CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

*TAFSIRI NZURI YA MAFANIKIO*


Habari zenu!!
Maishani mwetu zipo hulka nyingi sana na nyingine huzaa tabia nzuri au hatari,kila mmoja anatamani kufanikiwa sana na kuwa na kila kitu akitakacho....lakini jambo moja ambalo nimekuwa nalitafakari maishani mwangu ni hili,naishi ili iweje na mwisho wa maisha yangu utakuwaje? Nini kitasemwa au kuandikwa kuhusu mimi,naam nitasema nini mbele ya kiti cha enzi?
Na haya ndio mambo niliyojifunza na ninatamani kushare na wenzangu, Mafanikio sio magari na majumba,ila hayo ni matunda ya mafanikio,ukifanikiwa kuwa hivyo vyote ni vema sana lakini bado hicho siyo kipimio cha mafanikio....ni kama vile ukiamua kupika wali au ubwabwa,kwa hicho chakula kutoa harufu haizuiliki,ila hujapika ili upate harufu,basi na mafanikio hupimwa kwa ndoto au malengo uliojiwekea kufikiwa,na hata iweje hatuwezi kupimwa kwa kujifananisha na wengine kama tumefanikiwa au lah maana kila mmoja ana ndoto zake,kila mmoja ana makusudi yake na kila mmoja ana yake yakuyatimiliza!!
Usije ukaumia sana maishani kwa kujikakamua kupita kiasi,wala usije ukawagombanisha watu ili upate sifa kwa mmoja wao,wala usijitahidi kuwaonyesha watu vile usivyo!!
Usijisikie vibaya classmate wako akinunua gari ama kujenga kabla yako,au usikasirike mwimbaji mwenzio akitoa albamu nne hali wewe una moja,ama akialikwa hata nje ya nchi na wewe hujakwenda popote!
Maisha ni kama mtihani,sasa usijaribu kuangalizia majibu maana kila mmoja ana karatasi yake ya maswali!
Iko neema kumsaidia kila mmoja kufikia ndoto zake,kama akiwa consistent!
Kwanini nimesema hayo, nimeona katika maisha haya tunajitahidi mno kushindana,kusemana na kuhukumiana pasipo sababu,hivi mtu mwenye ndoto ya kutengeneza roketi na yule mwenye ndoto ya kujenga nyumba inayotembea,kama wakikamilisha ndoto zao watakuwa sawa??
Muhubiri amesema kuna mambo ameyaona chini ya jua nayo ni ubatili mtupu,akasema sio wenye akili ndio hufanikiwa ama wenye mbio sana ndio hupata medani,maana kuna wakati wale waouvu kabisa ndio hupata nafasi hivyo baki kwa njia ya hatma yako,usijitahidi kushindana na yeyote wala kutupa mawe kwa wengine!!
N.B; Sifurahii sana magomvi,ila najua yamkini yasiepukike,sasa kama ukipishana na mtu kwa namna yeyote ile usikimbilie kusema na kutangaza kila mahali ama kuandika kila mahali,tena wengine huenda mbali zaidi na kuingia kwa mitandao ya kijamii na kufungua akaunti mpya kwa majina mengine,yamkini kijana akajifanya binti na kuanza kutupa mawe kwa mwenzake,huo nao ni ubatili,maana kwa kufanya hivyo unakuwa umejifungia minyororo mwenyewe,jifunze kutafuta suluhu na kukaa kimya,ukiwa mwepesi wa kuongea sana kuhusu wengine kwa ubaya,saa utakayopatana naye tena mtu huyo hautakuwa na amani kila uonapo yote uliyomfanyia,na kwa kukosa amani moyoni ni kukosa mafanikio!!!


*Ni vema sasa ukafanya mambo yale ambayo yanakupa amani na utulivu maishani mwako,wombee wenzako wafanikiwe katika ndoto zao,usijisifu wala kusema wengine ni kitu gani ila wewe,maisha ni hatua na mafanikio ni mzunguko!!
Natamani tupendane kweli na kusaidiana na kushauriana katika kila hali,maana maisha haya si ya kudumu!!
Yamkini Mungu amekupa fedha ili uwasaidie wengine, lakini kinyume chake imekuwa fimbo kwa masikini,angalia sana yamkini pia hapo kwako zinapita tu-Muhubiri 2:26!


**Basi mafanikio ya kweli ni kuweza kuishi ndoto zako au aina ya maisha upendayo,kuwa na amani na watu wote na kumpendeza Mungu,kuwasaidia wenye uhitaji na kuwatia moyo wakuzungukao na na kuishi kwa staha pasipo kuwakwaza wengine,unaweza fanya yote haya hata kama unafedha kidogo sana,ilimradi moyo wako una amani na maisha unayoishi,basi fanya bidii ili uzidi kustawi katika yale uyatamaniyo kesho,amen**
MUNGU AWABARIKI SANA WANAOFANYA KAZI ZAO NA KUJITAHIDI KUWASAIDIA WENGINE KWA MAOMBI,USHAURI NA HATA KWA MALI,NINA HAKIKA THAWABU YENU IPO!!


Na King Chavala
0713883797