Leo ninawaletea habari njema zilizoambatana na mwaliko maalum kwa watu wote wenye mapenzi mema na Samuel Sasali, The Blogger, MC,Mzee wa Ideas mengi ambaye mara zote husema Mungu alimnyima urefu akamjalia Mdomo (kuongea sana) na kukosa aibu pia!!!
Baada ya sarakasi za kutosha za kutafuta mwenzi wa kumfaa hatimae pacha wangu amegota na kumpata mlimbwende wa pekee aliyewashinda wanawake zaidi ya Bilioni 4 duniani na kuwa wa pekee...Usukani mdogo unaoendesha Merikebu kubwa!!!
Ndio ni binti huyu Dk Milembe John Madaha ambaye ameteka moyo wa kaka Mkubwa na kwa huyu Papaa amegeuka rapper,mwana mashairi na mtiifu sana!!
Kama una kumbukumbu nzuri, blog hii imewahi kum-ZOOM kijana huyu kama mmoja ya vijana wanaopaswa kuigwa na vijana wengine,fuata link umfahamu vema;
.http://chavalamedia.blogspot.com/2012/08/salaam-leo-katika-kipengele-hiki.html
Basi habari njema ndio hii, jumapili hii wewe na wenzako wote ambao ni marafiki wa kweli Samuel Sasali au ni msomaji wake wa Papaa On Tuesday au ni Mwanachama wa Marafiki Huru au ni mpenzi wa Friends On Friday au umewahi kufundishwa na yeye popote pale,shuleni, chuoni au kanisani au hata kama amewahi kusherehesha shughuli yako yeyote ile..basi sasa ni saa ya kumuunga mkono kwa kumaanisha!!
Ni jumapili hii ya tar 23/06/2013 kuanzia saa nne asubuhi pale Mbezi Beach A katika kanisa la VICTORY CHRISTIAN CENTRE TABERNACLE (VCCT),Unaweza ukapanda gari mpaka mwenge na kupanda usafiri wa kanisa unaondoka hapo tatu na nusu ama ukachukua bajaji mpaka huko kanisa la hema,au ukapanda gari mpaka kawe mwisho na kupanda bajaji pia mpaka kanisani au ukashuka Mbezi Tanki bovu na kuchukua bajaji au bodaboda mpaka kanisani...lakini kama unakuja na private car njoo na barabara ya Mwai Kibaki(zamani old bagamoyo road) kisha baada tu ya daraja utaona kibao kushoto kwako kama ukitokea mwenge then fuata njia hiyo kwa hakika huwezi kupotea!!
Ni marufuku kuja mikono mitupu na ni marufuku kuja peke yako,namaanisha jaribu kubeba zawadi ya pongezi na usiache kuwajulisha wengine wanaomfahamu Papaa!!
Haitakuwa siku ya kawaida kwa hakika maana Papaa ni baadhi ya vijana nguli ambae tayari alikuwa kwenye kundi la ma-senior bachelors na sasa rasmi anaanza kuaga aga kundi hilo....na hata harusi yake itakuwa mwishoni wa October, kama hakutakuwa na badiliko lolote basi itakuwa 26TH OCTOBER.. hivyo mwenye macho na asome na kuelewa!!!
Mimi binafsi kwa niaba yangu mwenyewe na kwa niaba ya Blog hii na wafanyakazi wote wa Chavala Ideas Platform ninatamka baraka nyingi kwa rafiki yangu mkubwa na pacha wangu Samuel pamoja na Shemeji yangu,his wife to be ....Mungu awaonekanie katika kila hatua ya michakato hii mpaka hapo watakapooana!!!
Na kwa hakika tuko bega kwa bega,naam tuko tayari kutoa mchango wowote ule wa hali na mali utakaohitajika ili kufanikisha shughuli hii,KWA HAKIKA NINAMKUBALI SANA PAPAA KWA JINSI ALIVYO NA ALIVYO MCHAKARIKAJI,HE IS AMONG MY BEST FRIEND IN TOWN!!!
Kwa wale msiomfahamu zaidi basi msiache kutembelea Blog yake kila siku
"samsasali.blogspot.com"
NA MWALIKO HUU NIMEUTOA KWA HIARI YANGU KWA NIABA YAKE,HIVYO KAMA UKIKWAMA AU UKIWA NA SWALI LOLOTE NAMNA YA KUFIKA HAPO KANISANI BASI USISITE KUWASILIANA NASI,NASI TUTAKUSAIDIA KUFIKA!!
+255 713 883 797
King Chavala-MC