweka dawa na hiyo wale wanyama
wanapokua wanarudi wanatumbukia na hivyo automatically wanakua wamepata chanjo.
Hapa akachemka zaidi...nikamuuliza hivi kuogesha ng’ombe kwenye majosho ni
chanjo au ni kuua kupe na viroboto? Nikamuuliza kuna chanjo inafanyika juu ya
ngozi?...alipoona hana majibu akauma maneno mawili-matatu halafu akasema njia
ya pili wanayotumia ni kuwakamata wale wakubwa kama tembo na wengine na kuwapiga
sindano za chanjo....nikajizuia kucheka. Alipoona swali lingine linafuata kabla
hajaanza kuningiza kwenye “undani/details za deal” lenye commission ...akaomba
udhuru kidogo kuwa boss wao kaingia ofisini mara moja na hivyo atanipigia
baadaye kidogo...akakata simu na ukawa ndio mwisho wa mawasiliano
Alipokata simu tu
nikamtext kuwa angeendelea tu na ujinga wake maana nawafahamu vema na
wanachokifanya...na huo ukawa ndio mwisho wa ile number kupatikana hewani baada
tu ya ujumbe wangu kuwa delivered.
Ushauri Kidogo:
· Unapojikuta kwenye mazingira ya mtu
kujitambulisha kwako kwa nguvu kubwa huku ukiwa humfahamu, mpe nafasi ya
kuongea
· Unapojikuta kwenye mazingira ya
kudanganyika kuwa unaweza kunufaika na kupa utajiri kirahisi kwa mtindo wa
ki_DECI_DECI au kimuujizaujiza, usichanganyikiwe na kuanza kuutazama huo
muujiza kama ndio umeshakufikia. Utafanya la muhimu sana iwapo utaruhusu akili
yako kufanya kazi na kutafakari vema kila unachokiona au kukisikia
·
Kama unaweza, ni vema kurecord
mazungumzo ambayo una wasiwasi nayo
· Kama unaweza, una nafasi, na una
matumaini kuwa polisi wanaweza kuwa na msaada kwenye hili, basi wasikilize watu
hawa na kutafuta msaada wa polisi kwani utaokoa na wengine wasidanganyike
· Tambua tu kuwa watu hawa wana mtandao
mkubwa sana na mara nyingi wanafanya mambo yao wakiwa na taarifa za kuwatosha
na wamejipanga. Unaweza ukawa kwenye mstari mwembamba sana unaotofautisha
ukweli na uongo
· Kwa nini bado makampuni ya simu
yanaruhusu simu kutumika ikiwa haijasajiliwa? Na kama imesajiliwa, je wale
wanaoandikisha hizi simu, wana ujuzi wowote wa kugundua kitambulisho halali na
ambacho ni fake watu wanavyovitumia kusajilia simu zao?
Tukitumia vema ufahamu na akili tuzopewa na Mungu bila haraka ya mafanikio ya haraka, tunaweza kukabiliana na changamoto
nyingi za kitapeli tunazokumbana nazo
MM