CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

Papaa On Tuesday......Mwanga Wa Mbalamwezi Haukaushi Muhogo!!


Nimatumaini yangu ya kuwa wote tu wazima na tunaendelea vema na shughuli zetu za kile siku.

Katika kabila letu la Wanyasa, chakula cha asili cha kikabila ni ugali wa muhogo pamoja na dagaa kutoka Ziwa Nyasa. Kwa mnyasa kupata chakula cha namna hii basi unakuwa umemfikisha nyumbani kabisa kuliko kumpa chipsi mayai au kitimoto na ndizi. Nilipokuwa kijijini wakai fulani niliona jinsi mihogo inavyokaushwa, akina mama wa Kinyasa watajihimu asubuhi kuimenya mihogo hiyo na kuiloweka kwa muda kisha kuwekwa juani ili iweze kufaa baadae kwa kutwangwa kisha kupatikana unga wa muhogo wenye kupikwa ugali hupatikana. Kuna familia zingine ukifika wakati wa jioni huanua mihogo hiyo kwa kuiweka ndani kuhofia isiharibiwe na wanyama ama hata kuibiwa pia maana ndo deal kwa familia zilizokuwa zinaaminika kwa uchawi walikuwa wanaacha tu anayeiba yatamkuta ya kumkuta. Siku moja nikamuuliza Marehemu Babu yangu "Kwanini Wengine wanatoa Mihogo kuingiza ndani"?akaniambia kule kijijini kuna msemo wanautumia "mwanga wa mbalamwezi haukaushi muhogo". Nilitamani kufahamu maana ya msemo huo wenye kubeba maana kubwa sana nyuma yake.

Kuna mambo ambayo kwenye maisha huwezi yabadili ni kama kutaka kulazimishia mwanga wa mbalamwezi ukaushe mihogo, mihogo yake ni jua. Kuna watu wana tabia ya kulazimishia kufanya mambo wasiyo na uwezo nayo. Yaani unataka kufanya mambo ili watu wakukubali kuwa wewe mambo safi, unataka watu wakuone na wewe uko juu una Samsang Galaxy wakati matumuzi yako ni kupiga simu na kutuma SMS, unapiga picha event moja kesho una delete picha hizo hizo kuweka event ya pili. Kwenye vikao vya harusi walizojaa marafiki zako unatoa ahadi kubwa kubwa za harusi uonekane na wewe mambo safi. Kuna mambo ya mbalamwezi kuna mambo lake jua ndo yanaenda.
Kwanini unataka uishi zaidi ya vile ya ulivyo, kwanini unaishi maisha ya kujitahidi??kwanini usiishi vile ulivyo kwani unapoteza nini unapokuwa unaishi maisha yako ya kawaida. Hii tabia ya kutembelea kwa watu kishaukakuta wenzio wana flat screens na wewe ukataka, ukakuta wana Sub Woofers za Ukweli mwisho wa siku na wewe ukataka, Ukaenda kwa watu ukakuta wana Kengere na wewe ukataka, ukakuta mtu ana BlackBerry na wewe unajinyimaaaaaaaaaaaaaa eti na wewe uonekane upo kwenye Class kama uwezo wako ni kutoa mwanga basi usitake kukausha mihogo kuna mambo hayawezekani kwa sasa wala baadaae kwanini uyalazimishie?

Kizazi chetu kimekuwa na changamoto sana eneo mojawapo lenye kuleta changamoto ni kuoa na kuolewa. Unakuta saa nyingine kuna watu wanawafukuzia watu mpaka wanakera, na siku hizi wanawake wenye uwezo wamekuwa ni sababu ya kunyang'anya wanaume wa wanawake wasio kuwa na uwezo na wanaume wenye tamaa wamejikuta wakidondokea kwenye mikono ya wanawake mabaradhuri. Fedha ina ushawishi, fedha inatakatisha, fedha ni jawabu la mambo yote sababu ya uwezo wa mwanamke kuweza kumudu kununua mambo yanayoweza mfanya mwanaume aonekane nae katika jamii wamejikuta wakiacha mapenzi ya kweli na kuingia kwenye tamaa, kuna rafiki yangu amehongwa gari, gari kabisaaa lakini jamaa hana uhuru kabisa, kuna rafiki yangu amehongwa chain ya 1.5 Milioni na Blackberry juu lakini anafungwa kupita mbwa wa kizungu, inakufaidia nini kupata kila kitu na huku unapoteza mpaka uhuru wako wa kucheka, unayemcheka fulani unaulizwa, unapomtazama mtu mara mbili unaulizwa why?ni mara kumi kuwa na simu ya kitochi na kubaki na mapenzi ya kweli. Kuna wanawake na wanaume wako tayari kufanya chochote wanachoweza kutimiza tamaa zao za mwili, unaweza kupewa nyumba bure, unaweza kupata gari bure, unaweza kupewa investment bure lakini huwezi kupata amani ya kweli na uhuru wa kweli for free, kama unajua uwezo wako kutoa mwanga usitake kukausha mihogo.

Heshima ni kitu cha bure sana, lakini nani anataka kutunza heshima yake, rafiki yangu aliwahi niambia "Papaa tangu nimeanza kutunza heshima haijawahi nisaidia". Kwani unataka utunze heshima ili iukusaidie?kuwa na heshima ni msaada mkubwa sana kwenye maisha, kujiheshimu, kuheshimiwa, kushemiana ni jambo ambalo naona sasa linapoteza mkondo wake watu wanakuambia its a matter of time itashuka leo kesho watu wanasahau, leo unafanya jambo la kusikitisha jamii lakini kesho heshima inarudi mjini, katika kila uovu kuna mtu wa kukutia moyo. Mwenye mbili havai moja, na mwanga wa mbalamwezi hata siku moja hauwezi kausha mihogo, lina heshima yako ili uheshimiwe.

Kufikiria kutumia mwili wako kupata kazi, kufikiria kutumia mwili wako kupata gari ama nyumba basi jiandae tena kutumia mwili wako kupanda cheo, jiandae mwili wako kupata nafasi ya kwenda kusoma, jiandae kutumia mwili wako ili usipunguzwe kazini, jiandae kutumia mwili wako kupata hela ya mafuta, jiandae kutumia mwili wako kufanya service ya gari, jiandae kufanya chochote kutumia mlango ulioufungua kwenye maisha yako, kama unajua wewe ni mbalamwezi usitamani kazi za jua kila jambo lina makusudi yake hapa duniani.

Kila mtu atavuna alichopanda haijalishi unapanda hadharani ama gizani, mchana jua humulika na usiku mbala mwezi hutoa mwanga. Mwanga wa mbalamwezi haukaushi muhogo.

Think differently and make a difference 

....//Papaa
0713 494110