CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

John Shabani:Mwalimu na Mwimbaji wa Injili aliyepitia magumu ya maisha!!


John Shabani:Mwalimu na Mwimbaji wa Injili aliyepitia magumu ya maisha.
John Shabani

JOHN Shabani si jina geni masikioni mwa watu hasa wapenzi wa muziki wa injili na wanafunzi wa muziki huo.

John mzaliwa wa kijiji cha Kirando katika kitongoji cha Nyankima, kata ya sunuka, Wilaya ya Kigoma Vijijini, anatokea katika ukoo wa waumini wazuri wa dini ya kiislam.

Muimbaji huyo ambaye umaarufu wake uliwika baada ya kushiriki tamasha la pasaka ambalo anasem akuwa liliinua uimbaji wake na anatamani kama atapewa nafasi ya kushiriki tena kwa miaka ijao ikiwemo mwaka huu.

Anasema kuwa historia yake baada ya kumaliza elimu ya msingi katika shule ya msingi kirando, alijiunga na elimu ya sekondari, lakini kutokana na itikadi za kidini, alijikuta akiwa katika wakati mgumu wa kupigwa vita na wazazi, kwasababu ya uamuzi wake wa kujiunga na Dini ya kikristo hali iliyomsababishia muimbaji huyo kuishi miaka mingi akiwa mbali na wazazi wake.

Mwaka 1992, John akiwa kijana mdogo, alipata ufadhili wa kwenda nchini Kongo ambako huko alijifunza muziki na kusoma Chuo cha Biblia na ndipo kipaji chake cha kutunga nyimbo na kuimba kilijitokeza kwa kasi.

Muimbaji huyo anasema kuwa hakutaka kuona mtu yeyote akiwa katika hali ya kukata tamaa, maana alifahamu madhara yake kwasababu hiyo, alianzisha vikundi mbalimbali vya vijana akiwa na lengo la kuwaelimisha ili kujikwamua katika hali ya kukata tamaa na kutokujihusisha na vitendo viovu kama vile madawa ya kulevya, Ukahaba na anasa za kila aina mambo ambayo aliyapiga vita.

Shabani anasema kuwa ameishi miaka mingi kama yatima, lakini hali hiyo imemsaidia kujifunza mengi na kuwa na tabia njema, kumheshimu na kumthamini kila mtu, hali hiyo ilimfanya kupata kibali machoni pa wengi.

Anasema kuwa amekuwa msaada kwa vijana wengi ndani na nje ya nchi na kuwakwamua waliokuwa wamekata tamaa na kujihusisha na vitendo viovu.Pia kutokana na ujuzi wa muziki alioupata na kipaji alichonacho cha kutunga, kuandika nyimbo na kuimba, anasema kuwa amekuwa msaada kwa waimbaji mbalimbali binafsi na vikundi , hasa nyimbo za Injili.

Mwaka 2001 John alifunga pingu za maisha na Debora Shabani na mwaka 2002 walifanikiwa kupata mtoto wa kike aitwae Joyce, akiwa na maana ya kuyasahau maisha ya huzuni na shida na kujitabiria maisha ya furaha.

Mwaka 2004, John aliajiriwa katika kampuni ya Msama promotions ya jijini Dare es salaam, kampuni inayojihusisha na kuinua vipaji na pia kuwainua vijana na watu wa rika na jinsia zote waliokata tamaa ya maisha na hasa wale walioko vijiweni wakijihusisha na madawa ya kulevya, ukahabaa

Albamu yake ya kwanza Marufuku kukata tama anasema kuwa imewasaidia wengi waliokata tamaa na kuwapa matumaini mapya albamu hiyo na nyingine alioirekodi mwaka 2009 zilizoitwa huu ni wakati wangu na Moyo wangu.

John ametembelea nchi mbalimbali, akijifunza maisha ya watu ikiwemo kugundua kwamba karibu asilimia kubwa ya wanadamu, awe maskini, tajiri, msomi au asiye na elimu, wenye vyeo au waajiriwa, watoto kwa wakubwa, wanaume kwa wanawake, awe mzungu au mweusi n.k, wote kwa njia moja au nyingine wamepitia katika hali ya kukata tamaa au kukatishwa tamaa na jambo fulani, mtu, watu, hali au mazingira fulani.

Ndipo mwaka 2006, alipata maono na msukumo mkubwa wa kuandika Kitabu ambacho kitakuwa msaada kwa njia moja au nyingine kwa kila atakayekipata. Kitabu hicho kinaitwa Marufuku kukata tama. Kitabu hicho pamoja na kile kiitwacho “Mafanikio yatokanayo na kusifu na kumwabudu Mungu” vinategemea kukamilika baada ya miezi miwili.

Mwaka 208 sitausahau  ilikuwa ni siku ya huzuni na majonzi, siku ya kilio na kuomboleza. ni siku alipofariki mke wake mpendwa na mwimbaji maarufu wa muziki wa Injili, Debora Shabani, mwimbaji aliyegusa mioyo ya watu wengi ndani na nje ya nchi, niliumia sana lakini sikukata tamaa”anasema.

Shabani alitunukiwa tuzo ya heshima pamoja na cheti kwa kutambua mchango wake kwa ajili ya kuinua vipaji na pia kuchangia kuinua muziki wa Injili Afrika mashariki na kati. Pamoja na hayo amekua akianzisha vikundi mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu Tuzo anayosema kuwa ilitolewa na kampuni ya Christian promoters Ltd, Pia ni miongoni mwa waanzilishi na kiongozi wa Chama cha muziki wa injili Tanzania (Chamuita).

Mwaka 2011, John alipata heshima kubwa kama mwalimu, kuongoza kundi la waimbaji (Tanzania gospel all stars) kuimba wimbo maalum wa miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.

Anasema kuwa pamoja na mzigo mkubwa aliokuwa nao kwa kidogo anachopata,amehakikisha kuwa anaisaidia jamii, hasa watu wenye ulemavu, wajane na yatima Vijana waishio katika mazingira magumu, pamoja na wakimbizi. Tayari ameanza mikakati ya kusajili Taasisi Hope Foundation kwa ajili ya maono hayo.

Pamoja na malengo mbalimbali aliyonbayo Shabani, lakini pia ni kuwa na kituo cha watoto na vijana, lengo ni kuandaa kizazi chenye maadili mema, kuibua, kutambua na kuinua vipaji vya watoto na vijana, mbinu na mikakati ya kuwakwamua watoto

Pia anasema kuwa mpango huo unalenga kutafuta ufadhili kwa ajili ya kuaendeleza vijana kielimu pamoja na kuwawezesha pale inapobidi, kuandaa matamasha ya watoto na vijana, kuunganisha watoto na vijana wengine duniani, kuwapa kipaumbele watoto na vijana wenye elemavu, kuwa na kiwanja kwa ajili ya michezo mbalimbali ya watoto na vijan.

Kwa sasa anajishughulisha na kufundisha bendi,vikundi na waimbaji binafsi na kusema kuwa lengo ni Kufundisha kuimba au kunyoosha,Jinsi ya kuitumia sauti kuitunza na kuitawala,  Historia ya muziki na maadhi ya muziki, Sifa na mbinu za kuwa mwimbaji bora, Matumizi ya kipaza sauti,Kuwatungia nyimbo au kurekebisha nyimbo zilizotungwa tayari, Kutoa ushauri kwa wanaotatarajia kuingia studio, mbinu za kuitangaza albamu au nyimbo zikubalike na Kutengeneza muziki wenye viwango.