CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

Papaa On Tuesday....Siri Za Makosa Yetu Zinazogharimu Furaha Kwenye Maisha Yetu (2)(Hali Hii Itaendelea Mpaka Lini)??


Tunakila Sababu Ya Kumshukuru Mungu Kwa ajili ya Wakenya Kuamua Kiongozi ya Taifa lao ambapo Uhuru Kenyatta anakuwa Rais wa Nne wa Nchi hiyo, Kati ya Marais Wanne Watatu Wakikuyu na Mmoja Moi ndo alikuwa M-Karamajong kama alivyo Makamu wa Rais Wa Sasa Wa Nchi hiyo. Miaka ya Nyuma iliwahi sikika Kiongozi mmoja either kwa Kejeri ama hasira kuwa "Kenya Itatawaliwa na Wakikuyu Tu". Ninamtafuta Mzee Wa Upako Antony Lusekelo alitabiri "Raila Odinga" atashinda ili nimsikie atasema juu ya haya yaliyotokea nchini Kenya. Niwapongeze sana Wakenya.


Wiki Chache Zilizopita nikiwa ninatazama Tv nilimsikia Mzee Wa Upako Akihubiri, nikatega sikio Kumsikiliza kwa sisi watu wa habari Watu Kama Mzee Wa Upako hatutakosa la Kujifunza ama Kulidadisi katika mahubiri yake maana yeye ni Mzee Wa Transformer kazi kubwa ni kulipua mabomu. Juzi wakati anaongea alitoa mfano ambao nimekuwa nikiusikia mara nyingi na hata Mhe. Vicky Kamata Kuna wimbo wa kuhusu "Kuku" ametumia mfano huo huo aliotoa Mzee Wa Upako. Mfano huo unasema kulikuwa
kuna Watumwa Wawili ambao walikuwa wakifanya kazi kwa tajiri mmoja, siku moja ikatokea mfanyakazi mmoja kwa bahati mbaya akamuuwa kuku wa boss wao, kitendo hicho kikapelekea Mtumwa aliyeua kuku kuamua kufukia kwenye ardhi wakati anamfukia mfanyakazi mwenzake akamuona. Ikatokea yule aliyemuuwa kuku akitaka kupumzika na kazi zake yule aliyemwona anamwambia amsaidie kazi zake kufanya kama hataki anaenda kusema kwa Boss kuwa aliua kuku na kumfukia, Jamaa inabidi anyanyuke amsaidie mwenzake kazi zababu anapenda kibarua chake, Ikatokea akipata mshahara Yule mwanzake anasema anataka sehemu ya fedha ili aendelee kunyamaza ama sivyo ataenda kusema, jamaa anatoa fedha kumpoza, moja kwa moja akajikuta amekuwa Mtumwa wa Mabwana Wawili kwa Wakati mmoja. Jambo hili lilikuwa linamnyima sana raha kupita maelezo. Hakuwa na furaha sababu Kosa alilolifanya lilikuwa linamkosesha raha iwapo litajulikana. Siku Moja Yule Mtumwa aliyeua Kuku akajiuliza "Hali Hii Itaendelea Mpaka Lini"??Lile Swali la Kujiuliza Siri Hii huyu Jamaa ataendelea kuninyanyasa nayo mpaka lini lilikuwa kama limempa mwanga kwenye Maisha, siku hiyo hiyo akaweka azimio moyoni Mwake Liwalo na Liwe, akafunga Safari Mpaka Kwa Boss Wake, akajieleza Kosa lake akaomba sana Msamaha, Boss wake akamtazama akamwambia "Ulipokuwa umemuuwa Kuku na Kumfukia tangu Siku Ile Nilikuona Tokea hapa Dirishani, Nikasubiri Uje Kuomba Msamaha sababu niliona Haikuwa Makusudi, na Kwa sababu Ya Kulieleza hili Jambo na Kulikiri nimeamua Kukusamehe Kuanzia Leo Limeisha Kati yetu Uwe na Amani". Ghafla yule Mtumwa akajawa na furaha aliyokuwa ameipoteza kwa muda mrefu akajuta kwanini hakusema mapema. Akatoka kwa Boss wake akaenda kuendelea na kazi akiwa amemaliza kazi zake akaja yule Mtumwa anayemnyanyasa akamwambia "Twende Ukanisaidie Kazi Zangu" Mtumwa Mkosaji akamjibu Kwa Jeuri, "SIENDI", akamwambia Umesahau eeenh Ntaenda Kukusemea Kwa Boss Kwa Kosa lako la Kuuwa Kuku na Kumfukia, Yule Mtumwa akasimama akamwambia, Shika Njia Upesi Tena Kimbia Usichelewe Kamwambie, Yule Mtumwa Akashangaa Umepata wapi leo Jeuri??akasema Nimeshatengeneza na Boss Sina Kosa tena, Umenikosesha Furaha Kwa Kosa langu Kwa Muda Mrefu sasa ni Muda wa Kuwa na Amani na Furaha. Kweli Huweka Huru Kwenye Maisha.

Inawezekana ni mume ama mke, ama mchumba ama familia, ama ofisi unayofanyia kuna jambo ama mambo yanakufanya automatically ukiyakumbuka na kama wanaokuhusu wakijua yatakuweka katika wakati mgumu kwenye maisha, unakuwa mfungwa wa makosa yako mwenyewe. Umewahi muona mtu hamkutarajia kwenye mtihani agezee mara amekamatwa anagezea anavyokuwa, ama umewahi muona mtu ambaye anatumia vyeti vya mtu kusoma mpaka kufanya kazi ghafla wakatangaza either ofisini ama popote kuwa wanapitia vyetu vya wafanyakazi?huyu mtu anafanyika mtumwa wa kosa lake mwenyewe. Au umewahi kutana na mtu anayejua siri yako Fulani, then katika maongezi watu wanasema “Katika watu ninaowakubali kwa wokovu, Papaa namba moja” hapo hapo kuna mtu ambaye anajua kabisa kuna mchezo wa Siri tunafanyaga either kwenye biashara ama kwenye maisha…hapo hapo akasema “mmh nani?nyie hamjui Papaa, niseme ama nisiseme?ile sentensi moja kwa moja inakufanya unakuwa mtumwa wa yule mtu. Wengine kwao kutangaza nia si kwasababu hawataki kutangaza, ila wanajua wakitangaza kuna zahama zitatokea katika Jamii.
Kuna watu tunawaona upande mmoja na upande huo ndio tunaoujua kumbe hawa watu wanamaisha mengine, hahaha huwa najiuliza inakuwa vipi pale watu wanapojua Mumeo ama Mkeo ama Wazazi Wako Sifa yake kubwa mla Rushwa mkubwa, nyumba mnayoishi, gari mlilonalo ni matunda ya dhuruma inakuwa vipi pale tunapokuja kugundua mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili ni Changudoa, mtu yeyote mwenye faili lako la maisha unafanyika kuwa mtumwa kwake na kifungoni mpaka umekuwa muwazi.
Kuna mambo ambayo siku yakijulikana kwenye Jamii yatashusha heshima zetu lakini bado tunayang’ang’ania kuyatenda, na mara nyingi sana chakula cha kuiba ni kitamu kuliko cha kupewa. Kuendelea kuishi kwenye kifungo kinakusababisha kujibalaguza most of the time, yaani unaishi maisha yaliyochakachuliwa. Kosa la kulisema mwenyewe linasameheka kuliko kosa la kubainishwa, Kosa la kulikiri hata kama linagharimu maisha ni bora uwe wazi liwalo na liwe. Leo watu wananiona nina gari tena nasimama Kanisani natoa sadaka ya shukrani kuwa Bwana ametenda kumbe kuna mwanaume ama Jimama limenihonga, ama nimemzima mtu, baada ya miezi ama miaka watu wanagundua kuwa “niliwadanganya” unajua gharama yake?kwanini utumie jina la Tumaini wakati wewe ni Zakayo?kwanini useme mtoto ni wa Mwombeki wakati ni wa Nelson, Biblia inasema “Mtaifahamu Kweli nayo Kweli itawaweka Huru” kama hakuna ukweli hakuna uhuru.
Kuna Watu ambao Waume ama Wake Walionao Wamewapata Kwa Nguvu Ya Ushirikina, Umewahi kujiuliza kosa hili utalibebaje siku uthibitisho ukitoka??Kuna wadada Wana Watoto wa Kuwazaa lakini kwa sababu za Kuolewa wamewaacha Watoto wao kwa bibi ili wapate ndoa wameficha hii siri kwa muda mrefu wengine wamefanikiwa lakini hii siri ni nzito sana. Kuna Wanaume nao wana watoto huko nje lakini Wake zao Hawajui kuwa kuna familia 2 mumewe anahudumia. Pengine Baba aliyekutunza na Unaeishi ane si baba yako, si unajua baba wa mtoto amjuaye ni mama??Yamkini Kosa ulilolifanya ni la zamani sana nakitendo cha Kunyamaza pekee unaamini kinakupa Usalama, kwenye hii dunia ya sasa taarifa zinasambaa sana umewahi jiuliza iwapo siri itavuja???

Kuna Watu wamewahi Kubakwa, Kuna watu Wamewahi Kubaka, Kuna watu Wamewahi kuwa mashoga kuna Watu Wamewahi Kulawitiwa, kuna watu wamewahi kusaga ana Kusagwa, Kuna watu wamewahi kuwa na maisha fulani lakini kwa sasa wameachana nayo ni watu wema sana na wamebadilika yamkini wamewahi kukosa amani na kujutia maisha yao ya hapo kabla lakini kuna mambo yanamkosesha amani kila akikumbuka na kosa hili lina gharimu furaha yake maishani.

Yamkini haujawahi kufanya kosa inawezekana umewahi kufanyiwa kosa, ama umewahi ambiwa kosa la mtu na ukajua kuwa alikosa na kile kitu kila unapokumbuka kwenye ufahamu wako kina gharimu furaha yako. Huna amani kila ukikumbuka Kosa la unayemfahamu anaweza kuwa mumeo, Mkeo, baba yako, dada ama kaka ama mtu wako wa karibu anaweza kuwa hata Mchungaji wako..Umewahi Kujiuliza Kwanini Huwa unakosa amani ama furaha ama raha kila Unapokumbuka kosa ulilofanyiwa ama hadithiwa??Hali hii huzaa tabia, kuna tabia huzaliwa "developed" kwa mtu yeyote mwenye jambo ndani ya moyo wake,tabia moja wapo ni woga,kutokumuamini ama kuto kujiamini, unajikuta una mashaka, kuto mthamini mtu kama ulivyokuwa unamthamini, dharau, maimivu ya nafsi, Hasira, Matusi, Kiburi na kadhalika haya ni matokeo ya Jambo ama mambo yanayohifadhiwa moyoni. 

Swali la Kujiuliza Hali Hii Itaendelea hata lini???

Think Differently and Make a Difference

Papaa