CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

Papaa On Tuesday........Everyone Has A Story....Its a Matter Of Time


Ninawasalimu Kupitia Jina la Bwana Wangu Yesu Kristo siku hii Ya Leo. Nimatumaini Yangu Ya Kuwa wewe ni Mzima na Unaendelea Vema na Shughuli za Ujenzi Wa Taifa. Mwenzi January leo tunaugawa nusu kwa nusu ndio mwaka 2013 umeanza na kasi yake. Ninajua ni mwezi ambao kama unatafuta kukopa hela basi ujue unahitaji kuwa na vyanzo vya uhakika visivyopungua 15 maana ni mwezi ambao majority ya maisha ya kawaida ya Mtanzania tupo kwenye kuishiwa maana kwetu kujifunza kuwa kila mwezi january ni mwezi mgumu ni zoezi linalohitaji kugeuzwa nia. Kwa maombi maalum ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Vya Dar-es-Salaam, nimelazimika kufanya mwendelezo wa Papaa On Tuesday niliyoandika Mwaka Jana.



Kwenye maisha yetu haya ukiona mtu leo anaendesha gari, amejenga nyumba, ana huduma yake, amejenga kanisa, ameolewa. Kila Mmoja wetu anachokitu cha kusema. Ukimuona tu mtu unaweza kusema mambo yake yalikuwa mteremko sana wewe unapata tabu peke yako duniani. Kumbe laiti kama ungejua everyone has a story to tell.


Kuna watu huwa wanapenda kusema "afadhali ya Wewe", unapimaje afadhali??afadhali ni suala la Mtazamo kwa maana ninachojua afadhali zetu hazifanani, afadhali yako sio yangu, afadhali kama anasa, inawezekana Anasa kwangu kumbe kwako kawaida, haya ni maisha yetu ya kila siku katika maisha kila siku eti afadhali ya Jana. Kuna watu wamenyong'onyea kabisa kwenye maisha kama sio wamenyong'onyeshwa na wengine hapa duniani nakuona wao ndio hawafai katika maisha wao hawana bahati. Pengine kazi walizotegemea wamekosa, Tender walizotegemea Wamekosa, Wateja Waliowategemea Wamekimbia, Shule walizotegemea wamefukuzwa, Ndoa walizotegemea zingekuwa furaha leo kila Mtu analala kwake, Watumishi wa Mungu waliowategemea Wamewatenda, Wanaume ama Wanawake waliodhani Wange date wote Kumbe Wamewakosa, yaani kila Ukijitafakari wewe ndio unajiona taka taka, Watu wanakuona Unatabasamu Kila Ukiwa nao laiti kama Wangepata Access ya Moyo Wako nakuona wingu la Simanzi ulilolibeba basi wangepaswa kukupa ambulance ya Faraja kila sekunde. Kumbe Nyuso zetu zinaficha sana yaliyo ndani ya Mioyo yetu. Mwaka 2013 unaouona kama ni mrefu sana safari kwako imeanza na Ukakasi mwingi sana wa kutosha.
Kila Mmoja wetu ana sehemu ametoka, kuna watu ukisikiliza Historia zao, walikotoka lakini pale walipo sasa basi utaamini afadhali zetu hazifanani. Kwenye Maisha haya tunayoishi usione tu watu leo wanavaa tai, wengine wanavaa high hills ukatamani kuwa kama wao, thubutu yako ukiona mtu leo amekaa kwenye kaofisi unamwambia "heri wewe mwenye kazi" laiti kama ungalijua huyu mtu ilimgharimu nini leo kukaa kwenye hiyo ofisi usingediriki kumtamani wakati huo pengine ndio ungemkatisha tamaa.
Kuna watu leo wana ndoa nzuri sababu kuna wengine Mungu ameamua kuwapa faraja ya mioyo yao maana yake, hapo kabla mioyo ilikuwa ina viraka vya kutosha sana ya kuumizwa, kuna watu Mungu amewapa leo kazi nzuri kama faraja ya kule walikopitia, kuna watu wakikuambia historia za maisha yao utaona wameongezea chumvi ili kunogesha kumbe ni kweli. Kuna Wengine duniani ni Miujiza kila mume akikumbuka Mke aliyempa anatoa machozi maana ni "Muujiza". Kuna wengine Wazazi Wakituona Watoto wao Wanakumbuka Muujiza Mungu aliyotenda kwenye maisha yao.
Mimi ni Muujiza kwetu, mimi ni jibu la Maombi, mimi sio mtoto wa matokeo ya "Uzazi Wa Mpango". Baba yangu alipomuoa Mama Yangu, ndugu za Baba yangu hawakuwa Wamempenda Mama Yangu kwa sababu kadha wa Kadha hata kwenye harusi ya baba na Mama, Familia ya Kina baba wengi walikacha kwenda kwenye harusi kama sio wote. Shangazi yake na Baba alimwambia baba yangu kwa kuwa ameamua kuoa mwanamke wasie ridhia basi kama Itatokea Wakapata mtoto kwenye maisha yao akakate kidole gumba cha Shangazi yake. Unaweza pata picha unaenda kuanza maisha unaenda kuoa huku kila mtu amekunenea mabaya na wakitaraji mabaya yakupate ili wakucheke. Baada ya Ndoa ya baba na Mama ilipita Miaka ambayo ubongo ungeanza kusema yamkini hatutapata Mtoto, na wakati huo mama yetu alikuwa na afya mgogoro baada ya miaka kadhaa kupita bila mtoto. Mama aliwahi niambia akaingia katika maombi kumwambia Mungu Kwanza amponye, then ampe Kicheko kwenye maisha yake, sababu amekuwa mtu wa kudharauliwa sababu ameamua kumngojea Mungu, akiwa kwenye maombi akafanya nadhiri kwa Mungu akasema "Kama Mungu Ukinipa Mtoto, Ninaomba Mtoto Wangu Wa Kwanza Awe Wa Kiume, Nitamtoa huyo Mtoto Kwako Kama Sadaka, na Nitamwita Jina Lake Samuel, Sababu Samuel Maana yake Nalimuomba Kwa Bwana na Nikamtoa Kwa Bwana". Baada Ya Maombi hayo na baada ya Miezi Michache kupita Mama yangu Akapona Ugonjwa wake na Kisha akapata Ujauzito, Mtoto aliyezaliwa akaitwa Samuel Ze Blogger. Kila Mama yangu anaponitazama leo anakumbuka Mungu alivyomfuta machozi katikati ya waliomdharau leo ukiona hiki kichwa Cha Blogger kinatoa madesa ya ukweli, unasema "Lina Heri Tumbo Lililokuzaa" Ukitaka kupata mtoto kama mimi au zaidi ya mimi there is a PRICE to Pay.
Kuna watu sababu ya aibu na shida zinazowakabili waliwahi kujuta kwanini walizaliwa na kwanini walizaliwa katika Ukoo huo waliozaliwa, kujuta hakujawahi kumsaidia mtu kama sio kuamua kutenda. Maisha yetu kila mmoja kwa sehemu yake ni full adventure. Kuna familia zingine umeolewa ama umeoa huko basi full tegemezi yaani wanawategemea mpaka aibu ya kuwanyima inapotea kabisa. Kuna watu tumewahi ama Mtaa, Kuna watu wamewahi ama ofisi, kuna watu wamewahi kimbia nchi kama sio Mkoa kutokana na aibu na hali za maisha, bora kubeba mabox Uingereza kuliko kuwa dereva wa dala dala Bongo watu wamekimbia nchi zao, Watu Wamekimbia ndoa zao, life is full oF Stories, Kama tungekuwa tunaandika Biblia kutoka kule ulikotoka mpaka ulipo basi ungeweza tengeneza Sura Kadhaa katika Kitabu Cha Mwanzo. Niliwahi Kuandika kwenye Papaa On Tuesday moja kuwa "God's Ways Are Zigzag" yaani njia za Mungu zimepinda pinda sana Safari Ya Siku 40 inaweza kukugharimu Miaka 40 kama wana wa Israel, Haijalishi ni Miaka Mingapi lakini Kanani Utaingia.
Kuna Watu wako Bongo na pengine hawafanyi kazi nzuri kama wewe unayofanya na umewazi kipato lakini huwezi amini wamewajengea wazazi wao kama sio mzazi wake mahali pa Kujistiri, Kuna watu Wana hali mbaya sana lakini wao ndo Nguzo Za Familia, Kuna Watu nakumbuka nimesoma nao Chuo, Boom analopata ndilo anasomeshea mdogo wake nae apate Elimu. Unaongea nini wewe unayelalamika Mshahara hautoshi kutwa kucha kumbe tu unaongeza matumizi ya kutoka kupanda Bajaj kwenda Taxi kisa mshahara umepanda, kuna watu hawajawahi kuwa na kitu kinaitwa Mshahara kwenye maisha yao, wamekuwa Wakiomba Kila siku Usiku na Mchana Wapaje Japo Nusu ya Mshahara Wako unaopata na Wanaamini Wangefanya Maajabu duniani, mbaya kwako ni afadhali ya mtu duniani.
Huwezi Jua thamani ya Kitu Mpaka Utakapokuwa umepoteza kile ulichonacho cha sasa. Chukua dakika kadhaa tafakari maisha yako kwa muda, au tafakari mtu unayemfahamu na unatamani kuwa kama yeye, Muulize Kama hana Kitu Cha Kukuambia. Mimi nina amini Its a matter Of time.

Its a Matter Of Time, mwombe Mungu Kisha Komaa na Kile unachokifanya. Kulia haitakusaidia na haijawahi Msaidia Mtu, na hata Ukilia Lia Strategically , Usilie Kihasara, Umewahi Msikia Mtu anayeitwa Batmayo kwenye Biblia Usikie aliliaje alipazaje Sauti. Unakuta mtu ana shida analia mpaka anatia huruma kisha unamuuliza "Nikusaidiaje katika hili" anasema "hata Sijui". Batmayo ye alilia "Mwana Wa Daudi Unirehemu" Yesu akamuuliza 'Unataka Nikufanyie Nini?".."Nataka Kuona" akasema "Ona" Kitu na Box hapo hapo. Usipate tabu sana kujilaumu na kupoteza muda kuwaza namna ulivyojikwa Kimaisha na Kuanguka bali waza namna gani ninasimama na Kuendelea na Maisha. Lililokupata kuna mtu amewahi pata kama hilo pengine kubwa zaidi ya hilo lakini Mungu ni Mwaminifu na Mungu sio Anna Makinda. Every One has a Story.....Its a Matter Of Time.
Everyone has a Story......Its a Matter Of Time.....Think Differently and Make a Difference.
Papaa Ze Blogger.
0713 494110.