UKO HAPA DVD LIVE RECORDING
NA JOHN LISSU,
06/10/2013,CCC-UPANGA, DAR ES SALAAM, TANZANIA.
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI NA WATANZANIA WOTE;
SALAM Tanzania!
Shalom Dar es salaam, Shalom Tanzania!
Ndugu wanahabari na watanzania wote kwa ujumla!
Naamini tuko salama na tunaendelea na shughuli zetu za kila
siku alizotupatia Mungu wa mbinguni, tumshukuru Mungu sana kwa Amani na utulivu
aliotupa na tuendelee kumuomba ili atuepushe na kila aina ya dhahama na
uharibifu wa Yule adui!
Kama tulivyosikia hivi karibuni, yale yaliyotokea nchi jirani
ya Kenya, kwa hakika tunawapa pole sana kwa mkasa huo, pole kwa wale
waliowapoteza wapendwa wao na wale waliojeruhika tunawaombea wapone haraka,
tunaamini hekima ya Mungu itakuwa juu ya serikali yao kushughulikia jambo hilo
kikamilifu.
Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai, hata sasa tunapoende
kumalizia robo ya tatu ya mwaka 2013, tumeshuhudia mambo mengi sana mwaka huu
ya kila aina, yapo yale yalionza kwa mara ya kwanza na mengine yamekuwa ni
mwendelezo tu wa yale yadumuyo au yalioyaanza hapo kale, tumeshuhudia michezo
mbalimbali na vipaji lukuki vikiinuka na kuimarika katika maeneo mbalimbali ya
nchi yetu, na kwa yote mema na mazuri tunampa Mungu Utukufu kwa hakika!
UTANGULIZI;
John Lisu
ni mmoja wa waimbaji/Waabudishaji wanaoheshimika katika Tasnia ya muziki wa
Injili kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa katika kukuza na kuendeleza
muziki wa Injili nchini Tanzania na nje ya Nchi. Nyimbo nyingi alizozitunga na
kuziimba zimekuwa zikitumika katika makanisa mbalimbali kama nyimbo za kusifu
na kuabudu; pia waimbaji wengine waliokua wakiimba naye wameweza kukua na
kufikia uwezo wa kuwa waimbaji wa kujitegemea. John Lisu pia ametia hamasa
kubwa miongoni wa wanamuziki wa Injili kuanza kufanya muziki wa live. John Lisu
ameweza kufanya tours za ndani ya Tanzania, Africa na Bara la Ulaya kwa ajili
ya huduma.
John Lisu anategemea kufanya Project II ya
Live recoding inayojulikana kama "UKO HAPA" baada ya project ya
kwanza ya Jehova yu hai kufanya vizuri sana. Tamasha litafanyika ndani ya
ukumbi wa City Christian Centre (CCC) Upanga tarehe 6 Octoba 2013, kuanzia saa
8. mpaka saa 2 usiku. Tamasha litasindikizwa na waimbaji nguli kama Christina
Shusho, Neema Gospel Choir, Paul Clement, Pastor Safari Paul, Bomby Johnson
Waimbaji wote wamethibitisha kuwepo.
VENUE:
City
Christian Centre (CCC) mkabala na chuo kikuu cha mzumbe
Si
mbali saana kutoka Diamond Jubilee
USAFIRI
(basi zilizobandikwa matangazo ya tamasha) utakuwepo kutoka posta mpya kwenda
ukumbini kuanzia saa saba na nusu mchana kwa bei ya kawaida.
HABARI NJEMA-MUHTSARI!!!!!
Sasa kwa mara pili nchini Tanzania, mwimbaji WA NYIMBO ZA
INJILI na mwabuduji JOHN LISSU wa jijini Dar Es Salaam, atakuwa anafanya Ibaada
kubwa ama Tamasha la kusifu la Kuabudu(LIVE PERFORMANCE), litakalorekodiwa moja
kwa moja (DVD LIVE RECORDING) lenye jina “UKO HAPA” (Yaani Mungu na Uwepo
wake).
Tamasha hilo litafanyika jumapili ya Tarehe 6, Octoba
2013 katika Ukumbi mkubwa wa kisasa wa
Kanisa la City Christian Centre (CCC)- Upanga, mkabala na Chuo Kikuu Mzumbe –
tawi la Dar es salaam, kuanzia saa nane mchana.
Tunataraji watu 5000
kuwa sehemu ya tamasha hili la kipekee,Utakuwa sehemu ya tamasha hilo kwa
tiketi ya 10,000/= (kawaida), 20,000/= (VIP) na 3000/= (Watoto);
na Kwale
watakaohitaji tisheti maalum za tukio hilo, basi zinapatikana kwa kati ya
12,000-15,000/=, wewe wasiliana tu na (0713905118)
VITUO VYA
KUUZIA TIKETI;
1.
MWENGE
– Tarakea duka la Kanda
2.
KINONDONI
– DPC
3.
MLIMANICITY
– Silverspoon Restaurant
4.
KARIAKOO
– Mbogo Shop
5.
UKONGA
BANANA – KWA GIDO
6.
POSTA
- DUKA LA MSAMA
-T-shirts maalumu kwa wanaume na wanawake
zinapatikana katika vituo vya kuuzia tiketi kwa bei ya elfu kumi, mpaka elfu
15(kutegmeana na aina).
N.B; Kwa
tiketi ya VIP, mnunuzi atajipatia na Audio CD ya John Lissu ya “Uko Hapa”
USAFIRI
UTAKUWEPO!!
Siku ya
tamasha kutakuwepo usafiri kutoka Posta Mpya mpaka CCC-Upanga,eneo la tukio,
hivyo kama wewe ni mgeni na hupafahamu mahali hapo, basi utakachotakiwa kufanya
ni kupanda magari toka ulipo mpaka posta mpya kabla ya saa nane,na hapo
utayakuta mabasi yenye mabango ya Tamasha, basi utajongea humo na hapo
utawezeshwa kufika eneo la tukio, muhimu ni kuzingatia muda!
MUHIMU SANA!!
Tamasha
hili ni muhimu sana kwa Tanzania, hasa ukizingatia JOHN LISSU ni mmoja wa
waimbaji wa kwanza kuimba live kila mahali anapoalikwa na ni mwimbaji wa kwanza
binafsi kufanya LIVE DVD RECORDING pale Ubungo plaza, na ile ya kwanza iliitwa
“JEHOVA YU HAI” na sasa anafanya LIVE RECORDING kwa viwango vingine bora zaidi,
maana Mungu hutupa hatua moja zaidi kila siku.
Ni muhimu kwa kila mtanzania kujivunia kipaji na tukio hili
muhimu katika historia, njoo umwabudu na kumsifu Mungu pamoja, Njoo ujifunze,
Njoo umuunge mkono mtanzania mwenzako na njoo uje ufanyike sehemu ya Historia
hii kwa Utukufu wa Jehova.
MWALIKO
MAALUM;
Kipekee Ninapenda kuwakaribisha wachungaji, mitume, manabii,
wainjilisti, waalimu na viongozi wote wa makanisa na huduma mbalimbali,
ninawakaribisha viongozi wote wa kisiasa na kijamii kutoka serikalini na vyama
vya siasa vyote, ninapenda kuwakaribisha wanaharakati na wanataaluma wote,
ninapenda kuwakaribisha waimbaji wote wa nyimbo za injili na wanasanaa wote,
ninapenda kuwakaribisa wanafamilia wote, asiwepo wa kubaki nyuma, ninapenda
sasa kukukaribisha wewe unaesoma hapa, naam nisaidie kumkaribisha na mwenzako
na yeye aje na mwenzake, kimsingi tukio hili ni letu wote bila kujali kitu
chochote, njooni tumsifu na kumwabudu Bwana na Mungu hataacha kuibariki
Tanzania!
SHUKRANI;
Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Hakneel Production
(Wadhamini wakuu), na Jonn Lissu na timu nzima ya maandalizi; Kanisa la
CCC-Upanga; vyombo vya habari hususani Praise Power na WAPO Radio; Clouds TV
kupitia CHOMOZA na Clouds Radio kupitia GT; Sibuka Tv kupita Gospel Hits;
Bloggers hususani Christian Bloggers, magazeti na vyombo vingine vyote vya
habari! Shukrani hizi zimfikie kila mtu mmoja mmoja aliyetoa mchango wa mawazo,
fedha, ushauri, maombi, ubunifu, yaani mchango wowote wa hali na mali na Mungu
awabariki nyote!
MUHTASARI MKUU;
Tukio; TAMASHA
LA KUSIFU NA KUABUDU, LITAKALOREKODIWA
(DVD LIVE RECORDING CONCERT)
Mhusika; JOHN LISSU
Jina: “UKO HAPA”
Mahali; UKUMBI WA KANISA LA CITY CHRISTIAN CENTRE
(CCC)- UPANGA
Lini; 06TH OCTOBA, 2013
Muda; KUANZIA SAA NANE
MCHANA
Kiingilio; Tsh 10,000/= (kawaida); 20,000/= (VIP) na
5000/= (Watoto)
Wasindikizaji;
CHRISTINA SHUSHO, MIRIUM LUKINDO, PASTOR SAFARI, BOMBY JOHNSON, NEEMA GOSPEL
CHOIR-AIC Chang’ombe na PAUL CLEMENT.
Mengineyo; USAFIRI UTAKUWEPO TOKA POSTA MPAKA
CCC-UPANGA na Unaweza kujipatia Tisheti pia.
Wahusika; WATU WOTE MNAKARIBISHWA!
UKIPATA
HABARI HII USIACHE KUMSHIRIKISHA NA MWENZAKO, NAAMINI HAUTAKOSA TUKIO HILI
MUHIMU LA KIHISTORIA KATIKA NCHI YA TANZANIA KWA UTUKUFU WA MUNGU!!
PICHA
NA TAARIFA
MAWASILIANO:
O713 240 397 – JOHN
LISU
0713 905 118 –PROSPER MWAKITALIMA
– EVENT MANAGER
0713 883 797 - FREDY
CHAVALA - PUBLICITY
Imetolewa na;
Fredy E. Chavala <King Chavala (MC)>
Publicity Manager
+255 713 883 797
On Behalf of The Organizing Committee