Mabaka
Yasiyokuwa na Hisia ana Makovu yanayotokea bila mwanadamu mwenye kuwa
na uelewa kuwa kuna kitu kinaendelea kwenye mwili wake, hali hii
hupelekea mtu kutibu matokeo ya ugonjwa na sio ugonjwa wenyewe. Kati ya
dalili nyingi za wagonjwa wa ukoma ni waathirika kupata madhara pasipo
wao kuwa na taarifa (sense) katika miili yao. Wagonjwa wengi hata wale
wa Saratani Ya Ngozi hukuta tu wana mabaka ama makovu kwenye miili yao
ambayo yametokea pasipo wao ku-sense kama kuna mabadiliko katika miili
yao. Nilipokuwa Mbeya wakati fulani Pastor Matthew Sasali (Mdogo wangu)
alinikumbusha kuwa dhambi kwenye maisha ya mwanadamu ni kama makovu
yasiyo na hisia, huanza pole pole mwisho wake ni kama ambavyo inaelezwa
Mshahara wa dhambi ni Mauti.
Kila mtu kwa nafasi yake anaweza kuitazama Jamii ya leo na kuona, mambo mengi yanayotokea
sasa yalianza pole pole na kudhaniwa kuwa hayatakuwa na madhara makubwa
kwenye Jamii lakini kwa sasa matatizo hayo yamekuwa sugu vya kuchosha.
Issue za ufisadi zilianza pole pole kwenye Jamii yetu, leo hii kwenye
Jamii si ajabu mwovu anakumbatiwa na mwema anachukiwa, ukionekana
unaikosoa Serikali unaambiwa unahatarisha amani ya nchi. Leo hii watoto
wanadiriki kuwapeleka wazazi wao mahakamani, leo hii idadi ya mashoga
inaongezeka kwa kasi lakini kuna siku hali haitakuwa hivi sababu ni kama
Jamii imekufa ganzi. Watu wanaokamatwa na madawa ya Kulevya kila siku
wanakuwa wengi lakini mwisho wa siku tunazoea tu
Zamani
idadi ya wana cheat kwenye mahusiano ilikuwa ni ndogo sana na hata kama
mtu alikuwa anatoka nje ya ndoa ilikuwa ni Siri sana lakini siku hizi
yaani inajulikana kabisa ni nyumba ndogo, sio sasa wanandoa kuaminiana,
hali ngumu ya maisha na kupenda mafanikio ya haraka hataka yamepelekea
wanandoa wengi kusaliti ndoa zao, waume za watu hawaaminiki, wake za
watu mule mule, enzi hizo watu walikuwa wanaugopa Mungu kwa sana si
makanisani si misikitini, siku hizi kuna mambo yanatokea na watu kama
wanayapotezea lakini mwisho wa siku yatatengeneza maumivu na mateso
katika maisha na kutunyima furaha.
Angela
(sio jina kweli) niliwahi kukutana nae katika mojawapo ya mizunguko
yangu katika mashule na vyuo. Mdada huyu alikuwa ni kidato cha 6, baada
ya mimi kufundisha mambo kadha wa kadha ya maisha, dada huyu aliniomba
tuzungumze maana alikuwa anahitaji msaada. Katika maongezi yake
alinieleza kuwa alianza kuingiliwa kinyume cha maumbile akiwa kidato cha
kwanza, kwa wakati huo akiwa kidato cha sita alikuwa si kwamba si tu
anapenda mchezo huo bali amekubuhu, hajisikii raha kufanya mapenzi kwa
njia ya kawaida isipokuwa mpaka ameingiliwa kinyume cha maumbile. Na si
kwamba anapenda hiyo hali amejitahidi mbinu mbalimbali za kukataa hiyo
tabia ila alieleza huwa inaondoka na kurudi. Nilipomdadisi ilikuaje
mpaka akaingia katika huo mchezo alieleza boyfriend wake waliyeachana
ndiye aliyemfundisha na kumzoesha, alijua ni kitu cha kawaida na
kinaweza kuepukika lakini si hivyo. Unafanyaje pale mume wako wa ndoa
ama mchumba wako akataka kukuingilia kinyume cha maumbile, umewahi sikia
habari hii mara ngapi lakini ni kama watu wanaipotezea, hili ni kovu
linalotokea bila kusikia maumivu ya kidonda. Na mwisho wa siku tutakuwa
tumesharudi katika enzi za Sodoma na Gomora
Leo
hii umesikia mara ngapi matamko mbalimbali ya kidini yakitolewa kila
mmoja akimtishia mwingine, lakini hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa
kukomesha hali hiyo. Inawezekana hisia za kuhisi madhara yake kwenye
Serikali yetu zimekufa lakini kidonda hiki kina madhara makubwa hapo
baadae zaidi ya madhara ya ugonjwa wa Saratani. Kuna siku raia watajitoa
mhanga ndipo tutashuhudia kitu ambacho leo tunakidharau, watu wanapigwa
mabomu, watu wanapigwa risasi, risasi inaua, kuna siku watu watachoka
kukaa hai kufa kwao si tatizo sana, kwa kusema hivi lazima Jamii ianze
kutazama huu mwamko wa Kijamii kwa sasa na kila mtu kudai haki yake kwa
mabavu hata pale palipohitaji subira na busara tutafika wapi?hii hali
tusipoiona kuna siku yataibuka mambo.
Leo
hii kuna matatizo ambayo pengine yalianza zamani na kudhaniwa kuwa ni
madogo, wanaume wengi wanaoangalia pornography hawakuanza jana, ni kitu
ambacho wengine kimeshajengeka kwao, kuna wanaume wao kujichua ni kama
wameshikiwa risasi kuwa wasipofanya watakufa. Wengine ni wafanyakazi na
vyeo vyao lakini sasa wanateseka na tabia hiyo wengi wao hawapendi
kufanya hayo lakini wakati wanaanza walidhani ni kitu kidogo ambacho
hakiwezi kuathiri maisha yao. Wengine mpaka kwenye ndoa hawasikii raha
bila ya kujichua wao wenyewe. Haya ni Mabaka tuliyoyadharau kwa kudhani
hayana madhara leo hii yameacha alama zisizofutika kwenye tabia zetu.
Tabia
zetu wakati mwingine zimekuwa ni tatizo la kudumu, wengine wetu
uaminifu sasa imeanza kuwa issue, maana kuna wengine walianza tu
polepole kwa ahali ilivyo sasa sio kwamba hawataki kuwa waaminifu, No
wanapenda sana kuwa waaminifu issue inakuja tu kuwa wameshaathirika na
kutokuwa waaminifu, kwa kuupuuzia kwao mambo madogo madogo wamejikuta
wamepoteza opportunities nyingi sana kwenye maisha yao. Watu
wanatamani kukuamini lakini tabia huwa zina athiri sana maisha yetu ya
kila siku. Ndoa zetu zimeathirika na tabia zetu kazi zetu zimeathirika
na tabia zetu, mahusiano yetu na Mungu yanasua sua kutokana na tabia
zetu. Can Something good come out of you?
Asilimia kubwa ya Vijana wa Sasa wamesha experience maumivu kwenye mioyo yao juu ya mahusiano. Siku moja tukiwa kwenye Conversation kali kwenye Facebook Wall yangu, mmoja wa Marafaki zangu aliongea akisema kwa namna moja ama nyingine suala hili la kuumizana linatokana na Wanaume kutokuwa na Msimamo katika kile wanachokitaka. Kuto kuwa na Msimamo ni Matokeo ya kitu ambacho kinaendelea kwenye Jamii, kwanini watu hawana misimamo katika kusema sitaki A nataka B, Wadada wengi wamejikuta wakitupia wakaka lawama kwa kuwauzisha Sura mwisho wa siku inakula kwa Mdada. Kizazi hiki kinaona ndoa ni jambo la fahari kuliko jambo la fungamano ndo maana unakuta ndoa ilifungwa kwa mamilioni ya fedha baada ya mwaka watu wanataka kutoka, nani alaumiwe. Mioyo ya wengi imeshajeruhiwa na kubutuliwa kama kombolela hakuna tena penye sehemu ya kupenda. Ukitaka kujua una kovu lisilokuwa na hisia ni pale unapopata mpenzi mpya halafu ukabaini ameanza tabia kama za yule aliyekimbia kuna kitu kunaingia ndani yako ghafla si unajua uking'atwa na nyoka???
Asilimia kubwa ya Vijana wa Sasa wamesha experience maumivu kwenye mioyo yao juu ya mahusiano. Siku moja tukiwa kwenye Conversation kali kwenye Facebook Wall yangu, mmoja wa Marafaki zangu aliongea akisema kwa namna moja ama nyingine suala hili la kuumizana linatokana na Wanaume kutokuwa na Msimamo katika kile wanachokitaka. Kuto kuwa na Msimamo ni Matokeo ya kitu ambacho kinaendelea kwenye Jamii, kwanini watu hawana misimamo katika kusema sitaki A nataka B, Wadada wengi wamejikuta wakitupia wakaka lawama kwa kuwauzisha Sura mwisho wa siku inakula kwa Mdada. Kizazi hiki kinaona ndoa ni jambo la fahari kuliko jambo la fungamano ndo maana unakuta ndoa ilifungwa kwa mamilioni ya fedha baada ya mwaka watu wanataka kutoka, nani alaumiwe. Mioyo ya wengi imeshajeruhiwa na kubutuliwa kama kombolela hakuna tena penye sehemu ya kupenda. Ukitaka kujua una kovu lisilokuwa na hisia ni pale unapopata mpenzi mpya halafu ukabaini ameanza tabia kama za yule aliyekimbia kuna kitu kunaingia ndani yako ghafla si unajua uking'atwa na nyoka???
Wengine
wamekuwa wakihangaika na matumizi mabaya ya fedha kiasi kwamba
wanajitahidi kujidhibiti wanashindwa, kosa alilofanya mwezi uliopita
amejikuta na mwezi huu amelifanya, wengine wamejitahidi kuacha matumizi
ya hovyo lakini imeshindikana kilichotokea wamekubali kuwa hawawezi
kubadilika, ilipoanza ni kama haikuwa na madhara lakini wengine sasa its
too mucha na still hawaoni kama watasaidika katika hilo, wamekubali
matokeo. Wengine tabia za kuzira, ajabu unakuta mtu mkubwa kabisa eti
anazira, lakini hakuanza leo tabia hii imekuwa polepole bila ya watu
wenyewe kujijua imejijenga ndani yao. Wengine ni hofu, wamejawa na hofu
mpaka unnecessary. Kuna rafiki yangu yeye kila kitu anaogopa hasa
inapofika suala la ndoa yale aliyoyasikia kutoka kwa watu na
aliyoyapitia yamemjaza hofu kuwa katika dunia hii kama kuna mwanaume
ambaye yupo kabisa hawezi cheat na akabaki kuwa mwaminifu kwake peke
yake. Hofu anabadili namna ya kutazama mambo, hofu inamadili namna ya
kuishi na kuongea na kuamua mambo mengi, hofu ikikujaa unaweza ukaufunga
hata uwezo wako wa kuwaza na kupambanua mambo, hofu inatawala.
Inawezekana
kuna jambo ulishawahi dhani umelisamehe na kuliachilia lakini kila lile
jambo linapotajwa kuna mkwaruzo ndani ya moyo wako hutokea, kama
umewahi umizwa na mapenzi ukiwasikia watu wanaongelea mapenzi unatamani
usimkumbuke mtu aliyekutenda, ikitokea umemuona njiani anakuja unatamani
kubadilisha njia, yamkini uliwahi dhurumiwa ama pata hasara ya biashara
yale maumivu bado yameganda kwenye nafsi, inawezekana ni ofisi
waliyokufukuza sometimes back ukisikia jina la ofisi moyo unakuuma.
Makovu haya ya nafsi hu-develop tabia ambayo yamkini hukuwa nayo hapo
awali. Umejengeka na kuto samahe, umejengeka kuwa na tahadhari nyingi
zaidi, Umejengeka kuto amini amini mwenzi wako akishika tu simu unajua
anachat na wanawake wake unatamani kumwamini lakini nafsi yako imesha
develop tabia iliyotengenezwa kutokana na jeraha. Ukimsikia mtu anasema
"wanaume wenyewe wote vimeo" jua ana jeraha ama ukisikia mtu anasema
"wanawake wote wanafanana" jua ana jeraha lake la kwenye nafsi kila mtu
amejawa na hofu ya kuogopa kutoneshwa jeraha la nafsi alilowahi kupitia
hapo kabla.
Wengi
tunateseka si kwa sababu tunataka kuteseka, hofu zinatawala maisha
yetu, kujilaumu kumekuwa ni sehemu ya maisha yetu,kutokuamini wengine
imekuwa ni sehemu yetu. Wengine wanafanya biashara wakiwa wameshajiandaa
kupata hasara, wengine wameingia katika ndoa wakiwa wamejiandaa
kusalitiwa, wengine wameingia katika ajira wakiwa tayari kuiba. Mabaka
yasiyo na hisia yamekuwa kiasi kwamba tuko tayari kuumia au kuumizwa
hata kuumiza kila mtu yulo tayari kwa lolote ovu kutokea kuliko wema.
Haya mambo yalianza polepole katika maisha na jamii yetu sasa
yameshatuathiri. Unayosikia leo Tunisia au Misri hayakuanza tu ghafla
ila yalianza polepole.
Hakuna
mtu anayekufahamu vizuri kuliko wewe mwenyewe unavyojifahamu ipo haja
ya kujichunguza na kubadilika kabla mwaka haujafika mbali.
…//Papaa
0713 494110
samuel_sasali@yahoo.com