CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

Papaa On Tuesday.....Wengi tu Waathirika Wa Makovu Yasiyokuwa na Hisia!!


Nimatumaini yangu ya kuwa sote tu wazima wa afya njema na tunaendelea na ujenzi wa taifa letu .

Mabaka Yasiyokuwa na Hisia ana Makovu yanayotokea bila mwanadamu mwenye  kuwa na uelewa kuwa kuna kitu kinaendelea kwenye mwili wake, hali hii  hupelekea mtu kutibu matokeo ya ugonjwa na sio ugonjwa wenyewe. Kati ya dalili nyingi za wagonjwa wa ukoma ni waathirika kupata madhara pasipo wao kuwa na taarifa (sense) katika miili yao. Wagonjwa wengi hata wale wa Saratani Ya Ngozi hukuta tu wana mabaka ama makovu kwenye miili yao ambayo yametokea pasipo wao ku-sense kama kuna mabadiliko katika miili yao. Nilipokuwa Mbeya wakati fulani Pastor Matthew Sasali (Mdogo wangu) alinikumbusha  kuwa dhambi kwenye maisha ya mwanadamu ni kama makovu yasiyo na hisia, huanza pole pole mwisho wake ni kama ambavyo inaelezwa Mshahara wa dhambi ni Mauti.

Kila mtu kwa nafasi yake anaweza kuitazama Jamii ya leo na kuona, mambo mengi yanayotokea sasa yalianza pole pole na kudhaniwa kuwa hayatakuwa na madhara makubwa kwenye Jamii lakini kwa sasa matatizo hayo yamekuwa sugu vya kuchosha. Issue za ufisadi zilianza pole pole kwenye Jamii yetu, leo hii kwenye Jamii si ajabu mwovu anakumbatiwa na mwema anachukiwa, ukionekana unaikosoa Serikali unaambiwa unahatarisha amani ya nchi. Leo hii watoto wanadiriki kuwapeleka wazazi wao mahakamani, leo hii idadi ya mashoga inaongezeka kwa kasi lakini kuna siku hali haitakuwa hivi sababu ni kama Jamii imekufa ganzi. Watu wanaokamatwa na madawa ya Kulevya kila siku wanakuwa wengi lakini mwisho wa siku tunazoea tu

Zamani idadi ya wana cheat kwenye mahusiano ilikuwa ni ndogo sana na hata kama mtu alikuwa anatoka nje ya ndoa ilikuwa ni Siri sana lakini siku hizi yaani inajulikana kabisa ni nyumba ndogo, sio sasa wanandoa kuaminiana, hali ngumu ya maisha na kupenda mafanikio ya haraka hataka  yamepelekea wanandoa wengi kusaliti ndoa zao, waume za watu hawaaminiki, wake za watu mule mule, enzi hizo watu walikuwa wanaugopa Mungu kwa sana si makanisani si misikitini, siku hizi kuna mambo yanatokea na watu kama wanayapotezea lakini mwisho wa siku yatatengeneza maumivu na mateso katika maisha na kutunyima furaha.

Angela (sio jina kweli) niliwahi kukutana nae katika mojawapo ya mizunguko yangu katika mashule na vyuo. Mdada huyu alikuwa ni kidato cha 6, baada ya mimi kufundisha mambo kadha wa kadha ya maisha, dada huyu aliniomba tuzungumze maana alikuwa anahitaji msaada. Katika maongezi yake alinieleza kuwa alianza kuingiliwa kinyume cha maumbile akiwa kidato cha kwanza, kwa wakati huo akiwa kidato cha sita alikuwa si kwamba si tu anapenda mchezo huo bali amekubuhu, hajisikii raha kufanya mapenzi kwa njia ya kawaida isipokuwa mpaka ameingiliwa kinyume cha maumbile. Na si kwamba anapenda hiyo hali amejitahidi mbinu mbalimbali za kukataa hiyo tabia ila alieleza huwa inaondoka na kurudi. Nilipomdadisi ilikuaje mpaka akaingia katika huo mchezo alieleza boyfriend wake waliyeachana ndiye aliyemfundisha na kumzoesha, alijua ni kitu cha kawaida na kinaweza kuepukika lakini si hivyo. Unafanyaje pale mume wako wa ndoa ama mchumba wako akataka kukuingilia kinyume cha maumbile, umewahi sikia habari hii mara ngapi lakini ni kama watu wanaipotezea, hili ni kovu linalotokea bila kusikia maumivu ya kidonda. Na mwisho wa siku tutakuwa tumesharudi katika enzi za Sodoma na Gomora

Leo hii umesikia mara ngapi matamko mbalimbali ya kidini yakitolewa kila mmoja akimtishia mwingine, lakini hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa kukomesha hali hiyo. Inawezekana hisia za kuhisi madhara yake kwenye Serikali yetu zimekufa lakini kidonda hiki kina madhara makubwa hapo baadae zaidi ya madhara ya ugonjwa wa Saratani. Kuna siku raia watajitoa mhanga ndipo tutashuhudia kitu ambacho leo tunakidharau, watu wanapigwa mabomu, watu wanapigwa risasi, risasi inaua, kuna siku watu watachoka kukaa hai kufa kwao si tatizo sana, kwa kusema hivi lazima Jamii ianze kutazama huu mwamko wa Kijamii kwa sasa na kila mtu kudai haki yake kwa mabavu hata pale palipohitaji subira na busara tutafika wapi?hii hali tusipoiona kuna siku yataibuka mambo.

Leo hii kuna matatizo ambayo pengine yalianza zamani na kudhaniwa kuwa ni madogo, wanaume wengi wanaoangalia pornography hawakuanza jana, ni kitu ambacho wengine kimeshajengeka kwao, kuna wanaume wao kujichua  ni kama wameshikiwa risasi kuwa wasipofanya watakufa. Wengine ni wafanyakazi na vyeo vyao lakini sasa wanateseka na tabia hiyo wengi wao hawapendi kufanya hayo lakini wakati wanaanza walidhani ni kitu kidogo ambacho hakiwezi kuathiri maisha yao. Wengine mpaka kwenye ndoa hawasikii raha bila ya kujichua wao wenyewe. Haya ni Mabaka tuliyoyadharau kwa kudhani hayana madhara leo hii yameacha alama zisizofutika kwenye tabia zetu.

Tabia zetu wakati mwingine zimekuwa ni tatizo la kudumu, wengine wetu uaminifu sasa imeanza kuwa issue, maana kuna wengine walianza tu polepole kwa ahali ilivyo sasa sio kwamba hawataki kuwa waaminifu, No wanapenda sana kuwa waaminifu issue inakuja tu kuwa wameshaathirika na kutokuwa waaminifu, kwa kuupuuzia kwao mambo madogo madogo wamejikuta wamepoteza opportunities nyingi sana kwenye maisha yaoWatu wanatamani kukuamini lakini tabia huwa zina athiri sana maisha yetu ya kila siku. Ndoa zetu zimeathirika na tabia zetu kazi zetu zimeathirika na tabia zetu, mahusiano yetu na Mungu yanasua sua kutokana na tabia zetu. Can Something good come out of you?


Asilimia kubwa ya Vijana wa Sasa wamesha experience maumivu kwenye mioyo yao juu ya mahusiano. Siku moja tukiwa kwenye Conversation kali kwenye Facebook Wall yangu, mmoja wa Marafaki zangu aliongea akisema kwa namna moja ama nyingine suala hili la kuumizana linatokana na Wanaume kutokuwa na Msimamo katika kile wanachokitaka. Kuto kuwa na Msimamo ni Matokeo ya kitu ambacho kinaendelea kwenye Jamii, kwanini watu hawana misimamo katika kusema sitaki A nataka B, Wadada wengi wamejikuta wakitupia wakaka lawama kwa kuwauzisha Sura mwisho wa siku inakula kwa Mdada. Kizazi hiki kinaona ndoa ni jambo la fahari kuliko jambo la fungamano ndo maana unakuta ndoa ilifungwa kwa mamilioni ya fedha baada ya mwaka watu wanataka kutoka, nani alaumiwe. Mioyo ya wengi imeshajeruhiwa na kubutuliwa kama kombolela hakuna tena penye sehemu ya kupenda. Ukitaka kujua una kovu lisilokuwa na hisia ni pale unapopata mpenzi mpya halafu ukabaini ameanza tabia kama za yule aliyekimbia kuna kitu kunaingia ndani yako ghafla si unajua uking'atwa na nyoka??? 

Wengine wamekuwa wakihangaika na matumizi mabaya ya fedha kiasi kwamba wanajitahidi kujidhibiti wanashindwa, kosa alilofanya mwezi uliopita amejikuta na mwezi huu amelifanya, wengine wamejitahidi kuacha matumizi ya hovyo lakini imeshindikana kilichotokea wamekubali kuwa hawawezi kubadilika, ilipoanza ni kama haikuwa na madhara lakini wengine sasa its too mucha na still hawaoni kama watasaidika katika hilo, wamekubali matokeo. Wengine tabia za kuzira, ajabu unakuta mtu mkubwa kabisa eti anazira, lakini hakuanza leo tabia hii imekuwa polepole bila ya watu wenyewe kujijua imejijenga ndani yao. Wengine ni hofu, wamejawa na hofu mpaka unnecessary. Kuna rafiki yangu yeye kila kitu anaogopa hasa inapofika suala la ndoa yale aliyoyasikia kutoka kwa watu na aliyoyapitia yamemjaza hofu kuwa katika dunia hii kama kuna mwanaume ambaye yupo kabisa hawezi cheat na akabaki kuwa mwaminifu kwake peke yake. Hofu anabadili namna ya kutazama mambo, hofu inamadili namna ya kuishi na kuongea na kuamua mambo mengi, hofu ikikujaa unaweza ukaufunga hata uwezo wako wa kuwaza na kupambanua mambo, hofu inatawala.

Inawezekana kuna jambo ulishawahi dhani umelisamehe na kuliachilia lakini kila lile jambo linapotajwa kuna mkwaruzo ndani ya moyo wako hutokea, kama umewahi umizwa na mapenzi ukiwasikia watu wanaongelea mapenzi unatamani usimkumbuke mtu aliyekutenda, ikitokea umemuona njiani anakuja unatamani kubadilisha njia, yamkini uliwahi dhurumiwa ama pata hasara ya biashara yale maumivu bado yameganda kwenye nafsi, inawezekana ni ofisi waliyokufukuza sometimes back ukisikia jina la ofisi moyo unakuuma. Makovu haya ya nafsi hu-develop tabia ambayo yamkini hukuwa nayo hapo awali. Umejengeka na kuto samahe, umejengeka kuwa na tahadhari nyingi zaidi, Umejengeka kuto amini amini mwenzi wako akishika tu simu unajua anachat na wanawake wake unatamani kumwamini lakini nafsi yako imesha develop tabia iliyotengenezwa kutokana na jeraha. Ukimsikia mtu anasema "wanaume wenyewe wote vimeo" jua ana jeraha ama ukisikia mtu anasema "wanawake wote wanafanana" jua ana jeraha lake la kwenye nafsi kila mtu amejawa na hofu ya kuogopa kutoneshwa jeraha la nafsi alilowahi kupitia hapo kabla.

Wengi tunateseka si kwa sababu tunataka kuteseka, hofu zinatawala maisha yetu, kujilaumu kumekuwa ni sehemu ya maisha yetu,kutokuamini wengine imekuwa ni sehemu yetu. Wengine wanafanya biashara wakiwa wameshajiandaa kupata hasara, wengine wameingia katika ndoa wakiwa wamejiandaa kusalitiwa, wengine wameingia katika ajira wakiwa tayari kuiba. Mabaka yasiyo na hisia yamekuwa kiasi kwamba tuko tayari kuumia au kuumizwa hata kuumiza kila mtu yulo tayari kwa lolote ovu kutokea kuliko wema. Haya mambo yalianza polepole katika maisha na jamii yetu sasa yameshatuathiri. Unayosikia leo Tunisia au Misri hayakuanza tu ghafla ila yalianza polepole.

Hakuna mtu anayekufahamu vizuri kuliko wewe mwenyewe unavyojifahamu ipo haja ya kujichunguza na kubadilika kabla mwaka haujafika mbali.

…//Papaa
0713 494110
samuel_sasali@yahoo.com