CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797

CHOOSE TO ADVERTISE WITH US.....+255 713 883 797
YES!!! SEPTEMBER IS JUST HERE!!!...THE NEW TERM IS ABOUT TO BEGIN.....YOU ARE ENCOURAGED TO BRING YOUR CHILD BEFORE THE CLOSURE OF REGISTRATION!!!....HOTLINE +255 716 230441

UNAFIKI ULIOJIFICHA NYUMA NA MANENO YA MARAFIKI... "TUKO PAMOJA SANA"!!!





SALAM KWA WOTE!
Na amini watu wote tuko vizuri na bado tunakazana kuzifikia ndoto za maisha yetu!
Leo nimesukumwa kuzungumzia jambo moja hapa ambalo naona likiachwa hivyo litakuwa tatizo,tena tatizo kubwa.

UTANGULIZI;
Katika haya maisha hakuna mtu anaweza kuishi peke yake, sio tu kwa maana ya mwenza wa maisha ila namaanisha bila mtu mwingine yeyete, maana huwezi kuwa kila kitu na huwezi kufanya kila kitu mwenyewe kihusuyo maisha yako...una ndoto yako ya kumiliki Chuo kikuu ni sawa, lakini kuliweka hilo wazo kwenye maandishi ya kusomeka unahitaji watalaamu wa kuandika, kabla hujaanza kufanya lolote, unatakiwa upate mwongozo kwa wale waliotangulia na hapo unahitaji watu wengine.....kwa ufupi kila hatua utakayopiga utawahitaji watu,aitha kwa kuwaomba au kuwaajiri kwa maana ya kuwapa kazi na kuwalipa. hata ukitaka tu kutoka kwenda mjini lazima uhitaji dereva na konda na hata kama una gari binafsi kuna saa utamuhitaji muuzaji wa mafuta....KIMSINGI "KUISHI" NI KURAHISISHIANA MAJUKUMU KWA KILA MMOJA WETU KWA FAIDA YA KILA MMOJA WETU!.
Kwa msingi huo nataka utambue kuwa UNAHITAJIKA KUWASAIDIA WENGINE kama vile ambavyo na wewe UTAWAHITAJI WENGINE KUKUSAIDIA kufikia ndoto za maisha yako!

DHANA YA MAISHA;
Katika maisha yetu hakuna hata mmoja wetu ambaye yuko sawa na mwengine kwa maana ya makusudi ya kuishi kwake, kila mmoja alizaliwa peke yake (hata mapacha kila mmoja alitoka kwa wakati wake); kwa staili yake na hata sasa kila mmoja ana ndoto zake na anaishi maisha yake. Ukilitambua hili hutamuonea wivu mwenzako katika moja ya ndoto zake,ila na wewe utatia bidii katika za kwako ila ikifika saa ya kusema ama kuonyesha ni kwa kiasi gani amesonga na ndoto zake na wewe utakuwa na ya kwako ya kusema. Ubaya ni kwamba watu wengi hawajitambui, kwa hiyo wanafanya maisha yanakuwa magumu sana huku duniani,maana mtu mmoja anataka kufanya kila kitu na kwasababu anabahatisha katika kila, basi atakuwa anajitahidi kumkwamisha kila anayejaribu au kufanya kama yeye!


UNAFIKI NISIOUPENDA.....
Kama umejitambua na unajiheshimu ni wazi kuwa na watu wanatambua hilo na sawasawa na kujiheshimu kwako ndio na watu wanavyokuheshimu. Ukiona mtu amekufuata na kukuuliza jambo lolote lile aitha anataka kulifahamu ama anataka ushauri wako au zaidi anaomba ushiriki wako....basi imekupasa kwanza kumshukuru sana Mungu kwa nafasi hiyo, hata kama hutafanya lolote katika haya anayoweza kuwa anayahitaji....nasemma hivyo ili ujue yafuatayo;

KWANZA UMETAMBULIWA KUWA UNAWEZA KUWA MSAADA KATIKA HILO.
PILI UMEHESHIMIWA SANA, MAANA WAKO WENGI LAKINI UMEONEKANA WEWE
TATU ULICHONACHO NDIO KAZI YAKE HASWA,MAANA TUMEPEWA ILI KUFAIDIANA.

Sasa kama ni hivyo basi ukipata nafasi hiyo mshukuru Mungu na baada ya hapo Omba hekima ya namna ya kujihusisha na jambo hilo na kama unaona huwezi kuhusika kabisa unaweza kumjibu kwa hekima SAMAHANI MIMI SITAWEZA, na yamkini ni vizuri hata ukimwelekeza kwa mtu mwingine unayeona anaweza kuwa na msaada!

Sasa usije ukadhani kwasababu una elimu ya juu sana au una umaarufu mkubwa au una kipaji sana au ni kiongozi maarufu au pesa kuliko wengine, ndio maana ukafuatwa wewe HAPANA!!
jIFUNZE Kuwaheshimu na kuwakubali wengine katika yote wanayofanya yanayostahili heshima....na mara zote HEKIMA NA MAWAZO MAZURI hutokana na watu tusiowadhania!

SASA SIKU HIZI KUNA NAMNA WATU HUKWEPA MAJUKUMU NA KUDANGANYA KWA NJIA YA MZUNGUKO, MTU ANAOMBWA JAMBO AU ANASHIRIKISHWA AU ANAALIKWA SEHEMU FULANI....HALI AKIJUA HANA NIA WALA MPANGO MOYONI AU NAFSINI MWAKE KWA KUSHIRIKI AU KUSHIRIKIANA....ANAISHIA KUTOA MATUMAINI FEKI ATI....."TUKO PAMOJA" AU "HAMNA NENO MTU WANGU" na hapo unamuaacha huyo ndugu akiwa na matumaini makubwa na ikifika saa ya jambo lenyewe usitokee kabisaaaa!!


Sasa ninafikiri ni wakati mzuri wa kujirekebisha sasa, kama huna nafasi au huwezi kumsaidia mtu kwa namna yeyete ile wewe sema tu....SAMAHANI NDUGU KWA HILI SITAWEZA!
Naamini hii itakusaidia pia kuwa HURU na kuwa MKWELI!

HIYO TABIA YA KUMWAMBIA MTU TUKO PAMOJA NA KISHA NYUMA YAKE UNAMNG'ONGA SIO HATA KIDOGO....TUJIREKEBISHE!!!

Ukiona inakufaa unaweza kuendelea nayo lakini kuna wakati itakugharimu tena sana, maana watu huwa wanaambiana yote yanayokuhusu na kama ni mambo ya kukalaisha basi ndio habari husambaa zaidi kuliko hata nzuri!

MFANO HAI;
Kuna mtu mmoja mahali fulani alikuwa anajifanya yuko bize kuliko hata ubize wenyewe, basi hata akiletewa kadi za michango ya harusi au shughuli mbalimbali alikuwa akijibu aaah tuko pamoja aisee....basi zingine anachangia na zingine hakuchangia na hata zile alizochangia nyingi hakuwa anahudhuria....naam hata ikitokea misiba jirani alikuwa anatuma rambirambi na kusema aaah jamani tuko pamoja kisha anaondoka....basi watu walimvumilia sana na hakuna nafasi watu walipata wasaa wa kumsema zaidi ya marafiki mmoja mmoja ambao aliwachukulia poa na kusema...aaah nimewaelewa jamani....tuko pamoja sana!
Basi ilitokea siku mmoja siku moja alipata msiba wa Baba yake mzazi ambaye alikuwa anaugulia kwake, watu walipata taarifa za msiba na wengi wao wakasema hapa ndio mahali pa kumuonyesha UPAMOJA WETU....basi wengi walifika na kutoa pole na kuacha rambirambi (tena nyingi kuliko kawaida) na wao walisema tuko pamoja katika majonzi haya na kuondoka zao....basi kwa kadri muda ulivyokuwa unakwenda alikuwa akipokea rambirambi na pole za watu wanaokuja na kuondoka kama vile ile ni shule ya kutwa ama kituo cha kupigia kura....basi pale msibani palikuwa doro kabisa na hapo ndio akaanza kuona kimbembe cha "TUKO PAMOJA"....basi msiba ulikaa siku ya kwanza yote hamna kitu,basi akawachukua vijana ili awalipe na wakachimbe kaburi, na wao walichukua pesa na wakamwambia tuko pamoja na wao wakaenda makaburini na kuanza kupiga stori, mpaka siku ya pili inaisha baada ya kufoka sana ndio wakachimba tena refu kupita kawaida...naam siku ya tatu ndio ya mazishi hakuna hata mmoja anajigusa kwenda, na hapo alienda kwa kiongozi wa mtaa na kumuomba awaite watu, naam watu walikuja na wakaenda mpaka makaburini kimyakimya,hakuna mtu kulia wala kuzungumza na walipofika pale....watu walimtolea madukuduku yao yooote na wakasema ili iwe fundisho kwa wengine,kabla ya kuzika....ALALE JUU YA UDONGO ULE WA KABURI PALE JUU,NA HAPO AKACHARAZWA BAKORA ZA KUTOSHA MBELE YA MKWEWE,WATOTO NA NDUGU ZAKE NA ndipo ibaada ya maziko ikaanza na kila hatua ya kuzika alipaswa kushiriki ili ajue huwa inakuwaje....alisaidia kushusha jeneza chini na kabla mtu yeyeote hajagusa chepeo,alianza yeye kufukua mpaka alipochoka hoi ndio wakamsaidia,na hilo lokawa fundisho kwake na kwa wengine wote mtaani kuwa pesa sio kila kitu,ila unahitajika wewe!!!


ACHANA KABISA NA HUO UNAFIKI WA KUSEMA TUKO PAMOJA HALI HUNA HATA KIMOJA KINACHODHIHIRISHA UPAMOJA HUO!!!
(Watu wawili hawezi kwenda njia moja isipokuwa wamepatana.....hivyo hamna Upamoja wa maneno bila matendo na mapatano)

AHSANTE SANA, UBARIKIWE SANA KAMA UMENIELEWA!!!

Fredy Erasto Chavala
<King Chavala(MC)>
+255 713 883 797
facebook; King Chavala MC
Twitter @kingchavala

CHRIS MAUKI LIVE IN INTELLECTUAL MEETING AT VCCT ON 4TH AUGUST 2013!!!

............We all desire to move from the ground we are standing now to the higher ground we've been dreaming about. But the going is never easy, thats why you need to equip yourself everyday with new informations and skills... Yesterdays intelligency can not solve todays challenges... On that groud Chriss Mauki (A psychologist and Lecture from University of Dar-es-Salaam will be sharing on a topic SETTING GROUND FOR YOUR TAKE OFF at VCCT Tarbenacle this coming Sunday from 1630hrs.You will have a great time to exchange Ideas and Network with other professionals.. CEOs, Managers, Business people etc.. Please Plan not to miss, u will never be the Same.
 "BY PROSPER MWAKITALIMA"
 
FOR MORE INFORMATION,PLEASE DIAL 0713 905118
 
 KARIBUNI SANA NYOTE!!! 

Papaa On Tuesday.....Wengi tu Waathirika Wa Makovu Yasiyokuwa na Hisia!!


Nimatumaini yangu ya kuwa sote tu wazima wa afya njema na tunaendelea na ujenzi wa taifa letu .

Mabaka Yasiyokuwa na Hisia ana Makovu yanayotokea bila mwanadamu mwenye  kuwa na uelewa kuwa kuna kitu kinaendelea kwenye mwili wake, hali hii  hupelekea mtu kutibu matokeo ya ugonjwa na sio ugonjwa wenyewe. Kati ya dalili nyingi za wagonjwa wa ukoma ni waathirika kupata madhara pasipo wao kuwa na taarifa (sense) katika miili yao. Wagonjwa wengi hata wale wa Saratani Ya Ngozi hukuta tu wana mabaka ama makovu kwenye miili yao ambayo yametokea pasipo wao ku-sense kama kuna mabadiliko katika miili yao. Nilipokuwa Mbeya wakati fulani Pastor Matthew Sasali (Mdogo wangu) alinikumbusha  kuwa dhambi kwenye maisha ya mwanadamu ni kama makovu yasiyo na hisia, huanza pole pole mwisho wake ni kama ambavyo inaelezwa Mshahara wa dhambi ni Mauti.

Kila mtu kwa nafasi yake anaweza kuitazama Jamii ya leo na kuona, mambo mengi yanayotokea sasa yalianza pole pole na kudhaniwa kuwa hayatakuwa na madhara makubwa kwenye Jamii lakini kwa sasa matatizo hayo yamekuwa sugu vya kuchosha. Issue za ufisadi zilianza pole pole kwenye Jamii yetu, leo hii kwenye Jamii si ajabu mwovu anakumbatiwa na mwema anachukiwa, ukionekana unaikosoa Serikali unaambiwa unahatarisha amani ya nchi. Leo hii watoto wanadiriki kuwapeleka wazazi wao mahakamani, leo hii idadi ya mashoga inaongezeka kwa kasi lakini kuna siku hali haitakuwa hivi sababu ni kama Jamii imekufa ganzi. Watu wanaokamatwa na madawa ya Kulevya kila siku wanakuwa wengi lakini mwisho wa siku tunazoea tu

Zamani idadi ya wana cheat kwenye mahusiano ilikuwa ni ndogo sana na hata kama mtu alikuwa anatoka nje ya ndoa ilikuwa ni Siri sana lakini siku hizi yaani inajulikana kabisa ni nyumba ndogo, sio sasa wanandoa kuaminiana, hali ngumu ya maisha na kupenda mafanikio ya haraka hataka  yamepelekea wanandoa wengi kusaliti ndoa zao, waume za watu hawaaminiki, wake za watu mule mule, enzi hizo watu walikuwa wanaugopa Mungu kwa sana si makanisani si misikitini, siku hizi kuna mambo yanatokea na watu kama wanayapotezea lakini mwisho wa siku yatatengeneza maumivu na mateso katika maisha na kutunyima furaha.

Angela (sio jina kweli) niliwahi kukutana nae katika mojawapo ya mizunguko yangu katika mashule na vyuo. Mdada huyu alikuwa ni kidato cha 6, baada ya mimi kufundisha mambo kadha wa kadha ya maisha, dada huyu aliniomba tuzungumze maana alikuwa anahitaji msaada. Katika maongezi yake alinieleza kuwa alianza kuingiliwa kinyume cha maumbile akiwa kidato cha kwanza, kwa wakati huo akiwa kidato cha sita alikuwa si kwamba si tu anapenda mchezo huo bali amekubuhu, hajisikii raha kufanya mapenzi kwa njia ya kawaida isipokuwa mpaka ameingiliwa kinyume cha maumbile. Na si kwamba anapenda hiyo hali amejitahidi mbinu mbalimbali za kukataa hiyo tabia ila alieleza huwa inaondoka na kurudi. Nilipomdadisi ilikuaje mpaka akaingia katika huo mchezo alieleza boyfriend wake waliyeachana ndiye aliyemfundisha na kumzoesha, alijua ni kitu cha kawaida na kinaweza kuepukika lakini si hivyo. Unafanyaje pale mume wako wa ndoa ama mchumba wako akataka kukuingilia kinyume cha maumbile, umewahi sikia habari hii mara ngapi lakini ni kama watu wanaipotezea, hili ni kovu linalotokea bila kusikia maumivu ya kidonda. Na mwisho wa siku tutakuwa tumesharudi katika enzi za Sodoma na Gomora

Leo hii umesikia mara ngapi matamko mbalimbali ya kidini yakitolewa kila mmoja akimtishia mwingine, lakini hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa kukomesha hali hiyo. Inawezekana hisia za kuhisi madhara yake kwenye Serikali yetu zimekufa lakini kidonda hiki kina madhara makubwa hapo baadae zaidi ya madhara ya ugonjwa wa Saratani. Kuna siku raia watajitoa mhanga ndipo tutashuhudia kitu ambacho leo tunakidharau, watu wanapigwa mabomu, watu wanapigwa risasi, risasi inaua, kuna siku watu watachoka kukaa hai kufa kwao si tatizo sana, kwa kusema hivi lazima Jamii ianze kutazama huu mwamko wa Kijamii kwa sasa na kila mtu kudai haki yake kwa mabavu hata pale palipohitaji subira na busara tutafika wapi?hii hali tusipoiona kuna siku yataibuka mambo.

Leo hii kuna matatizo ambayo pengine yalianza zamani na kudhaniwa kuwa ni madogo, wanaume wengi wanaoangalia pornography hawakuanza jana, ni kitu ambacho wengine kimeshajengeka kwao, kuna wanaume wao kujichua  ni kama wameshikiwa risasi kuwa wasipofanya watakufa. Wengine ni wafanyakazi na vyeo vyao lakini sasa wanateseka na tabia hiyo wengi wao hawapendi kufanya hayo lakini wakati wanaanza walidhani ni kitu kidogo ambacho hakiwezi kuathiri maisha yao. Wengine mpaka kwenye ndoa hawasikii raha bila ya kujichua wao wenyewe. Haya ni Mabaka tuliyoyadharau kwa kudhani hayana madhara leo hii yameacha alama zisizofutika kwenye tabia zetu.

Tabia zetu wakati mwingine zimekuwa ni tatizo la kudumu, wengine wetu uaminifu sasa imeanza kuwa issue, maana kuna wengine walianza tu polepole kwa ahali ilivyo sasa sio kwamba hawataki kuwa waaminifu, No wanapenda sana kuwa waaminifu issue inakuja tu kuwa wameshaathirika na kutokuwa waaminifu, kwa kuupuuzia kwao mambo madogo madogo wamejikuta wamepoteza opportunities nyingi sana kwenye maisha yaoWatu wanatamani kukuamini lakini tabia huwa zina athiri sana maisha yetu ya kila siku. Ndoa zetu zimeathirika na tabia zetu kazi zetu zimeathirika na tabia zetu, mahusiano yetu na Mungu yanasua sua kutokana na tabia zetu. Can Something good come out of you?


Asilimia kubwa ya Vijana wa Sasa wamesha experience maumivu kwenye mioyo yao juu ya mahusiano. Siku moja tukiwa kwenye Conversation kali kwenye Facebook Wall yangu, mmoja wa Marafaki zangu aliongea akisema kwa namna moja ama nyingine suala hili la kuumizana linatokana na Wanaume kutokuwa na Msimamo katika kile wanachokitaka. Kuto kuwa na Msimamo ni Matokeo ya kitu ambacho kinaendelea kwenye Jamii, kwanini watu hawana misimamo katika kusema sitaki A nataka B, Wadada wengi wamejikuta wakitupia wakaka lawama kwa kuwauzisha Sura mwisho wa siku inakula kwa Mdada. Kizazi hiki kinaona ndoa ni jambo la fahari kuliko jambo la fungamano ndo maana unakuta ndoa ilifungwa kwa mamilioni ya fedha baada ya mwaka watu wanataka kutoka, nani alaumiwe. Mioyo ya wengi imeshajeruhiwa na kubutuliwa kama kombolela hakuna tena penye sehemu ya kupenda. Ukitaka kujua una kovu lisilokuwa na hisia ni pale unapopata mpenzi mpya halafu ukabaini ameanza tabia kama za yule aliyekimbia kuna kitu kunaingia ndani yako ghafla si unajua uking'atwa na nyoka??? 

Wengine wamekuwa wakihangaika na matumizi mabaya ya fedha kiasi kwamba wanajitahidi kujidhibiti wanashindwa, kosa alilofanya mwezi uliopita amejikuta na mwezi huu amelifanya, wengine wamejitahidi kuacha matumizi ya hovyo lakini imeshindikana kilichotokea wamekubali kuwa hawawezi kubadilika, ilipoanza ni kama haikuwa na madhara lakini wengine sasa its too mucha na still hawaoni kama watasaidika katika hilo, wamekubali matokeo. Wengine tabia za kuzira, ajabu unakuta mtu mkubwa kabisa eti anazira, lakini hakuanza leo tabia hii imekuwa polepole bila ya watu wenyewe kujijua imejijenga ndani yao. Wengine ni hofu, wamejawa na hofu mpaka unnecessary. Kuna rafiki yangu yeye kila kitu anaogopa hasa inapofika suala la ndoa yale aliyoyasikia kutoka kwa watu na aliyoyapitia yamemjaza hofu kuwa katika dunia hii kama kuna mwanaume ambaye yupo kabisa hawezi cheat na akabaki kuwa mwaminifu kwake peke yake. Hofu anabadili namna ya kutazama mambo, hofu inamadili namna ya kuishi na kuongea na kuamua mambo mengi, hofu ikikujaa unaweza ukaufunga hata uwezo wako wa kuwaza na kupambanua mambo, hofu inatawala.

Inawezekana kuna jambo ulishawahi dhani umelisamehe na kuliachilia lakini kila lile jambo linapotajwa kuna mkwaruzo ndani ya moyo wako hutokea, kama umewahi umizwa na mapenzi ukiwasikia watu wanaongelea mapenzi unatamani usimkumbuke mtu aliyekutenda, ikitokea umemuona njiani anakuja unatamani kubadilisha njia, yamkini uliwahi dhurumiwa ama pata hasara ya biashara yale maumivu bado yameganda kwenye nafsi, inawezekana ni ofisi waliyokufukuza sometimes back ukisikia jina la ofisi moyo unakuuma. Makovu haya ya nafsi hu-develop tabia ambayo yamkini hukuwa nayo hapo awali. Umejengeka na kuto samahe, umejengeka kuwa na tahadhari nyingi zaidi, Umejengeka kuto amini amini mwenzi wako akishika tu simu unajua anachat na wanawake wake unatamani kumwamini lakini nafsi yako imesha develop tabia iliyotengenezwa kutokana na jeraha. Ukimsikia mtu anasema "wanaume wenyewe wote vimeo" jua ana jeraha ama ukisikia mtu anasema "wanawake wote wanafanana" jua ana jeraha lake la kwenye nafsi kila mtu amejawa na hofu ya kuogopa kutoneshwa jeraha la nafsi alilowahi kupitia hapo kabla.

Wengi tunateseka si kwa sababu tunataka kuteseka, hofu zinatawala maisha yetu, kujilaumu kumekuwa ni sehemu ya maisha yetu,kutokuamini wengine imekuwa ni sehemu yetu. Wengine wanafanya biashara wakiwa wameshajiandaa kupata hasara, wengine wameingia katika ndoa wakiwa wamejiandaa kusalitiwa, wengine wameingia katika ajira wakiwa tayari kuiba. Mabaka yasiyo na hisia yamekuwa kiasi kwamba tuko tayari kuumia au kuumizwa hata kuumiza kila mtu yulo tayari kwa lolote ovu kutokea kuliko wema. Haya mambo yalianza polepole katika maisha na jamii yetu sasa yameshatuathiri. Unayosikia leo Tunisia au Misri hayakuanza tu ghafla ila yalianza polepole.

Hakuna mtu anayekufahamu vizuri kuliko wewe mwenyewe unavyojifahamu ipo haja ya kujichunguza na kubadilika kabla mwaka haujafika mbali.

…//Papaa
0713 494110
samuel_sasali@yahoo.com

MWISHO WA SEPTEMBER NDIO MWISHO WA KUTOA MICHANGO KWA SAMUEL SASALI!!!

Hello habari zenu!
Natumai nyote mko vizuri mnaposoma habari hii!!
Naamini habari ya habari za Useja wa Papaa ziliwasikitisha sana na mlitamani mseme ila hamkuweza, naam maombi yenu Mungu akajibu na akampata Mchumba, ndio ni mchumba mkubwa tu wa kutosha Kitanda ,dressing table na kabati na bado sehemu ya kutembea inabaki.
Mlipozidisha maombi macho yake yakafungukia paleeeeee HKMU Mikocheni, naamini wengi habari ziliwafikia na hata kwasababu ya ufukunyuku wengine mkajua hata kabla yeye mwenyewe hajajua.

Alifuata taratibu zote za kijamii na kifamilia,Mali akalipa (Kama anadaiwa atamalizia mwenyewe) na shughuli za kuthibitisha kuwa yuko serious zilifanyika nyumbani kwa binti na baadae kanisani kwa kumvisha pete ya thamani sana, ndio kwasababu anampenda sana.

Ahsante kwa kushiriki hayo yoooote yaliyopita kwa maneno na simulizi......sasa ni wakati wako wa kushiriki kikamilifu tena kwa hali na mali.
 
Tarehe ya Harusi imeshatangazwa, 26th October 2013 pale Victory Christian Centre Tabernacle (VCCT) pale Mbezi beach A kwa Dr.Huruma Nkone na baadae taafrija kufanyika katika bustani kubwa ya pale Lamada Hotel,Ilala-boma saa moja mpaka tano usiku.

Yawezekana wewe ni rafiki,jirani,shabiki,msomaji wa blog, ndugu, mwanahabari mwenzie, labda mnoni mwenzie au mtoto wa mchungaji mwenzie au unasali pamoja nae,au mmewahi kupiga picha pamoja au umewahi kumwona na kumfurahia hata mara moja tu au basi ni rafiki yako katika mitandao ya kijamii au humjui kabisa ndio unamjua leo....ni sawa tu anaitwa Samwel Sasali,Papaa,The Blogger....basi hii ni nafasi yako kushiriki shangwe hii sambamba na marafiki wote wa muhimu hapa mjini kama vile Wachungaji,Wafanyabiashara,Wanasiasa,waimbaji,wanafunzi na wengine kadha wa kadha bila kumsahau Askofu Mkuu wa TAG,Dr Barnabas Mtokambali na burudani live itaendeshwa na John Lissu na bendi yake.

Nafasi ni chache sana ukilinganisha na Uwingi wa matafiki wa kijana huyu, hivyo nakushauri uchukue kadi yako mapema na uchangie kabla ya Septemba 30, maana baada ya hapo hata kama utakuwa na hela nyingi mkononi utakosa kadi.

Naomba kusisitiza tena na tena kama rafiki, kama pacha wake na kama mwanakamati kuwa NI MUHIMU KUSHIRIKIANA NA MWENZETU, NI MUHIMU KUCHANGIA LAKINI KWA SABABU YA UWINGI WA MARAFIKI UKILINGANISHA NA IDADI TUNAYOITAKA,NAAMINI UTAZINGATIA KUCHANGIA MAPEMA NA KUPATA KADI YAKO.

Kadi zinapatikana kwa Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi,Bwana Noell Tenga, Bwana Harusi Mtarajiwa, Samuel Sasali, Renee Lyatuu,James Temu(Uncle jimmy) na Kwa King Chavala.

Hata kama siku hiyo haufikiri kuwepo harusini,haitakuwa vibaya kama ukichangia japo 50,000/=na kuendelea kwa kadri Mungu alivyokubariki.
Kwa Bloggers na wanahabari msiache kunitafuta maana nina kadi zenu!!

KUMBUKA;
Ni hao tu niliowataja ndio watakupa kadi na sio mwingeyo, Tunatamani chango wako usiwe chini ya 50,000 ili tuweze kufanikisha shughuli ya mwenzetu!!

Kwa Mawasiliano zaidi;
Samuel Sasali 0713 494110/0686 255 269
Happy Lwendo; 0717 149085
Noell Tanga; 0713 261425

IMETOLEWA NA KING CHAVALA KWA NIABA YA KAMATI NA CHINI YA UDHAMINI MKUBWA WA CHAVALA IDEAS PLATFORM.

ZOOMING ZONE 0004.......Na PROSPER A. MWAKITALIMA, The T-shirt Printer tycoon!!!



HELLO HABARI!
NAAMINI MKO POA NA MNAENDELEA VIZURI, NILIKUWA KIMYA KWA MUDA NA HII NI KWASABABU ZOOMING ZONE SIO MAKALA YA KILA SIKU AMA KILA MTU, HIVYO LEO LENZI IMEMULIKA KIJANA MMOJA HAPA MJINI NA HUYU NDIO ATAKUWA……Zooming Zone 004
************************************************************************************               
Zooming Zone 0004....Na Prosper A.Mwakitalima
Huyu sio mwingine basi ni kijana mjasiriamali “SWAHIBA” anayetamba na kujulikana sana kwa KUCHAPISHA T-SHRTS vizuri, nzuri na zenye maneno mazuri hapa Mjini, Tanzania.
Naam pia ndio huyu ambaye habari zake zilivuma sana hapa mjini kwa kupona“kufufuka” toka katika ajali mbaya sana sana pale maeneo ya River side Ubungo  23/11/2011 iliyohusisha lori la mafuta na gari yake ndogo,ajali ambayo ilichukua maisha ya watu kadhaa akiwemo mama mmoja mjamzito ambaye alikatika kichwa(ilitisha sana kwa kweli)….lakini Jambo la kushangaza ni kuwa kijana huyu alipona kabisa maana hakuvunjika mfupa wala mshipa Zaidi ya michubuko kadhaa tu,hakuna aliyeamini hata leo lakini huo ndio ukweli!
Huwezi kuamini lakini huu ndio ukweli!

Huyu pia ni mmoja wa washika dau na wawezeshaji wa Mtoko wa marafiki Mjini uitwao “FRIENDS ON FRIDAY (FoF)”, na ndio mbeba maono na mkurugenzi wa “SIFA TANZANIA”Mfululizo wa matamasha ya kumwinua Yesu hapa nchini Tanzania.
Huyu ni PROSPER ALFRED MWAKITALIMA a.k.a SWAHIBA a.k.a “The Next Billionaire” (King Chavala tu anaruhusiwa kumwita “MY PS”)
 
Prosper,Wambura na Chavala Singida
NILIBAHATIKA KUFANYA NAE MAHOJIANO HIVI KARIBUNI KWA KINA NA NIKAPATA MENGI SANA NA HAYA NI MACHACHE KATIKA MENGI, AMBAYO NAAMINI YANAWEZA KUKUSAIDIA KUMFAHAMU VIZURI NA YAMKINI KUJIFUNZA MENGI KUTOKA KWAKE, HUYU NI KIJANA WA KIPEKEE AMBAYE NI MFANO WA KUIGWA NA VIJANA WA KITANZANIA…..FUATANA NAMI KATIKA MAELEZO YANGU KUHUSU 

Papaa On Tuesday....Wakati Wa Jambo Ukipita, Itakusumbua..Kila Jambo na Wakati Wake!

Nina Kila Sababu Ya Kumshukuru Mungu aliyetupa nafasi hii ya leo Kwa ajili ya kuweza kulitimiza tena Kusudi la kuumbwa kwetu na kuwepo duniani.

Papaa On Tuesday ya leo ni Tafakari ya rafiki yangu wa Siku Nyingi Mussa Billegeya ambaye ni Mbunge Mtarajiwa wa Jimbo moja miaka michache ijayo katika Kanda Ya Ziwa. Tafarakari hii aliitoa katika forum ya Marafiki Huru.

Kuna Msemo wa Kibiblia usemao kila jambo lina wakati wake, Naamini huu msemo huwa uko sahihi kabisa. Lakini kifalsafa, Wanadamu huwa tunafarijiana kwamba Ukiwa Hai Bado, It's Never Too Late!

Hivi Majuzi rafiki yangu Mussa akiwa Ofisini pale MANCON na Mkurugenzi Prosper Mwakitalima, wakiwa wanazungumza mambo mbali mbali ya maisha ikafika time ya kuongelea suala moja linahusiana na Kuoa. Prosper aligusia huo msemo, na kueleza kwamba hata kuoa huwa kuna wakati wake, na mtu asipooa wakati wake wa kuoa unapofika, inaweza ikamsumbua kuja kuoa baadaye - hata kama atakuwa anataka!

Juu ya Msemo huo ninajenga Papaa On Tuesday ya leo!
Ni kweli kabisa kwamba kila jambo lina wakati wake, NA KILA WAKATI KATIKA MAISHA UNA JAMBO LAKE! Tangu utoto hadi uzee. Ni muhimu sana kuelewa jambo la kila Wakati (na sio tu wakati wa kila jambo)!

Kuna namna nyingi sana za kutambua wakati wa jambo unapofika, na mara nyingi, watu wengi, huwa tunakuwa na bahati ya kufahamu kwamba wakati wa jambo fulani maishani mwangu umewadia, au basi, huwa tunaweza kufahamu kwamba Jambo la Wakati Huu ni hili! Kwa bahati mbaya sana, watu wengi huwa tunaona kama vile linalowezekana leo hata kesho litawezekana - KOSA!


Wakati wa jambo unapowadia, huambatana na mambo mengi ikiwa ni pamoja na Nguvu ya Kulitekeleza, Hamu ya Kulitekeleza, Msukumo wa Kulitekeleza, Akili ya Kulitekeleza, Mafunuo ya Kulitekeleza, Faida za Kulitekeleza, Watu wa Kukusaidia kulitekeleza, Kibali cha Kulitekeleza... n.k n.k. Hali hii hujitokeza kwa jambo lolote katika maisha pale wakati wake unapofika - liwe ni wazo la kusoma, biashara, huduma, kuoa/kuolewa n.k.

Ni Sawa sawa na Mwanamke Mjamzito unapofika wakati wa kujifungua haijalishi alikuwa anaenda salon, ama anaenda Kanisani Wakati Wa Kujifungua ukifika kuanzia akili  na kila kiungo kinataarifa kuwa wakati wa ku-deliver umefika hata angekuwa anapenda chips mayai saa hizo hazina tena nafasi sababu wakati wa jambo kutokea umefika katika maisha.

Kwa Nini Watu Huzikosa Hizo Nyakati/Fursa?
Kama nilivoeleza hapo juu, watu wengi huwa wanapoona wakati huo umefika, huanguka katika mtego wa kudhani ni kawaida kwa huo wakati kufika, hivyo huo wakati hautaondoka mpaka WAO watakapofanya jambo husika.! Watu wengi huwa hawaelewi kwamba wakati wa kila jambo hupita ili kupisha wakati wa Jambo jingine! Linalowezekana leo, sio sahihi kudhani kwamba litawezekana HATA KESHO, Kesho inaweza kuwa ni wakati wa Jambo lingine!
Kwa watu wengi, pale wakati unapofika, huwa hawapendi kufanya haraka kulifanya jambo husika kwa sababu, wengi, huwa wanapenda kwanza KUU-ENJOY huo wakati ambao wanakuwa wanayaona mafanikio yao waziwazi vichwani na ndotoni mwao, hivyo hawaoni sababu ya kufanya haraka KUFANYA KWELI....

Ngoja-ngoja yao huendelea mpaka wakati wa jambo unapopita, huku wao wakiamini kwamba wakati huo hautaondoka KWA SABABU HAWAJAFANYA - KOSA!!!! Wakati huwa haumsubiri Mtu, Mtu anapaswa kwenda na Nyakati!

Ni kitu cha hatari kudhani kwamba kwa sababu leo unajisikia nguvu, msukumo, hamasa na una fursa ya kufanya jambo, ukadhani kwamba hali hiyo itaendelea siku zote - la, Hasha! "Kesho" unaweza ukaamka na ukashangaa ile nguvu, msukumo na hamasa uliyokuwa nayo jana imepotea ndani mwako, zaidi tu kwamba umebakia na kumbukumbu ya picha nzuri ya vile ambavyo hali ingekuwa iwapo ungelikuwa umechukua hatua na kufanya jamvo husika!
Nini Huwa Kinatokea Pale "Wakati Wako" wa Kufanya Jambo Unapokupita!

Kwa kawaida, mtu anapopitwa na wakati wake wa kufanya jambo hubaki na picha nzuri na "ladha" ya lile jambo ambayo aliipata wakati lilipomjia au wakati wake ulipokuwa umefika. Mtu hubaki akijifariji - nitafanya tu, nitafanya tu, kwa maana tayari nilishapata picha na mpango wa namna ya kufanya!!! Ndio maana kuna tahadhari kubwa sana ya Wadada ama Wakaka ambao wakati wa Kuoa ama kuolewa Ulipofika wakadhani bado wanamuda basi ule msukumo nao ukaisha ndio maana unaweza kuta mtu anabaki kusema tu enzi zangu ilikuwa a,b,c enzi zetu a,b,c ndio maana unakuta mtu ana kazi nzuri, ana mshahara mzuri ana maisha mazuri unashangaa kwanini huyu mtu hatafuti mwenza, kumbe ule msukumo wa kufanya ulishapita. Huwezi kuwa kijana siku zote wazazi wetu wengi wamebaki na story tu enzi zetu bana, enzi zetu bana basi na huo wakati nasi utatukuta ambapo watoto wetu watashangaa kwanini hatukununua viwanja kwa ajili ya miaka 10 ama 20 ijayo, watasema baba au mama ulikuwa wapi wakati wenzako wananunua??kila siku tunasema tutafanya kesho ama mwezi ujao mwisho wa siku hatufanyi.
Lakini anapokuja kutaka kujaribu, hushangaa jinsi ambavyo jambo lile lile ambalo juzi alikuwa analiona rahisi sana, leo linaweza kuwa gumu mno, zito mno, lenye kukatisha tamaa na kuanza hata kushawishika kwamba yawezekana yale matokeo mazuri na faida aliyokuwa anaidhania juzi labda haikuwa sahihi au haikuwa kweli! Mtu huanza kujifariji "Labda zilikuwa ndoto tu za mchana" au kama sungura "Sizitaki Mbichi hizi" wakati akiwa anakata tamaa na hata kuamua kuliacha lile jambo kabisa!

Kama ni Biashara, mtu hushangaa vile inavyoweza kuwa ngumu, wakati mwingine akijihisi kwamba hana mawazo mazuri au uwezo wa kuifanya, japo ni majuzi tu alikuwa anaiona kwamba ndiyo inaweza "kumtoa" kimaisha! Kama ni Kuoa/Kuolewa, mtu huweza kushangaa ghafla akaanza kuona kama vile Hakuna Mtu Anayefaa Kumuoa, kama Vile yeye hajakakaa kikuoa-oa vile (au ki-kuolewa-olewa vile); Anazidi kuona kama vile Hakuna watu wenye Sifa za Kuwaoa au wa Kumuoa yeye n.k. Kumbe???/
Kwenye Biblia tunasoma habari ya Mtu mwenye Kupooza ambaye alikaa kwenye birika miaka na miaka na Kila Mara Malaika alikuwa anakuja kutibua maji ndani ya kisima hicho anayekuwa wa kwanza kuingia yeye anakuwa mzima. Swali la Kujiuliza huyu kilema aliyekaa zaidi ya miaka 30 pale pembeni ya birika kweli kabisa alikuwa serious kupona??au alikuwa ana enjoy kuwepo pale, sababu hata Yesu alipomuuliza Wataka kuwa mzima akaanza story nyingi kuwa hakuna wa kumsogeza hakuna wa Kumsaidia. Mara nyingi sana tumekuwa tukilaumu wengine ndio wametusababishia hali tuliyonayo kumbe wakati ulipokuwa umefika hatukuwa tayari kwenda na wakati huo. Kwenye Kiingereza wanasema Golden Chance Never Come Twice. Nilisema wiki iliyopita miaka 10-15 ijayo utakuwa ukijilaumu kwa mambo ambayo ulitakiwa uyafanye leo ukadhani bado una muda. Uzee hauna taarifa, utu uzima hauna hodi ikilala ukiamka utu uzima huu hapa. Wazazi wanakaa na watoto wao kila siku ghafla wanashangaa watoto wamesha balehe ama vunja ungo still wao hata kiwanja hawajanunua.
Wiki iliyopita niliandika "Kama wengine Wanaweza Kwanini Wewe Usiweze" kuna watu ambao session hii kwa maana ya majira haya wanajisikia kabisa kufanya jambo fulani la kimaendeleo lakini wamejawa na woga wa kuamua. Hata siku moja Woga hawezi kukupa maendeleo kwenye maisha. Mara 2 kwenye maisha yangu baada ya kumaliza shahada yangu ya Kwanza nilijiunga na Masomo ya Masters ajabu nikakosa amani kabisa ya ndani ya kusoma  nika Postpone mwaka ukaja Mwaka uliofuata Siku soma tena baada ya kuingia class siku ya kwanza. Kila mwanadamu ana "inner voice". Sema kwa kuto kujua utasikia tunasema, Unajua nilisikia kakiktu ndani ama machale yalinicheza, ndio maana asilimia kubwa ya watu  waliowahi kutapeliwa ukiwauliza mpaka unatapeliwa ulikuwa hujui??atakuambia kuna kitu nilihisi nikapuuzia. Kuwa makini sana na nyakati tulizonazo maana kila Jambo Lina Majira yake na Kila Majira yana Mambo yake.

MALAIKA AKITIBUA MAJI, USIENDELEE KUJIULIZA NINI CHA KUFANYA, ZAMA UPONE, IKIKUPITA MWAKA HUU, UNAWEZA KUSUBIRI HATA MIAKA 40...!!!

Think Differently and Make a difference.

Papaa
0713 494110
samuel_sasali@yahoo.com
Facebook. Samuel Sasali
Tweeter: Samsasali
Sype: Sasalijr.

HEKIMA KUTOKA KWA MY PS......"KABILA HALIRITHIWI"!!!

Habari zenu!
Najua mmemiss hekima za MY PS sana!
Nimepata bahati ya kukaa na kuongea nae mara kadhaa na nakumbuka moja ya jambo ambalo alilisema wakati ninamuhoji kuhusu asili yake ni hili;

Nilimuuliza wewe "Prosper Mwakitalima" ni mnyakusa wa wapi?(Maana ninajua kwa hakika Mwakitalima ni mnyakusa)

Lakini chakushangaza alinijibu akasema yeye ni "MNYIRAMBA WA SINGIDA" ndio hapo sasa tukaanza mjadala kuhusu makabila na kwa hakika ilikuwa ni maada tata lakini mwisho wa siku tukafika muafaka kuwa kabila halirithiwi!!

Hebu zingatia mfano huu
1st Kizazi;
A-family>>Baba Msafwa na Mama Mchanga,wanaishi Mtwara na wanapata watoto huko,
B-family>>Baba Mnyamwanga na Mama Mpare,wanaishi Kigoma nao wanapata watoto huko

Sasa huyu Mtoto wa A-family aliyekulia Mtwara kwa wamakonde anakuja kumwoa Binti wa B-family aliyekulia Kwa Waha kigoma na hawa wawili wanaamua kuishi Songea kwa Wangoni.....Sasa wakipata watoto,watoto wao watakua kabila gani??

Utagundua kuwa inabaki tu majina lakini ukweli ni kwamba asili zimeshapotea sana na sio jambo la kushikamana nalo kabisa,hiyo My ps alivyoniambia yeye ni Mnyiramba alikuwa sawa maana amezaliwa huko singida na kukulia huko kabla ya kuja Dar akiwa mkubwa tu,hivyo anafahamu zaidi unyirama kuliko Unyakusa.


VIPI KWA MFANO HUU;
Mkurya mmoja wa Mwanza  alimpa mimba Dada wa Kigogo na kumtelekeza Shinyanga(Kwa wasukuma),basi binti yule kwa mateso alipojifungua tu akamviringisha mtoto na kumwacha jararani,hapo Dada wa kindali alimwokota na kumpeleka polisi na hapo alitokea msamaria mwema akamuomba mtoto akamtunze na huyu ni Mkinga anayeishi Mtwara....sasa ikiwa huyu hajui mzazi hata mmoja wa mtoto na yeye ni mkinga anaeishi na wamakonde....JE HUYO MTOTO ATAKUWA KABILA GANI AKIKUA????

Ukipata majibu yatunze sana,lakini cha muhimu ni kuwa KABILA HALIRITHIWI.....Ila pale umekulia na kulelewa ndio palipokushape na kukufanya hivyo uko now na hakuna half cast wa kabila hata siku moja!!

Unaweza ukaendelea kutafakari na yamkini kuuliza ama kuchangia pia

By King Chavala-MC
+255 713 883797
http://kingchavala.blogspot.com

DARE NOT TO MISS.....LIVE SEMINAR WITH AZIM JAMAL IN DAR!!!!

Christina Shusho Atwaa Tuzo Ya Mwanamuziki Bora Kutoka Africa Mashariki Katika "Africa Gospel Music Awards"


Hatmaye Kampeni Zilizokuwa Zikiongozwa na Media Mbalimbali Za Kikristo na Kipindi Chako Bora Kabisa Cha Chomoza Ya Clouds Tv zimezaa matunda baada ya Mwanamuziki wa Injili Kutoka Tanzania, Christina Shusho kufanikiwa Kutwaa Tuzo ya Inayowahusu Wanamuziki wa Injili Africa almaarufu Africa Gospel Music Awards.

Christina Shusho anatwaa Tuzo ya Pili kubwa baada ya Mwanzoni mwa Mwezi July Kutwaa Tuzo nchini Kenya kwenye Tuzo za Groove Awards zinazofanyika nchini humo, na katika Tuzo za Africa Gospel Music Awards Shusho alikuwa akishindanishwa na Wanamuziki 6 Kutoka Kenya, Wawili Kutoka Uganda na Mmoja Kutoka Tanzania yaani Martha Mwaipaja.


Katika Usiku wa tarehe 7 July, 2013 wakati Shusho akitangazwa kwenda Kuchukua Tuzo hiyo hakuwepo nchini Uingereza bali Blogger Maarufu Tanzania mwenye Kumiliki Blog ya Gospel Kitaa Ambene Michael aliyeko nchini Uingereza aliwakilisha vema upokeaji wa Tuzo hiyo ya Shusho

Kushoto  ni Blogger Ambene Michael aliyepokea Tuzo Kwa Niaba ya Shusho Nchini Uingereza


Viva Shusho Viva Tanzania.

#...NI MARUFUKU!!#(04)......KUFANYA MAREKEBISO JUU YA JAMBO LA KUAZIMA BILA RUHUSA!!!!

#.....NI MARUFUKU KABISAAAA#
Ni marufuku kabisaa kufanya mambo au marekebisho au matengenezo usiyoruhusiwa juu ya kitu au jambo la kuazima bila ruhusa ya mwenyewe!
Kwa kawaida kitu cha kuazima hakina uhuru wa kutosha,kwani umepewa kwa kipimo....waswahili wanasema...."Nguo ya kuazima haisitiri Matako"
Kuna mambo mengi tunajiamulia wenyewe juu ya vitu vya kuazima na kwa kweli huwa inakuwa sio sawa,kwa mfano;

a)Mtu anakuazima simu yako aongee na mtu mara moja maana yake imeisha airtime ambayo nayo alikopa na hapo mlipo hamna access ya kununua....sasa unakuta mtu baada ya kupiga kwanza anaanza *102#....hivi hicho ndio umeomba au? na haishii hapo unakuta ameongea na simu zaidi ya hata alivyoomba yaani unakuta mtu kajiachia kama yake vile na bado credit ikiisha na kwako eti anakopa na anapiga tena mpaka na hiyo inaisha na hapo hajakwambia kitu...sasa wewe unashangaa ukitaka kupiga yule mrembo anakwambia....hauna salio la kutosha kupiga simu...basi unanunua vocha faster....unashangaa message.....Ahsante kwa kulipa deni.....na bado unadaiwa ......ahhhh dah sasa ndio nini hivi?
Hapo ulipokuwa umemuachia basi kapiga picha,kafungua na picha zako na mpaka bundle yako ya internet imeisha eti kisa anadownload miziki...Sasa wenye tabia hiyo nawaambia Marufuku,acheni kuwakwaza wenzenu,mimi tabia ya hata tu kuazimana simu wala sioni kama ina mashiko sana kipindi hiki ambako simu ziko tele na mawasiliano ni rahisi kwa yeyote!!!.....Umewezaje kununua simu na unashundwa kununua vocha??

b)Mtu anakuazima gari na unampa kwa roho safi tu,halafu anakwaruzana huko na kikimbiza gari gereji mchwara huko wanaanza kukuharibia gari hali angekwambia wewe una fundi wako unayemwamini,sasa anafanya hayo yote na hasemi,wewe ukija kushtuka siku moja unakuta some spears kwenye gari hazipo....ama mtu anakwenda huko halafu anakutana na stickers basi ananunua na kubandika kwa gari yako....hivi umeazima gari yangu ukanipambie au utumie na kuirudisha,tena mbaya zaidi eti mtu anakuwekea masticker ya kipepo kabisa na yeye anafurahia...sijui Majani,Kappa au Monster Power...jamani Ni Marufuku kabisaaa,ukiazima kitu kirudishe hivyo hivyo na usijifanye wewe ndio mwenyejiiiiiiiii

c)Mtu amekuja kwako kukutembelea may be anakaa wiki moja au siku kadhaa,kwa kuwa ni mgeni hapa ni nyumbani pa kuazima...sasa unakuta mtu anaanza kupanga na kupangalua mara kochi hili ageuzie kule,pambo hili aweke kule yaani wewe ukitoka kwa mishe mishe unakuta everything has changed,jamani hapa kwako? hata kama umetamani kunisaidia kwanini usiniulize? unajua kuna saa mnavuruga mahusiano ya watu hivi hivi,yaani mwenyewe mlimbwende amepanga na kupamba na umekubali for sake of love halafu huyu mfukunyuku anakuja na kuharibu kisha anaondoka,unafikiri akija huyo mlimbwende siku moja unamwambiaje kama sio dharau hiyo!!!!

Ipo mifano mingi sana,lakini nimesema marufuku tena marufuku kabisa!!
HESHIMU MIPAKA YA CHOCHOTE UNACHOPEWA,SIO UNAKARIBISHWA SEBULENI WEWE UNAENDA MPAKA CHUMBANI AAAAH!!
......Sema neno na wewe kama tumeelewana!!!

N.B;Hii ni kwa faida ya mahusiano na urafiki wa ko na watu,na hii inawahusu watu wenye akili timamu tu na wanaojielewa na kujitambua!!

@Kwa hisani kubwa ya Chavala Ideas Platform <http://chavalamedia.blogspot.com/>
(c)2013

Papaa On Tuesday.....Tofauti Ya Kuweza na Kutokuweza Ipo kwenye Kuamua


Tunakila sababu ya Kumshukuru Mungu kwa ajili ya siku hii ya leo ya Jumanne ya kwanza kwenye nusu ya pili ya Mwaka 2013, mwaka umeisha ingia nusu wenye kumaliza vyuo wameshamaliza, wenye kuendelea wanaendelea wenye kusoma wanakazana, wenye mipango ya biashara wanakazana, wenye kuanzisha familia  nao wamo wapo pia ambao mpaka sasa hawajajisoma wapo wapo tu yamkini wala hawajui kama na Obama alikuwepo nchini kwetu.

Miaka michache iliyopita niliwahi kuwa na Supervisor Mchina ambaye tulikuwa na kawaida ya kukutana Dept yetu na ku-plan mambo ya wiki na pia kupitia report za utendaji kazi. Ninakumbuka siku moja tukiwa kwenye kikao alichora duara mbili moja ikiwa kubwa na nyingine ndogo ikiwa ndani ya ile kubwa. Namkumbuka Mr. Charles Guo aliniambia duara la nje linaitwa "Uwezo Halisi" na duara la ndani linaitwa "Uwezo wa Sasa". Tofauti ya Kile unachokifanya sasa na Kile unachoweza Kukifanya sasa kipo kwenye kitu kinaitwa "Kuamua". Nakumbuka alitumia mfano huo wakati tunaongea issue za Performance Management alisema Watu wengi sana wanafanya mambo mengi sio katika Uwezo wao halisi, Uwezo walionao kutenda ni Mkubwa zaidi kuliko kile wanacho kifanya na kinachotofautisha kile wanachokifanya sasa na Kile ambacho wanaweza kukifanya kinajengwa na tofali kubwa lenye kuitwa "KUAMUA KUFANYA". Kuamua kufanywa kunaletwa na Kichochezi (motivation) ama Catalyst ama sababu ya mtu kufanya ndio maana kwenye makampuni kuna incentives mbalimbali ili kuchochea uwezo wa wafanyakazi kwenda extra mile.

Wiki hii katika Ujio wa Rais wa Marekani nimekumbuka sana mfano huu wa Supervisor wangu kuwa mambo mengi sana ambayo tunayafanya sasa kumbe tunaweza kufanya zaidi ya pale tunapofanya ambapo ndipo kwenye uwezo wetu halisi iwapo tu TUTAAMUA kufanya kikamilifu. Wiki hii nimeshuhudia jiji la Dar-es-Salaam likiwa safi na likiwa halina foleni zisizo na sababu, barabara za katikati ya Jiji zinapigwa deki usiku na Mchana, Jiji limekuwa safi na Salama likarudisha maana halisi ya Jina tulipopewa na Sultan kutoka Oman kuwa ni "Haven Of Peace" ni "Bandari Ya Salama". Nimeona Watu wakilindwa usiku na Mchana kila kitu kimekaa kama kinavyopaswa, wamachinga wameondolewa kwa nguvu kupisha Obama apite, Barabara ya Ubungo pale kwenye Mataa ilikuwa na Makorogeshi ya Kutosha pametengenezwa usiku na Mchana taa zinawaka vizuri kumbe uwezo wa kufanya tunao sana iwapo tu tutaamua kufanya sisi kama Watanzania pasipo ujio wa Obama.
Kinachofanywa na Serikali ya Tanzania ni Reflection ya Maisha halisi ya Watanzania kama sio Waafrika kwa Ujumla. Nakumbuka Wakati ninasoma mpaka Chuo Kikuu ile wiki ya Kuelekea kwenye Mitihani ndipo unaona watu sasa ndo wanashika vitabu kisawasawa kumbe unajiuliza swali kwanini mtu anakesha namna hii kumbe alikuwa hajaamua kusoma, kama angeanza semester wakati inaanza yamkini maisha yake ya kusoma yangekuwa yako mbali uwezo na upeo wake ungekuwa wa kutisha lakini ajabu ng'ombe analishwa siku ya mnada. Sisi ni watu ambao kwenye nyumba zetu kuna vyombo ambavyo havitumiki mpaka waje wageni, hata kama mtakuwa hamna wageni miaka 800 lakini kuna glass ziko kwenye kabati, kuna sahani ziko kwenye kabati ambazo wenyeji hawazitumii mpaka aje mgeni utashangaa mgeni akija nyumbani ndipo siku hiyo mtakunywa na soda, ndipo siku hiyo mtatumia sahani nzuri, ndipo siku hiyo mtapelekwa kuoga mchana, ndipo siku hiyo utaona mpaka goti la mkeo ama mama akiwakaribisha wageni kwenda kuchukua chakula ajabu ni kwamba Mgeni ama wageni wakisha ondoka tunarudi katika maisha yetu yale yale ya sahani za plastiki na soda za sikukuu kumbe kuna siku tukiamua kama familia tunaweza kula kama kuna wageni na hakuna madhara.

Ninakumbuka enzi hizo ninasoma shule ya Msingi ilikuwa siku kama kuna wakaguzi wanakuja ama mgeni fulani kututembelea siku hiyo bustani zote ndipo zitatifuliwa, zitamwagiwa na kupendeza, kwaya ya shule itafanya mazoezi ya nyimbo za kumpamba mgeni rasmi mpaka atajiramba kwa sifa, tabia hii ipo kwenye nyumba zetu za Ibada na Makanisa penye ugeni tutafanya zaidi ya kawaida hata sare tutashona, tabia hii ipo kwenye maofisi yetu, tabia hii ipo kwenye familia zetu, zipo kwenye mahusiano ya boyfriend na girlfriend na wachumba uwezo wa kufanya zaidi ya kile unachofanya sasa na kuzorotesha ndoa yako upo kwenye KUAMUA. Kwneye maisha yetu ya kawaida pia kuna watu ambao hawavai vizuri mpaka wawe na ugeni hawasafishi vyumba vyao mpaka siku akisikia anatembelewa, hawabadilishi mashuka na mapazia mpaka uwepo ugeni haya mambo ndiyo ambayo yapo kwenye Jamii yetu tofauti ya kile tunachokifanya sasa na Uwezo wetu wa kufanya upo kwenye Kuamua.

Kila mtu anaujua uwezo wake wa kufanya zaidi ya kile anachokifanya sasa lakini tatizo hujaamua kufanya, yamkini unaimba, yamkini ni mwandishi, yakini unasoma, yamkini ni Mwajiriwa ama Mwajiri kile unachokifanya kwa sasa kama ukiamua kikweliii ukaweka miguu yote ndani ya hicho ukifanyacho basi ungekuwa mbali kupita maelezo. Inawezekana unachukulia pouwa kile unachokifanya kwa sababu hujaamua kwenda extra mile, assume leo ukaamua ubadilike ubadilishe aina ya huduma unayofanya, ukaamua leo upate feedback ya kile unachokifanya uone watu watakuambia nini yamkini unafanya kitu ambacho kinakuharibia biashara yako, yamkini unaweza ukawa unafanya jambo chini ya kiwango ambacho wateja wanategemea ukijichunguza kiukweliii unaweza kufanya zaidi ya hicho unachofanya. Leo hii ukiamua ufanye kwa uhalisia wako uwezo wako wa juu kabisa kufanya unadhani utakuwa wapi, leo hii nikaamua kusaka news kwa uwezo wangu kikweliii ninaweza kuwa na gazeti la Gospel Today, leo hii ukaamua kuboresha ndoa yako kwa uhalisia wake utafurahia ndoa yako, ukiamua leo kuongea na Wateja unaowafikia kwa biashara ama huduma yako unadhani wataongea namna gani yamkini kuna kazi umewahi fanya ukaharibu na yule uliyemfanyia amekuwa wakala wa kusambaza uharibifu wa kile ulichofanya kwenye kazi yake, yote yawezekana kwenye maisha UKIAMUA.

Tofauti ya waliofanikiwa na kwenye maisha na wale wasiofanikiwa ipo kwenye KUAMUA. Wengi wetu tumebaki kuwa wachambuzi na wakosoaji na sio watu wenye kuamua, wengi huwa wanasisimka wakisoma Papaa On Tuesday lakini kasheshe iko kwenye Kutendea kazi. Yesu akasema anaheri yule anayesikia na Kutenda. Upo hivyo ulivyo kwa sababu ya aina ya maisha uliyoyaamua na siku ukiamua kufanya utashangaa kwanini ulichelewa kufanya maamuzi sababu kubwa Unaweza kufanya lakini yamkini hujaamua kufanya ingawa unajua ndani ya Moyo wako UKIAMUA kikwelii kufanya unaweza kufanya na kubadilika. Yamkini umekuwa ukitamani kubadilika tabia fulani kwenye maisha yako lakini umekuwa ukiindekeza ili uendelee kuwa nayo huku ukitambua fika tabia hiyo ndiyo imekuwa kikuharibia kila siku kwenye maisha lakini hujaamua tu kubadilika ukiamua inawezekana.

Hatma ya Maisha yako yanategemeana sana na MAAMUZI unayoyafanya kwenye maisha, ukiamua kubadilika utaona mabadiliko ukipotezea mabadiliko utajipoteza mwenyewe, ukitazama duara lako kubwa la uwezo ulio nao halifanani kabisa na kile ambacho unakifanya na unajua UKIAMUA inawezekana tatizo halipo kwenye kile unachokifanya tatizo lipo kwenye Maamuzi yako ya kuamua kufanya kwa utashi wa ndani kabisa.

Kuna bloggers wengi sana bado hawajaamua kufanya, kuna wafanyabiashara wakubwa sana wenye mafanikio wanaogopa kufanya, kuna presenters wazuri sana lakini hawajaamua kufanya kile walichoumbiwa kufanya sababu ya wasiwasi wa ndani,sababu ya maneno ya watu, yamkini sababu ya kiimani, ama una mashaka watu watakuonaje watakuchukuliaje utaendelea kubaki kama ulivyo sababu tu hujaamua kuwa vile unavyotaka kuwa kwa kuangalia tu mazingira ya nje, adui nambari one wa mafanikio yako ni nafsi yako mwenyewe. Ukimtafuta mtu yeyote aliyefanikiwa kwenye maisha atakuambia "aliamua".

Tofauti ya Wewe na wale uonaoona wamefanikiwa ipo kwenye Kuamua, ukiamua kulala njaa siku 7 ili kutimiza ndoto yako itakuwa, ukiamua leo kuacha tabia za kijinga kwenye maisha yako utapiga hatua, ukiamua kutulia utaoa ama utaolewa, ukiamua kukuwa kiufahamu ndipo utakapofanikiwa kumbuka kuamua ndiko kutakutofautisha na wasio amua.

Amua Sasa.

Ze Blogger
0713 494110

Breakthrough Conference Kuanza Rasmi Leo...Kawe Makuti



Lile Kongamano Kubwa lenye jina la "Kongamano La Mpenyo" linatarajiwa kuanza rasmi leo katika Kanisa la Kawe Makuti chini Ya Apostle Onesmo Ndegi...

Akiongea na Chomoza Pamoja na blog Hii, Apostle Ndegi amesema Kongamano hilo litahudumiwa na watumishi Wa Mungu Kutoka Ndani na Nje Ya Tanzania. Kongamano hilo linatarjiwa kuanza rasmi tarehe 25 Mpaka Jumapili nani ya Kanisa la Hilo.

Campus Night 2013 Ndani Ya Mikoa Minne



Ile Event Kubwa ya Kujumisha Wanafunzi wa Tanzania almaarufu kama Campus Night mwaka 2013 itafanyika kwenye Mikoa Minne chini ya Coordination ya Kanisa la VCCT na Makanisa Shirikishi katika Mikoa husika.

Mchungaji Dr. Huruma Nkone aliongea na Blog Hii pamoja na Kipindi chako Nambari One Chomoza Ya Clouds Tv kuhusiana na Maandali ya Campus Night 2013 itakayofanyika Dar, Kilimanjaro, Arusha na Mbeya

KULA MATUNDA SIO LAZIMA USHAURIWE NA DAKTARI!!!

Habari zenu!
Watu wengi sana hawana tabia ya kula matunda ipasavyo! wengine huona kama ni chombezo mezani,wengine ni ziada na wengine ni mpaka daktari aseme!

KULA MATUNDA KUNA FAIDA NYINGI SANA,HIZI NI BAADHI YA HIZO CHACHE;
a.Matunda mengi ni dawa, maana yana virutubisho asilia
b. Matunda yana Vitamini nyingi sana na madini, na matunda mengi yana Vitamin C
c. Matunda hususani yale yenye nyuzi nyuzi (rouphages) husaidia mmeng'enyo na uyeyushaji wa chakula mwilini.
d. Matunda huongeza damu mwilini na kusafisha pia mfano ndizi huongeza vitamini K ,ambayo inasaidia sana kwa WALE WENYE MATATIZO YA KUTOKA DAMU PUANI.
e. Matunda yenyewe ni mlo wa kutosha kabisa na kwa mujibu wa wataalamu mtu anaweza kuishi kwa matunda tu na bado akawa na afya njema kuliko mtu anayekula vyakula vingine!
Punguza kula mafuta mengi na sukari kwa mbadala wa matunda!

Kuna matunda mengine watu wanaona ni kama viungo tu lakini nataka nikwambie matunda na mbogamboga kama vile NYANYA,KAROTI,LIMAO ni matunda safi sana na viungo kama TANGAWIZI,VITUNGUU SAUMU NA VITUNGUU MAJI unaweza kula kwa kutafuna maana husafisha mwili na damu sana!

UNAPOKULA MATUNDA UNAKULA VITU ASILI,DAWA ASILI,MADINI NA VITAMINI ASILI,MAJI NA SUKARI YA ASILI....Hivyo kama huna utaratibu wa kula matunda basi anza sasa!!!

Huna haja ya kunywa chai asubuhi kila siku,wakati mwingine anza na matunda tu na hata unapolala usijichindilie na chakula kingi kizito,unaupa mwili kazi ngumu na kisha unalala, hivyo utashangaa unamka mchovu na kitambi kinatoka bila mpangilio!!

ANZA SASA KULA MATUNDA KWA AFYA YAKO!!!!

Niulize nikushauri
0713883797

Papaa On Tuesday...Usione Ukadhani

Ikiwa ni siku ya pili tangu nilipoutangazia umma rasmi kuwa sasa nimeamua kuvunja Ukimya na Kumtangaza Mchumba wangu ninayetarajia kufunga nae ndoa nimekwisha anza ku-experience maisha mengine tofauti ya yale ya kabla ya Jumapili. Ni Kwa neema ya Mungu leo nimefika hapa.

Leo nimejisikia vema tukatazama kile ambacho Diwani ya Mloka tulikisomaga kinaitwa Usione Ukadhani. Watu wengi sana wakiona jambo ama wakimuona mtu wanadhani kwenye Kiingereza wao wanasema "dont judge a book by its cover" ingawa kuna mdhanio mwengine ni wakweli mwingine vema ukasikia ama ukapitia ilikuweza kuwa na majibu sahihi. Mara nyingi sana jamii imekuwa na wepesi wa kufikia hitimisho ya kile ambacho wao wanakidhani ni sahihi kumbe sio. Mara kadhaa kwenye maisha yangu kuna watu waliwahi  nidharau kuwa siwezi kufanya kitu kutokana na muonekano wangu kumbe sio kabisa usione ukadhani.

Kutokana na mfumo wa maisha ya Watanzania na Waafrika kwa ujumla mambo mengi sana tunajifunza ukubwani tukiwa wadogo ni familia chache sana zinatoa mwanya wa mtoto kuji express feelings zake na ndoto zake na tangu utotoni tulifundishwa kuwa mambo mengi ni mabaya pasipo kuambia ubaya wake na tulifundishwa kukosea jambo lolote ni vibaya zaidi ndio maana kuna watu wakifeli mitihani wanaamua kujiua sababu kwenye maisha yake ameambiwa kufeli ama kushindwa jambo ni kitu kibaya. Ukiwa mtoto ukiongea ongea sebuleni na kupiga piga meza ukawa unaimba nyimbo za kitoto utaambiwa kelelee, nyamazaaa basi unakuta unapoteza confidence na saikolojia yako inaambiwa hutakiwi kufanya jambo hili mbele ya wazazi. Ukiwa mtoto ukasema "mama mie mchumba wangu mtoto wa Mzee Charle" usiku huo huo utachapwa fimbo kuwa umeanza kuharibika matokeo yake saikolojia ya ufahamu inaambiwa kuwa kupenda mtu ni vibaya na kwa kuwa umri wa kutoka nyumbani kwa wazazi kwetu sisi ni pale unapoweza kujitegemea unajikuta mambo mengi sana unajifunza sio mbele ya wazazi ama watu waliokulea ndio maana kuna mambo mengi sana wazazi wetu hawajui kama tunajua kwa ufahamu wao wazazi wanadhani watoto wao hawajui kumbe watoto ndio wamegeuka waalimu.
Nakumbuka zamani enzi zetu wakati tunakuwa kabla video hatujaja kuangalia sebuleni baba na mama wanakuwa wanaingalia kwanza kama kuna sehemu sio nzuri basi alikuwa anakaa na remote control ikifika lile eneo anazima anapeleka mbele kidogo kisha tunaendelea. Kwa sisi watoto watundu tangu zamani tulikuwa tunamaswali hivi pale anapopeleka mbele kuna nini?basi wengine walienda extra mile tukavizia wakati baba na mama hawapo tukawasha tukaangalia mwanzo mwisho ila baba na mama wakirudi wanajua hatujui kuna nini. Tofauti na Kizazi cha sasa ambacho wao hutazama kanza kupitia mitandao kisha kama watatazama na familia watoto ndo wanawaambia wazazi sasa "baba hapo forward kidogo sio pazuri" sasa najiuliza mtoto ndo anamwambia baba aforward kwa manufaa ya nani baba ama yeye mtoto??Usione Ukadhani watu kizazi hiki hawajuio kwa taarifa yako watu huwa wanaambiana.

Usione leo mtu hana chochote ukadhani ataendelea kuwa kama alivyo, watu huwa wanabadilika kwenye maisha priorities nyingi sana za wanaume huwa zinabadilika pia kutokana na umri aliokuwa nao, majukumu aliyokuwa nayo na Marital Status yake pia. Kabla ya kuwa na mpango wa kuoa kwenye maisha atakuwa anawaza kula bata atakuwa anawaza kukutana na Jack, Rose, Mwamntumu, kwenda movie, kwenda mlimani City, akishaanza kuwa na mahusiano majukumu yanabadilika harusi ikikaribia kama mimi utakuwa unawaza Shella la Bibi harusi, Kiatu Cha Bibi harusi, Suti ya Bwa. Harusi Ukumbi, Mc pole pole akili inaanza kuwaza majukumu. Ukishapata familia sasa na mtoto utaanza kuwaza Pumpus za mtoto, mara bima ya afya ya Mtoto, ada ya shule, Mke nae avae,afanya kazi, mtaanza kufikiri Miradi ya kifamilia,mtawaza kujenga usione leo mtu yupo yupo ukadhani ataendelea kubaki alivyo. Akili hukuwa kwa kuzoeshwa ingawa inawezekana sio wote lakini Kibongo bongo tunakuwa kwa kukosea sana ukubwani hata namna ya kuishi na mume na mke tangu utotoni akili imejizoeza kujificha ficha hata kama ni halali.
Jambo usililolijua ni kama usiku wa giza unaweza ukaona leo mtu amekuwa na mafanikio ukadhani yalikuja kirahisi rahisi kwenye maisha. Kuna watu ukisikiliza hatua zao za maisha unajiona kabisa wewe unadeka unataka mafanikio wakati hata kushinda njaa mchana tu huwezi kuna watu mpaka leo wametoboa kwenye maisha wanahistoria ambazo ukizisikiliza kuna nyakati waliomba usiku usiingie sababu hawana sehemu za kulala walitamani kama kuna mahali wanaweza uza njaa basi wangeuza kwa bei yoyote ili wasiwenazo milele kuna watu walishinda njaa si kwa sababu walitamani kufunga la hasha hakuna chakula usione ukadhani kila kitu kinakuja bure. Tamaa mbaya ya mafanikio ya haraka haraka ndio inayopeleka mtoto wa masikini akiwa form four anawaza kuwa na blackberry yuko tayari kufanyiwa chochote apate blackberry used. Usione Mtu ukadhani kila mtu anaendesha gari leo amenunua kihalali wengine wamenunua ka kudhalilisha maisha yao ili waonekane. Usione leo watu wameajiriwa kwenye makampuni makubwa ukajua wameshinda interview za kazi walishinda interview za ngono ndio wakapataKama kuna kitu Watanzania kinatutesa ni Ulimbukeni. Usine Ukadhani.

Usione wanandoa wanaongoza kuingia kwenye ukumbi wa harusi wako pamoja wamevaa vizuri ukadhani hilo tabasamu ndilo walilokuwa nalo wakiwa nyumbani. Ungepata fursa ya kujua undani wao ndipo ambavyo ungefuta dhana yako ya kuolewa ili na wewe tu uwe na mume sababu uliosoma nao wameolewa, uliocheza nao wanawatoto, ungefuta dhana ya kuoa sababu mke wako ana umbile la namba 8, mke wako aonekane ana makalio, ama mweupe au mweusi kwani unaolea jamii ama unaoa kwa utashi wako mwenyewe wengi waliokimbilia ndoa kwa sababu za kijamii wamejikuta wamekwama na kama ingekuwa dini yetu ya Kikristo inaruhusu talaka wengi wangechukua talaka pamoja na kuto kuruhusu watu wanatoka wamechokaaaa. Rafiki yangu mmoja alinichekesha akasema kuna wengine wamefika stage wanaombea basi hata wafe ili wapumue maana hawa wanandoa wakiwa mbele za watu full matabasamu full kushikana mikono lakini wakiingia tu kwenye gari kurudi nyumbani maisha ya Chui na Paka yanarudi kuna wanawake leo wanatamani  wangeolewa na wanaume masikini wachume pamoja kuliko waliowachagua wanaume wenye uwezo wamejikuta wanaambulia majuto kuliko furaha usine ukadhani.

Usione watu wanavaa tai na sketi nzuri wanafanyakazi kwenye maofisi ukadhani wanafuraha na kazi zao, shida ndio zinasababisha waendelee kwenda ofisini wengine hawana hata mishahara wana mikopo kupita Serikali ya Tanzania, kuna watu wanaenda maofisini hawana hata mikataba ya ajira zao yaani hawana hatma ya kesho yao itakuaje kiajira, we usione watu wanavyojiupara na kula chips kuku ukadhani mambo yao safi, simu zao nzuri hazina vocha, mabegi yamejaa vipodozi vinavyokaribia kwisha, nguo wamekopa pale kwa mdada anayepitisha ofisini kwao kwa muonekano wa njee utadhani wanaraha kuliko wewe, ukitaka kujua uhondo wa ngoma uingie ucheze usione ukadhani ndugu yangu.

Maisha kila siku ni kujipanga unaweza ukadharaulika leo ukajipanga ukashangaa wale aliokuwa wanakucheka ndio baadae wanakupongeza watu huwa wanakawaida ya kudharau watu usitegemee kupendwa kabla ya kudharauliwa kwanza. Mtu mmoja anayekutia moyo wakati wa shida ni muhimu zaidi kuliko jeshi linalokushangilia baada ya ushindi. Usione ukadhani wewe jipange ili kuweza kusonga mbele. 

Think Differently and Make A difference.

Usione Ukadhani.

Samuel Sasali
0713 494110
Facebook: Samuel Sasali
Skype: SasaliJr