CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441
Showing posts with label zooming. Show all posts
Showing posts with label zooming. Show all posts

ZOOMING ZONE 0004.......Na PROSPER A. MWAKITALIMA, The T-shirt Printer tycoon!!!



HELLO HABARI!
NAAMINI MKO POA NA MNAENDELEA VIZURI, NILIKUWA KIMYA KWA MUDA NA HII NI KWASABABU ZOOMING ZONE SIO MAKALA YA KILA SIKU AMA KILA MTU, HIVYO LEO LENZI IMEMULIKA KIJANA MMOJA HAPA MJINI NA HUYU NDIO ATAKUWA……Zooming Zone 004
************************************************************************************               
Zooming Zone 0004....Na Prosper A.Mwakitalima
Huyu sio mwingine basi ni kijana mjasiriamali “SWAHIBA” anayetamba na kujulikana sana kwa KUCHAPISHA T-SHRTS vizuri, nzuri na zenye maneno mazuri hapa Mjini, Tanzania.
Naam pia ndio huyu ambaye habari zake zilivuma sana hapa mjini kwa kupona“kufufuka” toka katika ajali mbaya sana sana pale maeneo ya River side Ubungo  23/11/2011 iliyohusisha lori la mafuta na gari yake ndogo,ajali ambayo ilichukua maisha ya watu kadhaa akiwemo mama mmoja mjamzito ambaye alikatika kichwa(ilitisha sana kwa kweli)….lakini Jambo la kushangaza ni kuwa kijana huyu alipona kabisa maana hakuvunjika mfupa wala mshipa Zaidi ya michubuko kadhaa tu,hakuna aliyeamini hata leo lakini huo ndio ukweli!
Huwezi kuamini lakini huu ndio ukweli!

Huyu pia ni mmoja wa washika dau na wawezeshaji wa Mtoko wa marafiki Mjini uitwao “FRIENDS ON FRIDAY (FoF)”, na ndio mbeba maono na mkurugenzi wa “SIFA TANZANIA”Mfululizo wa matamasha ya kumwinua Yesu hapa nchini Tanzania.
Huyu ni PROSPER ALFRED MWAKITALIMA a.k.a SWAHIBA a.k.a “The Next Billionaire” (King Chavala tu anaruhusiwa kumwita “MY PS”)
 
Prosper,Wambura na Chavala Singida
NILIBAHATIKA KUFANYA NAE MAHOJIANO HIVI KARIBUNI KWA KINA NA NIKAPATA MENGI SANA NA HAYA NI MACHACHE KATIKA MENGI, AMBAYO NAAMINI YANAWEZA KUKUSAIDIA KUMFAHAMU VIZURI NA YAMKINI KUJIFUNZA MENGI KUTOKA KWAKE, HUYU NI KIJANA WA KIPEKEE AMBAYE NI MFANO WA KUIGWA NA VIJANA WA KITANZANIA…..FUATANA NAMI KATIKA MAELEZO YANGU KUHUSU 

ZOOMING ZONE 0003....Na DEO MECK, The Politician!!!

  Leo katika kipengele hiki naomba nimzoom kwa karibu zaidi  kijana mmoja aitwaye Deo Meck, Mwana Technohama mwenye wito wa Siasa!!!
(Deo Meck)

Leo katika lezi yangu naomba nimzoom kijana mmoja ambaye jina lake limevuma sana ingawa wengi hawamjui kwa sura!!

Huyu kaka ni kijana wa pekee mchakarikaji, ambaye hufanya mambo yake mengi kwa principles(hata kama nyingine zinamfaa peke yake),
 Ni kijana wa Kikurya aliyekulia Tarime na kusoma shule ya msingi Nyamisangura iliyoko tarime na hatimaye Shule ya Ufundi Musoma kabla ya kuja Dar es salaam(Benjamin High school) na hatimaye kwenda Kampala University,Uganda ambako amesomea Shahada ya Sayansi ya kompyuta na Teknolojia ya habari, 
huko aliwahi kuwa waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi ingawa alikuwa ugenini na alianzisha project ya kuuenzi utamaduni wa mwafrica ambayo hata sasa inaendelea, aliporejea tu nchini cha kwanza alijitosa kugombea ubunge kupitia CHADEMA kule Tarime baada ya kifo cha Chacha Wange lakini baadae akaridhia kumuachia na kumsaidia Mwera hata akashinda, na hata akapata bahati ya kuwa msaidizi wa mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho..
ana malengo ya mbali sana na naamini siku moja atakuwa kiongozi wetu...
.ameshafanya kazi na Vodacom,
Platinum na sasa anaendesha kampuni yake iitwayo OLYMPUS COMPUTERS,
<www.olympus-computers.com>
Ana uzalendo wa kweli, Anapenda maadili, thinker,Polite na anampenda Mungu kweli!!
(Deo Meck na Prosper Mwakitalima-Arusha)

N.B; Ameandika kitabu kiitwacho CHACHA ZAKAYO WANGWE!!!
(akijaribu kuelezea maisha ya mpambananaji huyo ambaye kifo chake kilighubikwa na utata na hata leo watu wana hasira nafsini mwao)
(Deo Meck akiwa na Jack, Aron, Belinda, Doreen na Richard Chidundo baada ya LACS VI)
Nimebahatika kufanya nae kazi kadhaa, na huyu ndio alikuwa mbele sana kunitia moyo wakati naanzisha project ya LAUGH AGAIN CONCERT SERIES(LACS), tamasha la kwanza kabisa, na zaidi alikuwa Event manager wa Episode IV na alikuwa mzungumzaji(Speaker) katika event ambayo niliandaa Arusha ambayo iliitwa "WHAT NEXT AFTER COLLEGE?"
THIS BROTHER TALK SENSE NA KWA WALE WALIOWAHI KUMSIKIA WATAKUBALIANA NAMI KUWA HUYU NI KIJANA WA KUIGWA, WE REAL NEED THIS BROTHER KWA MUSTAKABALI WA NCHI HII

From my heart i love this brother and real admire Him, we are friends and dare not to touch us kwa ubaya for your sake!

Huyu ni mfano wa kuigwa na natumai atafika mbali na kusaidia wengi!!!


(Deo Meck akiwa ofisini kwake)
KWA HUDUMA ZA KAMPUNI YAKE AMA KAZI ZA KOMPUTA NA KWA MAWASILIANO ZAIDI UNAWEZA KUMPATA KUPITIA
+255 753 481628
+255 715 481 628 

 **********************************************
NEVER HATE....APPRECIATE!!!!
**********************************************

+255-713-883 797/lacs.project@gmail.com
(Andika kama una swali au maoni....unaweza tu ku-comment post hii kama ukiwa member wa blog hii,karibu sana)

(c)Zooming Zone'2012  
Haki zote zimehifadhiwa na Chavala,The King!!

ZOOMING ZONE OOO2...Na ROSE MUSHI

 Shalom!
Leo katika kioo changu naomba nimzungumzie dada mmoja mrembo ninaemheshimu na kumpenda sana, na si yeye tu bali na kila kitu alichonacho na anachofanya!!
ROSE MUSHI .....The Author!! 

(An Economist by profession, Public Motivational Speaker, Entrepreneur, Author of Various Books Including, Why should you wait,What makes a Lady Attractive, Brothers In Relationships, and Keys to Academic Excellence)
Rose ni binti wa kichaga, mzuri, aliyeokoka na kumpenda Mungu sana, May 30 ndio tarehe aliyozaliwa (Ukweli ni kuwa watu tuliozaliwa May ni watu wa kipekee)
Rose amekulia hapa nchini Tanzania na kimsingi alisoma ASHIRA GIRLS, Marangu Kilimanjaro kabla ya kujiunga na Kitivo cha Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam!

Amekuwa kiongozi mara nyingi sana katika ngazi mbalimbali za kukua kwake, lakini zaidi nimemfahamu akiwa chuo kikuu cha Dsm, na wakati huo alikuwa ni kiongozi wa TAFES na alikuwa Mwimbaji mmoja mzuri sana, wakati huo na kundi lao la Annointed Girls!
Hakuna ambaye angeweza kudhani kuwa Rose atakuja kuwa Bonge la International Minister wakati huo kwa jinsi alivyokuwa mpole na mnyenyekevu sana!.....Lakini alakwata sasa wale waliomfahamu hapo kwanza wanatamani kama japo wangepiga nae tu picha hapo kale lakini hakuna nafasi hiyo tena!!


Rose alihitimu 2010 na baada ya hapo akaamua kutoa muda wake kufanya kazi katika ofisi za KKKT Dayosis ya Mashariki na Pwani(Idara ya Uchumi) na baadae akapewa kusimamia mradi wa uanzishaji wa Benki ya Dayosisi hiyo, ambayo mpaka sasa anasimamia mradi huo!!


Zaidi ya kazi za Ofisini, Rose amekuwa akifanya Semina ama kualikwa kama mzungumzaji katika semina mbalimbali za neno la Mungu, nyingi zenye mlengo wa kuwafundisha vijana, hususani mabinti kujielewa na kujitambua thamani zao, maana wengi wao hupoteza mwelekeo kabisa wanapoingia kwenye mahusiano!!!
Rose mushi ni mwandishi mzuri sana wa Vitabu na mpaka sasa ameshaandika vitabu sita na bado anaendelea, ni mwimbaji mzuri na Dada ambaye amekataa kuchezewa na mtu awaye yeyote yule baada ya kutambua thamani yake mpaka hapo atakopoolewa!!

HER FAVORITE QUOTES;

"You can not be mistaken for a pauper if you dress like a prince and you can not be mistaken for a prostitute if you dress like a princess..people see who you are before they have to hear what you say.

A beauty body is not enough to qualify a girl to be a wife..but a beauty mind-beauty character should be added.."




UKWELI NI KUWA DADA HUYU NI SHUJAA NA MFANO MZURI WA KUIGWA NA VIJANA WA KITANZANIA NA AFRICA HUSUSANI MABINTI!!!
 (King Chavala,the Blogger and Rose Mushi)

UJASIRI, KUJIAMINI , AKILI NA UZURI WAKE BILA KUSAHAU UCHAJI WA MUNGU NDANI YAKE, NDIVYO VILIVYONIPA UJASIRI WA KUM-ZOOM LEO ILI KILA MTU AJUE KUWA BINTI HUYU NI WA KUIGWA!!!!


NEVER HATE....APPRECIATE!!!!


+255-713-883 797/lacs.project@gmail.com
(Andika kama una swali au maoni....unaweza tu ku-comment post hii kama ukiwa member wa blog hii,karibu sana)

(c)Zooming Zone'2012  
Haki zote zimehifadhiwa na Chavala,The King!!

ZOOMING ZONE 0001....NA SAMWEL SASALI,THE BLOGGER!!!!


Salaam!!


Leo katika kipengele hiki natamani nimzungumzie kijana mmoja aitwaye



SAMWEL SASALI a.k.a PAPAA SEBENE,THE BLOGGER


(Natural African Activist Tanzanian patriot short funny loving caring brother, very God loving servant!!!)


Huyu ni lango katika nyumba ya Mzee Sasali na kwa ushuhuda na ukiri wake mwenyewe,yeye ni zawadi ya Mungu kwa familia hiyo na sadaka ya mama yake kwa Mungu!


Amebahatika kusoma Tanzania,sifa ya pekee ya kusoma kwake ni kusoma huku akifanya vitempo wakati wa likizo au wakati akisubiri kwenda hatua nyingine na Shahada yake ya kwanza ameipatia Chuo kikuu cha Mzumbe-Morogoro na hii ni Shahada ya Usimamizi wa Rasilimali watu(Bachelor Degree of Human Resource Management)



Amewahi kufanya kazi na halmashauri ya wilaya ya Ilala, Huwaei na sasa yuko na Benson Informatics Ltd kama HRM.


Samweli ni MC maarufu na anajimudu katika kazi yake, Preacher(Muhubiri/Mwalimu) wa neno la Mungu tangu kale, Thinker and Idea Developer

.........anafanya vitu vingi sana hapa mjini, na kilichofanya nimfahamu ni correllation ya mengi tunayofanya pamoja...nilikuwa namsikia tu but nilikutana nae face to face na kuzungumza nae mara ya kwanza mwaka 2007 pale MUFES kulikuwa na ibaada ya fundrising ya kununua vyombo vya muziki na yeye ndio alikuwa MC na mimi nilikuwa mgeni mualikwa tu.
...................................then urafiki na ukaribu ukaanza hapo hata leo na mpaka baadae sana!!


Samwel ni Blogger na anamiliki blog yake iitwayo
“samsasali.blogspot.com”
ambayo inafanya vema sana katika tasnia hii ya social medias, anapatikana pia facebook kwa saana na pia BBM 



Papaa ndio muanzilishi wa Mtandao wa marafiki uitwao MARAFIKI HURU....na mtandao huo baadae ukazaa maono mengine nayo ni mtoko wa marafiki wapendwa kila mwezi uitwao FRIENDS ON FRIDAY(FOF), ambao kwa sasa umeenea mpaka Mbeya,Arusha na kuna kila jitihada za kuanzisha Zanzibar


PAPAA amekuwa na experience nzuri sana ya publicity ya matukio mbalimbali hapa mjini,hivyo mafanikio ya matamasha au matukio kama LAUGH AGAIN CONCERTS; AFLEWO; CAMPUS NIGHTS; RIOTS; NA MENGINE MENGI yana mchango mkubwa sana wa huyu mkaka!.

Huyu kijana ni mzungumzaji mzuri(Motivational Speaker) na mwingi wa Idea kila kukicha, ana moyo wa kujitoa na kumsaidia kila afaaye kusaidiwa... zaidi ya yote huyu jamaa ni mwanaharakati wa kweli, maana akiamua kukomaa na issue huwa anajitosa tu hata kama inaonekana hatari mbeleni...alianza kufanya vibarua ili kujisomesha kabla haujaja huu mfumo wa mikopo ya serikali na amewahi kufanya utangazaji pale Praise Power na hivi sasa anajiandaa kuwa mbunge wa Mbinga!!




Namkubali sana,namuheshimu na najifunza vingi kutoka kwake!

Kila tukionana lazima nijichangamotishe kwa harakati zake, natamani sana vijana wa kitanzania tuuige mifano ya vijana wenzetu na hawa ndio wanapaswa kuwa Roll Model na sio hao wazungu na watu gani!!!


Ni bora niseme ukweli kwa yale yanipasayo kusema sasa,maana siku akifa haitafaa kitu kwake wala kwangu,itakuwa kama vile unatafuta kumfahamu!!


Siwezi kuandika hapa kila kitu but in summary, THE GUY IS MY HERO!!


“THINK DIFFERENTLY MAKE A DIFFERENCE”.....na huu ndio msemo wake wa moyo!!!


SISI NI MARAFIKI KWA HIYO TUNASAIDIANA, UKITAKA KUTHIBITISHA NJOO UMSEME VIBAYA KWANGU UONE KAMA UTAONDOKA MACHONI KWANGU SALAMA!!





NEVER HATE....APPRECIATE!!!!


+255-713-883 797(Andika kama una swali au maoni....unaweza tu ku-comment post hii kama ukiwa member wa blog hii,karibu sana)

(c)Zooming Zone'2012  
Haki zote zimehifadhiwa na Chavala,The King!!