MSAADA WA DHARULA WA CHAKULA UNAHITAJIKA KWA WOTOTO YATIMA WA HOCET!!!!
SHALOM!
HABARI ZENU WAPENDWA!!
NINAAMINI
MNA MOYO WA UPENDO, TENA WA KUWAJALI WENGINE KULIKO NINYI, NA HATA
ZAIDI BIBLIA INASEMA UPENDO WA KWELI NI ULE WA KUWAPENDA WENGINE ZAIDI.
*****HANANASIFU
ORPHANAGE CENTRE (HOCET)....HAWANA CHAKULA KABISAAAAA NA WEWE NA MIMI
PEKEE NDIO TUNAWEZA KUWALISHA KWA SIKU 120, KABLA HAWAJAANZA
KUJITEGEMEA****
LEO
NINALO OMBI MAALUM KWENU, NI MUHIMU SANA SANA....KUNA KITUO KIMOJA CHA
KULELEA WATOTO YATIMA (WATOTO WA MUNGU), KITUO KINACHOENDESHWA NA WATU
TU WALIOJITOLEA, NA HAPO AWALI KILIKUWAQ KINAFADHILIWA NA WAZUNGU
FULANI, LAKINI BAADA YA KUONA WATOTO HAO WAMEKAZANA NA MUNGU NA HAO
WAZUNGU (WAFADHILI) WAKAWEKA MASHARTI, ETI KAMA WAKITAKA WAENDELEE
KUPOKEA MISAADA YAO BASI WAACHANE NA HAYO MAMBO YA YESU YESU....NA KWA
KUWA HAKUNA BABA MWINGINE ZAIDI YA MBINGUNI NA HAKUNA NAMNA BINADAMU
ANAWEZA KUISHI KWA MISAADA YA BINADAMU MWINGINE BAADA YA KUMKANA MUNGU
WA KWELI.
SASA
WATOTO HAO WAKO KWENYE ENEO LAO LA SHULE WANASOMA NA WANAYO MIRADI
AMBAYO BADO HAIJAANZA KULETA FAIDA ILI WAWEZE KUJIENDESHA WENYEWE,
NAHIYO ITAKUWA HIVYO TU BAADA YA MIEZI MITATU AU MINNE KUANZAIA SASA.
WATOTO
HAWA KWA SASA HAWANA CHAKULA KABISA, NA HATA LEO WAMEKULA KWA MSAADA WA
KIJANA MMOJA ALIJITOLEA YEYE BINAFSI NA FAMILIA YAKE....MBALI NA
GHARAMA NYINGINE ZA UENDESHAJI KAMA MISHAHARA/POSHO ZA WALIMU;
************************************************************************************************
KITUO HIKI KINATUMIA UNGA KILO 30, MAHARAGE KILO 14 NA SUKARI KILO 5....NA IKIWA NI WALI,BASI HUHITAJIKA KILO 30 ZA MCHELE KWA MLO MMOJA....NA PIA UNAWEZA KUCHANGIA MAFUTA NA FEDHA KWA AJILI YA VITU VINGINE VINAVYOWEZA KUHITAJIKA.
************************************************************************************************
NINAAMINI
KWA MSAADA WA WATANZANIA WOTE WENYE MAPENZI MEMA NA WATOTO WA
KITANZANIA, WATOTO HAWA HAWATAKOSA CHAKULA KWA SIKU HIZI 120 ZA MPITO
KABLA HAWAJAANZA KUJITEGEMEA WENYEWE, SIO LAZIMA ULETE MSAADA MKUBWA
SANA, LAKINI NAAMINI UNAWEZA UKAJITOLEA CHAKULA KIASI JAPO KWA SIKU MOJA
TU KAMA SIO TATU, YAWEZA KUWA WEWE BINAFSI AU KAMPUNI AU FAMILIA AU
KANISA, LAKINI NINACHOKIAMINI NI KUWA KAMA KWELI TUNAAMINISHA KUMPENDA
MUNGU NA KUWAPENDA WATOTO WATANZANIA TENA WANAOLELEWA KATIKA MALEZI YA
KIMUNGU BASI LAZIMA WATOTO HAWA WATAISHI BILA HOFU YA CHAKULA KWA SIMU
HIZI 120, NA KWA HAKIKA BWANA ATAKUBARIKI SAWASAWA NA IMANI YAKO KWAKE
YAK 1:27 "....DINI
ILIYO SAFI ISIYO NA TAKA MBELE ZA MUNGUBABA NI HII, KUWATAZAMA WAJANE
NA YATIMA KATIKA DHIKI YAO NA KUJILINDA NA DUNIA PASIPO NA MAWAA"
MSAADA
HUO UNAHITAJIKA SANA SANA, NAAM KWA NAMNA YOYOTE ILE UNAYOWEZA
KUCHANGIA BASI USISITE,FANYA HIVYO...SADAKA YAKO YA KUWALISHA WATOTO
HAWA HAITASAHAULIKA HATA KIDOGO, UNAWEZA KULETA MCHANGO WAKO WA CHAKULA
PALE OFISI ZA NIIM COMPUTERS, MOROCO HOTEL AU UKATUMA MCHANGO WAKO WA
FEDHA KWA NJIA YA SIMU, NAAM KWA MAULIZO ZAIDI
TAFADHALI WASILIANA NA WASIMAMIZI NA WARATIBU WA ZOEZI HILI KWA NO.
0713
26 1425 na 0754 527955, pia 0783 757051
KWA
NIABA YA WASIMAMIZI WA KITUO HIKI NINAWASHUKURU HATA KABLA HAMJAFANYA
JAMBO LOLOTE MAANA NAAMINI UMEGUSWA NA UKO TAYARI SASA KUWASAIDIA WATOTO
HAWA...KAMA TUNAWEZA KUCHANGIA SHEREHE ZA HARUSI, NAFIKIRI HATMA YA
WATOTO HAWA NI ZAIDI,MUNGU AKUBARIKI UNAPOMSHIRIKISHA NA MWENZAKO!!
Imeandikwa na
KING CHAVALA MC
KWA UDHAMINI MKUBWA WA CHAVALA IDEAS PLATFORM.