CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

Papaa On Tuesday....Leo Hakuna Papaa On Tuesday


Unajisikiaje siku unaamka ukatarajia Jambo liwe kama unavyotarajia kisha unakuta jambo lenyewe halipo kama ulivyolitarajia. Unajisikiaje leo umejiandaa kusoma Papaa On Tuesday ghafla unakutana na heading "Leo Hakuna Papaa On Tuesday" nini kinakuja kwanza kwenye Kichwa Chako??Umewahi sikia ile Sera ya "Utii Pasipo Shuruti" kwa maana ya kwamba hakuna anayekulipa mshahara kwa kazi unayoifanya Hakuna anayekushikia fimbo kuhakikisha unafanya lakini unawajibika kuifanya kazi hiyo kikamilifu sababu kuna watu wanakutegemea ufanye, utajisikiaje pale ambapo siku mtu anasema "kwanza kazi yenyewe silipwi", "Kazi yenyewe nafanya basi tu". Inahitaji Moyo Kufanya kazi kila siku kuandika Papaa On Tuesday pasipo kushurutishwa pasipo kulipwa ili kupitia kile Mungu alichoruhusu kuongea na watu wiki hiyo uweze kukiachilia.

Unavyotaka watu wa kufanyie kwenye maisha basi na wewe unawajibika kwa kipimo kile kile kuwafanyia wao kwanza, inakera sana unapoamka asubuhi watu walikuwa wanahakika utawafanyia jambo fulani kisha unawaambia kuwa lile jambo haliwezekani tena, cha
kwanza watu wanasema sasa si ungetutaarifu mapema?kwanini haujatuma taarifa, kwanini zinakuwa nyingi sababu "Walitaraji" kutoka kwako. Kutenda wema kisha kwenda zako ni dalili ya Ukristo na Ubinadamu. Sio kila kitu unachofanya kwenye maisha unataka kulipwa, ukiona uko kwenye hiyo Level kuwa kila unachotaka kufanya iwe msikitini, Kanisani ama popote unauliza nitalipwa shilingi ngapi mimi binafsi nitafaidikiaje ni dalili ndogo sana ya mtu asiye na upeo. Mambo mengi nimejikuta nikifanya pasipo tarakia kulipwa lakini mambo hayo yamekuwa yakinitengenezea fursa kwenye maisha yangu. Sina ninakowajibika kwa kuandika Papaa On Tuesday sina ninaye Mlenga kuandika Papaa On Tuesday but I believe kuwa kuna watu ninawaandikia ili uwafae maishani. Nimekuwa na Wadau wakubwa sana wa Papaa On Tuesday si kwa sabab8u nina toza hela ila kile nilichonacho na kukiachilia kinanipa fursa zingine kwenye maisha.


Hakuna kitu kinavunja moyo watu walitarajia Ufanye kitu fulani then haukufanya kwa sababu zako yamkini umefanya lakini kwa kiwango cha chini. Tumekuwa na kawaida ya kuchukulia pouwa sana mambo ambayo tunayafanya maishani baada ya watu kutuzoea. Unakuta kwenye ajira kipindi cha Probation mtu anafanya wonders basi subiri azoee ofisi, unakuta mtu anapoanza mahusiano na mtu basi anakuwa very committed akishaoa tu kila mtu anaingia kwenye ndoa na "expectations" tena za hali ya Juu mwisho wa siku hakuna kitu, unakuta unatakiwa ufanya event pengine kuimba, au Mc au Comedian lakini sababu unahisi wale watu wanakufahamu unachukulia pouwa sababu tu hakuna anayekulipa ama kuwajibisha. Ninajua kuwajibishwa ni hulka ya binadamu lakini tunaweza kufanya pasipo masharti.

Kila siku unapoamka jua kuwa watu wanatarajia Kitu toka kwako, je umejiandaa kufanya vile vile kwa namna ile ile sababu unawafanyia wale wale ama utafanya kwa kiwango kikibwa, wafanyabiashara lazima wajue wateja wao wana matarajio mapya kila siku, walio maofisini wale tunaowahudumia wana matarajio mapya kila siku, walio kwneye ndoa lazima wajue wenza wao wana matarajio mapya kila siku, kufanya vile vile kwa namna ile ile huwa inachosha. Hata kama hakuna mtu wa kukusimamia je utafanya kwa kiwango kile kile utafanya kwa moyo hata kama hauoni malipo ya kushikika kwa sasa?je utafanya kwa ubora zaidi ukitarajia fursa kufunguka??Huu ni Mwaka wangu wa tatu kila Jumanne nina andika Papaa On Tuesday, ninafanya kwa moyo ninafanya kwa ajili ya Wasomaji Wangu ninao wafahamu na nisio Wafahamu, kila mtu anaamka leo akijua Papaa On Tuesday itatoka, Utajiskiaje Siku nikisema "leo Hakuna" Ule Ukakasi unaousikia na maswali unayojiuliza ndipo utajua watu pia huwa wanajisikiaje pale walipotarajia Utafanya kweli kisha haujafanya kwa raha zako tu binafsi au kwa ubinafsi ulio nao.

Huwezi Jua Mungu anakutumia katika nini kuwahudumia akina nani, change the way u think, usichukulie poa kila kitu sababu tu unataka kujua unafaidikaje katika hilo, unapopanda kwenye maisha ya watu ni kwasababu pia kuna watu walipanda kwenye maisha yako. Na Unavyotaka watu wakufanyie kwenye maisha basi wafanyie wewe kwanza. Ukijifanya Mjuaji, Unapenda Sifa Watu watakuongelea pembeni na kukubeza siku likitokea na kukupata.

Papaa Ze Blogger.
0713 494110