HELLO HABARI!
NAAMINI MKO POA NA MNAENDELEA VIZURI, NILIKUWA KIMYA KWA
MUDA NA HII NI KWASABABU ZOOMING ZONE SIO MAKALA YA KILA SIKU AMA KILA MTU,
HIVYO LEO LENZI IMEMULIKA KIJANA MMOJA HAPA MJINI NA HUYU NDIO ATAKUWA……Zooming
Zone 004
Zooming Zone 0004....Na Prosper A.Mwakitalima |
Huyu sio mwingine basi ni kijana mjasiriamali “SWAHIBA”
anayetamba na kujulikana sana kwa KUCHAPISHA T-SHRTS vizuri, nzuri na zenye
maneno mazuri hapa Mjini, Tanzania.
Naam pia ndio huyu ambaye habari zake zilivuma sana hapa
mjini kwa kupona“kufufuka” toka katika ajali mbaya sana sana pale maeneo ya
River side Ubungo 23/11/2011 iliyohusisha
lori la mafuta na gari yake ndogo,ajali ambayo ilichukua maisha ya watu kadhaa
akiwemo mama mmoja mjamzito ambaye alikatika kichwa(ilitisha sana kwa kweli)….lakini
Jambo la kushangaza ni kuwa kijana huyu alipona kabisa maana hakuvunjika mfupa
wala mshipa Zaidi ya michubuko kadhaa tu,hakuna aliyeamini hata leo lakini huo
ndio ukweli!
Huwezi kuamini lakini huu ndio ukweli! |
Huyu pia ni mmoja wa washika dau na wawezeshaji wa Mtoko wa
marafiki Mjini uitwao “FRIENDS ON FRIDAY
(FoF)”, na ndio mbeba maono na mkurugenzi wa “SIFA TANZANIA”Mfululizo wa matamasha ya kumwinua Yesu hapa nchini
Tanzania.
Huyu ni PROSPER
ALFRED MWAKITALIMA a.k.a SWAHIBA a.k.a “The Next Billionaire” (King
Chavala tu anaruhusiwa kumwita “MY PS”)
NILIBAHATIKA
KUFANYA NAE MAHOJIANO HIVI KARIBUNI KWA KINA NA NIKAPATA MENGI SANA NA HAYA NI
MACHACHE KATIKA MENGI, AMBAYO NAAMINI YANAWEZA KUKUSAIDIA KUMFAHAMU VIZURI NA
YAMKINI KUJIFUNZA MENGI KUTOKA KWAKE, HUYU NI KIJANA WA KIPEKEE AMBAYE NI MFANO
WA KUIGWA NA VIJANA WA KITANZANIA…..FUATANA NAMI KATIKA MAELEZO YANGU KUHUSU
YEYE NA UKIRI WAKE MWENYEWE NA PICHA MBALIMBALI AMBAZO ZINAONYESHA HISTORIA
YAKE HATA SASA!!!
HISTORIA;
Lazima yeye afanye tofauti tu! |
Prosper A.
Mwakitalima ni mtoto wa mwisho wa Mchungaji Alfred Mwakitalima, mnyakusa
alijichimbia na kujenga maisha yake huko Singida-Tanzania…Na huyu kijana mesema
yeye ni MNYATURU ingawa baba yake ni Mnyakusa,
na nilishangaa kwanini iwe hivyo
lakini akaniambia KABILA HUWA HALIRITHIWI (TRIBE IS ACQUIRED)….Prosper alisema
hawezi kuwa mnyakusa hali amezaliwa na kukulia Singida kabla ya kuja Dar es
salaam.
Tangu kale hata sasa Prosper ni mchangamfu.... |
Prosper
alisoma shule msingi iitwayo MGHANGA
PRIMARY SCHOOL na kasha kujiunga MWENGE
SECONDARY SCHOOL zote za mkoani
Singida,
Prosper akipokea Cheti |
kabla ya kwenda High School katika sekondari ya MILAMBO iliyo Mkoani
TABORA ambapo alisoma masomo ya Lugha. Akiwa hapo alisoma na watu wengi sana na
wachache kati ya hao ambao ni wa muhimu sana hapa nchini ni hawa Mchungaji Mathew
Sasali, Mkurugenzi wa Radio Ushindi yenye makao yake makuu jijini Mbeya pamoja
na Mwanaharakati Mussa Bilageya.
Prosper akipokea Cheti wakati wa mahafali |
Wengi hawaamini kuwa huyu kijana anaweza yote haya |
**********************************************************************
vipaji ndio viko lukuki kwa kijana huyu,ona alivyokuwa hapo kale....
Kipaji cha Ubotozi alikuwa nacho..... |
Uigizaji hakukosekana...... |
Kuimba ndio usisema hata sasa....... |
#Na hili ni jambo
ambalo Prosper alikiri kuwa yeye hakusoma chochote High school kama wengine
bali alisoma lugha tu, ambayo hakuendelea nayo huko chuoni ili kuwa mwalimu au
mtaalamu wa lugha#
HATIMAYE SAFARI YA KUJA
JIJINI DAR IKAANZA…..
Na hivi ndivyo alivyokaribishwa Jijini |
Na huo ndio
muujiza wa kuja mjini na hata sasa haujabadilika maana makazi yamebaki kuwa
jijini Dar….ndio alibahatika kujiunga na Chuo Kikuu Cha Dar es salaam na hapo
alisoma Shahada ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa jamii (Bachelor of Arts in
Political Science and Public Administration)
Mabibo Christian Fellowship ikiwa changa |
Alipokuwa
Chuo alikuwa mfano wa pekee wa kuigwa na Alikuwa anakaa Mabibo Hostel na hapo
aliimarisha mfumo rasmi wa Mabibo Christian Fellowship ambayo hata sasa
wanaifurahia wengi, yeye pamoja na wenzake wanahesabika kama waasisi wa MCF nay
eye huitwa Babu wa Fellowship hiyo.
Hatimaye akahitimu Chuo Kikuu |
Ni kweli
alimaliza hapo lakini jambo la kipekee ni kuwa hajawahi kurudi tena baada ya
kumaliza chuo hata leo na anachokifanya sasa hivi mtaani hakiendani hata kidogo
na kile alichosomea.
KAZI
Mungu
alikuwa mwaminifu sana kwake naye akabahatika kupata kazi nzuri sana, akafanya
kazi kama COORDINATOR wa Japan Engineering Consultancy (JEC), kampuni iliyokuwa
ikifanya kazi ya ushauri wa kiinjinia kwa mradi ulikuwa unafanywa na Japana
International Cooperation Agency (JICA) kwa ushirikiano na Wizara ya Miundo
Mbinu wakati huo, kazi ambayo aliifanya kwa miezi 27 na kuenjoy maisha kwa
kina……LAKINI JAMBO LA KUSHANGAZA AMBALO ALINIAMBIA PROSPER NI KUWA; ALIPATA
KAZI NZURI SANA YA KUMWINGIZIA MAMILIONI AKIWA HANA AKILI KABISA, MAANA
HAKUWAHI KUFANYA JAMBO LOLOTE LA MAANA KATIKA KUJENGA KESHO YAKE ZAIDI YA KULA
BATA MJINI, NAAM ILISHAPITA, HAJUTII SANA MAANA BAADA YA KUPATA AKILI SASA NDIO
AKAANZA KUJIAJIRI HATA LEO.
Prosper
Mwakitalima ni kijana mpambanaji mwenye ndoto za kuwa Billionea na katika
harakati zake mnamo Sept 2008 yeye na baadhi ya marafiki zake wakafungua
kampuni ya Printing iitwayo MANCON (E) Ltd na hapo wakaja na Product iitwayo
“Gospel Today”….Hii ilikuwa ni Free Advertising Magazine yenye mlengo wa
Kikristo na ilikuwa inatolewa kila mwezi na kwa bahati ya ujasiriamali ilidumu
kwa miezi mitatu tu.
Prosper
anasema…..Ingawa ile magazine ilitoka mara tatu tu, na tuliumia kushindwa
kuendelea lakini ndio ulikuwa mlango na msingi mkubwa sana wa kazi nyingi sana
za printing zilizokuja hata leo, maana watu walipenda sana Ubora na Ubunifu.
Pamoja na
kuyumbayumba kwa hapa na pale kwa biashara change, sasa kampuni imesimama na
wanaendelea na uchapaji wa aina zote….Kuanzia T-shrts, business cards,wheel
cover mpaka Advertising boards….wenyewe wana msemo wao; MANCON (E) LTD….MAKES YOU SAY
“WOW”
March 2009
alifungua kampuni nyingine ya IT iitwayo “THE BRIDGE” Inayo operate hata leo.
Kijana huyu amefanikiwa Kujitengenezea AJIRA yake na
kuwaajiri wengine sita(6) na mbali na hao kuna wengine wengi waliosaidiwa sana
kwa kujengewa uwezo na hawa ni kama kumi vile, mbali na wale wanasaidiwa kila
siku kwa ushauri na mikopo.
KILA MTU
MWENYE NDOTO HUWA ANAKUWA NA MFANO, MWONGOZO AU WATU AMBAO KWAO ANAJIFUNZA NA
KUTIWA MOYO ZAIDI ILIMASONGE MBELE SANA, BASI NILIPOMUULIZA PROSPER YEYE
ANAVUTIWA NA NANI ZAIDI(ROLL MODEL IN ONE WAY OR ANOTHER)
Prosper Mwakitalima akiwa na Paul Mashauri na rafiki yake |
Naye akasema
amesoma Vitabu kadhaa na kuwa inspired
na Robert Kyosaki sana and among the books, here are “7 Strategies for Wealth
and Happiness”; “Who Moved My Cheese” and “The richest man in Babylon”…..na kwa
hapa Tanzania amekuwa anamfuatilia na kumfurahia sana kijana mmoja anaitwa PAUL MASHAURI, Mwenyekiti wa East
Africa Speaking Bureau…..prosper anasema “Anamfahamu sana toka zamani akiwa
chuo na anamfurahia akiwa anakua kimaendeleo kila leo, na hata lile wazo la
kuanzisha “Gospel Today” nilijifunza toka kwake.
NI IPI MISINGI YA NDOTO ZAKO?
Prosper
alisema anaendeshwa na ndoto hii;
“…..I WANT TO MAKE JESUS FAMOUS!”,By raising people with God’s
character “Christian Celebrities”, that is why I have invested in Media, I
started in printing and now I am now going to Radio and TV.
Sifa Tanzania |
CHANGAMOTO
AMBAYO AMEISEMA ni kuwa “single”, anasema ukiwa Single unakuwa
unbalanced!....japo amepitia changamoto kadhaa katika mahusiano(Rasmi kama tatu
hivi) anasema akioa Mtakamatia mbali.
NILIMUULIZA PROSPER NI NINI MTU
ATARAJIE KWAKE AKIHITAJI MSAADA?
Naye akasema
Akija Mtu mwenye Ndoto/ Maono anaweza kupata mambo mawili matatu na PIA
asiyejitambua anaweza kumsaidia Akajitambua.
NILIMUULIZA PROSPER, NI NANI
UNATAMANI KUMPA SHUKRANI KWA SASA AMA KUUTAMBUA MCHANGO WAKE KWAKO MPAKA HAPA
ULIPO?
Prosper
alisema Anamshukuru Kila mtu aliyemsaidia kwa namna moja ama nyingine mpaka
kufika hapo alipofika, lakini aliwataja hawa wachache kipekee na kusema hawa
haachi kuwashukuru san asana kwa jinsi walivyo muhimu sana kwake( sio kwamba
wengine sio muhimu bali hawa wana kibali cha pekee)
Alfred Mwakitalima na Nathanael Sasali(Wachungaji) |
Kwanza
anawashukuru sana Wazazi wake; Mama yake ndio mjenzi mkubwa wa maisha yake ya
kiroho, maana yuko deep katika neno la Mungu na ni mwombaji sana; na Baba
amemfundisha kuwa na utegemezi kamili juu ya Mungu na kuishi kwa imani, maana anasema
hajawahi kumwona baba yake akiwa na hofu hata kuwa na nini.
Lakini pia
alisema anawashukuru sana marafiki zake kama Andrew Mzava, Papaa, Mussa
Bilageya, Jacob Mtalitinya na wengineo, lakini pia Anamshukuru sana Dk.Rev
Huruma Nkone mchungaji wa Victory Christian Centre Tabernacle (VCCT) maana
ALIMWAMINI SANA TANGU ZAMANI, na Imani ya mchungaji huyo ndio ilifanya hata
watu wengine wengi wamuamini.
NA KWA SASA
MARAFIKI ANAOTAMANI KUWASHUKURU NI HAWA;
(Na haya ni
maneno yake mwenyewe)
Ninawakubali
sana na kuwashukuru marafiki hawa kwasababu zifuatazo;
1.SAMUEL SASALI a.k.a Papaa
Prosper na Papaa |
…..Ni rafiki
mzuri sana tangu zamani na kinachonifurahisha kwake ni kuwa Ni mtu ambaye ni
VERY APPRECIATIVE!!!...Yaani hata kama wengine hawaoni wala kukubali
unachokifanya,lakini huyu amekuwa mtu wa kunitia moyo na kunikubali sana, nah
ii inanitia moyo kusonga mbele kila siku.
2. KING CHAVALA (MC/COMEDIAN)
Prosper na King Chavala |
….na huyu amekuwa rafiki ambaye
ananikubali na kuniamini sana, na nampenda kwasababu ya Ushauri na ni mtu
anaeona mbali na anajitambua……Thank you man for being appreciative hahahaha!
(Haya hakusema kwasababu nilikuwepo, lakini naamini anamaanisha toka moyoni)
(Haya hakusema kwasababu nilikuwepo, lakini naamini anamaanisha toka moyoni)
3. AMANI PAUL
Amani Paul |
… na huyu amekuwa karibu sana na mimi
kwa ushauri na kunitia moyo sana, na kwasababu naye ni mpambanaji basi tumekuwa
naye karibu sana wakati tunaanza kujisimsmia kibiashara na hata sasa baada ya
kupiga hatua bado ananichangamotisha.
PROSPER
ANAWASHUKURU SANA MARAFIKI HAWA PAMOJA NA WALE AMBAO HAWAJATAJWA HAPA NA KWA
NDUGU MSOMAJI NATAMANI UJIFUNZE JAMBO HAPA, HATA KAMA WEWE MWENYEWE HUJAFIKA
MBALI SANA LAZIMA UJIFUNZE KUWAKUBALI WENGINE “APPRECIATE NEVER HATES”
PROSPER NI
KIJANA AMBAYE ANAMPENDA SANA MUNGU NA ANAAMINI KAMWE HAWEZI KUFANIKIWA NJE YA
MUNGU, NINAJUA KUNA VIJANA WENGI AMBAO WANAFIKIRI ELIMU, KAZI NA BIASHARA NDIO
VINAWEZA KUWATOA NA WAKASAHAU MUNGU, AMBAYE NDIO KILA KITU KATIKA YOTE.
NA HAYA
NDIYO YALIKUWA MANENO YAKE YA MWISHO KWA KILA MSOMAJI;
“Ishi kwa kujiamini,
relax, Acha woga, Life is Adventure, Acha kuishi kwa kuwazia kula na kulala tu,
lazima uwe na ndoto ambazo hata wewe zinakutishia….Think things that challenges
You!”
AHSANTENI
SANA KWA KUSOMA NA KUMFAHAMU VIZURI PROSPER MWAKITALIMA, NAAMINI UTAKUWA
UMEJIFUNZA VYA KUTOSHA NA IWE NI CHANGAMOTO KWAKO KUJENGA MSINGI BORA WA MAISHA
YAKO KAMA KIJANA!
Imeandaliwa na
King Chavala
+255 713 883 797
E-mail; lacs.project@gmail.com
©Zooming Zone’2013