CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

UNAFIKI ULIOJIFICHA NYUMA NA MANENO YA MARAFIKI... "TUKO PAMOJA SANA"!!!

SALAM KWA WOTE!
Na amini watu wote tuko vizuri na bado tunakazana kuzifikia ndoto za maisha yetu!
Leo nimesukumwa kuzungumzia jambo moja hapa ambalo naona likiachwa hivyo litakuwa tatizo,tena tatizo kubwa.

UTANGULIZI;
Katika haya maisha hakuna mtu anaweza kuishi peke yake, sio tu kwa maana ya mwenza wa maisha ila namaanisha bila mtu mwingine yeyete, maana huwezi kuwa kila kitu na huwezi kufanya kila kitu mwenyewe kihusuyo maisha yako...una ndoto yako ya kumiliki Chuo kikuu ni sawa, lakini kuliweka hilo wazo kwenye maandishi ya kusomeka unahitaji watalaamu wa kuandika, kabla hujaanza kufanya lolote, unatakiwa upate mwongozo kwa wale waliotangulia na hapo unahitaji watu wengine.....kwa ufupi kila hatua utakayopiga utawahitaji watu,aitha kwa kuwaomba au kuwaajiri kwa maana ya kuwapa kazi na kuwalipa. hata ukitaka tu kutoka kwenda mjini lazima uhitaji dereva na konda na hata kama una gari binafsi kuna saa utamuhitaji muuzaji wa mafuta....KIMSINGI "KUISHI" NI KURAHISISHIANA MAJUKUMU KWA KILA MMOJA WETU KWA FAIDA YA KILA MMOJA WETU!.
Kwa msingi huo nataka utambue kuwa UNAHITAJIKA KUWASAIDIA WENGINE kama vile ambavyo na wewe UTAWAHITAJI WENGINE KUKUSAIDIA kufikia ndoto za maisha yako!

DHANA YA MAISHA;
Katika maisha yetu hakuna hata mmoja wetu ambaye yuko sawa na mwengine kwa maana ya makusudi ya kuishi kwake, kila mmoja alizaliwa peke yake (hata mapacha kila mmoja alitoka kwa wakati wake); kwa staili yake na hata sasa kila mmoja ana ndoto zake na anaishi maisha yake. Ukilitambua hili hutamuonea wivu mwenzako katika moja ya ndoto zake,ila na wewe utatia bidii katika za kwako ila ikifika saa ya kusema ama kuonyesha ni kwa kiasi gani amesonga na ndoto zake na wewe utakuwa na ya kwako ya kusema. Ubaya ni kwamba watu wengi hawajitambui, kwa hiyo wanafanya maisha yanakuwa magumu sana huku duniani,maana mtu mmoja anataka kufanya kila kitu na kwasababu anabahatisha katika kila, basi atakuwa anajitahidi kumkwamisha kila anayejaribu au kufanya kama yeye!


UNAFIKI NISIOUPENDA.....
Kama umejitambua na unajiheshimu ni wazi kuwa na watu wanatambua hilo na sawasawa na kujiheshimu kwako ndio na watu wanavyokuheshimu. Ukiona mtu amekufuata na kukuuliza jambo lolote lile aitha anataka kulifahamu ama anataka ushauri wako au zaidi anaomba ushiriki wako....basi imekupasa kwanza kumshukuru sana Mungu kwa nafasi hiyo, hata kama hutafanya lolote katika haya anayoweza kuwa anayahitaji....nasemma hivyo ili ujue yafuatayo;

KWANZA UMETAMBULIWA KUWA UNAWEZA KUWA MSAADA KATIKA HILO.
PILI UMEHESHIMIWA SANA, MAANA WAKO WENGI LAKINI UMEONEKANA WEWE
TATU ULICHONACHO NDIO KAZI YAKE HASWA,MAANA TUMEPEWA ILI KUFAIDIANA.

Sasa kama ni hivyo basi ukipata nafasi hiyo mshukuru Mungu na baada ya hapo Omba hekima ya namna ya kujihusisha na jambo hilo na kama unaona huwezi kuhusika kabisa unaweza kumjibu kwa hekima SAMAHANI MIMI SITAWEZA, na yamkini ni vizuri hata ukimwelekeza kwa mtu mwingine unayeona anaweza kuwa na msaada!

Sasa usije ukadhani kwasababu una elimu ya juu sana au una umaarufu mkubwa au una kipaji sana au ni kiongozi maarufu au pesa kuliko wengine, ndio maana ukafuatwa wewe HAPANA!!
jIFUNZE Kuwaheshimu na kuwakubali wengine katika yote wanayofanya yanayostahili heshima....na mara zote HEKIMA NA MAWAZO MAZURI hutokana na watu tusiowadhania!

SASA SIKU HIZI KUNA NAMNA WATU HUKWEPA MAJUKUMU NA KUDANGANYA KWA NJIA YA MZUNGUKO, MTU ANAOMBWA JAMBO AU ANASHIRIKISHWA AU ANAALIKWA SEHEMU FULANI....HALI AKIJUA HANA NIA WALA MPANGO MOYONI AU NAFSINI MWAKE KWA KUSHIRIKI AU KUSHIRIKIANA....ANAISHIA KUTOA MATUMAINI FEKI ATI....."TUKO PAMOJA" AU "HAMNA NENO MTU WANGU" na hapo unamuaacha huyo ndugu akiwa na matumaini makubwa na ikifika saa ya jambo lenyewe usitokee kabisaaaa!!


Sasa ninafikiri ni wakati mzuri wa kujirekebisha sasa, kama huna nafasi au huwezi kumsaidia mtu kwa namna yeyete ile wewe sema tu....SAMAHANI NDUGU KWA HILI SITAWEZA!
Naamini hii itakusaidia pia kuwa HURU na kuwa MKWELI!

HIYO TABIA YA KUMWAMBIA MTU TUKO PAMOJA NA KISHA NYUMA YAKE UNAMNG'ONGA SIO HATA KIDOGO....TUJIREKEBISHE!!!

Ukiona inakufaa unaweza kuendelea nayo lakini kuna wakati itakugharimu tena sana, maana watu huwa wanaambiana yote yanayokuhusu na kama ni mambo ya kukalaisha basi ndio habari husambaa zaidi kuliko hata nzuri!

MFANO HAI;
Kuna mtu mmoja mahali fulani alikuwa anajifanya yuko bize kuliko hata ubize wenyewe, basi hata akiletewa kadi za michango ya harusi au shughuli mbalimbali alikuwa akijibu aaah tuko pamoja aisee....basi zingine anachangia na zingine hakuchangia na hata zile alizochangia nyingi hakuwa anahudhuria....naam hata ikitokea misiba jirani alikuwa anatuma rambirambi na kusema aaah jamani tuko pamoja kisha anaondoka....basi watu walimvumilia sana na hakuna nafasi watu walipata wasaa wa kumsema zaidi ya marafiki mmoja mmoja ambao aliwachukulia poa na kusema...aaah nimewaelewa jamani....tuko pamoja sana!
Basi ilitokea siku mmoja siku moja alipata msiba wa Baba yake mzazi ambaye alikuwa anaugulia kwake, watu walipata taarifa za msiba na wengi wao wakasema hapa ndio mahali pa kumuonyesha UPAMOJA WETU....basi wengi walifika na kutoa pole na kuacha rambirambi (tena nyingi kuliko kawaida) na wao walisema tuko pamoja katika majonzi haya na kuondoka zao....basi kwa kadri muda ulivyokuwa unakwenda alikuwa akipokea rambirambi na pole za watu wanaokuja na kuondoka kama vile ile ni shule ya kutwa ama kituo cha kupigia kura....basi pale msibani palikuwa doro kabisa na hapo ndio akaanza kuona kimbembe cha "TUKO PAMOJA"....basi msiba ulikaa siku ya kwanza yote hamna kitu,basi akawachukua vijana ili awalipe na wakachimbe kaburi, na wao walichukua pesa na wakamwambia tuko pamoja na wao wakaenda makaburini na kuanza kupiga stori, mpaka siku ya pili inaisha baada ya kufoka sana ndio wakachimba tena refu kupita kawaida...naam siku ya tatu ndio ya mazishi hakuna hata mmoja anajigusa kwenda, na hapo alienda kwa kiongozi wa mtaa na kumuomba awaite watu, naam watu walikuja na wakaenda mpaka makaburini kimyakimya,hakuna mtu kulia wala kuzungumza na walipofika pale....watu walimtolea madukuduku yao yooote na wakasema ili iwe fundisho kwa wengine,kabla ya kuzika....ALALE JUU YA UDONGO ULE WA KABURI PALE JUU,NA HAPO AKACHARAZWA BAKORA ZA KUTOSHA MBELE YA MKWEWE,WATOTO NA NDUGU ZAKE NA ndipo ibaada ya maziko ikaanza na kila hatua ya kuzika alipaswa kushiriki ili ajue huwa inakuwaje....alisaidia kushusha jeneza chini na kabla mtu yeyeote hajagusa chepeo,alianza yeye kufukua mpaka alipochoka hoi ndio wakamsaidia,na hilo lokawa fundisho kwake na kwa wengine wote mtaani kuwa pesa sio kila kitu,ila unahitajika wewe!!!


ACHANA KABISA NA HUO UNAFIKI WA KUSEMA TUKO PAMOJA HALI HUNA HATA KIMOJA KINACHODHIHIRISHA UPAMOJA HUO!!!
(Watu wawili hawezi kwenda njia moja isipokuwa wamepatana.....hivyo hamna Upamoja wa maneno bila matendo na mapatano)

AHSANTE SANA, UBARIKIWE SANA KAMA UMENIELEWA!!!

Fredy Erasto Chavala
<King Chavala(MC)>
+255 713 883 797
facebook; King Chavala MC
Twitter @kingchavala