CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

JIEPUSHE NA MATAPELI WALIOKUBUHU HAPA DSM....IMENITOKEA MM LEO 02/02/2013 KWA MARA YA PILI


Kuna utapeli fulani unaendelea Tanzania na inaelekea wanaoufanya wamefanikiwa sana na wanaendelea kufanikiwa kwani ni wa muda mrefu sasa. Nadhani matapeli hawa wanatumia ujinga wetu maana sisi sio watu wakutafuta sana usahihi wa mambo kabla ya kusema au kutoa maamuzi, pamoja na ujinga wetu wa kutaka kufanikiwa kwa haraka kwa njia yeyote ile hata kama hatujafanya kazi na bila kutumia akili. Utapeli huu sio mwingine bali ni ule wa wale watu wanaompigia mtu simu wakijifanya wanakujua kabisa na wanaweza hata kukupa some backgrounds zako za kazi, ajira au elimu na meninge hadi ukashawishika kuwa unayeongea naye ni mtu unayemfahamu/munayefahamiana na hivyo kutokua na hofu na uhalisia wa anachokuambia. Baada ya hapo wanaanza kukushawishi juu ya kuwasaidia kupata madawa ya kuhifadhi nafaka kwa madai kuwa mawakala wao ambo wamekua wakizipata toka kwao wameanza kuleta uswahili hivyo kwa vile unayeongea naye ndio anahusika na suppy, basi ameona ni vema akutumie wewe “mpendwa anayekujua” ili angalau upate hiyo commission kubwa ambayo huwapa ho mawakala na mugawane kidogo. Mara nyingi wanasema wanafanya kazi na shirika la chakula duniani (FAO) au shirika la wakimbizi duniani (UNHCR) na wako Kigoma.

Papaa On Tuesday....Mtu Aonavyo Nafsini Mwake Ndivyo Alivyo


Ninakila Sababu ya Kumshukuru Mungu kula Inapoitwa leo kwa ajili ya Upendo wake kwangu kwenye maisha yangu, ninamshukuru Sababu nina ishi vile atakavyo na sio kama watu wengi watakavyo maana kwenye Kiswahili tunajifunza methali inayosema "Miluzi Mingi Inampoteza Mbwa" we unadhani uwongo??we ishi kama watu wanavyotaka nakuambia utapotea sana. Jua kwanini Upo na Unapaswa Kufanya Nini kwenye maisha utafurahia maisha yako.

Kwenye maisha nimekutana na watu wengine walitakiwa kuwa Wanajeshi wamekuwa Viongozi wa dini, nimekutana na watu walitakiwa kuwa Waalimu Kwa sababu mbali mbali wamekuwa Askari wa Barabarani, kuna watu walitakiwa kuwa Askari Magereza wamekuwa wake za Wachungaji kwani we unadhani bongo maisha yana formula??wengi tunafanya kazi ili tupate hela, kuna wacheza movie wengi sana wako maofisini, kuna waandishi wa habari wengi sana wanauza mitumba, kuna wabunifu wengi sana mambo wako sehemu kwa ajili ya

....IF YOU MANAGED TO THINK AND COME OUT WITH AN IDEA THEN TO START IT IS NOT A BIG DEAL....JUST START DOING WHAT IS NEEDED TO BE DONE NOW!!!

IT IS HIGH TIME GUYS SINCE I WROTE HERE CONCERNING ISSUES AND WORKABLE IDEAS TIPS!!
FIRST OF ALL I AM VERY GLAD TO BE CHOSEN TO SEE 2013, I BELIEVE I AM HERE FOR A SPECIFIC PURPOSE AND ALLOW ME TO SAY HAPPY NEW YEAR TO YOU!!!!
AFTER SAYING THAT....ALLOW ME TO SHARE A BIT ABOUT WHAT POWER IT TAKES FOR SOMEONE TO COME UP WITH IDEA!!! 

In this world we live Nothing is new at all,but we are the one who are new,that is why every time we come across with matter that we have never seen before we become so excited but those matters remain just normal, but in our heads/minds we have different configurations and settings upon everything we come across with and always high attention always catch those matters that we interested most basing on background informations that we have about those issues,and all that we call it MOTIVATION/PASSION....Then the process of our brain to suitably set up those motivations in course of action in our environment, we call it THINKING, this is work involve very many inputs,energy and time and honestly speaking THIS IS THE HARDEST JOB IN THE WORLD BUT THE MOST PAYABLE ONE,and very few people opt to do this!!!
Then after thinking you come out with the product called IDEA, it might be solution oriented or problem based idea but the most important issue to consider is workability of such an idea!!!

THEN THE PROCESS OF THINKING AND COMING OUT WITH A VERY GOOD WORKABLE IDEA IS THE BEST ONE AND INVOLVE ENOUGH OF YOUR BRAIN,then going on to start it is not the big deal at all!!
I have come across very many people with very good ideas(though i am not sure if they have not just copied somewhere) but they remain stacked with thousands of reasons!!...many claim Money to be an issue but i want to tell you that money has never been a problem in this earth but the problem is your seriousness with what you have

...One thing that you need to know is this BELIEVE IN YOURSELF,TRUST YOUR IDEA then CONVINCE PEOPLE TO PUT THEIR HANDS INTO YOUR IDEA!!!

However small the Idea might be just start to do what you can do for the time being!!!

"Everything in this Earth is done by Faith,you need not to see the whole staircase,just start the first step by faith" King Martin Luther

THE POWER THAT YOU HAVE USED TO THINK(IF YOU HAVE DONE THAT) AND COME UP WITH AN IDEA IS TEN TIMES THE ONE NEEDED TO START UP AN IDEA!!

I HAVE ENOUGH EXPERIENCE AND I HAVE ESTABLISHED MANY IDEAS AND UP TO NOW THEY ARE STILL OPERATING SO I AM SURE OF WHAT I AM ADVISING YOU TODAY,YOU DON'T NEED TO BE LIKE SOMEONE SOMEWHERE JUST BE YOURSELF!!
Clown Chavala
I HAVE NEVER DESPISED ANY IDEA HOWEVER SMALL IT MIGHT BE NOR ABASED ANYONE WITH AN IDEA FOR I KNOW THE BEGINNING OF ANY THING HAS SOME HARDSHIPS!!
So i want to insist once again as i am concluding my wisdom,if you think you have an idea then start working on that idea now!!!

THANK YOU FOR READING!!!
I REAL SALUTE ALL PEOPLE WHO HAVE IDEAS,AND I WANT TO ENCOURAGE YOU THAT KEEP ON PRESSING ON MPAKA KIELEWEKE!!!

By Chavala
President-ChIP
+255 713 883 797/+255 753 883 797
FACEBOOK;facebook.com/chavalapf
Twitter@kingchavala

HATIMAYE LAWRANCE NA WEMA NI WACHUMBA RASMI SASA!!

iLIKUWA VIGUMU KIDOGO KUAMINI WAZO HILI HAPO AWALI,LAKINI SASA TUNAPATA KUAMINI KUWA THAT IDEA OF LAWRANCE TO MARRY WEMA IS REAL AND WORKABLE!!
ALL THE BEST MAN!!!

LAWRANCE MWANTIMWA a.k.a GOLIATH ALIYE RAFIKI NA DAUDI KUMVIKA MTU PETE JPILI HII!!!

MAISHA NI SAFARI NDEFU SANA!!
HAKUNA HATA MMOJA AMBAYE AMEWAHI KUWAZA KESHO YA MWENZIE ITAKUWAJE!
LAWRANCE MWANTIMWA BY 2007

KUNA NYAKATI MTU HUPITA NA KUDHARAULIKA NA KILA MTU NA HATIMAYE SAA YA HESHIMA HUFIKA PIA NA SASA YULE KIJANA ALIYEKUWA SII KITU HAPO KWANZA NA HATA AKAAMUA KUSOMA KWA JUHUDI NA HATIMAYE SASA MUDA UMEFIKA IMEONEKA NA ASIKAE PEKE YAKE,MUNGU AMEMFANYIA MSAIDIZI WAKE!!

GODWIN GONDWE NA LAWRANCE
MMH JPILI HII ATAKUWA ANAMUWAHI ILI WALE WOTE WALIOKUWA WANAZUNGUSHIA MOTO WACHOMEKE WENYEWE!!

ANAJIITA LAWRANCE THE PRESIDENT AMA MC LAWRANCE MWANTIMWA,ILA MIMI KWANGU NAMUONA GOLIATH ALIYEPATANA NA DAUDI(YAANI BEHIND THE SCENE YA ILE YA BIBLE)

HAYA MKAKA NI IDEA NZURI SANA HIYO NA NDIO MAANA NIMEONA NIIANDIKE HAPA!!....NA MAPEMA TAR 14TH aPRIL ATAFANYA KWELI KABISA HAHAHAHAH!!

IBAADA HII YA KUMVIKA PETE YA UCHUMBA BINTI HUYU,ITAFANYIKA KATIKA KANISA LA CITY HARVEST,DAR-MANDELA RD-GEREJI MAHALI KILIPO KITUO CHA MAFUTA CHA VICTORIA KUANZIA SAA NNE ASUBUHI!!
WEMA MUNISI
NANI AJUAYE KUWA BAADA YA NDOA WATU HAWA WATARUDI KUISHI HUKU,MMMH JUST MY WORDS!!

NIKIRIPOTI KUTOKA MOYONI
ni mimi  DAUDI MPOLE!!

Papaa On Tuesday........Everyone Has A Story....Its a Matter Of Time


Ninawasalimu Kupitia Jina la Bwana Wangu Yesu Kristo siku hii Ya Leo. Nimatumaini Yangu Ya Kuwa wewe ni Mzima na Unaendelea Vema na Shughuli za Ujenzi Wa Taifa. Mwenzi January leo tunaugawa nusu kwa nusu ndio mwaka 2013 umeanza na kasi yake. Ninajua ni mwezi ambao kama unatafuta kukopa hela basi ujue unahitaji kuwa na vyanzo vya uhakika visivyopungua 15 maana ni mwezi ambao majority ya maisha ya kawaida ya Mtanzania tupo kwenye kuishiwa maana kwetu kujifunza kuwa kila mwezi january ni mwezi mgumu ni zoezi linalohitaji kugeuzwa nia. Kwa maombi maalum ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Vya Dar-es-Salaam, nimelazimika kufanya mwendelezo wa Papaa On Tuesday niliyoandika Mwaka Jana.

WOKOVU WETU SIO SABABU YA INJILI YA VITISHO BALI SABABU YA UPENDO WA MUNGU TU KWETU!!!


Inawezekana mtu uliokokoka baada ya kutishiwa au kutishwa na mwingine mkumbo ma labda mwingine aliumwa sana sana mpaka akakaribia kufa hivyo namna pekee ya kuwa salama ilikuwa ni wokovu,lakini sisi wengine hususani mimi na my PS tumeokoka kwasababu ya Neema yake tu!!
MIMI NAWEZA NIKAWA sina USHUHUDA KAMA WAKO ILA MIMI MWENYEWE NI USHUHUDA HAI UNAOISHI!

Leo nilipata bahati ya kuongea na my PS na nikagundua kuwa somehow tunashare track ya wokovu wetu,maana wakati anatamani kumtumikia Mungu bado alikuwa kama vile haamini au haelewi vile lakini siku moja alimwambia Mungu natamani niamke kuomba lakini kila siku naamamka kumeshakucha sasa nataka kesho uniamshe saa kumi alfajiri ili nikaombe....na basi MyPS akalala na alikuwa peke yake chumbani...na jambo la kushangaza...usiku sana aliguswa mkono kwa ishara ya kuamshwa(ni kama vile mtu alimuamsha kihalisia),na kwasababu alijua amelala peke yake na hakumwambia mtu yeyote amuamshe isipokuwa Mungu tu basi aliamka kwa mshtuko mkubwa sana huku moyo ukimwenda mbio na alipoangalia kote hakuona mtu na alipoangalia tu saa ilikuwa saa kumi kamili juu ya alama,aliogopa sana na kuanza kulia tu na kwenda kanisani kuomba na hapo ndipo alipothibitisha kuwa Mungu yupo na anamsikia na tangu hapo hata sasa Upendo wa Mungu ndio wimbo wa hekima wa my PS.

Na hata mimi nakumbuka wokovu wangu haukuwa sababu ya injili ya vitisho,bali upendo waMungu tu!!

NAWEZA KUWA SIFANYI VEMA SAAANA AU MY PS HAFAANYI VEMA SAAANA BUT WHAT I KNOW FOR SURE IS THAT WE LOVE GOD AND HE LOVES US SOOOOOO MUCH!!!

 BLESSED YOU ALL!!

Papaa On Tuesday.....Jipya Litoke Wapi Kwa Mwaka Mpya, Watu Wale Wale, Fikra Zile Zile Matokeo Yale Yale


Ninawasalimu rafiki zangu wote tulio ndani na nje ya Tanzania nimatumaini yangu kuwa tumeuanza mwaka 2013 kwa amani kabisa. Nami na team yangu nzima ya Utendaji Tunawatakia Happy New Year.
Mwaka 2013 umeanza kwa kasi sana juzi tu hapa tumesherekea mwaka Mpya Ghafla leo tarehe 8, nexr week nikiandika tayari katikati ya mwezi maisha yanasonga na siku zinasonga na mwaka utaisha tutaingia 2014.
Kati ya maneno ambayo watu wengi wanayo anaoanza kupanga mipango utasikia "mwakani nataka nianze kusoma" au "Mwakani nataka Nianze Kulima" mwingine ukumuuliza swali tu atakuambia Mwakani, utadhani mwakani huwa haifiki, Mwakani na Kesho vinapishana kidogo sana. Ukimwambia mtu tuonane lini anakuambia "kesho", au hela yangu unanilipa lini anajibu "kesho", ama ukienda maofisini kufatilia documents utasikia Njoo Kesho, Njoo Kesho ikianza hutaamini wengi huwa wanadhani Kesho iko mbali, Kesho haiko Mbali kama Mwakani ilivyo karibu.
Mwaka 2013 ndio huu umeshaingia kwa sasa yale uliyosema Mwakani sasa Mwaka ndo umeshaingia umejipangaje kutilimiliza uliyo yakusudia??kama bado una mawazo yale yale, fikra zile zile, mtazamo ule ule basi usitegemee tofauti na mwaka jana, nini kipya unacho unadhani kinaweza kukusababishia ukafanya jambo la tofauti??wengi wetu tumepanga mipango kwa ajili ya mwaka 2013 lakini ukitazama kwa kina mipango ya mwaka 2013 mingi inafanana na ile ile ya mwaka 2012 ni kama Ume Copy, Ume Edit na Ku Copy, kile ulichofanya mwaka jana ndio mwaka huu utafanya tena vile vile Jipya utakuwa umelipata wapi??Kwani umeona tofauti yoyote kwako kati ya tarehe 31 Dec, na tarehe 01 Jan, zote ziko vile vile kama Njaa iliuma kama jana, kama usingizi ulikushika kama jana, hakuna jipya linalotokea mwaka unapoanza mpya kiasi kwamba ukaamini kuna nguvu ya utendaji inakushukia kuanzia tarehe 01 January ambayo hiyo itakufanya wewe kuwa noma kuliko mwaka uliopita, mawazo uliyo nayo ni yale yale, mtazamo ni ule ule Jipya litatoka wapi??

Kuna mwandishi mmoja wa Vitabu aliwahi sema Huwezi Fanya zaidi ya Kile Unachokiwaza ama Kijua, kufanya jambo ambalo hujawahi kuwaza ana kutokulijua linaingia katika Category ya Miujiza, sababu Muujiza ni jambo ambalo hukuwahi kuwaza kuliweza ama kulipata na likakupata kwa njia ya ajabu, unless 2013 uamue kuishi kwa njia ya miujiza miujiza ndio utakuwa na matokeo mengi sana tofauti. Hata kama Umetabiriwa kwenye nyumba ya ibada kuwa mwaka 2013 wewe utakuwa unatisha funika sana haitakuwa kwako kama hautaamua kuwa na fikra mpya, Kama mawazo yako uliyonayo ndiyo yamekufikisha hapo Ulipo Kwanini Usibadilishe taarifa ulizo nazo ili uweze kufika mbalia, badilisha aina ya marafiki ulio nao, badilisha aina ya nguo ulizo nazo, badilisha aina ya taarifa ulizonazo katika ubongo, ikiwezekana badilisha hata sehemu ya kufanyia kazi, ikiwezekana develop tabia za kimaendeleo kwa afya ya akili yako. Huwezi kuwa na mawazo yale yale na fikra ile ile iliyokufikisha hapo ulipo kisha ukategemea mwaka 2013 ukafanya wonders. 

Kama unayoyajua yamekufanya umefika hapo ulipo kuna mambo mawili lazima ujue yatakutokea ukiendelea kuwa na mawazo hayo hayo, kwanza lazima ujue utabaki kama ulivyo kama hautaamua kubadilika ama utapitwa na wakati sababu mawazo uliyokuwa unatumia mwaka 2012 ni mawazo ya mwaka 2011 kama ambavyo uko 2013 unatumia mawazo ya mwaka 2012. Yamkini mwaka 2013 uko kwenye season yako, kila mtu anakutafuta wewe, kama umaarufu umekujongea tayari, kama ni fedha zinazidi kukufuata jua jambo moja ukiwa na mawazo yale yale na fikra zile zile watu watasema hauna Jipya. Na kweli Jipya utakuwa umelipata wapi wakati unawaza wale wale unafanya yale yale kisha watu watakuchoka na kukukimbia.

Think Differently and Make A Difference.

Papaa Ze Blogger
Tel. 0713 494110
Twitter: Sasalijr
Facebook: Samuel Sasali
Email: samsasali@yahoo.com

HERE THE 1st MODE CALANDER FOR 2013,YOU CAN HAVE IT IF YOU NEED!!!!

HERE IS MY GIFT TO ALL WHO WISH TO RECEIVE THIS GIFT!!!
IF YOU NEED IT(THIS ONE OR OTHER VERSIONS) JUST ORDER NOW 0713883797
HAPPY NEW YEAR 2013!!!

FoF KUFUNGA MWAKA NA "FOF EXTRAVAGANZA" NDANI YA MAKUMBUSHO 07/12/2012!!!

IKIWA NI SEASON YA PILI SASA, FOF WAMEAMUA KUMALIZA MWAKA NA EXTRAVAGANZA, IDEA IKIWA NI KUWAKUSANYA ARTIST WOTE WALIWAHI KUSHIRIKI KWENYE FOF NA HIVYO KUWA NA WAKATI WA KUMSHUKURU MUNGU PAMOJA NA KUAGANA MPAKA MWAKANI TENA APENDAPO BWANA!!
HUTAKIWI KUKOSA HII,JUST BUY YOUT TICKET NOW!!
NA UKINUNUA TIKETI 4 UNAPATA TSHRT BUREEE!!
NI 15,000 TU NA NI NDANI YA MAKUMBUSHO KUANZIA JIONI YETU MPAKA KARIBU NA SIKU MPYA VILE...YAANI HAPO ATAKUWEPO FLORA MBASHA,CHRISTINA SHUSHO,GLORIOUS CELEBRATION,CALVARY BAND,MC PILIPILI NA WENGINE WENGI,JONGEA MAPEMAAA!!!

PROSPER MWAKITALIMA ADHAMIRIA KUOKOA ROHO NYINGI SANA KUJA KWA YESU KILA TAR 23TH NOVEMBER,KWASABABU NDIYO SIKU YAKE YA KUZALIWA MARA YA TATU!!!

THIS IS SPECIAL MESSAGE/WISDOM FROM MY PS
TAR 23TH NOVEMBER, NILIKUWA SINGIDA MJINI KWA MWALIKO WA MY PS, NA HUKO KULIKUWA NA KITU KILICHOKUWA KINAITWA "SINGIDA YOUTHS AND STUDENTS FESTIVAL" KATIKA TAMASHA HILI AMBAKO HABARI NJEMA ZILIHUBIRIWA AMA KUWASILISHWA NA WATUMISHI WA MUNGU KATIKA MSINDIKIZO MKUBWA WA BURUDANI ZA KIKRISTO KAMA VILE SEBENE,COMEDY NA BURUDANI KADHA WA KADHA, KIUKWELI USIKU HUO ULIKUWA WA TOFAUTI KWANI ZAIDI YA WATU 300 WALIMPA YESU MAISHA!!!
SASA TUKIWA NA MUDA KIDOGO KANDO NA MY PS,ALINIAMBIA AMEAHIRISHA HILI TUKIO MARA TATU NA ALIKUWA HAJUI NI KWANINI NA BAADAE NDIO AKAGUNDUA KUWA EVENT HII IMEANGUKIA TAREHE AMBAYO MWAKA JANA ALIPATA AJALI MBAYA SANA NA HIVYO KUPONA(KUZALIWA MARA YA TATU), NA TANGU HAPO AMEDHAMIRIA KUFANYA MATUKIO MAKUBWA KILA MWAKA TAREHE KAMA HIYO(23 NOVEMBER) KATIKA KUADHIMISHA USHUHUDA HUO MKUBWA!!!

KWELI HILI LILINICHANGAMOTISHA SANA NA KWA KUWA NAMPENDA SANA MY PS,NIKAJIAMBIA MOYONI,MIMI NI NANI HATA NISIWASHIRIKISHE WENZANGU HEKIMA AU USHUHUDA HUU?
(NA GOOD ENOUGH NI KUWA TAREHE 23 YA KILA MAY NDIO BIRTHDAY YANGU...DAH YAANI)
WELL SAID MY PS AND I WISH YOU ALL THE BEST!!!

Papaa On Tuesday.....Kuelimika ni Kubadilika, Ujinga ni Kuamua

Zikiwa zimebaki siku 16 kabla ya Event Ya Friends On Friday Funga Mwaka yenye Jina la Extravaganza kufanyika pale Makumbusho, ninayo haja ya Kumshukuru Mungu kwa ajili ya Ulinzi wake, kipindi hiki cha Msimu wa Campus Night na shughuli zingine za Kijamii na Kitumishi nimekuwa nikitembea angani na barabarani lakini Mungu amekuwa Mlinzi Kwangu. Sina budi ya kusema asante kwa Mungu kwa Uzima na Afya na uwezo wa Kuwakilisha Papaa On Tuesday Kila inapofika siku ya Leo.

Tarehe 17 January, 2012 niliandika Papaa On Tuesday yenye heading Lile Ninalotaka Kulifanya Silifanyi, Nisilotaka Kulifanya Ndilo Ninalolifanya gonga hapa kama Hukusoma....http://samsasali.blogspot.com/2012/01/papaa-on-tuesdaylile-ninalotaka.html.
Mwaka wakati unaanza nilitoa tahadhari ya kuwa pamoja ya kuwa na Mikakati tuwe waangalifu maana yale tunayoyapanga mengi hatutayafanya. Jichunguze mambo mangapi ulipanga mwaka huu umeyafanya ukiacha yale yaliyoibuka tu na kukwamisha mipango yako ya mwaka huu. Zimebaki siku arobaini na moja (41) mwaka huu kumalizika jiulize swali kuna ulilofanya la kujivunia??




Ninakumbuka Miaka hiyo ya zamani wakati nasoma Makongo High School alikuwepo Mwalimu anaitwa "Kombaha" mwalimu huyu alikuwa na msemo aliokuwa anapenda sana kuusema tukiwa darasani hasa mwanafunzi anapokosea/misbehave alikuwa anasema "Mambo Huanzia Nyumbani". Siku moja nilimuuliza Mwalimu tukiwa Nje ya darasa maana hasa ya Msemo wake huo akanijibu "Ukimuona Mtu ameonesha tabia fulani mbaya basi jua alikuwa nayo tangu zamani sema ailikuwa haijapata nafasi, mabadiliko yoyote ambayo mtu anataka kuyafanya katika maisha lazima aanze na yeye mwenyewe, aanze na familia yake ndipo wengine watafuata" siku mwelewa mwalimu yule kutokana na Ufahamu wangu ulivyokuwa nyakati zile. Mabadiliko ya kweli huanza na mtu mwenyewe ndipo wengine watafuata. Pastor Carlos aliwahi sema "Huwezi waambia Watu Yesu anabadilisha Wakati wewe Mwenyewe hujabadilika". Kizazi chetu kina changamoto kubwa sana ya ku-deal na tatizo badala ya Ku-deal na chanzo cha tatizo hasa yale matatizo yanayotuhusu sisi wenyewe.





Sisi ni Kizazi kinachojua tatizo ni nini, na suluhisho ni nini, lakini hatutaki kufuata suluhisho linalotupasa kufanya halafu tunataka mabadiliko yawe chanya kana kwamba tumetumia njia inayotupasa kuifuata. Kizazi hiki kina jua kabisa Ukifanya jambo fulani matokeo yake ni fulani, lakini tunataka kutumia njia ile ile mbaya halafu tupate matokeo mazuri. Sisi ni kizazi kinachojua kabisa Ukifanya ngono zembe matokeo yake ni magonjwa ya Kuambukiza ama Mimba, lakini ajabu watu wanafanya ngono zembe halafu wanategemea kabisa magonjwa yasiwepo na wala mimba zisiwepo ndio maana vikitokea unakuta mtu anachanganyikiwa yaani ukimuuliza huyu mtu alikuwa hajui matokeo??atakuambia anajua sasa ajabu alitaka kutumia njia mbaya kumpa matokeo mazuri. Sisi ni Kizazi kinachojua kabisa usipoweka akiba ya fedha kwenye maisha yako utakuwa hauna maendeleo pamoja na kujua hayo yote sisi ndio watu tunaoongoza kwa kutumia fedha vibaya, sio wanafunzi, sio vijana sio watu wazima, kuna watu wanapata fedha kila iitwapo leo lakini hakuna cha maana anachofanya kwenye maisha ukimuuliza fedha zako unazifanyiaga nini cha maana utakuta hakuna cha maana anachofanya na fedha hizo.





Kuna mambo kadha wa kadha ambayo tunajua tusipoyafanya tutapata mabadiliko mazuri lakini mwisho wasiku tunaishia kufanya hayo hayo. Watu wanaofanya diet wanajua kabisa wakila Kitimoto na vyakula Vya Mafuta watazidi kunenepa, ajabu hiyo hiyo Diet aliyojipangia inamshinda. Wenye Vitambi wanawake kwa Wanaume na wale wanene wanajua kabisa ukifanya nini kwa Ukamilifu Kitambi kinapungua within a short time lakini ajabu hatufanyi, Wanafunzi wanajua kabisa Ukijiandaa tangu shule ama chuo kinafunguliwa hautakomaa kusoma siku za Mitihani lakini ajabu siku zingine zote mtu anatazama Movie mitihani ikiianza tu unamuona mtu ndo anaanza kusoma. Sisi ndio Kizazi ambacho mtu anajua anatakiwa kulipa Kodi ya nyumba mwenzi December, lakini miezi yote anakula hela zake ikifika kipindi cha Kodi ya Nyumba ndo anaanza Kukopa ili kulipa Kodi ya Nyumba, Sisi ndio Kizazi ambacho Kinamchagua Mgombea ambaye anatoa rushwa ili akatusaidie kumaliza tatizo la rushwa, sisi ndio Kizazi ambacho chombo kinachohusika kuchunguza Watoa Rushwa na Wala Rushwa kinapokea Rushwa ili kuwakinga wala rushwa, sisi ndio Kizazi ambacho Washauri Wa Mambo ya Ndoa za wengine Zikitaka Kustawi zinatakiwa ziwe vipi wakati za Kwao zinawashinda Kuziboresha, sisi ndo Kizazi ambacho Watu Unao Waamini ndio Wanaokusaliti, sisi ndio Kizazi ambacho timu zetu Simba na Yanga tunajua Tatizo ni Viongozi lakini Tunamfukuza Kocha. Sisi ni Kizazi Kinachojua madhara ya Sigala lakini tukaamua kuvuta.




Ni rahisi kuwasaidia wengine kuliko kijisaidia mwenyewe, ni rahisi kuwafokea wengine wanapokosea lakini tukasahau na sisi tunakosea, ni rahisi kuwanyoshea wengine vidole kwa mambo wanayokosea na kusahau sisi pia tunakosea. Matatizo mengi ya Msingi hatuko serious kuyatatua hata kama tunajua hiki tunachokifanya ni cha muda tu, siku za nyuma niliwahi andika Usizibe Shimo La Panya Kwa Kipande Cha Mkate..http://samsasali.blogspot.com/2011/10/papaa-on-tuesdayunaziba-tundu-la-panya.html. Wengi wa wanaoenda kuomba ushauri sehemu fulani mara nyingi sana huomba ushauri pasipo kueleza kiini hasa ila kasehemu tu ka kiini, unajikuta tatizo unalo deal nalo silo hasa linalopelekea tatizo kuwepo tabia hii imepenya kwenye Jamii yetu la kuto ku deal na tatizo la Msingi, tangu zamani tulipokuwa wadogo wazazi walitumia fimbo kutukataza mambo waliyokuwa hawayapendi kilichotokea walitujaza hofu ya kufanya mbele zao wengine fimbo ziliwasaidia wengine ziliwasaidia namna ya kubadilisha mbinu mbadala ili wasichapwe. Kufundishika ni Kubadilika huwezi kusema umeelewa wakati hujabadilika.




Mtu mwenye kuonesha kuwa amelielewa tatizo na ufumbuzi wake basi ni yule anayeamua kubadilika kueleka  kwenye maendeleo. Haitakusaidia kujua suluhu ya jambo kisha usifanye kwa faida yako na Jamii yako niliwahi andika kwenye Papaa On  Tuesday kuwa "Thawabu Ya Mtendaji, Haifanani na Msemaji" gonga hapa...http://samsasali.blogspot.com/2011/01/papaa-on-tuesdaythawabu-ya-mtendaji-wa.html. Mambo huanzia nyumbani, mabadiliko ni Mchakato, lakini ni mchakato wenye nidhamu pia. hakuna jambo baya kwenye maisha kama "Kuchukuliwa" ukisikia watu wanasema "tunakuchukulia sana" ujue wameshakuchoka sema ndo hivyo hawana namna. Inawezekana wamejitahidi kukusaidia wameona hausaidiki waka opt kukuchukulia kama mzigo ambao Mungu amewapa kwenye maisha. Kwenye ndo usipende kuchukuliwa ni ishara mbaya sana kwenye kizazi chetu, kwenye Jamii usiwe mtu wa kuchukuliwa. Kama unajua jambo fulani ukilikomalia utapata matokeo mazuri kwanini usilikomalie. Discipline ya kwenye maisha ni kitu cha msingi sana otherwise tutajua rushwa ni adui wa haki na sisi tutaendelea kutoa na kupokea, sisi tutajua kabisa ukifanya jambo A utakuwa na madhara ya afya lakini watu watasema "nimeshindwa kujizuia". Kujifunza ni Kubadilika Ujinga ni Kuamua. Mambo Huanzia Nyumbani.
Think Differently Make A Difference.
Papaa
0713 494110.

"News of VICTORY international Magazine" issue no.4 IS COOOMING OUT SOON!!!

THIS IS A NEW CHRISTIAN MAGAZINE, THAT IS BEEN RELEASED IN INTERVAL OF TWO TO THREE MONTHS AND HERE IS COVER OF THE NEXT ISSUE!!!
YOU CAN OPT TO LEARN DIFFERENT ARTICLES FROM DIFFERENT MINISTERS OF GOD AS WELL AS ADVERTISE WITH IT!!
THE MAGAZINE IS AVAILABLE IN ALMOST ALL CITIES OF TANZANIA!!!

FOR MORE INFO, PLEASE CALL +255 655 271 144

JE UNGEPENDA KUSHIRIKI ONGEA NA JANET TV TALK SHOW?? WAKATI NDIO HUU UNAKARIBISHWA SANA!!!!

ONGEA NA JANET SHOW NDANI CHAVALA IDEAS PLATFORM
HABARI NJEMA KWA WAPENZI WA CLOUDS TV, DSTV NA ONGEA NA JANET SHOW!!
KWA YEYOTE ANAYEPENDA KUSHIRIKI MOJA KWA MOJA KATIKA RECORDING YA VIPINDI HIVYO MUALIKO UKO WAZI KWA KILA MTANZANIA MWENYE AKILI TIMAMU BILA KUJALI RANGI, DINI WALA KABILA!!!
IKIWA UNAWEZA KUONGEA,KUCHEKA,KUPIGA MAKOFI,KUULIZA MASWALI NA KUCHANGIA MAADA ITAKAYOKUWA MEZANI SAA HIYO BASI WEWE NI MTU WA MUHIMU SANA!!
USILAZE DAMU AMUA KUSHIRIKI SASA, RECORDING ITAFANYIKA JUMATATU, JUMANNE NA JUMATANO PALE LION HOTEL, SINZA KIJIWENI,BARABARA YA TANDALE KUANZIA SAA NNE ASUBUHI MPAKA KUMI JIONI!!
(KILA SIKU ZITAREKODIWA SHOW NNE...MBILI KATI YA SAA NNE MPAKA SABA NA BAADA YA LUNCH MBILI ZINGINE)
HAKUNA KIINGILIO KAMA UKITAKA KUSHIRIKI, MUHIMU NI KUTHIBITISHA MAPEMA KUWA UTAHUDHURIA LINI NA UTHIBITISHO HUO MWISHO NI JPILI SITA USIKU!!!
WEWE TUMA TU UJUMBE WENYE JINA LAKO KUWENDA NAMBARI UZIONAZO HAPO JUU!!

ANGALIZO;
MAADA ZITATUMWA KWA WALE TU WATAKAOTHIBITISHWA KUSHIRIKI NA KUMBUKA WAANDAAJI WANASHIKIRIA HAKI YA KUMZUIA MTU YEYOTE KUSHIRIKI IKIWA ATAZINGATIA MISINGI NA KANUNI ZA KIPINDI!!!

KAMA MPAKA HAPA HUJAELEWA BASI ULIZA SASA KUPITIA
0713 883797

MC/COMEDIAN CHAVALA ASHERESHA BOTTLE PARTY(WELCOME FRESHERS) YA KILIMANJARO KWA MAFANIKIO MAKUBWA SANA!!!

HABARI ZENU!!
MC CHAVALA
KING CHAVALA
MWISHONI MWA WIKI ILIYOISHA, NAMAANISHA NOV 9, NILIBAHATIKA KUWEPO MKOANI KILIMANJARO KATIKA MKESHA MAALUM WA KUWAKARIBISHA FIRST YEARS NA WENGINE WANAORUDI KUENDELEA NA MASOMO YAO, LAKINI PIA MKESHA HUO ULIKUWA NA MALENGO KUTANGAZA RASMI MAANDALIZI YA CAMPUS NIGHT YA KILIMANJARO INAYOTARAJIWA KUWA KATIKATI YA JANUARY!!
BOTTLE PARTY HII ILIANDALIWA NA KUDHAMINIWA NA KANISA LINALOJISHUGHURISHA SANA NA VIJANA KATIKA MANISPAA YA MOSHI NALO SI LINGINE BALI NI "MANA TERBANACLE BIBLE CHURCH(MTBC) LILILOKO MAENEO YA KWA ALPHONCE UNAPOELEKEA KB.
COMEDIAN CHAVALA leading The Song "Tukue"
KATIKA PARTY HII VYUO MBALIMBALI VYA MOSHI MJINI VILIWAKILISHWA NA WANAFUNZI PAMOJA NA WALIMU WAO NA PIA VIJANA WASOMI TOKA MITAANI PIA WALIKUWEPO.
President Chavala motivating
KULIKUWA NA IBAADA YA KUSIFU NA KUABUDU YA NGUVU IKIONGOZWA NA MTBC PRAISE TEAM NA KWAYA ZA MUCCOBS NA KCMC PAMOJA NA WAIMBAJI BINAFSI KUTOKA VYUONI,


PIA KULIKUWA DRAMA, STAND UP COMEDY(BY KING CHAVALA);DANCE NA SPECIAL RELATIONSHIP AND LOVE AFFAIRS INTERVIEW, AMBAYO ILIONGOGWA NA MC CHAVALA NA COUPLE MBILI, MOJA YA MCHUNGAJI MR&MRS DICKSON MTALITINYA NA MR&MRS MSOKWA!!!
MC CHAVALA WITH MR&MRS D. MTALITINYA DURING THE LIVE INTERVIEW
MBALI NA HAYO YOTE KULIKUWA NA NYAMA CHOMA,CHIPS,VYAPATI,CHAI,KAHAWA, SODA NA VINGINE VINGI VIFAAVYO KWA PARTY!!!
HAKIKA ULIKUWA WAKATI MZURI SANA!!
NILIFURAHI SANA KUPATA FURSA HII NA ZAIDI HESHIMA NA KIBALI CHA KIPEE KWA MKOA WA KILIMANJARO!
MC CHAVALA WITH CHRISTIAN FASHION MODELS
JUMAMOSI NILIBAHATIKA KUPATA LUNCH UHURU HOTEL,HII NI HOTELI YA KISASA YA KKKT, IKO MAENEO YA SHUNT TOWN NA JIONI NIKAWA ZOMBA HOTEL, KWA LENGO LA KUWAPONGEZA VIJANA WALIOHITIMU KCMC NA MMOJAWAO ALIKUWA NI DENNIS KAPINGA.
NEEMA SHOO & KING CHAVALA
NILIBAHATIKA KUWA INTERVIEW NA KILIMANJARO FM JUMAPILI ASUBUHI NA BAADAE NIKAELEA ARUSHA KWA MAJUKUMU MENGINE YA KIKAZI,KITUME NA KIMAPUMZIKO!!!



MC CHAVALA DOING MODELLING
AHSANTENI SANA MARAFIKI NA WOTE KWA MAOMBI YENU, SAFARI BADO INAENDELEA!!!

HAPPY BIRTHDAY SAMUEL SASALI a.k.a Papaa Ze Blogger!!!

 CHAVALA IDEAS PLATFORM NA WAFANYAKAZI WAKE WOTE WANAYO FURAHA YA PEKEE KWA AJILI YA RAFIKI, KAKA NA MSHAURI PAPAA, KWA KUSHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA LEO!!!
TUNAJISIKIA VIZURI SANA NA TUNAKUTAKIA MAISHA MAREFU YENYE FANAKA NA BARAKA ILI UZIDI KUATHIRI ULUIMWENGU WAKO KATIKA MTAZAMO CHANYA!!!
TUNATAMBUA PIA MCHANGO WAKO KATIKA JAMII KUPITIA VIPAJI VYAKO MBALIMBALI...TUMEFARIJIKA KUWA UMEANZA KUANDIKA KATIKA KATIKA BLOG HII KILA JUMANNE(PAPAA ON TUESDAY)

“The people who get on in this world are the people who get up and look for the circumstances they want, and, if they can't find them, make them. ”


 “Life at its noblest leaves mere happiness far behind; and indeed cannnot endure it.... Happiness is not the object of life: life has no object: it is an end in itself; and courage consists in the readiness to sacrifice happiness for an intenser quality of life.”


 “Life is no brief candle to me. It is a sort of splendid torch which I am permitted to hold for the moment, and I want to make it burn as brightly as possible before handing it on to future generations.”


“If you have an apple and I have an apple and we exchange apples then you and I will still each have one apple. But if you have an idea and I have an idea and we exchange these ideas, then each of us will have two ideas.”
George Bernard Shaw (1856-1950);
Playwright, Nobel Prize Winner


MUCH LOVE BROTHER!!!

Fredy Chavala
President-Chavala Ideas Platform 
Dsm

Papaa On Tuesday......Shida Haina Mjuzi Wala Mwenyewe......Think Positive



Ikiwa imebaki siku moja iwe tarehe 14 Novermber kusheherekea siku yangu ya Kuzaliwa na kuhitimisha Mwaka wangu wa mwisho kabisa kuwa Single ili niweze kuingia katika Next Level ya Uandishi wa Papaa On Tuesday, sababu ninajua kila level ya maisha ina mtazamo wake wa kiufahamu katika kutazama mambo mbalimbali yanavyoendelea mtu anayefanya biashara kama angekuwa anaandika Papaa On Tuesday uandishi wake ungekuwa unatofautiana sana na yule anayefanya kazi za Ofisi, Mchungaji angekuwa anatofautiana sana Daktari vivyo hivyo Single na Mtu mwenye familia piga ua kuna namna tunatofautiana tunavyo experience maisha. I am so excited ninapoitazama Season 2 ya Uandishi wa Papaa On Tuesday.

Maisha tunayoishi na miaka tuliyonayo kila mtu analo neno la kusema kabisa kuwa kuna hatua amepiga na kuna mahali ametoka kwenda mahala pengine. Kupitia mashauri ya wazazi ana wazee na watu wazima na elimu tunayoisoma shuleni na mafundisho ya dini tunayosikia kila tunapokwenda katika nyumba za ibada yanatuelekeza namna ya kukabiliana na Changamoto mbalimbali katika maisha. Na katika maelekezo ama mafunzo haya yamkini huwa tunajiaminisha kuwa tumeelewa kabisa kile ambacho tunatakiwa kukifanya katika maisha. Kama kuna jambo halijawahi kukupata ni rahisi sana kukosoa na kuwacheka ama kumcheka yule linayemshinda ukijiaminisha kuwa either ni lege lege ama anajidekeza wazungu wakasema "experience is a good teacher" kwenye makala zangu za Papaa On Tuesday mwenzi june kuwa Usitukane Wakunga wakati Uzazi Ungalipo gonga hapa kama haukuwa umesoma...http://samsasali.blogspot.com/2012/06/papaa-on-tuesdayusitukane-wakunga.html. Jambo linapokuwa limekupata basi unajikuta masomo yale yote uliyojifunza kukabiliana na jambo ama shida yanapokuwa yanapotea na practically unaanza kukabiliana na hiyo Changamoto.
Shida haina mjuzi wala haina mwenyewe kuna nyakati tumekuwa tukijiuliza WHY ME??WHY ME Always??na kudhani shida ni zetu peke yetu na dunia nzima hawana shida kama sisi, na wakati mwingine tumeona kama kipimo cha shida za wengine ni kidogo kama sio chepesi kuliko tulichopimiwa sisi zinapotukabili na kuona wengine wana ujuzi nazo na wanaweza kuzikabili kuliko sisi tunavyoweza kuzikabili, nyakati zingine tumedhani maumbile yetu yamesababisha tupate shida tulizo nazo, wengine wanadhani wangekuwa na maumbile kama akina fulani leo hii wangekuwa wako mbali, wengine wanalaumu rangi walizonazo na kuona Mungu alikosea, wengine wanalaumu ukoo walio zaliwa wengine wanalaumu elimu walizozipata na kuzikosa na kudhani kama wangekuwa kama fulani basi shida zao zingetatulika kirahisi sana sana. Kuna siku Niliwahi andika laiti kama Mioyo ingekuwa ya Vioo gonga hapa usome...http://samsasali.blogspot.com/2011/07/papaa-on-tuesdaylaiti-kama-mioyo.html kuwa wengine wamenyamaza unadhani wao ni wajuzi wa shida walizonazo na wao hawana shida kuliko wewe. Shida haina mwenyewe wla shida haina Mjuzi.
Kuna nyakati zingine tumepata shida tuka waeleza watu badala ya kutusaidia ndio wakatukatisha tamaa kabisa, kuna nyakati tuliwaeleza watu shida zetu zikageuka kuwa matangazo kwenye jamii changamoto inayotukabili kizazi chetu nani yuko tayari kukabiliana na shida??hiki kizazi ambacho swali likiwa gumu mtu anaandika google, Kizazi ambacho level ya Uvumilivu na Kustahimili kinazidi kushuka, Kizazi ambacho watu wako tayari kuuwa wapate fedha, Kizazi ambacho mtu yuko tayari kufanya harusi ya mamilioni keshokutwa akamuacha Mkewe, Kizazi ambacho mtu anakaa na relationship miaka 8 kisha anamuacha mtu kwa sababu amepata mwenye fedha, Kizazi ambacho kwa sababu ya Njaa watu wamekuwa tayari kuuza miili yao kwa ushoga na uchangudoa ili kukabiliana na njaa, Kizazi ambacho Wanafunzi wanataka kuishi sawa na Wafanyabiashara kizazi kinachopenda 'Soft Touch and Appear". Nani yuko tayari Kukaa  kwenye ndoa ambayo hawana mtoto kwa miaka kadhaa, nani yuko tayari asisaliti imani yake ili mradi apitie jambo fulani.
Kila mtu ana shida na changamoto zake shida haina mjuzi wala mwenyewe unaweza ukawa na Kila kItu kwenye maisha ukawa na fedha ukawa na gari ukawa na mavazi mazuri na mke ama mume mzuri lakini hakuna amani ndani ya ndoa, unaweza kuwa na mshahara mzuri na nyumba nzuri lakini hauna inner satisfaction, inawezekana ukawa unafanya biashara unapata fedha kila siku lakini una ugonjwa unaokutesa, unaweza kuwa na elimu nzuri sana na akili njema sana ajabu hupati Usingizi na unakunywa mpaka madawa na sindano, yawezekana una umbile zuri sana na raha sana lakini ukiwa period mpaka hauoni thamani ya kuishi unatamani kufa, pengine una kila kitu unachodhani unapaswa kuwa nacho lakini unajiuliza kwanini wanaume wanakukimbia, asikuambie mtu shida haina mjuzi wala haina mwenyewe. Kuna mambo kadha wa kadha ambayo kwa watu wasiotujua kwa vile tumeamua kuyaficha tunaonekana tuko pouwa sana lakini kama leo ingekuwa kila mtu shida yake inaonekana Live Live kama CCTV ndipo ungejua kuwa shida haina mwenyewe wala haina mjuzi maana wewe unaloliweza mwingine linamshinda lile linalokushinda yeye analiweza unatamani mbadilishane lakini sasa sio fungu lake wala lako la kugawa shida hizo.
Unafanya nini unapotokea unashida???Unaomba Mungu, Unalaumu waliopelekea shida??Unalaumu Background yako??Unalaumu mwenzi wako na kujiona wewe ni bora kuliko mwenzako, Unamlaumu Mwajiri wako??Think Positive. Jijengee tabia ya Kukabiliana na Changamoto zinazokukabili wewe mwenyewe Kikamilifu chukua wajibu wa Kutafuta Ufumbuzi wewe mwenyewe pasipo kulaumu wengine, jione wewe pia ni sehemu ya tatizo na unapaswa kutafuta ufumbuzi kwa namna moja ama nyingine. Kuna Ujinga mmoja nimeuona kwenye maisha ya Usuluhishi tangu nilipopata neema ya kusuluhisha baadhi ya migogoro ya watu. Nakumbuka kulikuwa na ndoa moja ina misukosuko sana, mkaka ambaye ni mume kupitia Papaa On Tuesday ninazoziandika aliamini kabisa moyoni mwake kuwa akiongea na mimi suluhu itapatikana, simfahamu wala hanifahamu ila alijenga imani, nilipoongea nae akaniaelezaaaaa nikasikiliza nikaona kweli ni tatizo nikaomba nionane na mke wake nae nilipokutana nae akanielezaaaaa mwisho nikabaini shida iko wapi tukatengeneza appointment ya wote wawili, nikamwomba sana Mungu anipe mpenyo wa suluhu katika jambo hilo la wanandoa. Siku tuliyokutana kila mtu alielezaaaaaaaaa yaani kila mtua alifunguka ki hasa kisha tukauliza OK tumeshasikia What Next???Kila Mtu akaona kosa lake wakaombana msamaha yakaisha Ujinga niliokuja ubaini ni kwamba Mambo ambayo mngekaaa wenyewe nyumbani na kuongea na kufunguka eti mnahitaji awepo mtu Neutral ambaye yeye infact atakayoyaongea ninyi wenyewe ndo watekelezaji wa jambo hilo ambalo. Huwa ninajiuliza hivi Mshauri wa mambo nae yakimsibu ya Kumsibu anaendaga wapi??Ok labda niseme mimi yakinisibu huwa ninaenda wapi, na huko ninakoendaga nae yakimsibu ya Kumsibu anaendaga wapi???Shida haina mwenyewe.

Niliwahi kusema Ukizimia siku ya Taabu Nguvu zako ni Chache... http://samsasali.blogspot.com/2010/07/papaa-on-tuesdayukizimia-siku-ya-tabu.html.

Ze Blogger
0713494110