HARAKATI
ZA KUKUZA VIPAJI HALISI HUSUSANI
VICHEKESHO VYA KIKRISTO ZINAENDELEA KUZAA
MATUNDA PAMOJA NA CHANGAMOTO ZILIZOPO!!!!
Salaam!
Ni muda sasa umepita tangu harakati za kutambulisha
Christian comedy Tanzania zianze,matunda na matokeo mazuri yanaonekana japo
bado hakijafikia kile kiwango ambacho kinapendeza mbele ya macho ya dunia.
Ingawa bado ninaamini kuwa mwisho mwa mwaka huu 2012 tutakuwa tumepiga hatua ya
maana.
Nimeweza kufikia mikoa mingi ya Tanzania japo kufanya kidogo
utambulisho na kuangalia mazingira ya vipaji vya huko,mpaka leo ninaandika hapa
imebaki mikoa minne tu ya Tanzania Bara,ambayo ni Ruvuma,Rukwa,Mara na Kagera
na Pemba kwa Zanzibar ambapo bado sijafika, lakini naamini kabla Ya June 2013
nitakuwa nimefika kila sehemu ya Tanzania na kurudia tena kwingine!
Shauku yangu ni kuona watu hususani vijana wanaishi maisha
yao mazuri,wakila matunda ya vipaji vyao,lakini pia jamii ikielimika na
kuburudika kwa vipaji hivyo na si kukereka tu!
Kanisa linalo jukumu kubwa sana kuhakikisha vipaji na vipawa
vinavyoibuliwa na kukuzwa kanisani haviendi kupata umaarufu duniani kwa mwavuli
wa ulimwengu bali vibaki kuwa utukufu kwa Mungu kila vinapoonekana na
kutambuliwa.....sio sifa kwa kanisa kumsikia msanii wa ulimwengu akisema mimi
nilianzia kanisani kuimba kwaya au Sunday skuli,sasa unajiuliza kilichomkimbiza
ni nini? Kwanini ameacha kuimba kwaya? Majibu yake yatakuwa rahisi tu.....HUKU
NDIO KUNALIPA!!!!
Katika harakati zangu nimegundua mambo ambayo ni muhimu
kusema wazi wazi kabisa, kanisa lina shida,tena shida kubwa na shida yenyewe
inatokana na mambo kama haya;
a.
Vijana wengi hawajitambui wala kujielewa,sasa
usipojielewa vema hauwezi kuwa na utulivu mzuri,utakuwa unatangatanga huku na
kule ili mradi tu ubahatishe njia ya kutokea na ndio unajikuta watumishi wa
Mungu wanahaha mpaka wanavamia pesa chafu!
b.
Viongozi wengi wa makanisa hawana dira na
visomeo vya alama za nyakati,wengi wako na mitindo ya kizamani na hawawezi
kukubali haraka,kulea wala kukuza vipaji vya vijana wa kisasa...na ukweli ni
kwamba vijana wa leo wana namna yao ya kuwakilisha vipaji vyao.
c.
Kanisa halipendi kuwatia moyo kwa kulipia
sawasawa thamani ya vipaji hivyo ili viendelee kukua kanisani, wengi huwabana
vijana na kuwapa majukumu mengi,hata wakaacha mambo yao mengine lakini mwisho
wa siku wanaambiwa ni huduma na hivyo wanaambulia hamna kitu....hivi uliwahi
kuona wapi watu wanalipia kodi za nyumba zao na kula huduma?
d. Wakristo wengi hawana uzalendo na vipaji
vya nyumbani kwao,yaani vipaji vya makanisani; wengi wanapenda kazi za duniani
zaidi na hata kama ni za dini basi ni zile za kutoka nje. Na wakristo ndio wanaongoza kwa kudurufu au kuburn kazi za
wasanii, hivi kama sisi wenyewe tusipowaunga mkono kwa kununua kazi halisi, ni
nani atakayefanya hivyo?
e.
Na jambo lingine ni wale wasanii wenye majina
makubwa kutowapa support ya kutosha wale wasanii wanaochipukia, wasanii wakubwa
wamekuwa wakiwatisha makanisa machanga kwa kudai malipo makubwa kila wanapoitwa
au kualikwa na wengine wamekuwa wakisemwa kwa tabia mbaya wanayoionyesha mbele
ya jamii kama vile kiburi,majivuno,majigambo na uasherati/uzinzi.
NI MPAKA MATATIZO HAYA YATAKAPOPATIWA UFUMBUZI WA KUDUMU
NDIPO FURAHA YA VIPAJI HALISI KANISANI INAKAPOKUZWA MARADUFU NA HII INAANZA NA
KILA ALIYE MKRISTO...YAANI INAANZA NA WEWE!!!
Lakini bado nina imani kubwa kuwa tukiweka nguvu zetu za
kutosha huko mambo yatakuwa mazuri tu! Kanisa lazima liiongoze nchi kwa kila
kitu yaani kijamii,kisiasa,kiserikali,kiuchumi na kiroho.
Harakati bado zinaendelea na hazitakoma mpaka hapo
nitakapoona Vipaji halisi vya Kikristo,hususani Ucheshi wa Kikristo
unatambulika vilivyo.
Ninamshukuru Mungu sana kwani harakati hizi zimeibua vipaji
vya maana na bado vingi vinakuja zaidi....yaani ninapoona kazi za Richard
Chidundo; Gerald Mrema; Emmanuel Mathias Manu(MC pilipili); 1st Q
dancers na wengine wengi hata wale ambao walikuwa kwenye secular na sasa wako
huku kama vile Masanja Mkandamizaji,basi nafarijika sana na kutiwa moyo kuwa
saa inakuja ambayo kila mkoa utajivunia vijana wenye vipaji katika maeneo yao
huko.
Rai yangu ni moja tu....kila aliyeamua kumtumikia mungu kwa
kipaji chake,basi na afanye hivyo kwa kumaanisha na kwa lengo la kuujenga
ufalme wa Mungu na si vinginevyo....ubaya wala uchafu wowote usitajwe juu yako
na ushirikiano na wenzako uzidi zaidi na zaidi,juu ya yote ujitahidi kujifunza
kila siku ili ubunifu wako usipungue wala kuzoeleka.
Mungu wangu na awabariki,pamoja sana katika harakati hizi!!!
King Chavala
The great MC and Founder of Christian Standard and Stand Up
Comedy in Tanzania