CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

Papaa On Tuesday...Usione Ukadhani

Ikiwa ni siku ya pili tangu nilipoutangazia umma rasmi kuwa sasa nimeamua kuvunja Ukimya na Kumtangaza Mchumba wangu ninayetarajia kufunga nae ndoa nimekwisha anza ku-experience maisha mengine tofauti ya yale ya kabla ya Jumapili. Ni Kwa neema ya Mungu leo nimefika hapa.

Leo nimejisikia vema tukatazama kile ambacho Diwani ya Mloka tulikisomaga kinaitwa Usione Ukadhani. Watu wengi sana wakiona jambo ama wakimuona mtu wanadhani kwenye Kiingereza wao wanasema "dont judge a book by its cover" ingawa kuna mdhanio mwengine ni wakweli mwingine vema ukasikia ama ukapitia ilikuweza kuwa na majibu sahihi. Mara nyingi sana jamii imekuwa na wepesi wa kufikia hitimisho ya kile ambacho wao wanakidhani ni sahihi kumbe sio. Mara kadhaa kwenye maisha yangu kuna watu waliwahi  nidharau kuwa siwezi kufanya kitu kutokana na muonekano wangu kumbe sio kabisa usione ukadhani.

Kutokana na mfumo wa maisha ya Watanzania na Waafrika kwa ujumla mambo mengi sana tunajifunza ukubwani tukiwa wadogo ni familia chache sana zinatoa mwanya wa mtoto kuji express feelings zake na ndoto zake na tangu utotoni tulifundishwa kuwa mambo mengi ni mabaya pasipo kuambia ubaya wake na tulifundishwa kukosea jambo lolote ni vibaya zaidi ndio maana kuna watu wakifeli mitihani wanaamua kujiua sababu kwenye maisha yake ameambiwa kufeli ama kushindwa jambo ni kitu kibaya. Ukiwa mtoto ukiongea ongea sebuleni na kupiga piga meza ukawa unaimba nyimbo za kitoto utaambiwa kelelee, nyamazaaa basi unakuta unapoteza confidence na saikolojia yako inaambiwa hutakiwi kufanya jambo hili mbele ya wazazi. Ukiwa mtoto ukasema "mama mie mchumba wangu mtoto wa Mzee Charle" usiku huo huo utachapwa fimbo kuwa umeanza kuharibika matokeo yake saikolojia ya ufahamu inaambiwa kuwa kupenda mtu ni vibaya na kwa kuwa umri wa kutoka nyumbani kwa wazazi kwetu sisi ni pale unapoweza kujitegemea unajikuta mambo mengi sana unajifunza sio mbele ya wazazi ama watu waliokulea ndio maana kuna mambo mengi sana wazazi wetu hawajui kama tunajua kwa ufahamu wao wazazi wanadhani watoto wao hawajui kumbe watoto ndio wamegeuka waalimu.
Nakumbuka zamani enzi zetu wakati tunakuwa kabla video hatujaja kuangalia sebuleni baba na mama wanakuwa wanaingalia kwanza kama kuna sehemu sio nzuri basi alikuwa anakaa na remote control ikifika lile eneo anazima anapeleka mbele kidogo kisha tunaendelea. Kwa sisi watoto watundu tangu zamani tulikuwa tunamaswali hivi pale anapopeleka mbele kuna nini?basi wengine walienda extra mile tukavizia wakati baba na mama hawapo tukawasha tukaangalia mwanzo mwisho ila baba na mama wakirudi wanajua hatujui kuna nini. Tofauti na Kizazi cha sasa ambacho wao hutazama kanza kupitia mitandao kisha kama watatazama na familia watoto ndo wanawaambia wazazi sasa "baba hapo forward kidogo sio pazuri" sasa najiuliza mtoto ndo anamwambia baba aforward kwa manufaa ya nani baba ama yeye mtoto??Usione Ukadhani watu kizazi hiki hawajuio kwa taarifa yako watu huwa wanaambiana.

Usione leo mtu hana chochote ukadhani ataendelea kuwa kama alivyo, watu huwa wanabadilika kwenye maisha priorities nyingi sana za wanaume huwa zinabadilika pia kutokana na umri aliokuwa nao, majukumu aliyokuwa nayo na Marital Status yake pia. Kabla ya kuwa na mpango wa kuoa kwenye maisha atakuwa anawaza kula bata atakuwa anawaza kukutana na Jack, Rose, Mwamntumu, kwenda movie, kwenda mlimani City, akishaanza kuwa na mahusiano majukumu yanabadilika harusi ikikaribia kama mimi utakuwa unawaza Shella la Bibi harusi, Kiatu Cha Bibi harusi, Suti ya Bwa. Harusi Ukumbi, Mc pole pole akili inaanza kuwaza majukumu. Ukishapata familia sasa na mtoto utaanza kuwaza Pumpus za mtoto, mara bima ya afya ya Mtoto, ada ya shule, Mke nae avae,afanya kazi, mtaanza kufikiri Miradi ya kifamilia,mtawaza kujenga usione leo mtu yupo yupo ukadhani ataendelea kubaki alivyo. Akili hukuwa kwa kuzoeshwa ingawa inawezekana sio wote lakini Kibongo bongo tunakuwa kwa kukosea sana ukubwani hata namna ya kuishi na mume na mke tangu utotoni akili imejizoeza kujificha ficha hata kama ni halali.
Jambo usililolijua ni kama usiku wa giza unaweza ukaona leo mtu amekuwa na mafanikio ukadhani yalikuja kirahisi rahisi kwenye maisha. Kuna watu ukisikiliza hatua zao za maisha unajiona kabisa wewe unadeka unataka mafanikio wakati hata kushinda njaa mchana tu huwezi kuna watu mpaka leo wametoboa kwenye maisha wanahistoria ambazo ukizisikiliza kuna nyakati waliomba usiku usiingie sababu hawana sehemu za kulala walitamani kama kuna mahali wanaweza uza njaa basi wangeuza kwa bei yoyote ili wasiwenazo milele kuna watu walishinda njaa si kwa sababu walitamani kufunga la hasha hakuna chakula usione ukadhani kila kitu kinakuja bure. Tamaa mbaya ya mafanikio ya haraka haraka ndio inayopeleka mtoto wa masikini akiwa form four anawaza kuwa na blackberry yuko tayari kufanyiwa chochote apate blackberry used. Usione Mtu ukadhani kila mtu anaendesha gari leo amenunua kihalali wengine wamenunua ka kudhalilisha maisha yao ili waonekane. Usione leo watu wameajiriwa kwenye makampuni makubwa ukajua wameshinda interview za kazi walishinda interview za ngono ndio wakapataKama kuna kitu Watanzania kinatutesa ni Ulimbukeni. Usine Ukadhani.

Usione wanandoa wanaongoza kuingia kwenye ukumbi wa harusi wako pamoja wamevaa vizuri ukadhani hilo tabasamu ndilo walilokuwa nalo wakiwa nyumbani. Ungepata fursa ya kujua undani wao ndipo ambavyo ungefuta dhana yako ya kuolewa ili na wewe tu uwe na mume sababu uliosoma nao wameolewa, uliocheza nao wanawatoto, ungefuta dhana ya kuoa sababu mke wako ana umbile la namba 8, mke wako aonekane ana makalio, ama mweupe au mweusi kwani unaolea jamii ama unaoa kwa utashi wako mwenyewe wengi waliokimbilia ndoa kwa sababu za kijamii wamejikuta wamekwama na kama ingekuwa dini yetu ya Kikristo inaruhusu talaka wengi wangechukua talaka pamoja na kuto kuruhusu watu wanatoka wamechokaaaa. Rafiki yangu mmoja alinichekesha akasema kuna wengine wamefika stage wanaombea basi hata wafe ili wapumue maana hawa wanandoa wakiwa mbele za watu full matabasamu full kushikana mikono lakini wakiingia tu kwenye gari kurudi nyumbani maisha ya Chui na Paka yanarudi kuna wanawake leo wanatamani  wangeolewa na wanaume masikini wachume pamoja kuliko waliowachagua wanaume wenye uwezo wamejikuta wanaambulia majuto kuliko furaha usine ukadhani.

Usione watu wanavaa tai na sketi nzuri wanafanyakazi kwenye maofisi ukadhani wanafuraha na kazi zao, shida ndio zinasababisha waendelee kwenda ofisini wengine hawana hata mishahara wana mikopo kupita Serikali ya Tanzania, kuna watu wanaenda maofisini hawana hata mikataba ya ajira zao yaani hawana hatma ya kesho yao itakuaje kiajira, we usione watu wanavyojiupara na kula chips kuku ukadhani mambo yao safi, simu zao nzuri hazina vocha, mabegi yamejaa vipodozi vinavyokaribia kwisha, nguo wamekopa pale kwa mdada anayepitisha ofisini kwao kwa muonekano wa njee utadhani wanaraha kuliko wewe, ukitaka kujua uhondo wa ngoma uingie ucheze usione ukadhani ndugu yangu.

Maisha kila siku ni kujipanga unaweza ukadharaulika leo ukajipanga ukashangaa wale aliokuwa wanakucheka ndio baadae wanakupongeza watu huwa wanakawaida ya kudharau watu usitegemee kupendwa kabla ya kudharauliwa kwanza. Mtu mmoja anayekutia moyo wakati wa shida ni muhimu zaidi kuliko jeshi linalokushangilia baada ya ushindi. Usione ukadhani wewe jipange ili kuweza kusonga mbele. 

Think Differently and Make A difference.

Usione Ukadhani.

Samuel Sasali
0713 494110
Facebook: Samuel Sasali
Skype: SasaliJr