CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

Papaa On Tuesday.....Tofauti Ya Kuweza na Kutokuweza Ipo kwenye Kuamua


Tunakila sababu ya Kumshukuru Mungu kwa ajili ya siku hii ya leo ya Jumanne ya kwanza kwenye nusu ya pili ya Mwaka 2013, mwaka umeisha ingia nusu wenye kumaliza vyuo wameshamaliza, wenye kuendelea wanaendelea wenye kusoma wanakazana, wenye mipango ya biashara wanakazana, wenye kuanzisha familia  nao wamo wapo pia ambao mpaka sasa hawajajisoma wapo wapo tu yamkini wala hawajui kama na Obama alikuwepo nchini kwetu.

Miaka michache iliyopita niliwahi kuwa na Supervisor Mchina ambaye tulikuwa na kawaida ya kukutana Dept yetu na ku-plan mambo ya wiki na pia kupitia report za utendaji kazi. Ninakumbuka siku moja tukiwa kwenye kikao alichora duara mbili moja ikiwa kubwa na nyingine ndogo ikiwa ndani ya ile kubwa. Namkumbuka Mr. Charles Guo aliniambia duara la nje linaitwa "Uwezo Halisi" na duara la ndani linaitwa "Uwezo wa Sasa". Tofauti ya Kile unachokifanya sasa na Kile unachoweza Kukifanya sasa kipo kwenye kitu kinaitwa "Kuamua". Nakumbuka alitumia mfano huo wakati tunaongea issue za Performance Management alisema Watu wengi sana wanafanya mambo mengi sio katika Uwezo wao halisi, Uwezo walionao kutenda ni Mkubwa zaidi kuliko kile wanacho kifanya na kinachotofautisha kile wanachokifanya sasa na Kile ambacho wanaweza kukifanya kinajengwa na tofali kubwa lenye kuitwa "KUAMUA KUFANYA". Kuamua kufanywa kunaletwa na Kichochezi (motivation) ama Catalyst ama sababu ya mtu kufanya ndio maana kwenye makampuni kuna incentives mbalimbali ili kuchochea uwezo wa wafanyakazi kwenda extra mile.

Wiki hii katika Ujio wa Rais wa Marekani nimekumbuka sana mfano huu wa Supervisor wangu kuwa mambo mengi sana ambayo tunayafanya sasa kumbe tunaweza kufanya zaidi ya pale tunapofanya ambapo ndipo kwenye uwezo wetu halisi iwapo tu TUTAAMUA kufanya kikamilifu. Wiki hii nimeshuhudia jiji la Dar-es-Salaam likiwa safi na likiwa halina foleni zisizo na sababu, barabara za katikati ya Jiji zinapigwa deki usiku na Mchana, Jiji limekuwa safi na Salama likarudisha maana halisi ya Jina tulipopewa na Sultan kutoka Oman kuwa ni "Haven Of Peace" ni "Bandari Ya Salama". Nimeona Watu wakilindwa usiku na Mchana kila kitu kimekaa kama kinavyopaswa, wamachinga wameondolewa kwa nguvu kupisha Obama apite, Barabara ya Ubungo pale kwenye Mataa ilikuwa na Makorogeshi ya Kutosha pametengenezwa usiku na Mchana taa zinawaka vizuri kumbe uwezo wa kufanya tunao sana iwapo tu tutaamua kufanya sisi kama Watanzania pasipo ujio wa Obama.
Kinachofanywa na Serikali ya Tanzania ni Reflection ya Maisha halisi ya Watanzania kama sio Waafrika kwa Ujumla. Nakumbuka Wakati ninasoma mpaka Chuo Kikuu ile wiki ya Kuelekea kwenye Mitihani ndipo unaona watu sasa ndo wanashika vitabu kisawasawa kumbe unajiuliza swali kwanini mtu anakesha namna hii kumbe alikuwa hajaamua kusoma, kama angeanza semester wakati inaanza yamkini maisha yake ya kusoma yangekuwa yako mbali uwezo na upeo wake ungekuwa wa kutisha lakini ajabu ng'ombe analishwa siku ya mnada. Sisi ni watu ambao kwenye nyumba zetu kuna vyombo ambavyo havitumiki mpaka waje wageni, hata kama mtakuwa hamna wageni miaka 800 lakini kuna glass ziko kwenye kabati, kuna sahani ziko kwenye kabati ambazo wenyeji hawazitumii mpaka aje mgeni utashangaa mgeni akija nyumbani ndipo siku hiyo mtakunywa na soda, ndipo siku hiyo mtatumia sahani nzuri, ndipo siku hiyo mtapelekwa kuoga mchana, ndipo siku hiyo utaona mpaka goti la mkeo ama mama akiwakaribisha wageni kwenda kuchukua chakula ajabu ni kwamba Mgeni ama wageni wakisha ondoka tunarudi katika maisha yetu yale yale ya sahani za plastiki na soda za sikukuu kumbe kuna siku tukiamua kama familia tunaweza kula kama kuna wageni na hakuna madhara.

Ninakumbuka enzi hizo ninasoma shule ya Msingi ilikuwa siku kama kuna wakaguzi wanakuja ama mgeni fulani kututembelea siku hiyo bustani zote ndipo zitatifuliwa, zitamwagiwa na kupendeza, kwaya ya shule itafanya mazoezi ya nyimbo za kumpamba mgeni rasmi mpaka atajiramba kwa sifa, tabia hii ipo kwenye nyumba zetu za Ibada na Makanisa penye ugeni tutafanya zaidi ya kawaida hata sare tutashona, tabia hii ipo kwenye maofisi yetu, tabia hii ipo kwenye familia zetu, zipo kwenye mahusiano ya boyfriend na girlfriend na wachumba uwezo wa kufanya zaidi ya kile unachofanya sasa na kuzorotesha ndoa yako upo kwenye KUAMUA. Kwneye maisha yetu ya kawaida pia kuna watu ambao hawavai vizuri mpaka wawe na ugeni hawasafishi vyumba vyao mpaka siku akisikia anatembelewa, hawabadilishi mashuka na mapazia mpaka uwepo ugeni haya mambo ndiyo ambayo yapo kwenye Jamii yetu tofauti ya kile tunachokifanya sasa na Uwezo wetu wa kufanya upo kwenye Kuamua.

Kila mtu anaujua uwezo wake wa kufanya zaidi ya kile anachokifanya sasa lakini tatizo hujaamua kufanya, yamkini unaimba, yamkini ni mwandishi, yakini unasoma, yamkini ni Mwajiriwa ama Mwajiri kile unachokifanya kwa sasa kama ukiamua kikweliii ukaweka miguu yote ndani ya hicho ukifanyacho basi ungekuwa mbali kupita maelezo. Inawezekana unachukulia pouwa kile unachokifanya kwa sababu hujaamua kwenda extra mile, assume leo ukaamua ubadilike ubadilishe aina ya huduma unayofanya, ukaamua leo upate feedback ya kile unachokifanya uone watu watakuambia nini yamkini unafanya kitu ambacho kinakuharibia biashara yako, yamkini unaweza ukawa unafanya jambo chini ya kiwango ambacho wateja wanategemea ukijichunguza kiukweliii unaweza kufanya zaidi ya hicho unachofanya. Leo hii ukiamua ufanye kwa uhalisia wako uwezo wako wa juu kabisa kufanya unadhani utakuwa wapi, leo hii nikaamua kusaka news kwa uwezo wangu kikweliii ninaweza kuwa na gazeti la Gospel Today, leo hii ukaamua kuboresha ndoa yako kwa uhalisia wake utafurahia ndoa yako, ukiamua leo kuongea na Wateja unaowafikia kwa biashara ama huduma yako unadhani wataongea namna gani yamkini kuna kazi umewahi fanya ukaharibu na yule uliyemfanyia amekuwa wakala wa kusambaza uharibifu wa kile ulichofanya kwenye kazi yake, yote yawezekana kwenye maisha UKIAMUA.

Tofauti ya waliofanikiwa na kwenye maisha na wale wasiofanikiwa ipo kwenye KUAMUA. Wengi wetu tumebaki kuwa wachambuzi na wakosoaji na sio watu wenye kuamua, wengi huwa wanasisimka wakisoma Papaa On Tuesday lakini kasheshe iko kwenye Kutendea kazi. Yesu akasema anaheri yule anayesikia na Kutenda. Upo hivyo ulivyo kwa sababu ya aina ya maisha uliyoyaamua na siku ukiamua kufanya utashangaa kwanini ulichelewa kufanya maamuzi sababu kubwa Unaweza kufanya lakini yamkini hujaamua kufanya ingawa unajua ndani ya Moyo wako UKIAMUA kikwelii kufanya unaweza kufanya na kubadilika. Yamkini umekuwa ukitamani kubadilika tabia fulani kwenye maisha yako lakini umekuwa ukiindekeza ili uendelee kuwa nayo huku ukitambua fika tabia hiyo ndiyo imekuwa kikuharibia kila siku kwenye maisha lakini hujaamua tu kubadilika ukiamua inawezekana.

Hatma ya Maisha yako yanategemeana sana na MAAMUZI unayoyafanya kwenye maisha, ukiamua kubadilika utaona mabadiliko ukipotezea mabadiliko utajipoteza mwenyewe, ukitazama duara lako kubwa la uwezo ulio nao halifanani kabisa na kile ambacho unakifanya na unajua UKIAMUA inawezekana tatizo halipo kwenye kile unachokifanya tatizo lipo kwenye Maamuzi yako ya kuamua kufanya kwa utashi wa ndani kabisa.

Kuna bloggers wengi sana bado hawajaamua kufanya, kuna wafanyabiashara wakubwa sana wenye mafanikio wanaogopa kufanya, kuna presenters wazuri sana lakini hawajaamua kufanya kile walichoumbiwa kufanya sababu ya wasiwasi wa ndani,sababu ya maneno ya watu, yamkini sababu ya kiimani, ama una mashaka watu watakuonaje watakuchukuliaje utaendelea kubaki kama ulivyo sababu tu hujaamua kuwa vile unavyotaka kuwa kwa kuangalia tu mazingira ya nje, adui nambari one wa mafanikio yako ni nafsi yako mwenyewe. Ukimtafuta mtu yeyote aliyefanikiwa kwenye maisha atakuambia "aliamua".

Tofauti ya Wewe na wale uonaoona wamefanikiwa ipo kwenye Kuamua, ukiamua kulala njaa siku 7 ili kutimiza ndoto yako itakuwa, ukiamua leo kuacha tabia za kijinga kwenye maisha yako utapiga hatua, ukiamua kutulia utaoa ama utaolewa, ukiamua kukuwa kiufahamu ndipo utakapofanikiwa kumbuka kuamua ndiko kutakutofautisha na wasio amua.

Amua Sasa.

Ze Blogger
0713 494110