Ninakila sababu ya Kumshukuru Mungu kwa siku ya leo kwa kuweza kunipa nafasi hii muhimu kuongea na Marafiki kwa njia hii ya Fasihi Andishi. Wakati Tukisubiri Matokeo Ya Uchaguzi Kenya Basi Ipo haja ya Kujifunza Kutoka kwa wenzetu katika Kile Wanacho Kifanya
Najua wengine ni kizazi cha dot com hapa hawajasoma methali wala hawajui tafsiri zake, lakini wengi pia Watoto wa Mahospitalini utajulia wapi mambo ya maneno kama Wakunga??Leo nataka tuongelee
methali hii ya "Usitukane Wakunga Wakati Uzazi Ungalipo". Kwanza Kutukana ni kuongea maneno machafu, kuongea maneno mabaya, maneno ya dharau kwa Wakunga. Wakunga ni Watu waliokuwa Wakiwasaidia Wanawake wakati wa kujifungua kipindi hicho zama hizo kabla ya hospitali zetu, sikuhizi tunasema Wakunga wa Jadi, na Wakunga wa laptop. Neno Uzazi Ungalipo ilikuwa ni kama nahau ya kueleza kuwa hicho kitu unachokidharu leo utakihitaji tena siku nyingine, huu ni uhitaji endelevu. Maana hasa ya Methali hii ilikuwa kutoa fundisho kuwa Leo Hii wewe ni Mjamzito, Kisha Unawatukana Wale wanaokusaidia Kuzaa, Unasahau kuwa kesho na Kesho kutwa utashika mimba tena wale wale uliowatukana siku za nyuma unakutana nao tena uso kwa uso.
Papaa
0713 494110
methali hii ya "Usitukane Wakunga Wakati Uzazi Ungalipo". Kwanza Kutukana ni kuongea maneno machafu, kuongea maneno mabaya, maneno ya dharau kwa Wakunga. Wakunga ni Watu waliokuwa Wakiwasaidia Wanawake wakati wa kujifungua kipindi hicho zama hizo kabla ya hospitali zetu, sikuhizi tunasema Wakunga wa Jadi, na Wakunga wa laptop. Neno Uzazi Ungalipo ilikuwa ni kama nahau ya kueleza kuwa hicho kitu unachokidharu leo utakihitaji tena siku nyingine, huu ni uhitaji endelevu. Maana hasa ya Methali hii ilikuwa kutoa fundisho kuwa Leo Hii wewe ni Mjamzito, Kisha Unawatukana Wale wanaokusaidia Kuzaa, Unasahau kuwa kesho na Kesho kutwa utashika mimba tena wale wale uliowatukana siku za nyuma unakutana nao tena uso kwa uso.
Mojawapo ya mambo yanayodhihirisha tabia ya mtu ni kuwa "Pesa", Mhe. Chenge anaita Vijisenti. Kuna maneno mengi sana yametungwa kuhusiana na fedha, Biblia inasema Fedha ni Jawabu la Mambo yote, Fedha ni Sabuni ya roho, Kwenye udhia ingiza rupia, hii yote ni kuonesha namna gani fedha inaweza badilisha uchafu wa roho ya mtu.
Kwenye Kizazi chetu fedha inakupa nafasi hata katikati ya Vijana wenzio, fedha inakuletea marafiki na wanafiki, fedha inakufanya uitwe Handsome au sweetybaby hata kama haufananii hayo, fedha imewavulisha nguo Wake za watu na waume za watu, fedha imepelekea Maaskofu na Maimam kuchukuiana, wengi wetu tumebadilika pale tunapotoka hatua moja ya mafanikio kwenda hatua nyingine.
Dharau kwetu iko karibu kuliko heshima, pale mtu anapoanza kupata mafanikio. Kuna watu tumecheza nao, tumesoma nao, tulikuwa pamoja, kama ni Wanandoa Walipendana wakiwa hawana kitu, mafanikio yalipoingia tu kwenye ndoa, unakuta mmoja anabadilika na kumlaumu mwenzake kuwa ndo kapuku wa kutupa. Kuna watu waliwahi pata kazi kwenye Ofisi moja wakaondoka kwa dharau na makelele wakisema Ofisi hiyo wote ni Walugaluga, hawana mbele wala nyuma, ndugu yangu usinyee kambi, siku adui akikupiga ukashindwa kurudi.
Hivi kwanini umadharau mtu eti sababu wewe umepiga hatua mbele na wenzio umewaacha nyuma, kuna mdada alimpenda Mpenzi wake ambaye alikuwa si lolote wala si chochote, huyu mdada akampenda, akamkazania arudi shule akasoma, mdada akamtafutia mkaka pa kukaa, baadae akatamani mtu wake ajitegemee akamtafutia na kazi, siku zote huyu kaka alionesha mapenzi ya hali ya juu kwa huyu mdada, alipoaanza kazi akajua kuvaa tai, akajua nini maana ya Salary Slip, akajua nini nguvu ya Mshahara huyu Jamaa akaanza ku change, mara busy na kazi, mara kasafiri kikazi, ghafla dharau zikaingia kisa anamshahara mkubwa kuliko wa huyo dada, akaanza matusi kuwa eti mdada ana bahati kuwa na yeye, yeye ni level zingine, na huyu mdada si standard yake, dharau kebe wa kebe, mwisho wa siku Mkaka akamwambia mdada unataka nikulipe shilingi ngapi kwa fadhira zako ili kila mtu aende na maisha yake, maana amegundua Mdada sio type yake, tehe tehe ulisikia wapi Fadhira inalipwa Dharau, Uliwahi sikia Wema Unalipwa na Matarumbeta??Akatukana Wakunga Wakati Bado anajua kesho atashika tena Mimba ya Maisha.
Yule Mdada hakutaka kulipwa chochote aliumia akaumia akalia na kulia mpaka akakonda sababu ya maneno ya mtu mbaye amemsaidia kutoka mahala pa chini sana, Mungu sio Filikunjombe, Jamaa sababu ya tamaa ya fedha akawa anaiba ofisini, ghafla ikajulikana Vijana wa mjini wanasema "Kikanuka" tena kwa harufu ya choo cha uswazi, akafukuzwa kazi, Mwanawane wale wooote aliokuwa aliokuwa anadhani ndo type yake wakamkimbia, kama story ya Mwanampotevu Kijana akazingatia moyoni mwake akaona arudi kwa mdada, ha ha ha ha wakati we unasema "Cha Nini, Wenzio Wanasema Watapata Lini" mdada alishaolewa zake zamaniiii, Kijana akarudi Kitaa full adabu, kisa na Mkasa anatukana Wakunga.
Ukipata fedha usidharau watu ukajiona wewe ni bora kuliko wasiokuwa nazo, Ukipata nafasi ya kusoma na usiwaone wale wasiosoma sio kitu, hata kama ni Wazazi wako, huwezi kujifanya wewe ndo wewe ukawaambia Wazazi wako hawajaenda shule, kumbuka walinyima wewe uende shule, unapata Mshahara Unakula wote, kisa mshahara hautoshi, kawa taarifa yako hata wao ulikuwa haitoshi lakini walijipinda usome unaona Kero ukipewa matatizo ya home itakula kwako, we tukana wakunga kimoyo moyo kuwa "wamezidi". Ukipata Mchumba au hata Boyfriend ama Girl Friend basi usijione wewe ndo Beautiful kuliko Cleopatra, unawaona wenzio wasiopata watu ni "Magume gume". Ukiolewa wenzio wakikosa bahati usianze nyodo "Siongei na Wasio na Ndoa", Ukipata kazi sehemu nyingi bora kuliko hapo ulipo, usiondoke na mbwembwe za matarumbeta, hii dunia bwana huwezi jua.
Dharau haziwezi kutupeleka mahali popote, unayemdharau leo hujui kesho yake itakuaje, hapa ni duniani na malipo ni hapa hapa unachopanda ndicho utakachovuana, mbwembwe na majigambo ni utoto wa hali ya Juu ukikua utaacha, Sasa kwanini kufanya dharau sababu ya mafanikio yasiyodumu??hukuwahi sikia ama kuona watu waliokuwa na nyodo na mbwembwe wazazi wao wakiwa hai ghafla wazazi wakafaraki??hukuwahi sikia watu waliokuwa wanafanya mbwembwe na kufuru sababu ya wapenzi wao ghafla kikaumana??hujawahi sikia mtu aliondoka kwenye ofisi moja kwa mbwembwe huko alikokwenda kikanuka??yangu mimi ni macho, ninarudia kusema Usitukane Wakunga Wakati Uzazi Ungalipo.
Think Differently Make A Difference
Papaa
0713 494110