Niwape pole Watanzania Kwa Msiba Uliotupata kwa ajili ya Padri aliyepigwa risasi kule Visiwani Zanzibar. Wiki Iliyopita niliandika Papaa On Tuesday nikasema Kama hatuwezi Kuziba Ufa Tutaweza Kujenga Ukuta??leo tunashindwa kuwadhibiti watu wachache wanaofanya fujo kutowesha hii amani je kweli kabisa wakifanya fujo nchi nzima hawa ndugu zetu tutaweza kweli wazuia?
Nakumbuka mwaka 2010 tulishuhudia tukio la Ki-historia kuhusu ndugu zetu wa Chile ambao walikaa ardhini kwa muda mrefu lakini hatimaye walifanikiwa kutoka. Katika story ya Chile nimependa story ya Jamaa aliyekuwa ameziba shimo la panya kwa kipande cha mkate na matokeo yake akaharibu. Katika wale waliokuwa ardhini kuna jamaa alikuwa na mke wake na kumbe jamaa pia alikuwa na nyumba ndogo ambayo alikuwa anaihudumia muda mrefu kwa siri. Siku ya kutoka kwenye shimo wanawake wote wawili wakawa wanamijihamu ya kumuona na kuwa nae teh teh yaani unaokoka na mauti tu unafikia kesi. Kuna siku tu ukweli utajulikana kwenye maisha yetu, tutajua chanzo cha vurugu hizi kweli ni uchinjaji ama kuna mengine, tutajua tu kuwa unamwibia mwajiri wako, tutajua tu wewe sio mwaminifu kwenye ndoa yako watu watajua tu wewe sivyo hivyo unavyoonekana.
Kwenye maisha yangu nimejifunza kufanya kazi na watu wengi sana hasa vijana na wanafunzi wakati mwingine watu wazima kabisa. Kuna wakati watu wazima Mitume na Manabii, Wakurugenzi na Wafanyabiashara tumewahi kukaa na kuongea mambo mbalimbali ya kimaendeleo kwa ajili ya huduma
na Taifa. Kuna wakati Hata wazazi wamekuwa wakiniita na kujadiliana mambo ya kifamilia na wakati mwingine mambo yanayohitaji maamuzi magumu. Katika hayo yote nimejifunza jambo moja kujitahidi sana kutokujikweza ili kuonekana. Kwa taarifa yako sio jambo rahisi maana kama mwanadamu kuna wakati natamani recognition lakini unawezaje kutawala nafsi yako ukizingatia tumeumwa kwa personalities tofauti tofauti, wengine wakiwa mahali utajua tu, wengine wakifanya jambo utajua tu kuwa ni wao.
Juzi Juzi alikuja rafiki yangu kuniomba ushauri juu ya project yake, nilipomsikiliza nikatoa mawazo yangu mengine. Baada ya muda akaanza kufanyia kazi mawazo yangu jamaa akaanza kupiga hatua moja baada ya nyingine huku nina muona. Kuna siku jamaa akawa anongea mahali akijisifia ambavyo amekuja na idea ya namna ile tena hajawahi mshirikisha mtu yeyote katika kuianzisha na mie niko hapo hapo namtazama, nikatamani nisimame nimwambie aseme kweli, lakini nikajiuliza inanisaidia nini nikishasema. Inawezekana tumekuwa na mawazo mazuri ambayo kwa namna moja tuliowashauri wamepiga hatua sisi tuko pale pale na wala jamaa hakuwahi kuja tena kukushukuru, na wakati mwingine tukatamani hata waharibikiwe huko waliko ili wajifunze hii yote ni roho mbaya zetu.
Ukiamua kufanya na kumsaidia mtu tenda wema nenda zako, njia pekee ya wewe kuinuliwa ni kuwa kama mjinga, unapotezea. Nimejifunza kufanya impact kwenye maisha ya watu. Kuna wakati ninafanya kazi za watu bure bila malipo kuna wakati wengine wananidhurumu kuna wakati mwingine nimetowa mawazo kwenye familia na hata kanisani yakabadilika kuwa mawazo ya wote na sio ya kwangu tena yalipotekelezwa yakawa na impact wengine wanakuja wanakupa hongera na kukusifia wewe ni Kichwa unabaki kumshukuru Mungu aliyekupa huo uwezo. Hatuwezi kufanana wote kuna mambo mimi ninaweza kuna mambo siwezi unaweza wewe pale ninapofanya ama wengine wanapofanya tujifunze ku appreciate.
Inawezekana Ofisi yako inatumia mawazo yako kufanya kazi, inawezekana kuna rafiki yako anafanikiwa kupitia mawazo yako, inawezekana kuna mtu ameiba business idea yako na kuifanyia kazi, inawezekana kanisani kwako wanakutegemea sababu ya uwezo ulio nao, inawezekana jamii inakukubali katika yale uliyowahi kuyafanya, haijalishi ulichofanya kimebamba kwa kiasi gani.. A way to Go Up Is to go down…..If You want to go down try to go Up by yourself. Tunakila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kile kidogo ambacho ametuwezesha. Kuna wakati unaenda mahali unasifiwa mpaka unaona aibu. Kuna siku nilikuwa ninaenda kuhudumu kwenye kanisa moja, basi mchungaji alinisifia mpaka nikaona soo, niliposimama ikabidi niweke sawa kuna am very normal person. Hata kama tunaelimu kuliko ndugu zetu, kuliko wale wanaotuzunguka, let us go down to earth. Tufanye pasipo kutafuta kusifiwa ama kukubalika. Tusifanye jambo tukitaka tusifiwe na kutangazwa hadharani, hata kama mchango wako ni mkubwa katika hilo linatokea just humble yourself.
Nimeona watu wengi sana ambao wakifanikiwa wanawadharau wengine wale ambao hawajafanikiwa kuwa si lolote si chochote, unakuta mtu ni mbinafsi anahisi yeye ndo anajua kila kitu ukikaa nae yeye kazi ni kuponda wengine wanachofanya ila cha kwake ndo bora kuliko vya wengine, mtu wa namna hii ana marafiki wachache, na ukiwa na rafiki wa namna hii ujue unapunguza idadi ya marafiki wanaokuzunguka. Kwa hulka kila mwanadamu ameumbwa na ubinafsi, unapo appreciate wengine wanachofanya inafungua milango kwenye maisha yako. Mimi sina rafiki mmoja kwenye maisha yangu nina marafiki wengi sababu ninajua hapa nilipofika ni sababu ya watu. Swali ninalojiuliza unadhani unataka kwenda wapi na akina nani wanaweza kukupeleka unakotaka kwenda.
A way to Go Up is To Go down, think differently and make a difference.
ITAB- I take A Bow
…//Papaa